Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

Nice mkuu, good experience to share, umetufungua macho wengi mno na timeishi kwa niaba yako maisha tuliokuwa tunapenda kuishi hususani Mimi binafsi nilikua na kiu sana ya kufanya kazi kwenye NGO za kimataifa nipate experience na kufill maisha yanaendaje ila kwa hii experience yako nimeishi hayo kwa uchache na hata duku duku la kukosa kazi za miradi ya mashirika limeisha, salute sana mkuu. All the best in your new upcoming endeavors. Peace🙏
Pamoja mkuu. Peace be upon you too
 
Mbona kama imekua fupi sana... Anyway Asante sana mkuu kwa kutenga muda wako na kushare na sisi madini haya. Wish you all the best on your endeavors.
Hhaa hahaa ndio imeshia hapo, ofcourse kunamengi ningeweza kushea lakini mostly ingekuwa ni kama marudio.
 
Kama kuna mtu ana nafasi amor huyu jamaa.....
Ni mtu smart sana ukweli ni kuwa jamaa anaomba kazi ,lakin anatumia mbinu za cuba, ilà atakaye mpa hatojuta
Umepigilia msumari mle mle mkuu.
 
Refarii kwenye CV weka majina matatu ya Uongo na Email tengeneza tu zako,Mfano Mbuzi Mawe ndio mmoja wa refarii wako,hivyo kwenye email tengeneza mbuzimawe@yahoo.com,wanaotaka kukuajiri wakituma Reference kwenye Email kuuliza taarifa zako unazipokea wewe mwenyewe na kuzijaza kisha unawarudishia simple tu,maana unaweza ukaweka Boss wako wa zamani kisha akakusagia kunguni badala ya kukusaidia
 
UTANGULIZI
Wakuu habari.

Naandika hii story yangu ikiwa ni mwaka sasa nipo mtaani nikiendelea na harakati za kusaka ajira mpya toka mkataba wangu wa ajira ulipoisha mnamo Desemba 2022. Nimeamua kushea uzoefu wangu kwa mtindo wa Masimulizi (katika episodes) kwa kuamini pengine inaweza kuwa na mafunzo kwa waajiri, waajiriwa au wanaotegemewa kuajiriwa. Naomba moderatoes wa JF wauache huu uzi wangu hapa hapa kwenye Jukwa la Ajira kwani muktadha wa simulizi hii maswala ya kubadilishana uzoefu katika swala la ajira na sio mambo ya entertainment. Twende kazi.

Episode 1: Sikuogopa kujidhalilisha ili kupata reliable connection

Mwaka 2011 nilipomaliza my 1st degree kama ilivo kwa wanachuo wengine, nilikuwa na expectation kubwa sana ya kupata ajira nzuri ndani ya muda mfupi. Hii ilijengwa na kiburi kwamba mwaka mmoja before sijamaliza niliwaaproach ndugu na wadau kwenye network yangu kwamba mwakani namaliza. Kila mmoja alinipromise kunisaidia kupata job au kuniconnect na waajiri mbali mbali. Swala likawa ni kwamba wewe maliza tu chuo then utuambie ili tukafanyie mipango.

Kimbebe kilikuja baada ya kumaliza. Nilitulia kwanza mwezi mmoja then nikaanza kucheki walionipromise job kwamba I am available. Asee nilipigwa dana dana za kutisha na mwishowe wengine wakawa hata hawapokei simu zangu. Nikiwaibukia nyumbani au maeneo yao ya kazi wanaishia kunipa nauli ya kurudia na kuniambia ajira ngumu cha muhimu wewe endelea kumuomba Mungu. It was very disappointing situation at that time na nikafikia hatua ya kuanza kuwachukia bila sababu as if wao ndio wanaonisababishia ugumu wa kuajiriwa, hahahaaa.

Basi nikaanza kuumiza kichwa how to go about finding the job. Nikaaply sana kazi kupitia job adverts za mtandaoni lakini mimi mwenyewe nikaona as a fresh graduate I didn’t have the skills and required experiences. Nikaanza kuona hata elimu yenyewe may be course niliyosoma haina maana bora lile boom ningelitumia kwa kuanzisha hata kimradi cha kuchoma popcorn mtaani.

Hali ilikuwa mbaya to most of the graduates maana kila nikiwacheki wana nao wanalalamika kama mimi tuu isipokuwa wachache sana wenye connection tena za familia zao za kuzaliwa. Hapo nikakumbuka wakati naenda kuanza form 5 way back bro wangu aliwahi kuniambia “dogo huko shule nenda kawe na marafiki wa aina mbili, either wenye akili sana darasani au wale wanaotoka kwenye familia bora”. Nilikuja kumwelewa kipindi hiki ni nini bro alichomaanisha. Kwamba wale wenye akili sana darasani watakuinfluence kufauru na wale wanaotoka maisha bora ni future asset katika connection za ajira.

Sasa mimi kutoka na usela wangu mavi wa teenager sikuwa na hata mmoja kati ya hao. Roho ilikuja kuniuma zaidi nilipogundua nilipokuwa advance niligombana na jamaa mmoja ambaye kwao walikuwa wapo poa sana wa kutokea mkoa wa Iringa, nilipooulizia habari zake nikasikia kwa kipindi kile natafuta ajira alikuwa ni msimamizi wa kampuni ya usafirishaji mizigo(malori) na walikuwa na ofisi zao bandarini (clearing and forwarding). Laiti yule jamaa ningemfanya best friend ukute ingekuwa rahisi kwa yeye kunipa mchongo. Anyway, les forget about him.

Nakumbuka siku moja nikiendelea kusaga visigino katika harakati zangu za kutembeza bahasha, kwenye foleni nikamwona lecturer wangu mmoja hivi, tumuite Dr KJ (PhD ya kihaya hiyo) kwenye shangingi lake akiendeshwa na dereva wake kama kawaida. Huyu lecturer nilimkumbuka kwa sababu alikuwa na sifa sana kwenye vipindi vyake na alikuwa anafundisha somo la project Management.

Yaani huyu Muhaya alikuwa anatumia nusu ya muda wake kwenye lecture kujisifia. Ataanza kuwananga maprof kwamba japo yeye ana PhD ila hakuna prof anaemzidi akili na pesa chuo kizima, kwanza yeye anaendeshwa na mshahara anamlipa dereva wake ni sawa na wa tutorial assistant wa pale chuo. Alikuwa mdhalilishaji sana kwa wanafunzi hususani watoto wa kike au wanaofeli somo lake.

Ila watu walichompendea jamaa alikuwa sometimes anagawa sana maokoto akiwakuta wanafunzi njiani ila ndio mjue mtadhalilishwa. Jamaa alikuwa anatembea na dola au Euro akidai pesa za madafu ni nzito, hatukujua anapata wapi zile dola dola. Nakumbuka kuna semester alimlipia ada jamaa mmoja alikuwa anasoma kwa shida sana alikuwa hana boom. Alimlipia ada ya semester ya mwisho ila yule jamaa cha moto alikiona maana Dr KJ kwenye kila kipindi alichofundisha kwenye madarasa yake lazima amtolee mfano yule jamaa mpaka mlipiwa ada akawa famous chuo hahahaaa.

Basi bhana nilipomwona kwenye foleni Dr KJ vitu vingi vingi vikapita kama mshale kwenye mawazo yangu. Kwamba huyu jamaa anaweza akawa asset lakini anaweza akanidhalilisha vibaya sana na nitamuanzaje yupo kwenye gari. Je atanikumbuka maana wanafunzi tulikuwa wengi sana. Lakini nikifikiria pale geto nadaiwa kodi mwenye nyumba keshanivumilia kama two months (niliamua kukomaa mjini sikutaka kwenda mkoani).

Wakati naendelea kuwaza foleni ikaanza kutembea, asee sijui ni nini kilinikuta nikajikuta naikimbilia ile gari na kwenda kuisimamia kwa mbele nikiizuia isiende huku nikimwonyeshea ishara dereva apaki pembeni. Dereva alipoona anaweka foleni akamuuliza bosi wake wafanyeje hahaaa maana nacheka kama ni mazuri. Basi Dr KJ kwa wasiwasi akamwambia aweke pembeni.

Basi nikasogea upande wa Dr KJ akawa hataki kushusha kioo, akanielekeza niende upande upande wa dereva. Nikajua tuu boss anaogopa labda nitamdhuru so he decided to sacrifice his driver- hahahaa. Basi nikaenda upande wa dereva aliposhusha kioo nikamsalimia.

Mimi: shikamoo Dr KJ

Yeye: Unanifahamu?

Mimi: Ndio wewe ni mwalimu wangu wa somo flani nimemaliza mwaka jana.

Yeye: (Bado akiwa na wasiwasi) Nitaamini vipi na kwanini unanisimamisha kama jambazi?

Mimi: (Bila kujiuma uma) Naomba unisamehe sana Dr, ni kuvurugwa na hapa nimeona kama bahati
kukuona. Dr mimi nipo katika harakati za kutafuta kazi, nimekusimamisha ili nikuachie CV yangu maana naamini wewe network yako ni kubwa pengine unaweza ukaniconnect na wadau wako.

Yeye: (Akacheka sana huku akiniita niende upande wake). Kwa hiyo unatafuta kazi gani?

Mimi: Kwa sasa nahitaji sehemu yoyote ya kujishikiza ili nipate uzoefu, lakini uzuri wewe ni mwalimu wangu wa PM so unaweza ukaona ni wapi zile theory wapi naweza kuziapply.

Akaniangalia sana kisha akaniuliza unajua nini kuhusu project management na principles for effective project management? Nikamshushia madude kwa style ambayo nadhani ilimkamata kisawa sawa. nIkamsisitizia kwamba mimi sijawahi kushikwa kwenye somo lake. Baada ya kumjibu pale akaniambia. Mbona unaonekana una njaa sana? Shika hii nenda kale mimi nina mambo mengi sana na hapa unanichelewesha tuu. Sikupokea kwanza ile pesa ila nikamwambia Sir please just take my CV may you can see how you can help.

Akaniuliza, sasa CV yako umeandika nini wakati hujawahi kufanya kazi popote? Halafu sina muda wa kutembea na makaratazi kwa gari yangu. Akawa anafunga kioo, asee nikaking’anga’ania. Akaniambia unataka nini sasa pesa nimekupa umekataa. Nikamwambia, kama huwezi kutembea na makaratasi basi naomba email address yako ili nikutumie. Akaniangaliaa, kisha akatoa business card akanipa. Mimi nikaicheki nikaona ile biz card sio yake ni ya mdada. Nikamwambia mbona sio yako. Akaniambia “vizuri sana upo makini, mpigie huyo dada simu kesho muda kama huu”. Hiyo ilikuwa ni kama saa tisa hivi. Kisha akanipa ile pesa, akasepa zake.

Mwendelezo=>

Sehemu ya 2

Sehemu ya 3
Imefika sehemu ya ngapi vile? Mm ndio naanza leo
 
Tuendelee tulipoishia

Basi nikaachana na Dr KJ pale, nikahesabu ile pesa ilikuwa ni elfu 40. Kwanza njaa yote ilikata si unajua tena ukipata hela ambayo hujaitegemea. Nikarudi zangu home. Ile hela nikaclear some bills muhimu za pale geto ikiwemo umeme, maji na kwa mangi nilikokuwa nakopa kopa unga na mchele. Then ikabaki kama 10 hivi jioni nikasogea kijiwe cha kunywa banana nikavimba pale kwa banana zangu tatu, banana moja ilikuwa inauzwa sh 350, kwa msiojua banana ni kinywaji kimoja local kinatengenezwa kwa ndizi, ni kali mno kwa estimation ya ulevi banana moja ni kama safari moja na nusu hahahaaa.

Basi siku ya pili ilipofika saa tisa sharp nikaipiga ile namba. Kama nilivyotarajia akapokea mdada. Mazungumzo yetu yalikuwa:

Mimi: Habari, naitwa TAIDUME nimepewa namba yako hii na Dr KJ alinipa maelekezo nikupigie.
Yeye: Ok sawa nina taarifa zako. Sasa kesho saa 4 asubuhi njoo (akanitajia jengo na ofisi ilipo - Posta Dar)
kwa ajili ya interview.
Mimi: (Kwanza nikapigwa butwaa) Ok dada japo umenishtukiza ila nitakuja kwa wakati. Ila ninaomba
kama hutojali nitumie walau kipeperushi au website ya ofisi ili niweze kupata uelewa wa ofisi coz
ili kesho nikija niwe walau na abcd.

Yeye: Samahani kaka sikupewa hayo maelekezo na boss.
Mimi: Sawa nakuelewa, haina shida kuwa na amani tutaona hiyo kesho saa nne.

Basi nikakata simu pale. Siku hiyo ilikuwa Jumatano wakati napiga simu so nipaswa kesho yake Alhamis niibukie kule ofsini. Sasa nikawa na mawazo mengi sana. Nimeambiwa niende kwenye interview lakini sijui naenda kufanya interview ya position gani mbaya zaidi sijui hiyo ofisi yenyewe inadili na nini? Nikarudia kuisoma ile biz card upya nikaona jina la ofisi anayofanyia yule dada maana cheo chake alikuwa ni personal secretary. Ila lile jina la kampuni au tuite ofisi halikuweza kunipa mwanga wowote labda to predict what can be operational sector. Imagine nilikuwa kwenye wakati mgumu kiasi.

Nikaamua kuyaacha kama yalivyo hayo maswali yangu maana sikuweza kupata majibu. Nikamshukuru Mungu maana ilikuwa ndio mara ya kwanza kuitwa kwenye job interview japo hii ilikaa kimitego sana. Siku hiyo nililala mapema sana kwenye saa tatu tu nikawa nishalala, before nilibrash viatu vyangu na kunyoosha nguo kabisa.

Basi asubuhi nikajidamka saa kumi na moja nikajiandaa pale, mpaka kufikia 12 nishatoka geto nipo kutafuta usafiri. Kwenye saa mbili na nusu nikawa nishafika kwenye jengo lenye ile ofisi. Basi nikatafuta kijisehemu kwa nje wanapouza chai nikapiga tea mdogo mdogo huku nikisubiri subiri muda uende kusubiri saa tatu na nusu ndio niibuke. Ilipofika muda nikamcall yule dada akanielekeza nipande lift mpaka ofisi ilipo. Kweli akanipokea pale na kunikaribisha waiting room. Baada ya muda akanilitea kahawa na maji then akaniambia boss atachelewa kidogo ila ameagiza nipewe vipeperushi nisome wakati namsubiri.

Nikawa nasoma soma pale mpaka ilipofika mida ya lunch boss bado hafika. Nikaletewa lunch pale, ile ofisi wana utaratibu wa wafanyakazi kupewa lunch siku za kazi. Nikagonga vizuri tuu pamoja na wafanyakazi wengine, walikuwa watatu baadae nikaja kujua ni secretary wa boss, mhasibu na mtu wa usafi. Ilipofika saa tisa yule secretary wa boss akaniambia boss hawezi kuja kwa siku ile kwahiyo waliniruhusu niondoke ila watanitaarifu lini nitarudi kwa inyerview. Basi nikashukuru pale nikasepa zangu nikiamini kwa kuwa ilikuwa ni Alhamisi basi kwa vyovyote interview itakuwa next week. So, nikaomba baadhi ya vipeperushi ambavyo sikuvisoma nikasepa zangu.

Ilipofika ijumaa muda wote nilihakikisha simu ipo na chaji maana nilitegemea kupata simu kutoka kwa yule secretary ya kunialika tena kwenye interview. Mpaka Jumatatu jioni ya wiki iliyofata sikupigiwa simu yoyote kutoka kwa yule dada. Dah! Nikawa nawaza sijui nimpigie kumuuliza lakini nikaona haitakuwa busara kwa muda ule labda nisubiri walau ikipita ndio nimpigie. Basi nikaamua kupotezea huku nikijipa hope watanipigia tuu.

Nakumbuka ilikuwa Jumanne saa 2 asubuhi nikiwa napanga ile buku niliyonayo naipangila vipi ili siku ipite mara yule secretary akanipigia simu na kuniambia kama naweza boss atakuwa ofisini saa tano na amepanga kukufanyia interview. Nikamwambia consider this Is done, saa tano sharp nitakuwa hapo. Basi akaniambia haina shida nitawakuta maana boss alikuwa ameshafika na ananisubiri. Mimi nimefika pale by saa nne na nusu nikazama ndani. Basi bosi akaambiwa pale baada ya muda akaniita ofisini kwake.

Kiroho kikawa kinanidunda nikawa nasali sala zote unazozijua wewe, wee acha tu kwenye ile situation niimwachia Mungu tu. Basi ile nachoma ndani kwa boss mara paap namwona Dr KJ yupo pale ndani busy na laptop yake. Kiukweli sikutegemea kabisa kama Dr KJ ndio boss wa ile ofisi, mimi mawazo yangu yalikuwa labda Dr ameniconnect na watu wake na nilipanga kama ningefanikiwa pale kupata job basi ningetafuta namba yake au kumfata hata kule chuo ili kumshukuru.

Basi bhana, nikamsalimia pale. Jamaa akaniitikia kama ndio tunaonana kwa mara ya kwanza. Akawa anaendelea kufanya fanya shughuli zake baada ya kama 10 minutes ndio akaniuliza email address yangu. Then akaniambia niende kwa secretary kuna laptop atanipa kuna email amenitumia niisome then nimjibu. Basi nikapewa laptop na kufungua email. Nikakuta amenifowadia email ilikuwa kutoka kwa wadau wake wamemtumia document.

Sasa nafkiri kwa sababu Dr KJ alikuwa busy hakuweza kuisoma ile doc maana ilikuwa na page nying sana. So alichonitaka ni kuisoma ile doc niielewe then nimwandikie summary isiyozidi page mbili then nimtumie. Wakati mimi naendelea na kuisoma ile doc yeye akawa akawa anaondoka akamwagiza secretary wake kwamba nikimaliza nimtumie then niondoke. Kwa hiyo hakuna interview tena kwa mara nyingine. Basi baada ya muda mimi nikamaliza ile kazi nakumbuka ilikuwa kwenye saa na nane hivi. Basi ukaletwa msosi pale tukagonga then mimi nikaaga. Secretary akaniambia bosi akimwambia chochote atanijulisha. Nikatembea zangu huku nikiamini labda kesho nitajulishwa interview itakuwa lini.

Nikasubiri Jumatano mpaka Alhamisi kimya. Nakumbuka Ijumaa yake kwenye saa 3 asubuhi naona namba ya landline inanipigia, unajua sikuwa nimewahi kabisa kupigiwa na landline basi nikajua labda ni namba kutoka nje ya nchi, wakati huo nilikuwa nimejaribu jaribu kuapply scholarship za kusoma vyuo vya nje masters. Basi nikahisi labda mchongo umetiki hahahaa. Nikapokea huku mwenyewe nikijiandaa kubonga ung’eng’e mara naskia “Kaka TAIDUME mbona hujaja kazini siku mbili hizi, boss amekuja leo amekuulizia na amekuwa mkali sana”. Alikuwa ni yule secretary wa boss.

Kwanza nilishangaa sana na sikuelewa anamaanisha nini. Nikamuuliza anajua anaongea na nani maana mimi sijaaliwa popote. Akaniuliza wewe si ni TAIDUME last week ulikuja kwa ajili ya interview ofisini, kwani hamkuongea na boss? Maana leo ameingia ofsini cha kwanza amekuulizia nilipomwambia haujaja tangu tulipoahirisha interview amefoka sana kwa nini huji kazini. Nikaona sasa haya mashkolo mageni kwangu. Nikamuuliza kwahiyo ina maana kazi nimepata? Na je niende muda huo au boss kasemaje? Akanijibu boss amesema Jumatatu akukute job. Nikamuuliza muda wanaofungua ofsi pale akanijibu, basi tukakubaliana Jumatatu niende zangu ofsini.

Nikawaza sana ina maana ndio nimepata kazi au vipi na kwa nini boss anilaumu wakati mimi sikupewa taarifa yoyote ya interview wala ya kuendelea kwenda kule ofsini. Nikahisi labda nimeboronga ile kazi ilitakiwa niifanye kwa siku mbili. Kwa kuwa nilikuwa na laptop langu niliyokuwa natumia chuo nikafungua ili kuisoma tena vizuri ile kazi aliyonipa boss nikaona mbona ipo sawa tuu. Basi niakaona nisijichoshe bure majibu yote nitapata Jumatatu.

Jumatatu ilipofika nilikuwa wa kwanza kufika pale ofsini, baada ya muda kidogo alikuwa yule mtu wa usafi ni mmama mtu mzima kidogo basi akafungua ofisi pale na kuendelea na majukumu yake. Mimi nikasubiri pale mpaka wafanyakazi wengine walivyofika. Yule secretary wa boss akanitania kwa kuniambia Karibu boss TAIDUME, unaweza kuchagua ofisi hapo kati ya hizo mbili zilizo wazi. Nikamwabia natamani hizo ofisi ila ni mpaka nifaulu interview, ila akaniambia yaani wewe na boss mnanishangaza sana.

Wewe unasema hujui kama umepata kazi wakati boss kaniambia nikuandalie ofisi ili uendelee na kazi, au mnaniona mimi bibi yenu? Ikabidi nishangae tuu pale. Basi nikaoneshwa ofisi huku sijui nafasi yangu, majukumu yangu ya kazi wala stahiki zangu. Lakini nikasema yoote hayo nitayajua boss akija inaoneka hii ni ofisi ya one man show.

Nimekaa pale huku nikisoma soma docs mbalimbali za ofisi ili kujifamiliarize operations za ofisi. Kwenye saa 6 mchana Dr KJ akanipigia simu kwa kupitia simu ya secretary wake akaniambia amemtuma dereva wake anifate anipeleke alipo kwenye mkutano so nijiandae akanielekeza na doc za kubeba ambazo secretary atanipa, akakata simu. Nikabaki kushangaa tu pale. Mara dereva akaja pale so secretary akanipatia zile docs zinazohitajika tukaondoka.

Njiani nikawa najaribu kumdodosa dereva wa boss mambo general ya ofisi akawa ananipa abcs pale. Tulipofika ilikuwa ni kwenye ofisi za TAMWA, kulikuwa na wadau kutoka NGOs mbalimbali walikuwa wanaadhimisha kuanzisha mtandao unaitwa Jukwaa la Katiba Tanzania ambalo lengo lake lilikuwa kuunganisha Asasi za Kiraia (CSOs na NGOs) za Tanzania ili kudai katiba mpya Tanzania. (Kwa mnaokumbuka lile vuguvugu la katiba mpya Tanzania kipindi cha Kikwete mpaka kuundwa kwa lile bunge la katiba ambapo Mh Rais Samia alikuwa mwenyekiti mwenza, ndio nazungumzia wakati huo) My task was to take notes on the key issues that Dr KJ will need to include in his report.

Basi kikao kilienda vizuri na wakati wa kujitambulisha pale Dr KJ alinitambulisha kama Afisa Program (Program Officer) wa Shirika lake. Nikashtuka kidogo ala kumbe mimi ni program office, japo sikuonesha kwa watu. Na baada ya hapo kuna series ya vikao vya Jukwaa la Katiba nilishiriki ambapo niliweza kujenga network na kufahamiana na wadau wengi wa NGOs au CSOs. Nakumbuka kwenye kupata wawakilishi wa kuwakilisha NGOs na Asasi za kiraia katika bunge la katiba ndipo alipoibuka bwana Polepole.

Mchakato wa kumpata mwakilishi ulihusisha kupigiwa kura ambapo walihitajiki wawakilishi wasiozidi watano kama nakumbuka sawasawa. Huyu bwana Polepole hata mimi nilimkubali sana wakati anagombea uwakilishi maana jamaa alikuwa anajua kupangilia sana hoja zake na alionekana angekuja kuwachallenge vizuri sana wale ambao wangeenda agaist CSOs coalition’s interests.

Turudi kwenye mada yetu sasa. Basi ule mkutano uliisha jioni hivyo boss akaniambia tukutane kesho ofsini kama kawaida. Kesho yake nilifika ofisini kama kawaida na baada ya muda boss alifika. Tukaitwa wafanyakazi wote pamoja na dereva. Officially Dr KJ akanitangaza kwamba mimi ni mfanyakazi mpya wa lile shirika na nafasi yangu ilikuwa ni Program Officer Advocay nafasi ambayo iliniweka kuwa wa pili kimadaraka baada ya bosi kwa usimamizi wa office. Baadae nikapewa mkataba wangu pale ili kuupitia na kufahamishwa majukumu yangu, probation period, kasalali kenyewe na blahblah nyingi za kimkatabata.

Tukutane sehemu inayofata – Episode 3
Du! Huku ndio kunaitwa kupata job kimasikhara!
 
Yaani misoto inafunza sana yani Mama yako anafikia hatua anakupiga tafu ya kodi hakuna anayejua …watu wanakuona unatoka kwako Geto kumbe kibarua hakikufanyi ulipe kodi zaidi ya kula ..kumbe mlipa kodi ni mama yako na anakufichia siri hakuna ndugu anajua yaani!

Mkuu Nakuhakikishia ni swala la muda tuu! Mungu ni mwema sana hatomuacha Mama alie na kuumia milele….mara nyingi tukiwa katika hali hii tunakuwa hatuoni kama kuna pakutokea na hata mimi sikuwai ona kama kunapakutoke lakini nina hakika hata wewe utatoka tuu! Huyu Mungu ni wetu sote !
Halafu kuna watoto wa Jezebel wakishatoboa wanawasahau wazazi..
 
Uzi mzuri sana nijifunza mengi. Cha ziada tu mwandishi kingereza chake kirefu na rasmi sana kama lugha ya wanasheria. Anahitaji kutumia kingereza cha kawaida kama kilivyo kiswahili chake
 
Siku mkijua tunasoma wengi alafu mnaleta lugha za malkia acheni zarau
 
N
Matokeo yake tunapata viongozi incompetent. Kwa sababu asilimia kubwa ya watu wanapoenda kujishusha(of which ni unafiki kwani wakishasogea nao ni viburi tu) ni wale wenye uwezo mdogo sana kiakili.

Watu wengi wenye akili naturally ni arrogant, hawapendi kuburuzwa na kupelekwa pelekwa na wanajiamini kitu ambacho mara nyingi hutafsiriwa kama kiburi.

Mwisho wa siku nchi tumejaza viongozi na decision makers incompetent sana. Hadi mtu unajiuliza huyu alifikaje hapa. Kumbe katumia silaha ya kujishusha a.k.a unafiki!
Nail on the coffin.
 
EPISODE 2: Kwenye mazingira mapya ya kazi, JIONGEZE. Ugeni mwisho wiki ya kwanza

Here I am talking abouth the ability to adapt to new situations and learn quickly. Demonstrate a willingness to learn and take on new responsibilities kwa uharaka. Employers value employees who can quickly acquire new skills and knowledge to keep up with evolving job environment and requirements.

Bhasi bana nikaenda kwenye ofisi yangu niliyoichagua na kuanza kuupitia ule mkataba. Nakumbuka mchecheto mkubwa kwenye kuusoma ule mkataba ulikuwa kwenye salali kuliko hata vipengele vingine. Chaajabu kwenye mkataba ule hakukuwa na kipengele cha “remuneration” ambapo ndio utaona maswala ya salali yako na benefits mbalimbali kama vile bima ya afya, posho za likizo nk. Ila kulikuwa na kipengele cha majukumu tuu tu ya kazi na blabla nyinginezo.

Kichwa iliwaka sana moto nakumbuka. Nikajiuliza maswali mengi sana sasa hii inakuwaje, its my first job contract – yes, but how can it miss such a crucial contract segment!! Ahahaaa. Nikaskuti pale je nikamuulize boss au yule dada mhasibu? Maana yule dada Mhasibu alikuwa ana act pia as HR wa shirika. Nilichoamua kufanya kwa muda ule ni kutousaini ule mkataba, kwanza sikupewa time frame ya kuusoma na kuurudisha kwa boss ukiwa umesainiwa.

Japo sikuwa nimesettle kiakili ila niliamua niendelee kujisomea vipengele vingine vilivyoainisha majukumu yako as a Program Officer – Advocacy. Yaani hata hiyo the meaning and approaches to advocacy nilikuwa sijui, kaazi kwelikweli. Hapo nikagundua kwamba nilikuwa empty kabisa kwenye ile position kwa maana ya kukosa uzoefu na hata baadhi ya majukumu sikuelewa kabisa yanataka nifanye nini. I missed the technical know.

Kiufupi nilijifanyia a quick self assessment of my knowledge, skills and experience related to the job responsibility, nikajiona labda nina qualify kwa not more than 15%. Kwanza niliogopa, pili nikajicheka, tatu nikaona hata kile kipengele cha salali nikisema niulizie na nikiulizwa unataka ulipwe sh ngapi na shughuli ipi utakazofanya nitajibu nini? Anyway nikajipa moyo lazima kutakuwa na job orientation kutoka kwa mzoefu hususan Dr KJ mwenyewe ili nipate uelewa wa kazi.

Basi wakati nasubiri utaratibu mwingine, nikaenda kwa yule secretary nikamuomba anipe docs zinazohusiana na projects za pale ofisini hususani kama kuna reports zozote. Nikapewa pale madocs kibao nikaendelea kujisomea. Hii at least ilinipa mwanga zaidi wa nini kinachofanyika pale ofisini. Ilipofika muda wa mchana kabla ya lunch nikamsikia Dr KJ akimuaga (kwa sasa nitakuwa natumia neno boss) secretary wake kwamba anaondoka nyumbani hajisikii vizuri. Mimi hakuja kuniaga sikujali sana nikajua labda ni kutojisikia vizuri kwake. Nikaendelea kujisomea zile docs mpaka muda wa kufunga ofisi ulipofika. Nikaondoka. Hiyo ilikuwa ni first day officially employed in my entire life. Kwakweli Nilisali sala ndeeeefuu sana ya kumshukuru Mungu nilipofika magetoni kwangu.

Kwa ile wiki nzima boss hakuja kabisa ofsini. Nakumbuka siku ya tatu nikaomba namba yake kwa secretary nikampigia boss wangu kumjulia hali. Hakupokea zaidi ya mara tatu so nikamtext kumjulia hali lakini hakujibu. Ila yule secretary akimpigia simu anazipokea na boss alikuwa anampigia mara kwa mara yule Mhasibu kumpa maelekezo ya flani flani kwenye department yake. Nikaona sio kesi madam nimeshamtext tena kwa kujitambulisha basi atajuwa mwenyewe. Hakuja ofisini wiki nzima.

Sasa mimi zile docs za report na programs mbali mbali nilimaliza kuzipitia na kuna baadhi ya mambo nikawa siyaelewi na nikijaribu kumuuliza secretary au mhasibu hakuna wanalolijua. Uzuri pale ofisini kama zilivyo ofisi nyingi nyingine kulikuwa na strong internet you connect through wi-fi. Basi kwa zile mambo ambazo nilikuwa sizielewi nikajiongeza kuingia youtube ili kupata tips. Asee pale ndio nilijua kumbe youtube ukiitumia vizuri inaweza kuwa chuo kikuu ada yake ni bando lako tuu.

Kwa ile wiki ambayo boss hakuja ofsini nilikula shule ya kutosha youtube, na nilikuza uelewa wa majukumu yangu walau kwa 60%. Kwa kuwa kulikuwa na projector pale ofisini kuna wakati nikuwa naproject zile youtube lectures ili nisichoke kitu ambacho kiliwafanya hata wale madada wengine wa ofisini nao kujiunga na mm kufatilia, hususani yule secretary, maana yeye ukiacha kupokea wageni na kusoma emails zinazotumwa Info, majukumu yake mengi alikuwa nayo boss anapokuwa ofisini (Kumbuka yule alikuwa ni Personal Secretary wa boss, kuanzia sasa nitamwita PS)

Nakumbuka Ijumaa wakati tunajiandaa kuondoka ofisini boss alinipigia simu kunitaka niandae training manual kuhusiana na training flani ambayo inatakiwa akatrain watu weekend hiyo (kesho yake Jumamosi). Uzuri nilishapitia youtube maana moja ya majukumu yangu ilikuwa ni kutrain raia wa huko vijijini kuhusiana na maswala ya PETS na SAM – Kama huyajui hayo mambo zama you tube. Bai kwa reference za you tube na kureview mariport ya pale ofisini nikatengeza ile manual fasta tuu then kwenye saa 11 nikamtumia. Nikampigia simu kumueleza kwamba nishamtumia kazi, hakupokea ila akanitext tuu weekend njema. Basi nikafunga ofisi pale nikasepa maana walinipa copy ya funguo za ofisi.

Wiki ya pili ofisini ilianza Jumatatu kama kawaida. Bosi alifika ofisini mapema sana angalau nikajua may be anaweza kunielekeza maswala ya kazi na pengine kupata muda wa kudiscuss kuhusiana na salali maana ishu ilikuwa bado pending. Baada ya muda akaniita ofsini kwake, akaniambia nijiandae kwa safari kesho tunaenda Tanga (Handeni na Kilindi) kutrain watu maswala ya PETS na SAM. Hakuongelea chochote kuhusiana na ile kazi aliyonipa ila nikamuuliza tu natakiwa kuandaa nini kwenye hiyo safari?

Asee gafla tu boss alinichenjia kinoma noma akafoka kwa sauti mpka ofisi nzima ikawa inasikia. “Yaani officer mzima hujui majukumu yako kwenye safari, mbona unakuwa mzembe mzembe sana, unashindwa hata kutumia akili kidogo tuu kujiongeza? Hii ndio shida ya kusaidia watu wasiojielewa” aling’aka boss KJ. Kisha akaanza kukohoa mfululizo kikohozi kile kama cha TB sugu mpaka PS akaja kumpetipeti na kumtuliza. Nakweli boss akawa calm kisha akatuambia tuondoke ofsini kwake anataka kupumzika, ila mimi niandae safari.

Unajua nilipigwa butwaa ambalo sikuwahi kupigwa nalo kwenye maisha yangu yoote hapa duniani. Nikajiuliza pale nimekosea kipi hasa mpaka bosi kukasirika mpaka anakohoa kama anataka kukata utepe wa kifo? Uzuri nikamkumbuka yule dereva wake basi nikaenda parking kumtafuta (yule dereva huwa haingii ofsini labda akiitwa nilikuja kujua badae kwamba boss alimwambia yeye ofisi yake ni kwenye gari hivyo akae ofisini kwake. Na ole boss ashuke chini ili waondoke na asimkute atawashiwa moto balaa).

Unajua hawa madereva wa maboss wanakuwa wanajua mambo mengi sana ukiwatumia vizuri utafaidika sana. Basi nikamuuliza driver bosi huwa anafanyaje fanyaje mnapoendaga kutain watu vijijini? Kwa kweli alinisaidia sana kunipa hints na vingine akaniambia nikamuulize muhasibu hususani namna ya kuandaa bajeti. Wakati naondoka nirudi juu dereva akaniambia huku akijichekesha “bwana Taidume karibu kwenye ofisi yetu bwana hapa kazi zako itabidi uzijue kwa kufosi hakuna wa kukuelekeza” Na mimi nikajichekesha pale nikamshuru.

Kwa msaada wa yule dreva na muhasibu nikaweza kuandaa safari ile vizuri tu tuu kama vile kuandaa bajeti ya mafuta, malipo ya ukumbi, chakula, nauli za washiriki pamoja na posho zetu za safari. Kuhusiana na notes za kufundishia yule PS alinipa training manuals pale zenye kila kitu, nilichoshangaa tuu iweje boss last week aliniambia nimwandalie training manual wakati zilikuwepo. Badae nikaja kujua alikuwa ananipima tuu na uzuri nilitembelea karibu mule mule isipokuwa vitu vichache sana.

Kumbuka ile safari ilikuwa ni very short note binafsi hata sikujiandaa lkn kwa kuwa nilikuwa naishi mwenyewe kininja nilifurahia sana tuu na hivi Tanga nilikuwa siifahamu. Wakati nasubmitt budget kwa boss for his approaval akaniambia niongeze na bajeti ya PS wake, kwahiyo tulitakiwa kuondoka watu wanne yaani Boss, mimi, PS na dereva. Na pia akanipa orodha ya coordinators wa kule field niwasiliane nao ili kufatilia maandalizi.

Kesho yake tulianza safari ya Handeni tukafika mapema tu na moja kwa moja tukaenda kuonana na wenyeji wetu pamoja na kukagua maandalizi ya semina kama vile ukumbi, mtu wa chakula nk. Ila kwenye kutafuta lodge za kulala nikagundua PS na Boss wameshafanya booking hivyo tulivyowaacha lodge kwao mimi na dereva tuakatafuta logde nyingine. Sikutaka kuhoji sana na pia nikajiongeza. Jioni ile PS akanicheki twende kula so tukakutana nae sehemu ila boss hakuwepo. Nikamuuliza akasema boss hali yake sio nzuri na sio mtokaji tokaji sana wa usiku na ameshakula. Basi tukapata msosi pale na drinks mbili tatu then tukamrudisha kwake na sisi tukarudisha majeshi logde kwetu.

Asubuhi nilitakiwa kuwahi ukumbini boss alinipigia akaniambia angekuja badae kidogo. Kwahiyo nilihakikisha logistics zote zipo sawa pale watu wameshajiregister, stationaries zimegawiwa, projector iko connected n.k. Boss alipofika alianza moja kwa moja kuendesha ile training huku mimi nikichukue key notes kwa ajili ya report. Ile session ilikuwa ni ya siku tatu pale Handeni then tukamailizie Kilindi siku tatu zingine kisha tugeuze. Boss alikuwa ni trainer mzuri sana na mcheshi sana kwa washiriki kitu ambacho nilikipenda na alikuwa tofauti sana na yule anayefoka foka ofsini. Nilimfatilia kwa makini sana na kujifunza mengi kwake.

Kiukweli hali ya boss kiafya haikuwa nzuri nakumbuka siku ya mwisho ya ile training pale Handeni asubuhi aliniita kule lodge kwake akanipa zile notes akaniambia nipitie session ya siku hiyo kwani mimi ndio nitaanza kufundisha siku hiyo yeye atakuwa anaintervine atakapoona panafaa. Kidogo nilishtuka na kawoga kaliniingia lkn nikasema nitaogopa mpaka lini? Nikamwambia sawa, nikarudi lodge kujiandaa maana ilikuwa ni saa moja na session zinaanza saa tatu.

Muda wa semina ulipowadia nikaanza kuwatrain pale. Sitaisahau hii siku kwani nilitumia akili mingi sana ili kuendana na hiyo kazi. Ujue kuna vitu vingi sana vya kuzingatia ambavyo boss nilimwona anafanya. Mfano inatakiwa ubalance speed yako, uwe very interactive and allow members participation, toa mifano mingi sana iwezekanavo, fahamu tabia za trainees wako kwani wana upeo na behavior tofauti tofauti, kingine mimi nilikuwa very junior kwa umri halafu wengi wao pale walikuwa ni watu wazima hivyo ilitakiwa kuwa makini sana na lugha. Mpaka unafika muda wa lunch boss hakuintervene popote na wala na sikuweza kuisoma sura yake kama nafanya sawa au nimeenda OP.

Niliendelea na ile session mpaka mwisho kwa siku hiyo, boss aliniachia nimalize yeye alifanya ile session ya kufunga tuu na hivyo tukawa tumemaliza pale Handeni. Jioni kama kawaida mimi na PS tulijumuika kupata msosi na drinks. Yule dereva alikuwa hakai na sisi kabisa nikajua labda ni very introvert au misingi yake ya kazi haimruhusu, sikuweza kupata majibu maana hiyo ilikuwa ni wiki ya pili tuu ofsini. Basi kwenye kupiga piga story na PS pale akaniambia;

PS: Unajua Taidume unaweza ukaenda mwenyewe Kilindi?

Mimi: Kivipi mbona sikuelewi

PS: Ndio hivyo, maana jamaa amekuelewa sana yaani leo amekusifia sana tulipokuwa lodge kwamba umepiga mzigo fresh.

Mimi: Aisee! Sasa mbona itakuwa mtihani, huko Kilindi mimi simjui yeyote, basi at least tungeenda wote walau siku moja halafu nyie mgeuze.

PS: Mh sidhani maana kwanza boss ameshukuru wewe upo kwa kuwa hali yake kiafya sio nzuri so amesema atakuacha wewe umalizie. Lakini kaka Taidume mbona umepiga mzigo fresh tuu boss anaumwa wacha tu arudi Dar.

Mimi: Dah poa ila sio mbaya kwahiyo mnaondoka kesho?

PS: Nafikiri hivyo, ila atakupigia.

Basi tukaachana pale kama kwenye saa 4 hivi usiku. Na kweli ile nafika tu chumbani boss akanipigia huku akikohoa mfulizo kwamba kesho asubuhi saa moja niende pale kwake kuna maagizo. Nikajifanya sijui lolote nikamwitikia tu sawa. Asubuhi nikaenda kwake pale akaniita chumbani nikakuta wameshafungasha mabegi. Basi akanipa maagizo pale kwamba wao wanageuza Dar hivyo mimi nitamalizia Kilindi.

Sikubisha wala kuhoji chochote maana PS alishanitonya jana yake. Basi nikaachiwa mpunga pale wa kufacilitate session za kule Kilindi. Dereva alikuwa hajui kama watageuza kurudi Dar na mimi sikutaka kumwambia, hivyo ikabidi tutoke pale wote ili wapitie mzigo wa dereva wasepe. Hiyo ilikuwa Jumamosi, Session ya Kilindi ilikuwa inaanza Jumatatu ya next week. Hivyo niliamua mchana nianze safari ya kwenda Kilindi ili nipafahamu na Jumapili niweze kufanya maandalizi.

Jumapili nilifanya maandalizi muhimu ikiwemo kuonana na coodinators wa kule hivyo kila kitu kilienda sawa. Jumatatu nikapiga session zangu na nilifanikiwa kumaliza salama Jumatano Mchana wa saba. Siku hiyo hiyo nikabatika kupata usafiri mpaka Tanga mjini maana Kilindi kulichosha sana nikaona bora nikalale Tanga town. Alhamis niligeuza zangu Dar ambapo ijumaa nilienda ofisini. Boss hakuwepo ila nilimpigia simu kwamba nimerudi na akaniambia tuu tutaonana Jumatatu na akanipa ruhusa ya kwenda kupumzika nyumbani. Basi mimi nikafanya retirement pale na kukabidhi madocuments na some change kwa muhasibu nikasepa zangu. Nakumbuka ile weekend ilikuwa mujarabu sana, wacha tuu. Jumatatu yake nikaandaa report na kumtumia boss kwenye email yake. Aliireview huko huko alipokuwepo maana hakuja ofsini siku hiyo. Aliweka some few inputs akaniambia niiprint na kuifile.

See you soon guys kuna mengi yanakuja!!!!!!! NENDA PG # 116
Dah kaka...ubarikiwe tu kwakweli umenitia moyo sana sana.
 
EPISODE 16: Mthamini sana mtu anayeona una kitu ambacho wewe mwenyewe hukioni

Katika maisha yetu ya kawaida iwe kwenye ajira, mtaani au shuleni kuna wale watu ambao wanaweza wakakushauri au kukulazimisha ufanye mambo ambayo wewe jukuwa na wazo nalo au hukujua kama unauwezo wa kulifanya jambo husika. I want to talk about the importance of appreciating and valuing individuals who recognize qualities, potential, or aspects of yourself that you might be unaware of or underestimate, in supporting one's life.

Baada ya kumaliza kile kikao Dodoma tulirudi ofisini kuendelea na majukumu kama kama kawaida. Namshukuru Mungu nilimaliza probation period salama na officially nikawa full employed pale. Kwa ambao mnategemewa kuwa waajiriwa wapya msishangae nakazia kazia sana swala la kumaliza probation period salama, labda niwaambie tuu hiki ni kipindi muhimu sana kwa mfanyakazi mpya kwenye kazi yako au ajira yako mpya. Ni kipindi ambacho mwajiri wako anakupima kama kweli unaweza kuleta tija kwenye kampuni au ni mzigo. Hii inaenda sambamba na kukupima kwenye uwezo wa kutekeleza majukumu yako, uwezo wa kujifunza au kumasta mazingira ya kazi kwa haraka, namna unavyoshirikiana na wenzako pale kazini, maadili ya kazi na swala la nidhamu kwa ujumla, just to mention the few. Makampuni au mashirika mengi mara ntyngi wanatoa kati ya miezi mitatu mpaka sita kulingana na utaratibu wa ofisi husika. Na katika kipindi hiki mara nyingi unakuwa hupewi kwanza stahiki zako zote muhimu mfano bonus kazini na wengine wanakupa kwanza nusu mshahara. Ukifanikiwa kumshawishi mwajiri basi unakuwa unapewa barua yako kwamba you have been successfully completed your probation period and you are endorsed as full employee. So kwa mfanyakazi mpya hicho ni kipindi cha kuwa makini sana ili usiwape sababu ya kukupiga chini au kukuongezea muda wa probation (Probation extension period).

Basi bhana nikawa napiga mzigo pale kutekeleza majukumu yangu kama kawaida. Sasa kwenye ile program mimi nilikuwa na-lead social deparment. Lakini kulikuwa na department nyingine kama medical na M&E. Sasa kwenye kufanya fanya kazi pale karibia tunamaliza mwaka mmoja tangu ile program ianze, ikatokea msala wa mambo ya safeguarding issues pale ofisini. Kwa wasiofahamu, safeguarding issues are the actions or behaviors by employees that may harm or compromise the well-being, safety, dignity, or rights of the individuals the project aims to assist. Inaweza kuwa maswala ya upendeleao, kuomba ngono kwa wanufaika wa progamu, any form of harassment, fraud nk. Ili kupambana na maswala ya safeguarding issues mara nyingi mashirika au makampuni yanakuwa na sera au miongozo ya kuwalinda wafanyakazi na wanufaika wa miradi by providing regular training to employees, establish reporting mechanisms, and conduct thorough investigations when concerns are raised.

Baada ya investigation ule msala uliondoka na watu wengi tu pale ofisini akiwemo jamaa aliyekuwa ana-lead department ya medical. Ile ishu ilichafua hali ya hew asana pale ofsini na kulitokea kuwa na magepu mengi ya kazi. Wazungu wapo seriazi sana na mswala ya safeguarding yaani wanayachukulia kwa uzito mno. Sikuwahi kuexperience hasira za wazungu kwenye kazi lakini kwenye ile ishu walikasirika mno, ilitumwa timu ya investigators kutoka makao makuu Europe pamoja na Nairobi kuja kufanya uchunguzi pale. Nakumbuka shughuli za ofisi zilisimama kama mwezi kupisha uchunguzi na kila mmoja aliwekwa kitimoto hadi CD mwenyewe.

Watu matumbo yaliwaka moto, yaani moja haikai mbili haisimami. Unajua kwenye haya mambo yanayohusisha uchunguzi usiwe unajiamini moja kwa moja hata kama hujafanya maana anaweza akaibuka mtu mwenye visa na wewe akakupigilia kitu kizito ukajikuta na wewe upo kwenye victims. To survive in such issues ni Mungu aingilie kati. Hata baadhi ya watu waliopigwa benchi akiwemo yule leaders wa medical department binafsi ilinguwa ngumu sana kuamini ila ndio hivyo majibu ya uchunguzi yaliomdaka na yeye. Wakati wote wa uchunguzi watu tulikuwa tunaogopana kama ukoma pale ofsini kifupi ilikuwa uwe umehusika au hujahusika kujiamini kulipungua kama sio kutoweka kabisa. Ni kama unapokuwa unasubiria majibu ya ukimwi hata kama ni bikra wa kiume au kike kale kamoment ka kusubiria kanakuletea kahofu flani ka kutokujiamini amini hahaaa.

Basi siku ya siku majibu yakakamilika, kikaitishwa kikao cha staff wote pale ofsini, tukaunganishwa na management ya Nairobi na makuu then report ikasomwa. Kisha maamuzi yakatolewa kwa waliokutwa na ule msala wanaachishwa kazi mara moja kwa mujibu wa sera ya safeguarding. Victims wakaaambiwa kama hawajaridhika na maamuzi wanaweza kwenda kwenye vyombo vya sheria ndani ya mwezi mmoja na kwa muda huo walitakiwa wakabidhi kila kitu cha ofisi. Kwa sisi survivors tulipigwa mkwara mzito kwamba ofisi haitakuwa na mswalie mtume kwa yoyote itakapothibitika kwamba mfanyakazi amejihusisha na violation of safeguarding policy.

Kwa kuwa maamuzi yalikuwa yameshatolewa mara paap wakaingia polisi pale, nafikiri waliandaliwa mapema ili kusimamia zoezi la kukabidhiana ofisi. Nadhani walijihami maana huwezi jua mtu atalipokeaje swala la kufukuzwa kazi tena gafla unaweza ukadundwa au kuuliwa hivi hivi. Basi zoezi la kukabidhi ofisi lilifanikiwa na kwa wale waliokuwa na madeni wanaodaiwa na ofisi wazungu waliamua kuwasemehe, yaani kama walikuwa wanaona kero hata kuendelea kuwadai. Nakumbuka kuna mshikaji mmoja ndio alikuwa ametoka kuchukua advance salalry ya miezi minne na alikuwa hajaanza hata kulipa/kukatwa akawa ametimuliwa na ofisi haikujali.

Nakumbuka baada ya wenzetu kuondoka na wale investigators kurudi kwao maisha yalikuwa magumu sana pale ofisi watu ni kama morale ilishuka sana. Hata shughuli nying zilikuwa haziendi kwa sababu nafasi nyingi zilikuwa wazi. Ikabidi makao makuu wafikiria kurestructure ofisi ya Tanzania ili kuangalia ni namna gani ya kurudisha ufanisi wa ofisi na kujaribu kudhibiti swala kama lile lisijirudie tena. Ikabidi CD na Head of Programs wasafiri kwenda makao makuu kwa ajili ya kulishughulikia hilo. Maana hao ndio walikuwa ndio mabosi wenyewe wa pale ofsini. Iko hivi pale ofisini kulikuwa na nanagement team na baadhi ya wafanyakazi tunaweza kusema ni kudumu kwamaana ya kwamba hawakuwa wanaajiriwa na miradi. Yaani ni hivi hapa tuwekane sawa kidogo, mfano mimi na wenzangu wengine tuliajiriwa na mradi ambao tulikuwa tunautekeleza kwa miaka minne. Kulikuwa pia na miradi mingine tofauti tofauti ambayo nayo pia ilikuwa inaajiri project team yake. Sasa project staff mnaajiriwa na mradi na mnaondoka mradi ukiisha, labda kama kuna mradi mwingine unaweza ukaomba endapo mradi wenu utakuwa umeisha. Lakini kulikuwa na wale ambao tunaweza sema ni wakudumu yaani wao wanaajiriwa pale bila kutegemea miradi ndio akiwemo huyo CD na huyo Head of Programs. Ndio ilivokuwa sijui kama nimeeleweka.

Kule ulaya kwenye kikao chao walikuja na strategies mbalimbali na mabadiliko kidogo ili kuendana na kasi ya utekelezaji wa mradi wetu. Baada ya two weeks walikuwa wamesharudi ofisini na wakaitisha kikao cha staff wote. One hour before the meeting CD akaniita niende ofsini kwake. Nilisthuka kidogo maana haikuwa kawaida CD kukuita ofsini. Mara nyingi kama kulikuwa na jambo anataka mjadiliane alikuwa anakuja mwenyewe kwenye ofisi yako. Ishu ya kuitwa ofsini wafanyakazi wa pale tuliichukulia kwa uzito kidogo. Kihoro kikanishika sana nikajisemea isije ikawa wale investigaors walilisahau jina langu na sasa ndio naenda kuhukumiwa. Usicheke ile situation ilikuwa ni ngumu mno kwa siku ile. Nikasema huyu labda anataka kuniandaa kisaikolojia ili kwenye kikao nikipigwa na kitu kizito isiwe cha kunishtukiza.

Basi nikaingia akanikaribisha pale na straight forward akanimbia “Taidume, the management has entrusted you with leading the medical department, and now you will serve as our medical-social coordinator”. Nikashtuka sana nikamtumbulia macho pale huku nikiwa nina maswali mengi sijui hata nianze kuuliza lipi lifate lipi. Maana nikawa nakiuliza mimi mtu wa massosholoji huko wapi na wapi leo kulead mambo ya madakatari? Alipoona nashangaa akagongomelea kwa kuniambia najua unashangaa hususani kwa kuwa wewe sio daktari na tunakutaka uchukue nafasi ya dakta ………… (akamtaja yule daktari aliyetimuliwa), lakini nikuhakikishie tuu sisi kama menejimenttumekujiridhisha kwamba utaweza.

Binafsi sikukubaliana naye kabisa nakumbuka kile kikao cha mimi na yeye kilichukua kama nusu saa nzima. Mimi nilikuwa nampa hoja zangu za kukataa ile nafasi lakini yeye anazipangua kwa kuniaminisha kwamba naiweza ile nafasi. Sasa, mimi sio kwamba nilikuwa tu siitaki ile nafasi lakini nilikuwa naona napwaya na italeta shida kwenye ufanisi wangu. Maana kwanza nilikuwa nawaza kwa harakaharaka pale namna yule dakatari alikuwa anafanya kazi zake. Yeye shughuli zake kubwa alikuwa anafanya na madakatari wenzake mikoani na wizarani, maswala ya kusimamia upimaji, utoaji dawa na ufuatiliajo wa maendeleo ya walengwa wetu. Kwanza nilikuwa namsikia tu hayo mabombastic ya kidaktari anaovoongea na madaktari wenzie basi mimi nikawa navurugwa tuu nikaona huyu CD vipi huyu naona ananitafutia tuu sababu ya kunitimua kazi maana performance ikiwa ndogo nayo ni ishu sana kufanya kazi na wazungu.

Nakumbuka tulivutana sana kwenye hilo. Mwisho wa siku CD akanipa job description ya ile position akasema tuzijadili moja moja. Yeye akawa anasoma kipengere kimoja kisha ananiuliza nimekiewlewaje? Nikawa naelezea kile kipengele nilivokielewa. Kwa ufuoi inaonekana aliridhika na jinsi nilivovielewa vile vipengere vya job description. Mwisho wa siku akaniuliza hapo sasa ni ni kigumu kwako? Kiukweli nilivyovipitia ile vipengere vya majukumu, asilimia zaidi ya 70 ilikuwa ni kuoragnize na kucoordinate the project implementation partners watekeleze majukumu yao within time and budget, baasi. Sikuhitajika kuwapima walengwa, wala kutoa dawa, wala kutoa ushauri wa kidaktari, hizi zote walikuwa wanatakiwa kufanya madakari wa mikoa husika huko tunakofanya kazi. Kwahiyo sikuhitajika kuvaa koti jeupe na Stethoscope kama madaktari wanavofanya. Yale mambombastic ya kidaktari zilikuwa ni mbwembwe za kututisha wengine hahaaa. Maana nakukumbuka kwenye zile reflection meetings au weekly feedback meeting na kupeana updates za mradi yule bwana daktari alikuwa anashusha vigongo sana mpaka wengine tukawa tunajisemea kumbe udaktari ni mgumu hivi na inaonekana wanaakili sana madaktari (jokes).

Basi nakumbuka CD akanikumbusha ile ishu niliyoorganize meeting na watu watu wa wizara ya afya wakati tunaenda kuutambulisha mradi, ile ambayo nilipata msala wa kusekwa sello. Akaniambia, that was an excellent entry point that the management team built trust in my coordination abilities. Nikajisemea laiti mngejua nililazwa selo sijui ingekuwaje hahaha. CD akaniambia “Taidume wewe una kitu kikubwa sana sema tuu hujijui. Naweza nikakuambia ilikuwa rahisi sana mimi kushawishi menejimenti kukubaliana tukuongezee hiyo idara kwa sababu naamini una skills na uwezo wa kudili na complex issues katika kudeliver project results”. Mimi nikamwambia kama vipi anipe muda nikafikirie, akanikatalia na kuniambia that was like an order to me and he is going to officially announce that to all staff in the meeting. Akaniambia tukimaliza mkutano atanipa my new contract.
Kwa upande mmoja nilikuwa na hofu lakini kwa upande mwingine nilikuwa nilikuwa na furaha. Hofu ilikuwa vipi je nitaweza kuhandle yale majukumu maana ilikuwa ni kama nafasi mbili kwa moja. Lakini pia niliassess the situation nikasema hapa lazima vijimaneno vitazuka maana wakati wa investigation kama ilivokawaida kunakuchomana sana, sasa nikawa nahofu kwamba lazima kuna watakaofikiria kwamba niliwachoma watu na asante yake ndio hiyo nafasi. Maswala ya uchawa hayo. Kwaupande mwingine nilifurahi kwa sababu hakuna kitu kizuri kama kuaminiwa tena wakati wewe mwenyewe ukiwa haujui kama una huo uwezo. Inakupa faraja sana, nilishawahi kuaminiwa katika maswala mbali mbali lakini haikuwa kwenye levp ya surprise kama ile. Nikajisemea mwenyewe let me take it, mambo mengine yatajiset juu kwa juu.

Basi tulikubalina hivyo. Muda wa kikao ulipofika staff wote tulikuwepo. Basi CD pamoja na mabo mengine akatoa mrejesho wa safari yao ya makao makuu. Akatoa feedback ya mikakati mbali mbali waliyokubalina na management team namna bora ya kuendesha ofisi ili swala lile lisijirudie tena. Watu wakauliza maswali na yakajibiwa na kusisitizana kuhusu hiyo mikakati mipya, mwisho wa siku CD akatangizia kwamba kuna baadhi ya nafasi zitatafutiwa watu wengine lakini kawaambia kuhusu ishu ya mimi kuwa appointed to lead also the medical unit of our project. Watu wengi hawakutegemea na walipigwa na mshangao, lakini ilibidi wakubaliane na ukweli huo maana ilikuwa tayari imeshaamuliwa na management tena kwa kupewa Baraka zote kutoka makao makuu. Basi walinipongeza pongeza pale na ndio ikawa stori kubwa ya siku.

Tulipomaliza mkutano, nikaenda ofisini kwa CD nikamkuta wakiwa na HR. basi nikakabidhiwa contarct yangu nikatakiwa niisaini by kesho yake maana ile position ilitakiwa ianze immediately. Nikaingia ofsini kwangu nikawa naipitia mdogo mdogo. Najua wengi mtataka kujua kama kulikuwa na nyongeza ya mshahara. Ofcourse kambuzi kaliongezeka kidogo japo kalikuwa bado hakajanona kiviile. Mimi nikausaini hapo hapo na kurudisha nakala moja kwa HR, officially nikaanza majukumu mapya. CD aliandika barua kuwasiliana na partners wetu hususani wale wapya kwangu (madaktari) kuhusiana na mabadiliko ya ile nafasi, huku akiwaomba ushirikiano.

Nikapanga mkakati wa kwenda kutembelea maeneo yote ya mradi ili kufahamiana na partners ili kwa pamoja tuweze kuweka mikakati mipya. Kwakweli nashukuru walinipa ushirikiano wa kutosha sana na tulifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa sana. Changamoto ndogondogo ni kitu cha kawaida na tulifanikiwa kuzimaliza na kusonga mbele.

Kiufupi na kwa ile ofisi ya wazungu nilifanikiwa kujiimarisha au kuongeza ujuzi katika maeneo yafuatayo
  • Experience in designing and implementing projects.​
  • Skills in project planning, budgeting, and resource management.​
  • Understanding of project lifecycle from inception to evaluation.​
  • Knowledge of fundraising strategies and techniques.​
  • Leadership skills in supervising personnel and resources.​
  • Ability to coordinate with implementing partners including government officials​
  • Skills in monitoring program effectiveness and impact.​
  • Relationship-building with community leaders, government, and local organizations.​
  • Identifying and addressing training needs for staff, partners, volunteers, and local organizations.​
  • Presentation skills for sharing program reports and findings with management, donors, and stakeholders.​
Nilifanya ile kwa muda wa miaka minne na tukafanikiwa kuhitimisha na kuumaliza ule mradi salama salmini. Mradi uliisha tangu Disemba 2022 lakini mimi niliombwa kubakia pale ofsini kwa miezi mingine mitatu kusaidia kukamilisha baadhi ya mambo hususani mfadhili wa mradi alikuwa anayahitaji. So officialy nilirudi uraiani mwezi wa tatu na kuanza harakati mpya za kusaka ajira nyingine.

MWISHO:
Wadau wangu yapo mengi sana ambayo ningeweza kushea nanyi naomba mniwie radhi kama haya machache hayakuwatosha. However, as I reflect on the chapters of my professional journey, each episode has been a lesson with the vibrant sort of experience. Your time invested in reading my story is sincerely appreciated. In sharing these moments of growth, challenge, and achievement, my hope is that you have found inspiration and some thing to takehome as an assignment.

Nimesoma na nitaendelea kuzisoma koments zenu kwa umakini mkubwa na binafsi nimefarijika kwa maoni, maonyo, mafunzo na mijadala ambayo imekuwa ikiibuka katikati ya stori, hahaa hii ni kawaida. Kwa pale nilipoweza nilitoa na nitaendelea kutoa ufafanuzi na kwa wale wanaonifata PM for more detals, I respect and salute you guys.

Kwa kipindi hiki ambacho nahangaika huku na huko kusaka sehemu nyingine nafanya kazi za kujitolea kwenye maeneo mbalimbali hususani vile viNGO vidogo ambavyo ndio vinaanza. Pia kuna watu hata humu JF wapo tunasaidiana kudizaini concept notes na kuandika full project proposals. Huwa najitolea kwa wale ambao nimehakikisha hawana uwezo, maana hata mimi nikiangalia nilikopita pita mpaka hapa nilipo sijawahi kutoa hata sh10 ili kusaidiwa.

Nipo hapa pia kuendelea kutoa uzoefu wangu kwa yeyote ambaye anaona nitafaa kushea naye ninachokifahamu muda na wakati wowote. Na pia ninawaahidi kama nitafanikiwa kupata sehemu nyingine ya kupiga mzigo basi niatwashirikisha hapa hapa. Kwa sasa bado natafuta kazi.

Thank you guys niwatakie maandalizi mema ya sikuku za mwisho wa mwaka na heri sana ya mwaka mpya 2024 kwenu woote. Na kama kuna mtu kwa namna moja ama nyingine nimemkwaza naomba anisamehe, Mungu awabariki sana.

MIALIKO YA SIKUU INAKARIBISHWA PIA

TaiDume 0748 586 059​
Napenda kutoa shukrani zangu za shati kwako kaka yangu. Binafsi nimefarijika na nimejifunza mengi kutoka kwako katika yote uliyoeleza tangu mwanzo katika Uzi huu. I am glad I could definitely resonate with some of your past experiences during your early years of work.

Ningekuwa mtu mzito mwenye hela zake, ningekuajiri uwe hata personal advisor wangu katika miradi yangu. Ila kwa kweli ningependa kufanya kazi na mtu kama wewe.

Godspeed in your job search, career growth and personal development!

.........................................................................................
NB: Kwa nia nzuri na mimi naomba niwashirikishe kidogo wadau wenzangu wa JF kuhusu uhitaji wangu wa ajira. Thank you in advance.

Wasifu: Mimi ni kijana mkarimu na mchapakazi, mwenye umri wa miaka 27 ninayepatikana Ukonga Mombasa (karibu na Gongo la Mboto).

Elimu: Nina shahada ya Menejimenti ya Uhandisi wa Viwanda kutoka Chuo Kikuu Mzumbe; nime'base zaidi katika masuala ya utafiti, miradi, uvumbuzi na teknolojia, pamoja na menejimenti.

Uzoefu: Nina uzoefu wa miaka 3 katika kazi za mtandaoni, utafiti, usimamizi miradi na operesheni. Nimefanya kazi mtandaoni kama Data Entry and Research Volunteer katika kampuni mbili za kiteknolojia za Ulaya (Compaira, Deal Lite); Personal and Delivery Assistant wa CEO katika Hamashiach Bookshop; Organizing Team Leader wa Employability Africa program kutoka SC Konsult; Operations and Digital Platforms Manager katika kampuni ya usafirishaji (Afritrust Holdings Limited). Pia, nimefanya kazi kama Field Officer na Enumerator katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Nje na kazi, mimi ni mjasiriamali niliyepata mafunzo kutoka UDIEC GEP 2021 na Digify Tech 2021; Mwanaharakati wa masuala ya vijana niliyepata mafunzo maalum kuhusu elimu, kazi na afya ya akili kutoka katika mkutano wa kimataifa wa YOUNGA 2022; Msaidizi wa mtandaoni (Virtual Assistant) niliyeidhinishwa na ALX Africa baada ya kuhitimu vizuri mafunzo 2022.

Mapendeleo: Napendelea kufanya kazi kama Research Assistant, Project Assistant, Personal or Executive Assistant (wa mtu binafsi, shirika au kampuni), Tutorial Assistant, Training Assistant, Customer Service Officer, Digital Platforms Manager, Data Entry Specialist au Data Manager, katika maeneo yoyote (ikiwemo Posta, Mnazi mmoja, Makumbusho, Masaki, Tegeta, Bunju, Mbagala) ndani ya mkoa wa Dar es Salaam. Mimi ni mtu niliye'flexible hivyo naweza kufanya kazi katika mazingira ya aina yoyote (office, hybrid, work-from-home, fast-paced, collaborative, travel). Napendelea kufanya kazi ya part-time au kwa mkataba (lakini ikibidi, nipo tayari kufanya kazi full-time au hata kwa kujitolea).

NB: Kwa kuwa pia mimi ni Msaidizi wa Mtandaoni, naweza kufanya mbalimbali za uandishi (content writing, proofreading/grammar checking, English-Swahili translation) na za mtandaoni (account management, email management, documentation, online navigation, phone/computer backup, digital skills training, Windows and Office local activation). Huwa nafanya kazi kwa umakini, usiri na ubora.

Mawasiliano:
Simu - 0743744471
 
Back
Top Bottom