Mambo matano aliyosema Rais Samia jana yaliyonisikitisha

Wewe ukiitwa mpumbavu kabisa utakasirika? Kazi ya rais wa nchi mwenye kila aina ya zana za kuongoza nchi ni nini? Unamaanisha hii nchi inaendeshwa na kundi la mapapa na siyo rais? Kama ni hivyo rais anafanya nini pale ikulu? Mawazo ya kipumbavu kabisa haya.
Wewe ndio mpumbavu baada utetee hoja yako unatukana kama kuku aliekatwa kichwa mimi nimetoa maoni yangu hvyo sio lazima ukubaliane nayo na ww sio lazima kila mtu akubali mawazo yako maana nyie ndio mlikuwa vinara wa kumtukana magufuli leo mmehamia kwa samia mnataka raisi wa aina gani sasa.
 
Unasubiria? kweli una macho lakini hayaoni, una masikio lakini hayasikii. Hivi huelewi kuwa sasa hivi kariakoo inajengwa upya na soko la zamani sasa lipo asilimia 99? Watu wanawekwa sawa wahamie tu.

Na area nzima ya Kariakoo, kila mahali kuna Rebuilding na reforms za ajabu, haijawahi kutokea, unaishi mkoa gani?

Ikiwa huyaoni yanayoendelea basi hata kusikia husikii? utasubiri sana. Jikumbushe:

View: https://youtu.be/yx2bAloztJU?si=zqOmircmU2qo056L

Usichanganye KARIAKOO SOKONI na SOKO LA KIMATAIFA LA KARIAKOO.
 
Tatizo letu Kwa sasa Tanzania ni Rais ni mkweli sana na anapenda kufanya good governance, wakati watanzania hawajazoea kusikia ukweli, wala hawajazoea kuwa good citizens...Tumepewa right president at a wrong time and to the wrong people
Statement yako ni ya kutoka kwa mtu mwenye akili na upeo mkubwa sana.
HUlka yetu wanadamu wengi hatupendi kuambiwa ukweli ambao ni Negative, ni sawa na mwanamke usimpodanganya unaweza usimpate maana yeye anahitaji kusikia Positive Hopes
 
Huyu mpya kaambiwa asikubali kuwapendezesha , ampendezeshe Rais pekee yake. Ni kama Rais kazidiwa nguvu na watu au kundi Fulani humo TRA.
'Chura Kiziwi' upeo wake ni mdogo sana.

Kila analo jaribu kulieleza, hata ukijaribu kulielewa maana yake ni nini hasa inakuwa vigumu kuelewa amelenga kufikisha ujumbe gani!

Ni maneno tu yanamtoka kinywani bila ya kuwa na maana yoyote.
 
Maneno yake saa zingine Yana ukakasi.
 
Hili hajaongea?
 
Attachments

  • IMG-20240707-WA0018.jpg
    IMG-20240707-WA0018.jpg
    85.4 KB · Views: 2
Yule mama yetu kwa sasa ni kama kachanganyikiwa kimtindo, halafu kwa sasa anaongoza kwa hofu na wasiwasi mnoo huku akikosa kujiamini na kutaka kujionyesha kuwa anaweza kumpendeza kila mtu ikiwemo wale anao watumbua.
Wewe umefunga mada.
Na atakayekubishia ni mbumbumbu mzungu wa reli asiyejua kutafsiri mambo.
 
Wakati Rais Samiah akiwaapisha Viongozi Jana , Kuna mambo matano aliyasema kwenye hotuba yake ambayo yalinisikitisha.

1. Jambo la kwanza Rais kadai mikopo inaifanya Tanzania inyayasike

Nimehuzunika Rais anapokiri ya kwamba mikopo tunayokopa inatufanya tunyanyasike. Huyu ni udhaifu mkubwa wa Rais wa Nchi kukiri hadharani ya kwamba anapoenda kukopa huko nje huwa ananyanyasika. Kwa maana nyingine Rais amekiri kwamba hii mikopo Ina masharti magumu kabla ya kukopa na hata baada ya kukopa yanayoifanya nchi inyanyasike Kama alivyosema Rais.

Pia kwenye muktadha huo, Rais kadai tunakopa nje na kunyanyasika kwa sababu watu hawalipi Kodi. Kwa maana nyingine Rais alikuwa anajua Kodi hazilipwi ila akawa anafidia kwa kukopa mikopo huko kwa wanyanyasaji, Sasa unyanyasaji umekidhiri kaamua kudai Kodi ilipwe.

Swali langu kwa Rais kwanini unakubali nchi inyanyasike kwa mikopo mnayokopa?. Na hayo manyanyaso ni yepi tuyajue, isije kuwa Kuna masharti magumu yanayoingilia uhuru wa Taifa wa kiuchumi, kisiasa, kisheria na hata kitamaduni. Tuweke wazi kwenye hili.

2. Jambo la pili Rais kadai Pale Kariakoo kuna siasa nyingi.
Rais amedai ya kwamba alituma wajumbe wake kwa Siri kule kariakoo na kugundua ya kwamba Kuna wafanyabiashara wengi walikuwa wanafungua maduka au kuingia kwenye mgomo bila ya kujua sababu ya mgomo.

Nimeshangaa kwa kauli hii ya Rais. Maana mwaka Jana wafanyabiashara wa Kariakoo walifanya mgomo na mwisho wanafanya kikao na Waziri Mkuu pamoja na Waziri wa Fedha, na walieleza sababu nyingi Sana za kwanini wanagoma Tena live kwenye vyombo vya habari.

Inakuwaje Tena hao hao wafanyabiashara ndani ya muda mfupi wadai hawajui kwanini wanagoma? Ok, tufanye hawajui wanachogomea, ni kwanini Serikali ilisitisha baadhi ya kanuni kwa muda? Kama vile matumizi ya EFD na Faini ya kutotumia receipt kwa wafanya biashara wa Kariakoo?. Ina maana Rais pamoja na kupata taarifa ya wafanyabiashara kutojua wanagomea nini bado aliendelea na kusimamisha kanuni?.

Naona Kama Rais amejichanganya au anatuchanganya kwenye hili eneo, au yeye ndio analeta siasa kwa kudai wanaogoma hapo kariakoo hawajui sababu kwanini wanagoma na bado serikali ikasimamisha kanuni hapo kariakoo.

Swali langu ni kwamba je wale wafanyabiashara hawakuwa na sababu za kugoma? Na ni kwanini Serikali imeukubali kutii baadhi ya malalamiko ya watu ambao inajua hawajui wanachogomea?.

3. Jambo la tatu, Rais kaingiza mambo ya jinsia kwenye kazi za Serikali
Wakati anamtambulisha Waziri mpya wa viwanda na biashara, Ndugu Suleiman Jaffo, Rais kadai amaemua kumteua Jaffo maana pale kariakoo Kuna mikikimikiki mingi ambayo Dr Ashatu Kijaji asingeiweza kwa sababu ni mwanamke. Nikajiuliza kwanini alimteua kwenye nafasi hiyo Kama alijua kwa mikiki iliyopo kwa Waziri mwanamke hataiweza?.

Rais akaendela kudai ya kwamba ameamua kumteua Dr Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Mazingira na Muungano, ili ashughurikie mambo ya nishati ya gesi ya kupikia. Akadai amemteua yeye pamoja na Naibu Katibu Mkuu mawanamke maalim kwaajili ya kushughulikia gesi ya kupikia. Na akadai kwasababu wao ni wanawake amewateua makusudi na wakishindwa atashangaa wanashindwaje na wao ni wanawake.

Swali langu la msingi ni je Kuna Wizara zinazowafaa wanawake tu? na Kuna Wizara zinazowafaa wanaume tu?. Na Kama zipo ni Wizara zipi hizo?. Na kwanini Rais anazijua na bado amateua jinsia tofauti kwenye Wizara husika?

4. Jambo la nne Rais kadai kuwa Wafanyakazi wa TRA walifanya sherehe Kidata alipohamishwa TRA
Rais kwenye hotuba yake kadai kwamba taarifa za kuhamishiwa zilipofika TRA, wafanyakazi wengi walifurahia Sana na kuamua kufanya sherehe. Kwa maana nyingine Kidata alikuwa very strict kwenye kazi yake lakini bado Rais akamuondoa.

Kwenye muktadha huo huo Rais kadai Kidata hakuoendwa na TRA na pia hakuoendwa na Ikulu maana alikuwa mchapa kazi Sana na amenyooka. Sasa ikamwa najiuliza Kama una Kamishna mkuu wa TRA anayejituma na kusimamia taratibu, inakuwaje unamtoa hapo?. Unadai atakuwa mshauri wako, kwanini awe mshauri wako ilhali alikuwa anasimamia taratibu na anajua kazi?.

Swali langu ni kwamba Kama Kidata alikuwa amenyooka mpaka kuchukiwa na Ikulu pamoja na wengine , inakuwaje Rais kamtoa? Rais anahitaji mtu wa aina gani mwingine?. Kama Kidata hakuwa Mtendaji mzuri kwanini Rais adanganye?.

5. Jambo la mwisho, Rais kamuomba Kamishna Mkuu wa TRA kutoshirikiana na TRA kuiba
Kwenye hili Rais kakosea Sana kuliweka alivyoliweka. Maana kauli yake ni kwamba anathibitisha ya kwamba TRA Kuna wezi. Sasa Kama kiongozi wa nchi unajua Kuna wezi ndani ya TRA kwanini huchukui hatua?. Na kwanini umewaacha wezi qanaendelea kuiba na Wala huwa kamati mpaka unamshauri Kamishna mpya wa TRA asishirikiane na wezi waliopo ndani ya TRA.

Swali langu ni kwamba hawa wezi ndani ya TRA ni akina nani?

By Econonist.
WEZI NI WANACCM
 
Kama ulimsikiliza alisema jana kwamba kidata mpaka baadhi ya watumishi wa ikulu na viongozi wa serikali walikuwa hawampendi itafakari vizuri hyo kauli.
Pamoja na hayo mimi pia nimesikitika kumsikia rais anachanganya kiswahili na kiingereza kwenye hotuba huku rais za Msumbiji akiongea kiswahili safi. Alafu rais anatuambia kiswahili kiongelewe duniani kote. Mimi sijawahi kumuona mwingereza anayeongea kiingereza na kuchanganya maneno ya kiswahili.
 
Ameanza kuelewa kwamba vita ya uchumi ni mbaya.
 
Back
Top Bottom