Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Ndugu hili nitakwa la kisheria Section 186 of company act lazima wawepo angalau wawili . Sasa tafuta mke/mume, rafiki au hata ndugu mpe asilimia kidogo kuanzia 1-5% ya share utakuwa na nguvu kama unamiliki pekee yako.

Nimekuwa nikiskia kampuni haimilikiwi na mtu mmoja, je nitafanyaje kama nina mtaji wa kutosha kufunga kampuni ninyohitaji lakini ama sitaki kuwa na wanahisa wengine kwenye kampuni yangu au sina watu wengine wa kuwa wanahisa wa kampuni yangu?

Ahsante.
 
Ndugu hili nitakwa la kisheria Section 186 of company act lazima wawepo angalau wawili . Sasa tafuta mke/mume, rafiki au hata ndugu mpe asilimia kidogo kuanzia 1-5% ya share utakuwa na nguvu kama unamiliki pekee yako.
sawa shukrani kwa elimu, je kama share nikiwaweka wanangu ambao ni wadogo ki umri kuwa miongoni mwa wamiliki wa kampuni kuna tatizo lolote kwenye hizo company acts?
 
Director wa kampuni lazima afikishe umri wa miaka 21. Kuna baadhi ya kampuni nimeona wamewekwa kama member na sio director naamini kwa hapo embu tafuta ushauri wa kisheria zaidi itakuwa nzuri.

sawa shukrani kwa elimu, je kama share nikiwaweka wanangu ambao ni wadogo ki umri kuwa miongoni mwa wamiliki wa kampuni kuna tatizo lolote kwenye hizo company acts?
 
Naamini wiki hii umeweka mambo yako sawa na angalau unajua mwanga wa hesabu zako zilikaaje mwaka jana na kwa mbali kama unamtaalamu mzuri wa mahesabu ambaye anajua kazi yake sasa unaweza ukapata makisio ya mwaka huu. Ushauri wangu ni kwamba wiki mbili hizi zijazo fanya makisio yako peleka TRA na jiandae kulipa kabla ya tarehe 31/ March/2018 ndio siku ya mwisho wa kulipa. Na wakati huo huo ukikamilisha mahesabu yaliyokaguliwa ambayo yanatakiwa kupelekwa kabla ya tarehe 30 June. Kama unaendeesha kampuni yako vyema ni vizuri kila wakati kufanya haya mambo mapema utapata muda mzuri zaidi wa kujua mwelekeo wa biashara yako.
 
Hii ndio wiki ya kufile VAT kama wewe ni VAT registered kwa mauzo uliyofanya mwezi wa kumi na mbili. Na hivyo kuhitimisha repoti yako ya mwaka jana. Mambo machache ya kuzingatia angalia EFD yako kama unaendana na mauzo yako kwa kipindi hiki ili usiwe na namba ambazo itakuwa ngumu kuelezea. Ni vyema jambo hili lifanyike mapema ili mpaka au kabla ya tarehe 20 mwezi huu itakuwa nzuri sana.
 
Wakati mwaka unaanza na watu kutakia heri ya mwaka mpya siwezi kusisitiza kuwa na plan ya biashara yako katika hali ya sasa na vilevile kufanya mpango wako wa malipo ya kodi (Tax planning). Wenye biashara nyingi za kati wanakuwa hawana plan yao na hivyo kuelekea mara nyingi swala la kodi kuonekana kama ni mshutuko kwao au ni kitu hatari. Kumbe ikifanya mpango wa kodi (Tax planning) unaweza kujua kwa hukakika kuwa ni kodi gani utazilipa na hivyo kuwa na mpango wa kulipa muda wake unavyofika. Kwahiyo ni ushauri kabla ujafanya makadirio yako kwenye robo ya kwanza basi tengeneza hesabu zako za mwaka uliopita ili kujua ni nini utakisia mwaka huu. Sio kukisia tuu bila kujua hata mwaka uliopita ulifanyaje. Have a great week end
 
Habari za leo jambo lingine muhimu ambalo inaweza kukusaidia katika kuendesha biashara yako kwa ufanisi ni kupanga matumizi kwa ajili ya professional advice. Swala hili nimekuwa sio taratibu hasa kwa makampuni madogo madogo jiwekee budget hata kama ni ya milioni 2 tafuta mwanasheria, muhasibu na washauri wengine kabla ujapata tatizo kuwa na MOU nao na hata walipe retainer fee hii inakuwa kama insurance hata kama unawalipa kidogo kidogo kila mwezi siku ukipata issue huna haja ya kuangaika sana unatumia. Hiyo ukiona ngumu basi weka account maalumu kwa ajili hiyo na kuweka fedha uko kila mwezi inakusaidia siku ikipata issue ambayo huduma hizo zinatakiwa unakuwa na fedha ya kulishughulikia. Ni muhimu kuliko maelezo kwa sababu kuna siku utajikuta unahitaji huduma zao.
 
Mm nilifungua kampuni mwaka 2012 nikaoperate mwaka mmoja tu na in that yr sikufanya cha hesabu zozote zile wala Tra sikwenda kulipa na baada ya hapo nikapata matatizo sikuendelea tena na biashara mpaka leo so nafanyeje sbb km ni mapenalties yatakua ya kufa mtu nishauri hapa mkuu.
 
Pole sana na matatizo. Sasa unahitaji kuendelea na biashara hiyo au unataka kufunga embu nijibu hapo nione ninaweza kukushauri vipi utoke kwenye hii changamoto.

Back
Top Bottom