BIG Africa
Member
- Oct 15, 2022
- 85
- 118
Habari zenu wana JF,
Wiki moja iliyopita nilifanikiwa kusafiri kutoka mkoani Arusha hadi mkoani Tanga hasa katika wilaya ya Handeni vijijini. Kwakweli tembea uone. Nilipofika Handeni vijijini kuna kijiji kinaitwa (Kwamgwe) nilishangazwa na mambo makubwa mawili. Mambo gani hayo?
Jambo la kwanza ni umasikini wa kutupwa, yaani watu waishio Handeni vijijini hasa katika kijiji hicho ni fukara sana. Mfano nyumba nyingi ni za miti iliyokandikwa na udongo na juu zimeezekwa kwa nyasi. Asilimia 97 ya watu waishio katika kijiji hicho nilichokitaja wanaishi hivyo. Kiufupi Maisha yao ni mabaya sana.
Nimefanikiwa kutembea maeneo mengi nchini na kuoña umasikini ambao tumeuzoea, kama vile nyumba duni zilizojengwa na matofali ya udongo pamoja na kuezekwa na bati za kawaida lakini kule Handeni vijijini nyumba za miti ndio nyingi na nyingi zimeezekwa kwa nyasi.
Baadae nilijiuliza maswali mwenyewe kwamba kwamba familia za kule hazina kipato cha kuwasaidi kufyatua matofali ya tope au ndio wameamua tu kuishi hivyo?
Jambo la pili lililonishangaza Uziguani nadhani litakuwa ni sehemu ya mila za watu wa huko (Wazigua).J ambo Hilo ni kutembea peku peku tena umbali mrefu. Wazigua wa Handeni vijijini wanapenda sana kutembea peku peku kwa watu wa rika lote iwe vijana, watu wazima, au wazee.
Mfano wakati nafika huko lilikuwa ni kipindi cha mvua sasa nikawa naona tu watu wakikanyaga tu matope peku peku wakiwa wanaenda katika shughuli zao mbalimbali. Karibu na wewe kama una chochote cha kuchangia.