Mambo matano aliyosema Rais Samia jana yaliyonisikitisha

Mambo matano aliyosema Rais Samia jana yaliyonisikitisha

Ssa hivi unaweza kugoma kwa kudeka na ukasikilizwa, unaweza kufanya maandamno kwa kudeka na ukasikilizwa na yote hayo na ulinzi juu unapewa.

Sasa hivi tunaona wapinzani wanawaalika CCM kwenye mikutano yao na wanapewa nafasi ya kuongea, tulimuona Rais mamam smia akilianzisha hilo kwa kina mama wa chadomo, juzi nimeona tena Mkuu wa wilaya fulani huko Tanga na yeye aliombwa awakaribishe wilayani kwake wa upinzani,

Hujaiona tu nguvu ya Rais mama Samia?
Hiyo ni nguvu ya Samiah au uungwana wa upinzani?. Maana hata maandamano yamekuja baada ya CHADEMA kususia mikutano yake ndipo alipowaomba waongee naye chemba na ndipo alipokubali. CHADEMA kumaribisha kwenye event yao ilikuwa ni gesture of friendship ila Rais akawageuka alipokataa katiba mpya na kuleta ngonjera za miaka mitatu ya elimu ya Katiba.
 
Ndio mwenye shida, haiwezekani watu wote wawe na shida,atafanya kazi na nani? Yaani Nchi ipate hasara ya Migomo kisa Kidata? Hizo akili mtafany Machadema sio Samia.
Ok, ndio maana ufisadi hautaisha ndani ya serikali ya CCM. Mzuri akizidiwa na wabaya anatolewa.
 
All in all mama astaafu 2025. Tupate Rais atakaye kusanya Kodi na kupunguza Deni la nje.
 
Hiyo ni nguvu ya Samiah au uungwana wa upinzani?. Maana hata maandamano yamekuja baada ya CHADEMA kususia mikutano yake ndipo alipowaomba waongee naye chemba na ndipo alipokubali. CHADEMA kumaribisha kwenye event yao ilikuwa ni gesture of friendship ila Rais akawageuka alipokataa katiba mpya na kuleta ngonjera za miaka mitatu ya elimu ya Katiba.
Hakuna uungwana wa upinzani wala nini, kuw mkweli wa nafsi yako. Hiyo ni falsafa ya "Reconciliation" ya Rais mama Samia Suluhu Hassan.

Wakati wa mwendazake, mzee wa kujimwambafai, mliweza kufanya maandamano? hata mikutano mlikatazwa, na anayefanya kwinyu, anafinywa.

Hakika watwana ni wepesi wa kusahau.
 
Leta reforms za mama.
1) uchumi; Tanzania sasa hivi ina viwanda vingi kuliko wakati wowote, sekta ya utalii sasa inaingiza kipato mpaka tanzania hoteli za kitalii hazitoshi. kwa ufupi kila sekta ya uchumi inakuwa kwa kasi.

Kilimo: Kwa mara ya kwanza Tanzania tunaona mazao ya kilimo cha chakula yakiuzwa mpaka nje kwa takwimu kabisa. Kuibiwa ibiwa kiholela kumeanza kwisha.

Siasa: chadomo sasa wanafanya maandamano mpaka wenyewe wnachoka, wanafanya mikutano ya hadhara mpaka wanachoka.

Elimu" Shule za mama Samia za kisasa kabisa, walimu wanapata ajira na wanapandisshwa madaraja na mishahara inaongezwa. Kabla ya mama Samia mika mingapi madaraja hayajapanda na mishahara haijaongezwa kwa waliumu?

Unalo?
 
Dada, Kuna kitu hutaki kukubali. Unapodai sheria zote msingi wake ni katiba , je hizo sheria zinaweza kubadilishwa na kwenda kinyume na Katiba?. Sheria zote lazima ziendane na Katiba.

Rais alitakiwa aanzie kwenye Katiba kwanza sio kwenye sheria. Kwa mfano kwenye sura ya kwanza ya Katiba Tanzania inafuata mfumo wa ujamaa na kujitegemea. Je kwenye uhalisia Tanzania ni nchi ya Kijamaa?. Je sheria zetu zinafuata misisngi ya Kijamaa?.

Tuna Katiba iliyopitwa na wakati ambayo ndio kikwazo Cha reforms nchini. Huwezi kuwaza kuwa na uchumi wa juu wakati Kattiba yako ni ya mwaka 77, 84 na mara ya mwisho imerekwbishwa 2005 miaka kumi na Tisa iliyopita.

Tunataka reforms tuanze na Katiba kwanza mengine yafuate.
Sheria haziwezi kubadilishwa na kwenda kinyume na katiba.
 
Unachekesha kweli. Nikikuuliza unitajie rekebisho hata moja kwenye katiba utakuwa nalo?. Unataka kuniambia Rais huyu aliyesema Katiba ni kijitabu ndio ataleta katiba mpya?.

Kama huyo Rais angetaka reforms za kweli angeanza na mchakato wa Katiba Mpya ili kutengeneza Tanzania tuitakayo, halafu Katiba ndio itaanalyze reforms zote , ambazo kila mmoja atazishikilia.

Na mchakato ulikuwa very simple. Wataalamu wa Katiba wangekaa na kuja na Rasimu wananchi wanaipitia na baadaye kujipigia kura. Ndipo reforms zinaanza rasmi kwa kubadilisha sheria ziendane na Katiba Mpya. Sio hizi stori za kisiasa za Rais.
Hivi unafikiri katiba ni za nini kwa nchi zinazofata mfumo wa katiba?
 
1) uchumi; Tanzania sasa hivi ina viwanda vingi kuliko wakati wowote, sekta ya utalii sasa inaingiza kipato mpaka tanzania hoteli za kitalii hazitoshi. kwa ufupi kila sekta ya uchumi inakuwa kwa kasi.

Kilimo: Kwa mara ya kwanza Tanzania tunaona mazao ya kilimo cha chakula yakiuzwa mpaka nje kwa takwimu kabisa. Kuibiwa ibiwa kiholela kumeanza kwisha.

Siasa: chadomo sasa wanafanya maandamano mpaka wenyewe wnachoka, wanafanya mikutano ya hadhara mpaka wanachoka.

Elimu" Shule za mama Samia za kisasa kabisa, walimu wanapata ajira na wanapandisshwa madaraja na mishahara inaongezwa. Kabla ya mama Samia mika mingapi madaraja hayajapanda na mishahara haijaongezwa kwa waliumu?

Unalo?
Ambao hawalipi kodi ni kina nani hadi rais alalamike na kwenda kukopa?
 
Ndio mwenye shida, haiwezekani watu wote wawe na shida,atafanya kazi na nani? Yaani Nchi ipate hasara ya Migomo kisa Kidata? Hizo akili mtafany Machadema sio Samia.
Pamoja na udhaifu wa kidata ambao ulijulikana toka pale aliteuliwa mwanzo, wizara ya fedha na waziri wake na serikali wote ni sehemu ya matatizo ya TRA, kodi nyingi ni kandamizi! service levy kwa mfano ilielezwa bayana namna ilivyoanza na vile inavyopaswa kuondolewa..mwaka jana waziri mkuu alielezwa yote haya, nini kimefanyika??? halafu unamuondoaje Kamishna au hata kubadili waziri wa biashara kwa sababu ya shida za soko la kariakoo??? kwa hiyo Jafo ni waziri wa kariakoo na huyo mwenda ni kamishna wa dar es salaam sababu amezaliwa mjini! very poor reasoning!
Mfumo mzima wa kodi Tanzania ni mbovu!! mnataka muambiwe mara ngapi msikie???? tafuteni mshauri atizame kiwango cha maisha na uchumi wetu na rasilimali zake ili a-set viwango vipya vya kodi vinavyoendana na hali halisi na viwe vinabadilika kulingana na mabadiliko yote inapotokea! huwezi ukawa na kampuni ina wateja zaidi ya million 15 halafu hata kwenye walipa kodi watatu bora haimo! kwa nchi zetu benki haziwezi kuwa ndio walipa kodi bora! hiyo ni dalili hasi kiuchumi! hakuna uwekezaji, watu ni masikini, sekta binafsi ni dhaifu, una sekta isiyo rasmi kubwa zaidi ya asilimia 50, level za amana ni chini sana..benki inakuwaje mlipa kodi bora???
Kuendelea kuwaachia tiss waweke mtu/watu wao TRA ni kutengeneza matatizo, kwanza si jukumu lao kuingilia mambo ya kodi, hivi tumekosa kabisa mtu wa kutia adabu hawa watu???
 
Sasa Kidata ndio ameleta Kodi kandamizi?
 
Wakati Rais Samiah akiwaapisha Viongozi Jana , Kuna mambo matano aliyasema kwenye hotuba yake ambayo yalinisikitisha.

1. Jambo la kwanza Rais kadai mikopo inaifanya Tanzania inyayasike

Nimehuzunika Rais anapokiri ya kwamba mikopo tunayokopa inatufanya tunyanyasike. Huyu ni udhaifu mkubwa wa Rais wa Nchi kukiri hadharani ya kwamba anapoenda kukopa huko nje huwa ananyanyasika. Kwa maana nyingine Rais amekiri kwamba hii mikopo Ina masharti magumu kabla ya kukopa na hata baada ya kukopa yanayoifanya nchi inyanyasike Kama alivyosema Rais.

Pia kwenye muktadha huo, Rais kadai tunakopa nje na kunyanyasika kwa sababu watu hawalipi Kodi. Kwa maana nyingine Rais alikuwa anajua Kodi hazilipwi ila akawa anafidia kwa kukopa mikopo huko kwa wanyanyasaji, Sasa unyanyasaji umekidhiri kaamua kudai Kodi ilipwe.

Swali langu kwa Rais kwanini unakubali nchi inyanyasike kwa mikopo mnayokopa?. Na hayo manyanyaso ni yepi tuyajue, isije kuwa Kuna masharti magumu yanayoingilia uhuru wa Taifa wa kiuchumi, kisiasa, kisheria na hata kitamaduni. Tuweke wazi kwenye hili.

2. Jambo la pili Rais kadai Pale Kariakoo kuna siasa nyingi.
Rais amedai ya kwamba alituma wajumbe wake kwa Siri kule kariakoo na kugundua ya kwamba Kuna wafanyabiashara wengi walikuwa wanafungua maduka au kuingia kwenye mgomo bila ya kujua sababu ya mgomo.

Nimeshangaa kwa kauli hii ya Rais. Maana mwaka Jana wafanyabiashara wa Kariakoo walifanya mgomo na mwisho wanafanya kikao na Waziri Mkuu pamoja na Waziri wa Fedha, na walieleza sababu nyingi Sana za kwanini wanagoma Tena live kwenye vyombo vya habari.

Inakuwaje Tena hao hao wafanyabiashara ndani ya muda mfupi wadai hawajui kwanini wanagoma? Ok, tufanye hawajui wanachogomea, ni kwanini Serikali ilisitisha baadhi ya kanuni kwa muda? Kama vile matumizi ya EFD na Faini ya kutotumia receipt kwa wafanya biashara wa Kariakoo?. Ina maana Rais pamoja na kupata taarifa ya wafanyabiashara kutojua wanagomea nini bado aliendelea na kusimamisha kanuni?.

Naona Kama Rais amejichanganya au anatuchanganya kwenye hili eneo, au yeye ndio analeta siasa kwa kudai wanaogoma hapo kariakoo hawajui sababu kwanini wanagoma na bado serikali ikasimamisha kanuni hapo kariakoo.

Swali langu ni kwamba je wale wafanyabiashara hawakuwa na sababu za kugoma? Na ni kwanini Serikali imeukubali kutii baadhi ya malalamiko ya watu ambao inajua hawajui wanachogomea?.

3. Jambo la tatu, Rais kaingiza mambo ya jinsia kwenye kazi za Serikali
Wakati anamtambulisha Waziri mpya wa viwanda na biashara, Ndugu Suleiman Jaffo, Rais kadai amaemua kumteua Jaffo maana pale kariakoo Kuna mikikimikiki mingi ambayo Dr Ashatu Kijaji asingeiweza kwa sababu ni mwanamke. Nikajiuliza kwanini alimteua kwenye nafasi hiyo Kama alijua kwa mikiki iliyopo kwa Waziri mwanamke hataiweza?.

Rais akaendela kudai ya kwamba ameamua kumteua Dr Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Mazingira na Muungano, ili ashughurikie mambo ya nishati ya gesi ya kupikia. Akadai amemteua yeye pamoja na Naibu Katibu Mkuu mawanamke maalim kwaajili ya kushughulikia gesi ya kupikia. Na akadai kwasababu wao ni wanawake amewateua makusudi na wakishindwa atashangaa wanashindwaje na wao ni wanawake.

Swali langu la msingi ni je Kuna Wizara zinazowafaa wanawake tu? na Kuna Wizara zinazowafaa wanaume tu?. Na Kama zipo ni Wizara zipi hizo?. Na kwanini Rais anazijua na bado amateua jinsia tofauti kwenye Wizara husika?

4. Jambo la nne Rais kadai kuwa Wafanyakazi wa TRA walifanya sherehe Kidata alipohamishwa TRA
Rais kwenye hotuba yake kadai kwamba taarifa za kuhamishiwa zilipofika TRA, wafanyakazi wengi walifurahia Sana na kuamua kufanya sherehe. Kwa maana nyingine Kidata alikuwa very strict kwenye kazi yake lakini bado Rais akamuondoa.

Kwenye muktadha huo huo Rais kadai Kidata hakuoendwa na TRA na pia hakuoendwa na Ikulu maana alikuwa mchapa kazi Sana na amenyooka. Sasa ikamwa najiuliza Kama una Kamishna mkuu wa TRA anayejituma na kusimamia taratibu, inakuwaje unamtoa hapo?. Unadai atakuwa mshauri wako, kwanini awe mshauri wako ilhali alikuwa anasimamia taratibu na anajua kazi?.

Swali langu ni kwamba Kama Kidata alikuwa amenyooka mpaka kuchukiwa na Ikulu pamoja na wengine , inakuwaje Rais kamtoa? Rais anahitaji mtu wa aina gani mwingine?. Kama Kidata hakuwa Mtendaji mzuri kwanini Rais adanganye?.

5. Jambo la mwisho, Rais kamuomba Kamishna Mkuu wa TRA kutoshirikiana na TRA kuiba
Kwenye hili Rais kakosea Sana kuliweka alivyoliweka. Maana kauli yake ni kwamba anathibitisha ya kwamba TRA Kuna wezi. Sasa Kama kiongozi wa nchi unajua Kuna wezi ndani ya TRA kwanini huchukui hatua?. Na kwanini umewaacha wezi qanaendelea kuiba na Wala huwa kamati mpaka unamshauri Kamishna mpya wa TRA asishirikiane na wezi waliopo ndani ya TRA.

Swali langu ni kwamba hawa wezi ndani ya TRA ni akina nani?

By Econonist.
Uyo Mwwnda si wanajua ni mwanasiasa mwenzao watabebana waendelee kutuoiga.
 
Mnamuonea tu mama wa watu ila pale TRA kuna mapapa mpaka magufuli aliwashindwa tena watu wazito kutoka serikalini na wafanyabiashara wakubwa na wanalindwa na mfumo wengine ni viongozi wastaafu wa CCM na serikali washaingia mpaka ikulu unadhani hyo vita mama anaiweza acheni kumuandama mambo sio rahisi kama unavyodhani.
Cheo cha RAIS kuna watu/kundi anaweza kiogopa
 
Bado unaendelea na ujinga wako? Kichwa chako kina kamasi au ubongo?
Mi mtu akitanguliza matusi tu basi namuona bogus kwani huwezi kutetea hoja mpaka utukane mkuu ukikosoa ukubali kukosolewa sio lazima kila mtu akubaliane na unavyotaka wewe.
 
Back
Top Bottom