Mambo matano aliyosema Rais Samia jana yaliyonisikitisha

Wakati Rais Samiah akiwaapisha Viongozi Jana , Kuna mambo matano aliyasema kwenye hotuba yake ambayo yalinisikitisha.

1. Jambo la kwanza Rais kadai mikopo inaifanya Tanzania inyayasike.

Nimehuzunika Rais anapokiri ya kwamba mikopo tunayokopa inatufanya tunyanyasike. Huyu ni udhaifu mkubwa wa Rais wa Nchi kukiri hadharani ya kwamba anapoenda kukopa huko nje huwa ananyanyasika. Kwa maana nyingine Rais amekiri kwamba hii mikopo Ina masharti magumu kabla ya kukopa na hata baada ya kukopa yanayoifanya nchi inyanyasike Kama alivyosema Rais.

Pia kwenye muktadha huo, Rais kadai tunakopa nje na kunyanyasika kwa sababu watu hawalipi Kodi. Kwa maana nyingine Rais alikuwa anajua Kodi hazilipwi ila akawa anafidia kwa kukopa mikopo huko kwa wanyanyasaji, Sasa unyanyasaji umekidhiri kaamua kudai Kodi ilipwe.

Swali langu kwa Rais kwanini unakubali nchi inyanyasike kwa mikopo mnayokopa?. Na hayo manyanyaso ni yepi tuyajue, isije kuwa Kuna masharti magumu yanayoingilia uhuru wa Taifa wa kiuchumi, kisiasa, kisheria na hata kitamaduni. Tuweke wazi kwenye hili.

2. Jambo la pili Rais kadai Pale Kariakoo kuna siasa nyingi.

Rais amedai ya kwamba alituma wajumbe wake kwa Siri kule kariakoo na kugundua ya kwamba Kuna wafanyabiashara wengi walikuwa wanafungua maduka au kuingia kwenye mgomo bila ya kujua sababu ya mgomo.

Nimeshangaa kwa kauli hii ya Rais. Maana mwaka Jana wafanyabiashara wa Kariakoo walifanya mgomo na mwisho wanafanya kikao na Waziri Mkuu pamoja na Waziri wa Fedha, na walieleza sababu nyingi Sana za kwanini wanagoma Tena live kwenye vyombo vya habari.

Inakuwaje Tena hao hao wafanyabiashara ndani ya muda mfupi wadai hawajui kwanini wanagoma? Ok, tufanye hawajui wanachogomea, ni kwanini Serikali ilisitisha baadhi ya kanuni kwa muda? Kama vile matumizi ya EFD na Faini ya kutotumia receipt kwa wafanya biashara wa Kariakoo?. Ina maana Rais pamoja na kupata taarifa ya wafanyabiashara kutojua wanagomea nini bado aliendelea na kusimamisha kanuni?.

Naona Kama Rais amejichanganya au anatuchanganya kwenye hili eneo, au yeye ndio analeta siasa kwa kudai wanaogoma hapo kariakoo hawajui sababu kwanini wanagoma na bado serikali ikasimamisha kanuni hapo kariakoo.

Swali langu ni kwamba je wale wafanyabiashara hawakuwa na sababu za kugoma? Na ni kwanini Serikali imeukubali kutii baadhi ya malalamiko ya watu ambao inajua hawajui wanachogomea?.

3. Jambo la tatu, Rais kaingiza mambo ya jinsia kwenye kazi za serikali.

Wakati anamtambulisha Waziri mpya wa viwanda na biashara, Ndugu Suleiman Jaffo, Rais kadai amaemua kumteua Jaffo maana pale kariakoo Kuna mikikimikiki mingi ambayo Dr Ashatu Kijaji asingeiweza kwa sababu ni mwanamke. Nikajiuliza kwanini alimteua kwenye nafasi hiyo Kama alijua kwa mikiki iliyopo kwa Waziri mwanamke hataiweza?.

Rais akaendela kudai ya kwamba ameamua kumteua Dr Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Mazingira na Muungano, ili ashughurikie mambo ya nishati ya gesi ya kupikia. Akadai amemteua yeye pamoja na Naibu Katibu Mkuu mawanamke maalim kwaajili ya kushughulikia gesi ya kupikia. Na akadai kwasababu wao ni wanawake amewateua makusudi na wakishindwa atashangaa wanashindwaje na wao ni wanawake.

Swali langu la msingi ni je Kuna Wizara zinazowafaa wanawake tu? na Kuna Wizara zinazowafaa wanaume tu?. Na Kama zipo ni Wizara zipi hizo?. Na kwanini Rais anazijua na bado amateua jinsia tofauti kwenye Wizara husika?

4. Jambo la nne Rais kadai kuwa Wafanyakazi wa TRA walifanya sherehe Kidata alipohamishwa TRA.

Rais kwenye hotuba yake kadai kwamba taarifa za kuhamishiwa zilipofika TRA, wafanyakazi wengi walifurahia Sana na kuamua kufanya sherehe. Kwa maana nyingine Kidata alikuwa very strict kwenye kazi yake lakini bado Rais akamuondoa.

Kwenye muktadha huo huo Rais kadai Kidata hakuoendwa na TRA na pia hakuoendwa na Ikulu maana alikuwa mchapa kazi Sana na amenyooka. Sasa ikamwa najiuliza Kama una Kamishna mkuu wa TRA anayejituma na kusimamia taratibu, inakuwaje unamtoa hapo?. Unadai atakuwa mshauri wako, kwanini awe mshauri wako ilhali alikuwa anasimamia taratibu na anajua kazi?.

Swali langu ni kwamba Kama Kidata alikuwa amenyooka mpaka kuchukiwa na Ikulu pamoja na wengine , inakuwaje Rais kamtoa? Rais anahitaji mtu wa aina gani mwingine?. Kama Kidata hakuwa Mtendaji mzuri kwanini Rais adanganye?.

5. Jambo la mwisho, Rais kamuomba Kamishna Mkuu wa TRA kutoshirikiana na TRA kuiba.

Kwenye hili Rais kakosea Sana kuliweka alivyoliweka. Maana kauli yake ni kwamba anathibitisha ya kwamba TRA Kuna wezi. Sasa Kama kiongozi wa nchi unajua Kuna wezi ndani ya TRA kwanini huchukui hatua?. Na kwanini umewaacha wezi qanaendelea kuiba na Wala huwa kamati mpaka unamshauri Kamishna mpya wa TRA asishirikiane na wezi waliopo ndani ya TRA.

Swali langu ni kwamba hawa wezi ndani ya TRA ni akina nani?

By Econonist.
3. Unaijuwa mikiki ya kariakoo au unaisikia tu?
. Halafu wewe unawajuwa wasaidizi wa Rais kuliko Rais mwenyewe?
 
Hata mimi nimesikitika
 
Kama ulimsikiliza alisema jana kwamba kidata mpaka baadhi ya watumishi wa ikulu na viongozi wa serikali walikuwa hawampendi itafakari vizuri hyo kauli.
Kuna jambo Moja ambalo liliniaminisha JPM was right about this guy...Ule ulikuwa uonevu wa mchana Kwa mfanya biashara mmoja aliomfanyia
 
Tatizo letu Kwa sasa Tanzania ni Rais ni mkweli sana na anapenda kufanya good governance, wakati watanzania hawajazoea kusikia ukweli, wala hawajazoea kuwa good citizens...Tumepewa right president at a wrong time and to the wrong people
The right president should be one who takes action. Sio rais anakuwa anatoa mipasho kama vile yupo kwenye kikao cha familia yake.

Yani president una mandate yote hiyo unaufahamu ukweli na una admit in public kuufahamu uozo wote huo still you just keep on watching it unfold?

Ingekuwa ni the right president saa hii watu wangekuwa jela, mahakamani na walishafilisiwa mali za umma walizoiba.

So sir please, we have the wrong president. Samia does not fit the office. She ain't fit for the job.
 
Nikimkumbuka JPM na Leo Samiah Wana kitu fulani in common!!wanaongozwa kuongoza nchi!!

Yaani Kuna utashi mwingine unaamua wazungmzaje waharibu vipi wakurupukaje wateuaje hata waleje na wote wanaowangoza kuongoza wanawaingiza chaka Ili wapoteze upili was mihula yao!!!

Yaani ipo dhahiri kabisa kwamba wanaowaongoza kuongoza wanataka waharibu Ili wasipate muhula was pili wa uawamu zao!!

MAONI HURU KUTOKANA NA FIKRA HURU!!
 
Tatizo letu Kwa sasa Tanzania ni Rais ni mkweli sana na anapenda kufanya good governance, wakati watanzania hawajazoea kusikia ukweli, wala hawajazoea kuwa good citizens...Tumepewa right president at a wrong time and to the wrong people
Uko sawa kichwani Mkuu? 😅😅
 
Back
Top Bottom