Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Nyumbalao

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
494
Reaction score
522
Habarini za leo wanajamii,

Leo nimeona kidogo nitumie fani yangu ya ushauri wa maswala ya biashara na uchumi kuweka mambo muhimu katika uendeshaji wa biashara kwa nchi yetu pendwa ya Tanzania.

Hapo miaka ya nyuma kulitokea na watu wengi waliosajili makampuni (LTD Companies) na wengine walienda mbali kidogo wakapata na Tax Indentification Number (TIN) kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA). Sasa wanapotaka kuanza kufanya kazi wanakutana na penaty kubwa na fine.

Ni Moja ya kushukuru Mungu sijui waheshimiwa walipita hapa katika budget ya mwaka 2018/2019 wametoa TAX AMNESTY kwenye fine na penalty kwa kipindi cha miezi sita toka July 1 to Nov 30, Sasa Maelekezo yametoka na form ziko online na kwenye ofisi za TRA hii ni nia nzuri mno ya serikali na mimi natoa kongole kwa jambo hilo. Hii uliyo na rangi hii ni maongezo toka kwenye original post

Ni kutokana na kadhia hiyo nataka kutoa ushauri kidogo kwa yeyote mwenye kampuni vitu hivi vitatu ni vya muhimu sana hata kama kampuni yako haiyafanya biashara.

Mosi hakikisha kila mwaka unapeleka majeresho yako (Annual returns) brela kwenye tarehe ile ambayo ulisajiliwa na hizi ni vyema ziambatane na hesabu zilizokaguliwa ( Audited financial). Kuanzia February 01, 2018 suala hili linafanyika kwenye mtandao wa BRELA, kama utahitaji msaada wa kufanya unaweza kuwasiliana nami PM.

Mbili, hakikisha unapelewa returns zako TRA zile za provisional returns ambazo zinatakiwa kupelekwa kuanzia tarehe 01 January mwisho wake ni tarehe 31 March. Haya ni makisio unayotegemea kuwa nayo kwa kipindi cha mwaka huo. Na hapa ndio kumekuwa na mtihani kwa wale waliokuwa na kampuni lala kuwa mimi sijafanya biashara kabisa, Kama hutegemei kufanya bishara weka au fill Nil returns ( RETANI ZERO) inakubalika ila unajulikana na kutofanya hivyo inakarabisha fine.

Na haya makadirio unaweza kuyabadilisha kwa wakati wowote hali yako ya biashara itakapobadilika. Hivyo hivyo kwenye VAT unatakiwa kupeleka returns zako za VAT kila mwezi hata kama ujafanya biashara kama umesajiliwa kwa VAT. Na Vile vile hakikisha kuwa mahesabu yako ( Audited Financial) zinawakilishwa kila mwaka kabla ya tarehe 30 June.

Tatu, kodi zote nyinginezo kama withholding tax, PAYE na SDL zinapelekwa ila hapa utata umekuwa mkubwa kwenye withholding tax kwenye pango (rent) kwa mujibu wa sheria ni yule anayelipa ndio anatakiwa kukata na kupeleka TRA kwahiyo kama pango lako kwenye mkataba ni laki tano kwa mwezi na wewe umelipa miezi mitatu. Unatakiwa umpe mwenye nyumba 1,350,000/ halafu hiyo 150,000/ Unapeleka TRA, hivyo ndivyo sheria inavyotaka.


Naomba kuwakilisha.
 
SDL utalipa tu mpaka pale utakapokuwa na wafanyakazi wanne na zaidi hayo ndio matakwa ya sheria. Kwahiyo kama mko wawili tu hamna haya ya SDL. Na rate ya mwaka huu ni 4.5% Ahsante

Ahsante kwa hii elimu mkuu.SDL naikwepa vipi kisheria?kampuni ina directors wawili ambao ni ndiyo founders/shareholders.
 
Kusajili kampuni inakuwezesha kuwa na mtu mwingine zaidi ya wewe. Maana kampuni ni kitu kamili ( Entity) na sheria nyingi za kodi zinaonyesha kulinda zaidi kampuni zaidi kuliko aina nyingine za biashara. Yani zile za watu binafsi (Sole Proprietor ) au zile za Ubia (Partnership).

Kwa kuwa kampuni inaweza kushitaki na kushitakiwa ( Entity) na hivyo kuwezesha kuwa na ukomo kwa hisa zake tu ( Limited to its share) na hivyo inaweka cover fulani kuliko aina nyingine. Na faida nyingine kubwa ni uwezo wa kutoa matumizi ya biashara katika faida unayotengeneza.

Na huo uhuru wa kuweza kukadiria kodi mwanzoni wa mwaka tofauti ya ile ambayo biashara nyingine unakadiriwa tu then unalipa. Ila uhuru huo unalimit usije ukapungua zaidi ya 20% unaweza kukutana na penalty.
ukitaka kusoma zaidi unaweza kutembelea link hii Advantages and Disadvantages of the Corporate Form of Business



Ninafaidika nn nikisajili kampuni
 
SDL utalipa tu mpaka pale utakapokuwa na wafanyakazi wanne na zaidi hayo ndio matakwa ya sheria. Kwahiyo kama mko wawili tu hamna haya ya SDL. Na rate ya mwaka huu ni 4.5% Ahsante
Ahsante mkuu,elimu imenyooka na nimekuelewa vyema ila TRA wenyewe hawakuambii kuwa ni kuanzia staffs 4
 
SDL utalipa tu mpaka pale utakapokuwa na wafanyakazi wanne na zaidi hayo ndio matakwa ya sheria. Kwahiyo kama mko wawili tu hamna haya ya SDL. Na rate ya mwaka huu ni 4.5% Ahsante
Mkuu nimekutumia PM mkuu naomba ucheki
 
Mkuu hiyo penalty inaweza kufikia sh ngapi? na pia annual return huwa ni lini?
 
Penalty of non filling ni Tshs 225,000 kwa kila mwezi uliochelewa. Annual returns inatakiwa iende mwisho ni miezi sita baada ya kumaliza mwaka wako wa kimahesabu ambapo kampuni nyingi ni tarehe 30/ June unatakiwa kuwa umepeleka hizo returns TRA


Mkuu hiyo penalty inaweza kufikia sh ngapi? na pia annual return huwa ni lini?
 
Kwa mfano nimesajili kampuni brela lakini haijafanya kazi(sijaanza biashara )mpaka mwaka umepita,je nitapigwa fine na brela ?

Kusajili kampuni inakuwezesha kuwa na mtu mwingine zaidi ya wewe. Maana kampuni ni kitu kamili ( Entity) na sheria nyingi za kodi zinaonyesha kulinda zaidi kampuni zaidi kuliko aina nyingine za biashara. Yani zile za watu binafsi (Sole Proprietor ) au zile za Ubia (Partnership). Kwa kuwa kampuni inaweza kushitaki na kushitakiwa ( Entity) na hivyo kuwezesha kuwa na ukomo kwa hisa zake tu ( Limited to its share) na hivyo inaweka cover fulani kuliko aina nyingine. Na faida nyingine kubwa ni uwezo wa kutoa matumizi ya biashara katika faida unayotengeneza. Na huo uhuru wa kuweza kukadiria kodi mwanzoni wa mwaka tofauti ya ile ambayo biashara nyingine unakadiriwa tu then unalipa. Ila uhuru huo unalimit usije ukapungua zaidi ya 20% unaweza kukutana na penalty.
ukitaka kusoma zaidi unaweza kutembelea link hii Advantages and Disadvantages of the Corporate Form of Business
 
Barua kwa TRA mara nyingi ni biashara binafsi (Sole propriator) na Ubia ( Partnership) ukifanya hivyo huna haja ya kupeleka. Ingawa kwenye makampuni ukweli ni kwamba ukiwa umefunga kampuni maana ume wind up kwa sheria ya makampuni Section 345 unakuja TRA tu kuangalia ni kiaisi gani wanakudai kwama hawakudai ndio unapewa TAX Clearance unafunga kampuni. Kama unadaiwa huwezi kupewa uwezo wa kufunga kampuni mpaka umemaliza deni lako.

Ikiwa nimefungua kampuni na nikaitolea ripoti TRA kwa barua kwamba haifanyi kazi nimeifunga, bado nitalazimia kuandaa hizo ripoti za miezi?
 
Hapana Brela wanachotaka ukimaliza mwaka mmoja upeleke returns zao ambazo mara nyingi inaonyesha mabadiliko katika owenership structure.

Ila Kwa TRA kama kampuni unatakiwa upeleke hiyo nil returns bila kukosa yaani muda wake mwezi wa tatu na annual unajaza na kupitishiwa na Certified Public Accountant


Kwa mfano nimesajili kampuni brela lakini haijafanya kazi(sijaanza biashara )mpaka mwaka umepita,je nitapigwa fine na brela ?
 
Back
Top Bottom