Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Members mu hali gani? Mwaka 2014 nilisajili business name, mungu mkubwa muda huu nataka kusajili kampuni kwa kutumia ile business name ya 2014. Nimehangaika sana naombeni process za kufuata ili niitumie/badili business name kuwa company name
 
Kwanza unatakiwa update online hiyo business name na hapa ni lazima uwe na kitambulisho cha nida halafu unaifunga hiyo business name na wakati huo huo unaifungulia kampuni kwenye jina hilo hilo.


Members mu hali gani? Mwaka 2014 nilisajili business name, mungu mkubwa muda huu nataka kusajili kampuni kwa kutumia ile business name ya 2014. Nimehangaika sana naombeni process za kufuata ili niitumie/badili business name kuwa company name
 
Naomba niwatakie HERI NA FANAKA katika mwaka huu mpya wa 2020.
Naombanikumbushie kwa ufupi mambo ambayo kama mfanya biashara hasa wale wenye makampuni mambo ambayo ni muhimu kuzingatia.
1. Hakikisha kuwa Kampuni yako au jina la biashara yako limekuwa updated BRELA kwenye mfumo wa online yaani Online Registration System (ORS).
2. Hakikisha kuwa makadirio yako ya 2019 yamelipwa kwa quater zako nnne TRA.
3. Fanya makadirio ya mwaka huu mapema kabla ya tarehe 31 March ushauri sio mbaya kwa mwaka huu utawaita wataalamu wakushauri na kufanya tax plan kwa mwaka huu ili uweze kuchukua ushari wa kitaalamu katika biashara yako
4. Hakikisha hesabu zako za 2019 zinafanya na kukaguliwa kabla ya June 2020 ili kuziwasilisha on time.
5. Pata your tax clearance mapema iwezekanavyo ikiwezekana anza kuifuatilia leo maana hii ni kuwa wahi kufanya makadirio na asilimia 10% ya pango hakikisha kuwa imelipwa na lipa asilimia 1% ya stamp duty inayotokana na bei ya mkataba wa pango.
6. Weka malengo makubwa zaidi ya fanyie tadhimini kila wiki na kila mwezi .
Nawatakieni Mwakwa Mwema
 
Mimi Nina swali hapa mkuu kama mahesabu yanawasilishwa tra kabla ya 30 June na hii kodi ambayo kampuni inajikadilia before ya 31 march itafanyikaje? Na nilijua Yale mahesabu unayowasilisha tra ndio yatatumika kukupa mafasi wewe ya kulipa kodi ile ya 30% kutoka kwenye faida? Au mm ndio bado sielew dhana ya kodi kwa kampuni? Msaada tafadhali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makadirio ya mwaka husika yanfanyika kabla ya mwisho ya robo mwaka TRA wanaamini kabisa mpaka robo ya mwaka utakuwa unajua mwelekeo wa mwaka na haya makadirio ukifanya na kama kuna mabadiliko yoyote unaweza kubadilisha unavyoona inafaa kwahiyo hizo lazima ziende kabla ya tarehe au 31/3. Mahesabu yaliyokaguliwa ndio ya mwaka wa nyuma mfano 2019 yanatakiwa kwenda kabla au tarehe 30/06/2020.
Nafikiri nimeelezea kwa mwanga kidogo kama unahitaji maelezo zaidi atanijuza



 
SDL utalipa tu mpaka pale utakapokuwa na wafanyakazi wanne na zaidi hayo ndio matakwa ya sheria. Kwahiyo kama mko wawili tu hamna haya ya SDL. Na rate ya mwaka huu ni 4.5% Ahsante
Je naweza kufungua kampuni kwasasa lakini mipango yangu ya kujakuendesha ni baada ya miaka 2 au 3 baadaye?
 
Ndio unaweza ila kiushauri kama bado unaona ujawa tayari subiria tu mpaka hapo utakpokuwa tayari italeta maana zaidi. Moja kwasababu siku hizi kampuni inakuwa number ndio inakuwa namba yako ya TIN ingawa inakulazimu kwenda TRA ili upate TIN na hapa ukishaingia maswala ambayo kampuni inatakiwa kufanya yataanza kukuhusu moja kwa moja wakati utakuwa huna uwezo wa kufanya hilo inaweza kukukatisha tamaa zaidi ya kujingea.
Nawasilisha.
Je naweza kufungua kampuni kwasasa lakini mipango yangu ya kujakuendesha ni baada ya miaka 2 au 3 baadaye?
 
Nimeelewa zaidi kwa kiwango cha mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari ya kwako mkuu!

Samahani naomba kueleweshwa tofauti kati ya company name, business name, registered trademark na unregistered trademark.

Tukifanyia mfano wa Coca-Cola ®, Pepsi ® na Kilimanjaro™

Ikiwezekana pia na taratibu zake zakufanya usajili
 
Kstibu.
Naomba kukumbusha kuwa siku za kufanya makadirio ya kodi kwa ajili ya mwaka 2020 ndio umebakiza siku 34 tu. Kwahiyo wafanyabiashara Binafsi, mwenye makampuni na wabia na wadau wote huu ndio muda muafaka wa kwenye TRA kufanya makadirio na kupata tax clearance. Ili ikusaidia kupata lesini pale leseni yako inapoisha.

uzi murua kabisfa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba leo nikumbushe swala la kodi za waajiriwa hasa hii SDL ambayo kampuni au biashara yoyote iliyo na wafanyakazi zaidi ya wanne kila mwezi inawajibika kupeleka asilimia 4.5 ya malipo yao TRA naona watu wengi hili nalo wamesahau. Hii inabidi ipelekwe tarehe kabla au tarehe 07 ya kila mwezi na hii ni garama ya mwajiri sio mwajiriwa. Unapoepeleka hii unatakiwa upeleke na PAYE ambayo umemkata mfanyakazi. Penalty yake kwa sasa kutopeleka ni Tshs 225,000/ kwa kila mwezi unaochelewesha
 
Wakati mahesabu ya 2019 yamewasilishwa na returns zake mambo muhimu yakuangalia sasa July 2020 kwanza Finance act ya 2020 imetoka ni muhimu kuipitia kujua mabadiliko mbalimbali kwenye biashara nimeimbatanisha hapa unaweza kuipata. Pili ni muda wakuangalia kama makadirio yako yanahitaji kuongezwa au kupunguzwa kutokana na mwenendo wa biashara yako mpaka sasa. Tatu muda huu kwenye biashara za nchi yetu ndio robo mwaka inayotakiwa kukupahela nyingi kutokana na kwamba mzunguko ni mkubwa sasa tembelea vyanzo vyako vya mapato nakuangalia jinsi gani unafutia wateja wengi zaidi
 

Attachments

Habari za Leo Tarehe 13 August nilizungumzia kwa kiasi fulani juu ya kuanzishwa kwa mfumo mpya wa Efilling wa TRA na kuelekeza jinsi gani mfumo wa zamani hatakuwa ukiendelea wa kupeleka returns hasa kwa makampuni. Baadhi ya mikoa ya kikodi imeshaanza kutopokea nakala ngumu has mkoa wa Ilala. Ila leo ningependa zaidi kujikita katika KODI ya PAYE ( Inayolipwa na wafanyakazi ya LIPA kutokana na unavyopata) na Ile kodi ya Maendelezo ya ujuzi (Skill Development Levy) (SDL). Kwa kampuni sasa ni lazima hizi ziwe filled kwenye mfumo ili uweze kupata debit number na uweze kulipia usipozifanya kwa sasa ukija ukasign kwenye mfumo unaweza kuona kuwa ujalipa.
Mbili Ushauri kwa TRA wajitahidi hii mifumo iende pamoja yaani ya zamani na wa sasa maana kuna mambo ambayo mfano kufanya reestimate ya kuongeza kodi kwa mwaka huu kwenye system bado ni changamoto.
Nawatakia siku njema yenye baraka zote za Mungu
 
Uzi ulimipita huu kitambo sana, lakini pia nimeupata kipindi nina uhitaji nakimbilia kufungua biashara
Nina maswali yafuatayo:
1.TIN yangu niliofungulia biashara mkoa fulani je ni lazima nihamishe kwenye mkoa naenda kufungua biashara

2.nilifungua biashara lakini haikuoperate na nikalipa kodi ya kwanza niliyokadili 133000 sasa ni kwanini walinidai wakati bishara ilikua dormant


3. sahivi nashindwa kufungua biashara ingine bila wanasema ni mpaka nihamishe TIN na hiyo TIN ina deni la, awali je ni lazima kufanyike clearance

4.hakuna namna naweza kusamehewa kodi ya awali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…