Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Members mu hali gani? Mwaka 2014 nilisajili business name, mungu mkubwa muda huu nataka kusajili kampuni kwa kutumia ile business name ya 2014. Nimehangaika sana naombeni process za kufuata ili niitumie/badili business name kuwa company name
Mimi Nina swali hapa mkuu kama mahesabu yanawasilishwa tra kabla ya 30 June na hii kodi ambayo kampuni inajikadilia before ya 31 march itafanyikaje? Na nilijua Yale mahesabu unayowasilisha tra ndio yatatumika kukupa mafasi wewe ya kulipa kodi ile ya 30% kutoka kwenye faida? Au mm ndio bado sielew dhana ya kodi kwa kampuni? Msaada tafadhali?Naomba niwatakie HERI NA FANAKA katika mwaka huu mpya wa 2020.
Naombanikumbushie kwa ufupi mambo ambayo kama mfanya biashara hasa wale wenye makampuni mambo ambayo ni muhimu kuzingatia.
1. Hakikisha kuwa Kampuni yako au jina la biashara yako limekuwa updated BRELA kwenye mfumo wa online yaani Online Registration System (ORS).
2. Hakikisha kuwa makadirio yako ya 2019 yamelipwa kwa quater zako nnne TRA.
3. Fanya makadirio ya mwaka huu mapema kabla ya tarehe 31 March ushauri sio mbaya kwa mwaka huu utawaita wataalamu wakushauri na kufanya tax plan kwa mwaka huu ili uweze kuchukua ushari wa kitaalamu katika biashara yako
4. Hakikisha hesabu zako za 2019 zinafanya na kukaguliwa kabla ya June 2020 ili kuziwasilisha on time.
5. Pata your tax clearance mapema iwezekanavyo ikiwezekana anza kuifuatilia leo maana hii ni kuwa wahi kufanya makadirio na asilimia 10% ya pango hakikisha kuwa imelipwa na lipa asilimia 1% ya stamp duty inayotokana na bei ya mkataba wa pango.
6. Weka malengo makubwa zaidi ya fanyie tadhimini kila wiki na kila mwezi .
Nawatakieni Mwakwa Mwema
Mimi Nina swali hapa mkuu kama mahesabu yanawasilishwa tra kabla ya 30 June na hii kodi ambayo kampuni inajikadilia before ya 31 march itafanyikaje? Na nilijua Yale mahesabu unayowasilisha tra ndio yatatumika kukupa mafasi wewe ya kulipa kodi ile ya 30% kutoka kwenye faida? Au mm ndio bado sielew dhana ya kodi kwa kampuni? Msaada tafadhali?
Sent using Jamii Forums mobile app
Je naweza kufungua kampuni kwasasa lakini mipango yangu ya kujakuendesha ni baada ya miaka 2 au 3 baadaye?SDL utalipa tu mpaka pale utakapokuwa na wafanyakazi wanne na zaidi hayo ndio matakwa ya sheria. Kwahiyo kama mko wawili tu hamna haya ya SDL. Na rate ya mwaka huu ni 4.5% Ahsante
Je naweza kufungua kampuni kwasasa lakini mipango yangu ya kujakuendesha ni baada ya miaka 2 au 3 baadaye?
Nimeelewa zaidi kwa kiwango cha mwishoMakadirio ya mwaka husika yanfanyika kabla ya mwisho ya robo mwaka TRA wanaamini kabisa mpaka robo ya mwaka utakuwa unajua mwelekeo wa mwaka na haya makadirio ukifanya na kama kuna mabadiliko yoyote unaweza kubadilisha unavyoona inafaa kwahiyo hizo lazima ziende kabla ya tarehe au 31/3. Mahesabu yaliyokaguliwa ndio ya mwaka wa nyuma mfano 2019 yanatakiwa kwenda kabla au tarehe 30/06/2020.
Nafikiri nimeelezea kwa mwanga kidogo kama unahitaji maelezo zaidi atanijuza
Habari ya kwako mkuu!Karibu
Uzi ulimipita huu kitambo sana, lakini pia nimeupata kipindi nina uhitaji nakimbilia kufungua biasharaHabarini za leo wanajamii,
Leo nimeona kidogo nitumie fani yangu ya ushauri wa maswala ya biashara na uchumi kuweka mambo muhimu katika uendeshaji wa biashara kwa nchi yetu pendwa ya Tanzania.
Hapo miaka ya nyuma kulitokea na watu wengi waliosajili makampuni (LTD Companies) na wengine walienda mbali kidogo wakapata na Tax Indentification Number (TIN) kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA). Sasa wanapotaka kuanza kufanya kazi wanakutana na penaty kubwa na fine.
Ni Moja ya kushukuru Mungu sijui waheshimiwa walipita hapa katika budget ya mwaka 2018/2019 wametoa TAX AMNESTY kwenye fine na penalty kwa kipindi cha miezi sita toka July 1 to Nov 30, Sasa Maelekezo yametoka na form ziko online na kwenye ofisi za TRA hii ni nia nzuri mno ya serikali na mimi natoa kongole kwa jambo hilo. Hii uliyo na rangi hii ni maongezo toka kwenye original post
Ni kutokana na kadhia hiyo nataka kutoa ushauri kidogo kwa yeyote mwenye kampuni vitu hivi vitatu ni vya muhimu sana hata kama kampuni yako haiyafanya biashara.
Mosi hakikisha kila mwaka unapeleka majeresho yako (Annual returns) brela kwenye tarehe ile ambayo ulisajiliwa na hizi ni vyema ziambatane na hesabu zilizokaguliwa ( Audited financial). Kuanzia February 01, 2018 suala hili linafanyika kwenye mtandao wa BRELA, kama utahitaji msaada wa kufanya unaweza kuwasiliana nami PM.
Mbili, hakikisha unapelewa returns zako TRA zile za provisional returns ambazo zinatakiwa kupelekwa kuanzia tarehe 01 January mwisho wake ni tarehe 31 March. Haya ni makisio unayotegemea kuwa nayo kwa kipindi cha mwaka huo. Na hapa ndio kumekuwa na mtihani kwa wale waliokuwa na kampuni lala kuwa mimi sijafanya biashara kabisa, Kama hutegemei kufanya bishara weka au fill Nil returns ( RETANI ZERO) inakubalika ila unajulikana na kutofanya hivyo inakarabisha fine.
Na haya makadirio unaweza kuyabadilisha kwa wakati wowote hali yako ya biashara itakapobadilika. Hivyo hivyo kwenye VAT unatakiwa kupeleka returns zako za VAT kila mwezi hata kama ujafanya biashara kama umesajiliwa kwa VAT. Na Vile vile hakikisha kuwa mahesabu yako ( Audited Financial) zinawakilishwa kila mwaka kabla ya tarehe 30 June.
Tatu, kodi zote nyinginezo kama withholding tax, PAYE na SDL zinapelekwa ila hapa utata umekuwa mkubwa kwenye withholding tax kwenye pango (rent) kwa mujibu wa sheria ni yule anayelipa ndio anatakiwa kukata na kupeleka TRA kwahiyo kama pango lako kwenye mkataba ni laki tano kwa mwezi na wewe umelipa miezi mitatu. Unatakiwa umpe mwenye nyumba 1,350,000/ halafu hiyo 150,000/ Unapeleka TRA, hivyo ndivyo sheria inavyotaka.
Naomba kuwakilisha.