EPISODE 15: Sometimes, in the workplace, it's better to be lucky than talented
Hii experience sikupanga kushea hapa lakini niliwiwa baada kuona coment ya mkuu
mzabzab akimjibu
Leak “Ndio una ambiwa better to be born lucky than gifted”. Nikapromise nitashea hii experience kwenye situation ambayo naweza kusema ilifasadifu hii phrase.
I totally agree that in certain situations or work environments, having luck (good fortune or favorable circumstances) can be more advantageous than possessing talent or skill. It highlights the idea that unpredictable events or chance occurrences can sometimes play a significant role in one's success at work. It doesn't diminish the value of talent, but it emphasizes the role of luck in certain contexts.
Ipo hivi nakumbuka baada ya kama miezi miwili pale kwenye shirika la wazungu wakati nikiwa ndio najitahidi kuwaimpress pale ili nimalize probation period yangu salama, ikataokea tunatakiwa watu watu wanne including dereva, tusafiri kwenda Dodoma kulikuwa na meeting na watu wa wizara ya afya. Ile meeting ilikuwa ni kwaajili ya kuutambulisha ule mradi wetu kwa viongozi wa wizara, lakini mimi nilitakiwa nitoe presentation ya namna gani stakeholders wa mradi watakuwa engaged kwenye mradi. Ilikuwa ni very crucial presentation na ofisi ilinitegemea mimi nikasimamie show. Na mimi namshukuru Mungu nilijiandaa vya kutosha.
Uzuri ni kwamba katika kuorganize ile meeting ya kule Dodoma mimi ndio nilipewa hilo jukumu nadhani kwa sababu ya historia yangu ya kuwahi kufanya kazi na wizara mbalimbali lakini pia nakumbuka I was just volunteered for this to increase my visibility pale ofisini. A piece of advice, be very smart unapokuwa kimbelembele. Focus on those professional issues that will make people see your importance in the office, not engaging in inappropriate matters kama unoko unoko kwa staff wenzio etc. You won't succeed at all, and your end won't be good. Kiufupi imi niliamua kuwa kimbelembele kwenye kusimamia show kuanzia kuinitiate communication na watu wa wizara, kuplan the meeting agenda na kufacilitate the meeting tukiwa kule Idodomya pamoja na kuandaa bajeti na kilakitu. Nikawa ndio contact person kwa pale ofisini kwa ajili ya hiyo meeting.
Basi nikafanya maandalizi yote yanayohusiana na safarai na kuorganize that particular meeting. Nakumbuka tuliondoka siku ya Jumapili asubuhi ili Jumatatu tufanye hiyo meeting then Jumanne tugeuze zetu Dar. Mkuu wa msafara kutoka pale ofisini aliku ni Country Representative (CD) mwenyewe, mimi, mdada mwingine na dereva. That was my first work trip with that organization. Safari ilikuwa nzuri tuu na wote tulifikia hotel moja kwa ajili ya malazi an makazi kwa hizo siku mbili. Nakumbuka tuliingia Dodoma kama saa kumi na moja hivi jioni. Baada ya kila mmoja kupata chumba watu wakawa wamejipumzisha vyumbani kwao. Mimi kwa kuwa nilikuwa sijala mchana kutwa nikaamua kwenye kutafuta msosi ile saa kumi na moja. Nikapata msosi wangu pale pale hotelini then nikaingi room kupumzika. Wakati nasubiri msosi pale nikacheki na contact person wa wizara kumwambia kwamba tumeshawasiri akasema sawa atanicheki ili walau tuonane jioni ile ile tuangalie final touches ili tuwe na letu moja na kwa vile tulikuwa tunaongea tu kwenye simu akasema ni bora sisi wawili tukafahamiana jioni ile. Mimi nikaona ni point haina ubaya. Nikamwelekeza hotel tuliyofikia, akaniambia atanishtua mida mida.
Sasa kama timu tulikubalina kwamba watu wapumzike then sambili kamili tukutane restaurant pale pale ofsini kwa ajili ya dinner. Kama nilivyowadokeza kwenye hii stori kwa pale ofisini swala kujali muda lilikuwa ni kipaumbele kikubwa sana, hii iliwaingia wafanyakazi wote hata kama ishu haitahusisha maboss, swala la time management and punctuality lilipewa msisitizo mkubwa sana, otherwise unadharura toa taarifa mapema. Basi kweli sambili ilipofika wote tukawa tupo mezani ila mimi sikugonga msosi maana nilikuwa nishakula na nilikuwa pale tu kuwapa kampani. Wakati tunakula pale jamaa wa wizara akanipigia kuniambia ameshafika pale hotel basi nikamwelekeza tulipo nay eye akajumuika nasi pale. Tukawa tunapiga naye story mbili tatu then nay eye akaagiziwa msosi plae. Badae tukaplan meeting ya kesho lakini akasema atatujulisha kupitia mimi ni mda gani exactly kesho tutaonana mana katibu wa wizara naye alikuwa interested kushiriki lakini hakujua ratiba yake exactly sangapi atakuwa na nafasi.
Basi tukaachana pale kila mmoja akaenda kupumzika au kuendelea na ratiba zake. Nikiwa nipo tuu room jamaa yule wa wizara akanicheki kwa simu kunitaarifu kwamba katibu mkuu amesema kikao kianze saa tano asubuhi siku inayofata badala ya saa tatu tuliypnga sisi. Kufanya kazi na watu wa serikali ni kawaida sana kubadilishwa badilishwa ratiba kwa maana kusogeza muda au siku nyuma au kupelekwa mbele, so inabidi muwe flexible kwa yote. Kwakuwa haikuwa usiku sana nikawatext niliokuja nao kwamba kikao ni saa tano so nikashauri badala ya kuanza kuondoka pale hotelini saa mbili asubuhi basi tuondoke saa nne maana ilikuwa ni mwendo wa kama dk 20 tu toka pale Rafiki Hotel mpaka kule UDOM ambako majengo ya wizara yalikuwepo kwa kipindi kile, kule mtumba walikuwa bado hawajahamia. Basi tukakubaliana hivyo.
Sasa mimi nikawa sina usingizi kabisa. Kwenye saa tano hivi usiku nikasema ngoja nitoke niende maeneo ya makole pale kuna kajigrossary flani nilikuwa nimekazoea nikazuge zuge mpaka saa sita then nirudi kulala. Pale grossary ilikuwa ni kama uwanja wa nyumbani nikiwaga Dodoma, mpaka leo hii nikienda mara nyingi huwa nabuy time pale kwa sababu wadau wengu wa pale nawafahamu na hivyo inaniondolea sana ugeni. Huwa sipendi kubuy time kwenye pub kubwa sijui bambalaga au pestana, hayo yanakuwa sio maeneo yangu kabisa labda kampani niliyonayo iwe ina interest sana na sehemu kama hizo. Naamini naepukwa na vitu vingi usiniulize kanini.
Basi n ikatoka pale nikakamata boda huyoo mpaka grossary. Sasa muda huo kulikuwa na kitu tunafatilia kwenye tv ilikuwa ni live sikumbuki vizuri kama ni hizi ndondi za kibongo au ni mambo haya mamiss, sikumbuki vizuri. Lakini ilikuwa wadau wachache tunafatilia huku tunapiga stori mdogo mdogo. Nikajisemea mwenyewe wacha niangalia mpaka mwisho then nikalale maana nilikuwa sina ulazima wa kuamka mapema hiyo kesho kwani meeting ni saa tano.
Basi wakati tunaendelea pale kupiga piga stori na huku tunafatilia kile kipindi mara paap wazee wa kazi haoo, polisi wakatuweka chini ya ulinzi. Wakadai kwamba tumezidisha muda wa kukaa pale grosary maana inatakiwa pafungwe saa sita kamili. Nakumbuka ilikuwa ni kama saa sita kama na dk 10 hivi nakumbuka. Bahati nzuri mmiliki wa ile grosari nae alikuwepo kwahiyo akatuambia wateja wake tusiwe na wasiwasi yeye atadili nao. Basi akawa anawaplease pale waende nje wakamalizane wale njagu wakawa wanakataa. Wakaweka msimamo wote tulikuwepo pale inatakiwa tubebwe. Sisi wengine tukajiongeza tukajua labda mmiliki ametoa dau dogo. Basi tukajichanga changa pale tukapata ela kuongezea, tukawaambia wale polisi tunaongeza pesa kidogo ili watuachie wakagoma.
Nakumbuka yule mmiliki alisema mbona mnatukomalia sisi tuu mbona wengine mnawaacha? Kwenye ule mtaa kuna vigosary vingine kama vitatu vipo karibu karibu. Wale polisi wakamwambia angalia kama wenzio wanauza muda huu. Jamaa kuangalia akashangaa kweli inakuwaje leo wamefunga mapema na sio kawaida yao na mara nyingi kuna mmoja nasikia ndio huwa anakesha karibia kila siku ila siku hiyo nayeye alifunga mapema. Basi kuna jamaa mmoja kati ya wale wateja akasema hii ni michezo itakuwa na lengo maalum cha muhimu akawaambia wale polisi kama wanaajenda na mwenye grosari basi waturuhusu wengine tuondoke. Hoja kubwa ilikuwa kesho ni siku ya kazi hivyo waturuhusu kwa gharama yoyote. Wale polisi wakakaza.
Kama masihara vile hao tukaingizwa kwenye karandinga waliokua nayo. Hahakukuwa na watuhumiwa wengine kwenye gari lao ni sisi tuu. Yaani pale tulisombwa wote kuanzia wahudumu walikuwa wawili, mwnye grosary, wateja, jamaa mchoma chips na dogo mmoja alikuwa mwanafunzi wa sekondari tena yeye alikupita tu njia kununua maji akajumlishwa. Tukajua mchezo tutaucheza kwenye gari lakini wakagoma. Kuna jamaa akaongeza dau awape laki mbili ili wamwachie yeye pekeyake, lakini jamaa wakagoma. Tukaambiazana mule kwenye gari kwamba jamaa wanataka labda mpaka tufike kituoni ndio watakapochukua mzigo maana wataamini kwamba kitioni lazima tutatoa kila tulichonacho.
Basi tukafika mpaka kituoni. Mimi nikiwa sielewi elewi maana ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana na msala wa namna hiyo. Basi kufika kituoni tukawekwa chini pale kaunta. Then tukaambiwa tuvue sijui mikanda, viatu,saa, cheni kama unayo n.k. binafsi nikaona hii ishu sasa inaenda kuwa serious. Basi tukaanza kuoanda madau pale ili watuachie kama tulivoamini. Jamaa wakagoma kata kata. Hapo tukaamini kwamba kweli ile ishu ilikuwa ni mpango maalum. Kama utani vile tukakabidhi vitu vyetu kaunta baada ya kuandikisha. Sasa mimi nilikuwa na waleti, simu kubwa na kitochi. Kwenye ile waleti nikatoa pesa niliyokuwa nayo nikabakiza eflu tano, then kile kisimu cha tochi nilikificha pamoja ela ili niingie nazo ndani. Nilifanya hivyo incase nikifanikiwa kupita navyo kile kitochi kinisaidie kufanya mawasiliano na wadau wa Dodoma kunirescue na ile pesa niliificha kusudi maana nilisiwahi kusikia kwamba mara nyingi zile pesa huzipati zote pindi uiachiwa kama sio wanazikomba zote basi watakuachia nauli tuu.
Basi nikafanikiwa kupita pale na kuingizwa mahabusu nikiwa na simu na pesa zangu. Haikuwa ela nyingi ni kama elfu 40 hivi ambazo waligoma kuzichukua ili waniachie. Mule sro kwa kweli kulikuwa na hali mbaya. Experience niliyoipata mle ndani sitakuja kuisahau nikazikumbuka stori za vijiweni kuhusu mahabusu kwa kweli pale ni kama ilikuwa worse zaidi. Hali ya mule ndani kwangu haikuwa ishi sana, ishu ilikuwa itakuwaje endapo ntaka mule ndani mpaka kesho na vipi wasiponiachia itakuwa kuhusu maswala yangu ya kazi.
Kumbuka ile ilikuwa ni trip yangu ya kikazi tena kwenye ofisi mpya mbay zaidi watu nilikuwa sijawazoea na sijui vizuri Tabia, mbaya zaidi CD mwenyewe alikuwepo. Nitaeleweka vipi mimi? Itawajengea picha gani kuhusu mimi? Nahapo kumbuka wakati wa kuajiriwa walikuwa wanafatilia mpaka criminal recors ya mtu halafu leo hii hata probation sijamaliza nakutwa na misala ya police case. Asee nilivurugwa sana. Akili ikawa inapanga na kupangua. Walau ningekuwa nikasema sijui niwajulishe niliokuja nao kwamba kwamba nipo police au lah. Kila nikipanga kuwajulisha staff na boss wangu akili inakataa. nikasema hii itaniletea matatizo na hivyo wanaweza wakaconlude mambo ambayo hata sikuwa nayo ila ndio hivyo nimeshikwa na ngozi.
Kichwa iliwaka moto sana. Wale jamaa wengine nilikouwa nao nao mmoja alikuwa amepagawa nae kama mimi tuu inaonekana nay eye alikuwa na ishu muhimu sana hiyo jumatatu maana mpaka wakati huo ilishakuwa ni saa saba inaenda saa nane. Basi mimi nikamkumbuka jamaa yangu mmoja ambae ni mkazi wa pale Dodoma nikawaza nimpigie au nimtumie meseji. Yule jamaa aliyepagawa kama mimi akawa anawaita polisi wa zamu pale kaunta anaomba simu yake aongee walau dk 1 kuna ishu muhimu sana inatakiwa atoe maagizo. Wale polisi wakawa wanamjibu apambane na hali yake na kama akiendelea kuwapigia kelele watamwamisha pale wakaweke sehemu mbaya zaidi. Basi mimi kusikia vile kwa kuwa nilbahatika kuiingia na simu nikamwambia mimi nina simu hapo kama ni ishu muhimu nitampa wacha nimcheki jamaa yangu kwanza. Akaniambia poa yeye kuna jamaa yake ni mkubwa mkubwa wizara ya mambo ya ndani pale hivyo akimpata tu jambo letu linakuwa limeisha. Kusikia vile nikampa yeye simu kwanza aongee na jamaa yake.
Basi jamaa akaichukua ile simu akaniambia tusogee upande wa kule kwenye madebe ya kinyesi na mikojo ambako kunakuwa hakuna watu kabisa labda wanaoenda kujisaidia, humu humo kwenye vyemba vya mahabusu lakini na hakuna kitu kinachotenganisha ni ku auwazi tuu, wee acha tuu. Basi ile jamaa anaajiandaa tu kupiga simu mara tunasikia jamaa anapiga kelele “nyaparaa, wameingia na simuu”. Nyapara kusikia vile alikuja pale tulipo kama mbogo akawa anafoka vibaya mno kwa nini tumeingia na simu mule ndani. Nayeye akasogea mlangoni pale akawaita maafande wa zamu kuwaeleza kwamba kunawatu wameingia na simu mle ndani. Jamaa alikuwa mnokjo kweli kweli.
Sasa pale nikanote kitu kimoja, hawa manyapara wanasikilizwa sana na maafande kwani ndio wasemaji wakuu wa mahabusu mnapokuwa mle ndani. Na vigezo vya kupewa unyapara kwanza uwe umeishi mule mahabusu mda mrefu yaani unakuwa kama mtoto wa nyumbani vile na pili uwe na tabia za unoko. Zamani nilikuwa nafikiri ili uwe nyapara unatakiwa uwe mbabe ila pale nikaja kujua kale kanyanpara hakakuwa na ubabe wowote ispokuwa kalikuwa ndio kainfoma ka polisi na pale selo yeye ilikuwa ni kama nyumbani kwao yaani akikaa uraiani wiki hamalizi anapiga tukio ilimradi arudishwe pale. Alinishangaza sana. Nakumbuka wakati sisi tunampiga biti hata mahabusu wengine waliokuwemo mle ndani ambao waliishi naye kama siku mbili au wikinao walitaka hadi kumdunda ila wakawa wanaogopa maana yule nyapara alikuwa akikuchoma kwa wale polisi utakachokipata hutakisahahu.
Basi wal polisi wakaitana kama wanne hivi watatu wakiwa na bunduki wakafyungua selo ili kutuchukua sisi tuliokuwa tunajaribu kupiga simu. Nakumbuka kabusa maneno yao mmoja akasema ni kidume gani hicho chenye kib** (tusi) kinachompa kiburi cha kuingia na simu humu ndani? yule nyapara akatuonesha sisi huku akitamba mtaona mtakachoenda kukutana nacho nyie mak** (tusi), si mnajifanya wajanja? Nikajua leo kazi. Simu yangu alikuwa bado anayo yule jamaa. Wakataka watoke nae peke yake. Ila mimi nkasema wanichukue na mimi maana ile simu ni yangu. Sijui nini kilinifanya niseme ukweli maana yule jamaa alikuwa radhi ule msala aubebe yey kama yeye. Wale polisi wakasema sawa twende na wewe. Basi tukatoka pale huku wale polisi wakisema sikumbuki wanatupeleka sijui chemba gani, inaoneka huko ni kubaya zaidi, yaani huko ni mpaka useme.
Basi tukatolewa pale sasa tukawa tunazungushwa kwa uwani ili tuelekee huko tunakopelekwa. Sasa kabla hamjapelekwa huko utaratibu inaonekana pale kunaruhusa au maelezo inabidi wayatolee maelezo kwa mkubwa wao au sijui ni mtu wa kitengo gani, maana mimi sijua sana kuhusu ranks na mambo kama hayo ya idara ya polisi. Sasa wakati tumekalishwa chini kwenye ile ofisi ya kule uwani jamaa wanatolea maelezo kwa nini tuhamishwe akaingia mdada mmama-mdada mmoja inaonekana ndio alikuwa anaondoka au ndio anaingia zamu. Inaonekana kuna kitu alikuja kukifata mara moja kwenye ile ofisi.
Sasa wakati yule mdada anatoka tukagongana macho. Akshituka sana ile kama ananifananisha akawa ananiangalia sana. Mimi nipomuona nikamgundua mara moja. Nikamwambia ni mimi usinifananishe ni rafiki yake na D, nikamtaja mdogo wake. Yule dada akaniuliza wewe sio Taidume wewe? Unafanya nini hapa? Siku hizi uumekuwa jambazi? Akaniouliza maswali mfululizo pale. Nikamwambia ni ndie mimi na wala sio jambazi. Basi ikabidi awaulize wale polis waliotuleta pale nina kosa gani. Wale polisi walikuwa hawajui hata nimeletwa pale kwa kosa gani isipokuwa wametulea pale ofsini kwa sababu mimi nilikuwa nimeingia na simu. Basi akawaambia wale polisi wasinipekele kwanza huko wanakotana kunipeleka wamwachie yeye anihoji kwanza.
Kikweli nilipata ahueni ya nguvu sana. Yule mdada alikuwa ni kama sista angu kwa sababu mdogo wake D ni mmoja wa best frend zangu. Hivyo kupitia huyo mdogo nilikuwa nafahamika na ndugu zake wengine. Nakumbuka hata kwenye harusi yake huyo mdada wakati mimi na mdogo wake tupo advance nilikuwa ni mmoja niliovaa sare ya kuwasindikiza maharusi ukumbini. Kwahiyo alikuwa ni sista anga kiufupi. Mpaka mda ule nikajua walau sasa naweza kuchomoka kwenye ule msala lakini nikasema niwe na subira.
Basi yule dada akanichukua maelezo pale mbele ya wale polisi wengine. Ndio tukamweleza ilivokuwa tangu tulipokuwa kule grosari. Ndio kuna polisi mmoja akasema ile ishu ilikuwa ni maelekezo ya wakubwani maswala ya ushindani wa kibishara. Nilivoelewa mimi inaonekana mwenye ile grosari tuliokuwepo alikuwa anauza sana kuliko wengine mpka ikawalazimu wengine kukesha ili walau waokoteze wateja jamaa akiwa amefunga. Maana jamaa yetu mida yake ya kufunga ilikuwa haizidi saa saba hata kama ni wikend. Mpaka yeye afunge wengine ndio wauze, sasa sijajua alikuwa anatumia maneuver gani ila mimi nilipapenda sababu mazingira yake, wahudumu wenye heshima na jamaa alikuwa mcheshi sana. Kwahiyo mpango uliokuwepo ni kukamata wateja wake kila inapofika saa sita mpaka wateja wamkimbie jamaa, kwa kigezo kwamba muda wa kufunga biashara umefika. Ndio mana siku ile ilipofika saa sita na dk 5 wazee hao wakatimba kutukamata na mimi nikiwa ni victim.
Basi yule dada akaniambia kwa ishu ile ilivyo kuachiwa inaweza ikachukua hata siku mbili maana mpango ulikuwa tufunguliwe kesi ya uzururaji. Nilipomweleza lengo lililonileta Dodoma na situation ambayo niko nayo pale akawa very concerned. Chakushangaza na yule jamaa niliyekuwa naye nayeye alikuwa ni mfanyakazi wa wizara ya afya na ndio alikuwa anategemewa kutuhost kwenye kile kikao.maana wakati mimi namuelezeza yule sistaang akaniulize wewe unatoka shrike flani? Nikamwambia ndio na kumuuliza mbona kuniuliza? Ndio akaniambia nay eye anahitajika sana kwenye hicho kikao cha saa tano na sisi na yeye ndio anatakiwa kuendesha kile kikao. What a coincidence? Basi yule sista akashughulikia lile swala kwa mbinu anazozjiua yeye mwenyewe tukaachiwa pale kama kwenye saa tisa na nusu alfajiri.
Mimi mpaka nafika hotelini ilikuwa ni kama saa kumi alfajiri. Basi nikaoga pale na nikaweka alam iniamshe saa mbili kamili asubuhi. Nikapiga mbonji mpaka alam iliniponiamsha nikajiandaa fasta saa nne kamili nikaungana na timu tukaenda tukaenda kwenye meeting. Kufika kule meeting ikawa inaendelea kama kawaida huku mimi na jamaa yangu mara nyingi tukiangaliana na kuishia kuchekea tumboni hahahaa. Tkamaliza meeting pale kama saa nane hivi. Wakati naondoka yule jamaa yangu akanipa contact akaniambia nijitahidi badae tuonane. Jioni nikamtafuta tukaonana mahali ikawa ndio mwanzo wa kuwa marafiki mpaka hivi leo nina namba yake na tunawasiliana mara moja moja. Kama yupo humu atajijua na atanipigia hahahaa.
That day I was lucky indeed kukutana na yule dada angu. maana nilikuwa naharibu hiyo kazi. See you next time for more personal experiences on my career path.