Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
Inawezekana kuna watu unawaona wa ajabu sana, unaona kama ungepewa uhusika wao basi ungefanikiwa ndani ya dakika moja 😊 Inawezekana ikawa kweli wapo kwenye nafasi wasizojua kuzitumia vyema au ikawa sio kama uonavyo ukiwa sio muhusika.
Kuna watu wakikusimulia utaona kama vile wanakutisha hivi, yawezekana ikawa kweli wanakutisha au wakawa wanakupa ukweli ambao kwako unaona haiwezekani kwa sababu bado hujawa muhusika.
Mambo sio magumu ila pia sio rahisi lakini majibu sahihi utayapata siku ukiwa muhusika lakini kwa tahadhari tu ni kuwa sio wahusika wote ni wavivu au hawajui kutumia nafasi zao vizuri bali kuna mengi ambayo ukiwa nje ya mchezo huyaoni na ukitaka ufurahie mchezo jiandaye kutokata tamaa kirahisi kwani mchezo huwa hautaki jamii ya wakata tamaa kirahisi.
Ukianza kulipwa mshahara ndio utajua hautoshi ila ukiwa nje ya mfumo utaona watu wana mishahara mikubwa ila hawajui kuitumia.
Ukimaliza shule ukawa mtaani ndio utajifunza kuwaheshimu waliopo mtaani kwa miaka mitano bila kulia lia njaa.
Usiwe mtu wa kuhukumu sana ukiwa nje ya mchezo bali ukiona ni kama hawatumii vizuri nafasi zao wewe tumia kama funzo ili siku ukiwa muhusika basi utumie vizuri nafasi yako.
Mwanasayansi Saul kalivubha.
Fikia Ndoto Zako.