Mambo matano aliyosema Rais Samia jana yaliyonisikitisha

Sidhani, JPM pamoja na Mimi kutokubali ni mara kumi zaidi ya Samiah. JPM asingeanza kulalamika mikopo inatunyanyasa
Asingelalamikia mikopo kwa sababu alikuwa mpenda sifa, mpenda kujiamini na kutaka watu wameone sio wa kawaida.

Hulka za Samia na hayati JPM ni mbili tofauti. Nakuhakikishia hakuna mradi aliouacha JPM ambao Samia hataumaliza na pia anaendeleza miradi aliyoianzisha ndani ya miaka hii mitatu akiwa ikulu.
 

Kwa nini asiiendeleze wakati alikuwa makamu wa rais?
 
Alisema Mwenda naye alikuwa mwizi kwa hiyo anamtuma mwizi akawadhibiti wezi wenzake kwa sababu anajua mianya ya wizi!
 
Umenikumbusha Kwenye ishu ya TRA, Magu aliwahi kusema kuna watu wao ni Untouchable pale TRA. Sasa sijui inakuwaje Raisi ana vyombo vyote anashindwa kudeal na watu wapuuzi wapuuzi pale TRA.
 
Hiki ni kichekesho yaani unataka zero brain ijue kupambanua mambo kweli? Tuna hasara kama Taifa!
 
Uki peleka nje faida lazima utakopa Tu. Maana faida ni sehemu ya mtaji wa kuongeza utajiri wako na kukuza uchumi na kutoa ajira.
Sasa unapo binafsisha Bandari Kwa dipiweldi , Adidas na wengineo ni kusafirisha faida . Na kunyima fursa za kazi za watu wako, matokeo yake ni haya ya kukosa Fedha za kigeni, ukosefu wa kazi kuongezeka, kufifisha uhuru wa Nchi , kwani aliyekodishwa bandari na kupewa faida bila kupanda ndio atakuja kutuchagulia viongozi ili mikataba zaidi ya aina hiyo apewe yeye , na ukitaka kumtoa, umlipe mapato ya miaka iliyo Baki ya mkataba wake na uongo mwingine wa vifaa alivyoweka na vingine vyetu, Kwa sababu ya kukosekana uwazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…