"CCM kujikita mahali" Yaani ulivyo isema ni kama li dude fulani [emoji23][emoji23][emoji23]Jimbo linaloongozwa na CCM na Juma Aweso Waziri wa Maji.
Handeni wananchi wote ni CCM ili ujue na ujifunze madhara ya CCM kujikita mahali
Habari zenu wana JF,
Wiki moja iliyopita nilifanikiwa kusafiri kutoka mkoani Arusha hadi mkoani Tanga hasa katika wilaya ya Handeni vijijini. Kwakweli tembea uone. Nilipofika Handeni vijijini kuna kijiji kinaitwa (Kwamgwe) nilishangazwa na mambo makubwa mawili. Mambo gani hayo?
Jambo la kwanza ni umasikini wa kutupwa, yaani watu waishio Handeni vijijini hasa katika kijiji hicho ni fukara sana. Mfano nyumba nyingi ni za miti iliyokandikwa na udongo na juu zimeezekwa kwa nyasi. Asilimia 97 ya watu waishio katika kijiji hicho nilichokitaja wanaishi hivyo. Kiufupi Maisha yao ni mabaya sana.
Nimefanikiwa kutembea maeneo mengi nchini na kuoña umasikini ambao tumeuzoea, kama vile nyumba duni zilizojengwa na matofali ya udongo pamoja na kuezekwa na bati za kawaida lakini kule Handeni vijijini nyumba za miti ndio nyingi na nyingi zimeezekwa kwa nyasi.
Baadae nilijiuliza maswali mwenyewe kwamba kwamba familia za kule hazina kipato cha kuwasaidi kufyatua matofali ya tope au ndio wameamua tu kuishi hivyo?
Jambo la pili lililonishangaza Uziguani nadhani litakuwa ni sehemu ya mila za watu wa huko (Wazigua).J ambo Hilo ni kutembea peku peku tena umbali mrefu. Wazigua wa Handeni vijijini wanapenda sana kutembea peku peku kwa watu wa rika lote iwe vijana, watu wazima, au wazee.
Mfano wakati nafika huko lilikuwa ni kipindi cha mvua sasa nikawa naona tu watu wakikanyaga tu matope peku peku wakiwa wanaenda katika shughuli zao mbalimbali. Karibu na wewe kama una chochote cha kuchangia.
Juliasi alishasema tuna maadui watatu: UJINGA, MARADHI, na UMASKINI. Bado wapo!
Kwamba kuna watu ukiwawekea utari hapa na umasikini pale wanachagua UMASIKINI???Kuishi maisha ya kifukara wakati mwingine ni kutaka mwenyewe.
Inamaana hawajui umuhimu wa viatu, raha ya kuwa na nyumba nzuri nk? Hakuna serikali itakayokuchukulia fimbo uvae vizuri kama hautaki
Hiyo wilaya watu ni masikin sana aisee shida pia wana iman za kishirikina sana.Habari zenu wana JF,
Wiki moja iliyopita nilifanikiwa kusafiri kutoka mkoani Arusha hadi mkoani Tanga hasa katika wilaya ya Handeni vijijini. Kwakweli tembea uone. Nilipofika Handeni vijijini kuna kijiji kinaitwa (Kwamgwe) nilishangazwa na mambo makubwa mawili. Mambo gani hayo?
Jambo la kwanza ni umasikini wa kutupwa, yaani watu waishio Handeni vijijini hasa katika kijiji hicho ni fukara sana. Mfano nyumba nyingi ni za miti iliyokandikwa na udongo na juu zimeezekwa kwa nyasi. Asilimia 97 ya watu waishio katika kijiji hicho nilichokitaja wanaishi hivyo. Kiufupi Maisha yao ni mabaya sana.
Nimefanikiwa kutembea maeneo mengi nchini na kuoña umasikini ambao tumeuzoea, kama vile nyumba duni zilizojengwa na matofali ya udongo pamoja na kuezekwa na bati za kawaida lakini kule Handeni vijijini nyumba za miti ndio nyingi na nyingi zimeezekwa kwa nyasi.
Baadae nilijiuliza maswali mwenyewe kwamba kwamba familia za kule hazina kipato cha kuwasaidi kufyatua matofali ya tope au ndio wameamua tu kuishi hivyo?
Jambo la pili lililonishangaza Uziguani nadhani litakuwa ni sehemu ya mila za watu wa huko (Wazigua).J ambo Hilo ni kutembea peku peku tena umbali mrefu. Wazigua wa Handeni vijijini wanapenda sana kutembea peku peku kwa watu wa rika lote iwe vijana, watu wazima, au wazee.
Mfano wakati nafika huko lilikuwa ni kipindi cha mvua sasa nikawa naona tu watu wakikanyaga tu matope peku peku wakiwa wanaenda katika shughuli zao mbalimbali. Karibu na wewe kama una chochote cha kuchangia.
Inasikitisha sana kwakweliHuko Tanga ni mbali mkuu, juzi nilkua naangalia ITV kipindi cha ripoti maalumu nililia mkuu. Katikati ya jiji la Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi na imejengwa Ikulu kuna watu ni maskini wa kutupwa maana tukisema uwazike utakua umewapandisha hadhi. Hapo Dodoma kuna soko la Msalato, wakazi wa jiji wanaenda kuoteza mabaki ya mifupa ya nyama kwa ajiri ya mlo.!!!!
NakaziaNjoo na huku kisarawe vijijini ujionee,wilaya ipo karibu na daresalam lakini ni masikini ya kutupwa.
Siku zote penepo uchawi na ndumba sana maendeleo ni kuyasikia kwenye bomba.🤔
Watu wa Tanga waambie mapenzi na kupika.Habari zenu wana JF,
Wiki moja iliyopita nilifanikiwa kusafiri kutoka mkoani Arusha hadi mkoani Tanga hasa katika wilaya ya Handeni vijijini. Kwakweli tembea uone. Nilipofika Handeni vijijini kuna kijiji kinaitwa (Kwamgwe) nilishangazwa na mambo makubwa mawili. Mambo gani hayo?
Jambo la kwanza ni umasikini wa kutupwa, yaani watu waishio Handeni vijijini hasa katika kijiji hicho ni fukara sana. Mfano nyumba nyingi ni za miti iliyokandikwa na udongo na juu zimeezekwa kwa nyasi. Asilimia 97 ya watu waishio katika kijiji hicho nilichokitaja wanaishi hivyo. Kiufupi Maisha yao ni mabaya sana.
Nimefanikiwa kutembea maeneo mengi nchini na kuoña umasikini ambao tumeuzoea, kama vile nyumba duni zilizojengwa na matofali ya udongo pamoja na kuezekwa na bati za kawaida lakini kule Handeni vijijini nyumba za miti ndio nyingi na nyingi zimeezekwa kwa nyasi.
Baadae nilijiuliza maswali mwenyewe kwamba kwamba familia za kule hazina kipato cha kuwasaidi kufyatua matofali ya tope au ndio wameamua tu kuishi hivyo?
Jambo la pili lililonishangaza Uziguani nadhani litakuwa ni sehemu ya mila za watu wa huko (Wazigua).J ambo Hilo ni kutembea peku peku tena umbali mrefu. Wazigua wa Handeni vijijini wanapenda sana kutembea peku peku kwa watu wa rika lote iwe vijana, watu wazima, au wazee.
Mfano wakati nafika huko lilikuwa ni kipindi cha mvua sasa nikawa naona tu watu wakikanyaga tu matope peku peku wakiwa wanaenda katika shughuli zao mbalimbali. Karibu na wewe kama una chochote cha kuchangia.
Kaongezeka adui wa nne sasa UFISADI...Juliasi alishasema tuna maadui watatu: UJINGA, MARADHI, na UMASKINI. Bado wapo!
Huyo ni Pangani.Jimbo linaloongozwa na CCM na Juma Aweso Waziri wa Maji.
Handeni wananchi wote ni CCM ili ujue na ujifunze madhara ya CCM kujikita mahali
Zama hizi ni marafiki wakubwa wa ccm.Juliasi alishasema tuna maadui watatu: UJINGA, MARADHI, na UMASKINI. Bado wapo!
Kwamgwe mna computer/simu janja na internet?Ulifata nini kwamgwe? Uliingilia michungwani? Vipi ulipita Ngojoro, Kambini je?
Sasa ngoja nikufungue.
kile kijiji ndio kilikua cha kibiashara enzi hizoo.Kilikua na utajiri mkubwa uliotokana na kiwanda cha kuchakata mkonge tunakiita Korona. Kipo mbele kidogo kuna kota za kambi.
Palizaa matajiri wakubwa tu wa Tanga mfano Sefu Mwarabu aliyekua anamiliki mabasi ya Zafanana.
Pia kulikua na utajiri wa kikoloni aka Rupia watu washatoka sana pale.
Kule mkundi ulifika? Kuna kisima cha kijerumani kina maajabu, wwakati wa mvua (masika) maji hupungua lakini wakati wa ukame (kiangazi) maji hujaa na kumwagika.
Siku nyingine ukija kwamgwe aka Bondo niambie nikutembeze nikuonyeshe maeneo ya historia.
Ogopa Sana eneo ambalo CCM inanguvu
Aweso yupo Pangani, Handeni ni Hamis Mwinjuma