Mambo mawili yaliyonishangaza Tanga

Mambo mawili yaliyonishangaza Tanga

Habari zenu wana JF,

Wiki moja iliyopita nilifanikiwa kusafiri kutoka mkoani Arusha hadi mkoani Tanga hasa katika wilaya ya Handeni vijijini. Kwakweli tembea uone. Nilipofika Handeni vijijini kuna kijiji kinaitwa (Kwamgwe) nilishangazwa na mambo makubwa mawili. Mambo gani hayo?

Jambo la kwanza ni umasikini wa kutupwa, yaani watu waishio Handeni vijijini hasa katika kijiji hicho ni fukara sana. Mfano nyumba nyingi ni za miti iliyokandikwa na udongo na juu zimeezekwa kwa nyasi. Asilimia 97 ya watu waishio katika kijiji hicho nilichokitaja wanaishi hivyo. Kiufupi Maisha yao ni mabaya sana.

Nimefanikiwa kutembea maeneo mengi nchini na kuoña umasikini ambao tumeuzoea, kama vile nyumba duni zilizojengwa na matofali ya udongo pamoja na kuezekwa na bati za kawaida lakini kule Handeni vijijini nyumba za miti ndio nyingi na nyingi zimeezekwa kwa nyasi.

Baadae nilijiuliza maswali mwenyewe kwamba kwamba familia za kule hazina kipato cha kuwasaidi kufyatua matofali ya tope au ndio wameamua tu kuishi hivyo?

Jambo la pili lililonishangaza Uziguani nadhani litakuwa ni sehemu ya mila za watu wa huko (Wazigua).J ambo Hilo ni kutembea peku peku tena umbali mrefu. Wazigua wa Handeni vijijini wanapenda sana kutembea peku peku kwa watu wa rika lote iwe vijana, watu wazima, au wazee.

Mfano wakati nafika huko lilikuwa ni kipindi cha mvua sasa nikawa naona tu watu wakikanyaga tu matope peku peku wakiwa wanaenda katika shughuli zao mbalimbali. Karibu na wewe kama una chochote cha kuchangia.
Watu wa uswaz wanakauli wanasema maisha yetu kivyetu vyetu, sema iyo lifestyle iko kwny idadi kubwa vijijini atleast kwa kigoma vijijini kuna matumiz ya tofali za kuchoma na mabati kwa sana
 
Nikiwa mdogo watu wa makabila mengine wakija wilayani kwetu wanashangaa jinsi wilaya yetu ilivyo masikini! Aise baada ya kutembea mikoa karibu 12 ya tanzania. Tanzania ni moja aise, ukiacha maeneo ilipo halmashauri ndani ndani ni shida...hata wale waliotucheka nikaona sisi ni afadhali....
 
Jimbo linaloongozwa na CCM na Juma Aweso Waziri wa Maji.

Handeni wananchi wote ni CCM ili ujue na ujifunze madhara ya CCM kujikita mahali
Mkuu Aweso ni mbunge wa Pangani, lkn kote ndo hivyo hivyo tu hakuna tofauti kubwa. Umasikini bado ni janga kubwa sana kwa taifa
 
Habari zenu wana JF,

Wiki moja iliyopita nilifanikiwa kusafiri kutoka mkoani Arusha hadi mkoani Tanga hasa katika wilaya ya Handeni vijijini. Kwakweli tembea uone. Nilipofika Handeni vijijini kuna kijiji kinaitwa (Kwamgwe) nilishangazwa na mambo makubwa mawili. Mambo gani hayo?

Jambo la kwanza ni umasikini wa kutupwa, yaani watu waishio Handeni vijijini hasa katika kijiji hicho ni fukara sana. Mfano nyumba nyingi ni za miti iliyokandikwa na udongo na juu zimeezekwa kwa nyasi. Asilimia 97 ya watu waishio katika kijiji hicho nilichokitaja wanaishi hivyo. Kiufupi Maisha yao ni mabaya sana.

Nimefanikiwa kutembea maeneo mengi nchini na kuoña umasikini ambao tumeuzoea, kama vile nyumba duni zilizojengwa na matofali ya udongo pamoja na kuezekwa na bati za kawaida lakini kule Handeni vijijini nyumba za miti ndio nyingi na nyingi zimeezekwa kwa nyasi.

Baadae nilijiuliza maswali mwenyewe kwamba kwamba familia za kule hazina kipato cha kuwasaidi kufyatua matofali ya tope au ndio wameamua tu kuishi hivyo?

Jambo la pili lililonishangaza Uziguani nadhani litakuwa ni sehemu ya mila za watu wa huko (Wazigua).J ambo Hilo ni kutembea peku peku tena umbali mrefu. Wazigua wa Handeni vijijini wanapenda sana kutembea peku peku kwa watu wa rika lote iwe vijana, watu wazima, au wazee.

Mfano wakati nafika huko lilikuwa ni kipindi cha mvua sasa nikawa naona tu watu wakikanyaga tu matope peku peku wakiwa wanaenda katika shughuli zao mbalimbali. Karibu na wewe kama una chochote cha kuchangia.
Hii nchi umasikini ni mkubwa Sana tembea uone!!
 
Jimbo linaloongozwa na CCM na Juma Aweso Waziri wa Maji.

Handeni wananchi wote ni CCM ili ujue na ujifunze madhara ya CCM kujikita mahali
Nakusahihisha, Waziri Aweso ni mbunge wa Pangani.
Hata hivyo Tanga yote ni fukara sababu za uvivu na kutowakubali wageni kirahisi. Laiti wangeruhusu wageni kutoka mikoa iliyochangamka pengine maendeleo yangekwenda huko.
 
Huko Tanga ni mbali mkuu, juzi nilkua naangalia ITV kipindi cha ripoti maalumu nililia mkuu. Katikati ya jiji la Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi na imejengwa Ikulu kuna watu ni maskini wa kutupwa maana tukisema uwazike utakua umewapandisha hadhi. Hapo Dodoma kuna soko la Msalato, wakazi wa jiji wanaenda kuoteza mabaki ya mifupa ya nyama kwa ajiri ya mlo.!!!!
Kwa kina mpwayungu ambaye husinda akiwatukana walimu kama kwamba yeye ni tajiri
 
Nakazia
 
Kwa kina mpwayungu ambaye husinda akiwatukana walimu kama kwamba yeye ni tajiri
Yule Mpwayungu Village ni mwalimu wa diploma na kuna storry yake alienda Lindi kufundisha, pia alishawahi kuomba ushauri hapa jukwaani kama anaweza kutumia matokeo yake ya diploma ya ualimu kusoma sheria UD!!

Huyu Dogo kwao panaitwa Kidachi ni mgogo pure. Sasa nahisi aliajiriwa akiwa na matumaini makubwa ya kumake life!! Baada ya kwenda field akakutana na umasikini uliotukuka ndo akaanza kuutukana ualimu [emoji1787][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji1787]
 
Huko Tanga ni mbali mkuu, juzi nilkua naangalia ITV kipindi cha ripoti maalumu nililia mkuu. Katikati ya jiji la Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi na imejengwa Ikulu kuna watu ni maskini wa kutupwa maana tukisema uwazike utakua umewapandisha hadhi. Hapo Dodoma kuna soko la Msalato, wakazi wa jiji wanaenda kuoteza mabaki ya mifupa ya nyama kwa ajiri ya mlo.!!!!
Umenikumbusha kipindi nasoma seminary hapo Dodoma asee kuna vijiji fulani Mpamaa, na kingine kiko ndani ndani hivi nimesahau jina. Yani tulienda huko ilikuwa ni kama tumerudi kwenye middle stone age.

Watu wanaishi kama hunters and gatherers mpaka wanakula vyura yani pakame hamna hata tone la maji. Wakipata maji wanajitengenezea choya tu wanalewa na kufanya ngono ili kusahau shida zao kwa muda.
 
Naomba niongezee na kijiji kinaitwa Burukeri kipo katika kata ya magugu wilaya ya Babati, jamani jamani..tembeeni muone. No umeme no maji, hao watoto wanatembea umbali mkubwa sana kwenda shuleni. Watu wamevaa kofia za chama tu. Siasa hizi zinatuchelewesha sana. Ila sasa kuna wazawa ambao hawaambiliki. Hata muwaambie nini hawana huo muda wa kuwasikiliza.
 
Sehemu kubwa ya Tanzania vijijini ni maskini sana.....unaweza fika sehemu hapohapo kimoyomoyo na ukaanza kufanya toba na kuhisi unafanya anasa na udhalimu mkubwa sana katika dunia kwa kutazama maisha ya watu wengine

Utaleta toba kwa kujigundua pia wewe ni mchoyo wa fadhila, mbinfsi na mchache sana wa kushukuru kwa mola wako kwa neema alizokupa

ila ndio maisha ya walio wengi katika watu

Kama taifa tuna safari ndefu sana! Huoni hata daslam yenyewe 70% ni uswazi tu

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kuna dogo wa huko tulikuwa nae hapa Dar es salaam alikuwa anasomea ualimu
Baada ya kumaliza akapata kazi shule private Moshi nilipotezana nae kama miaka miwili nikaja kuonana nae ndiyo akanielezea kwamba alikuwa moshi sehemu fulani ni kijiji jirani na kijiji nnachotoka mimi
Basi tukaongea mambo mengi sana kuhusu kule
Basi anasema moshi unaweza kukuta msela tu ambaye ukimuangalia ni kama haelewekieleweki lakini ana kwake pazuri tu analima mpunga ana mashamba au anafuga mbuzi mafuta ni mtu ana hela na maisha mazuri tu
Lakini kwao unaweza kuta mzee anayeheshimika kijijini na maarufu kabisa lakini hapo anapolala sasa utachoka yani hakuendani kabisa na wameridhika wenyewe

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
SELIKALI imeshindwa kuwapa WATANZANIA Elimu Bora ya kuwawezesha Kujinasua na Dimbwi la UMASIKINI na ujinga.

NCHI INA VIONGOZI WA HOVYO SANA.
 
Back
Top Bottom