Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Darasa ni tamu sana, naomba kujua taratibu za kufungua kampuni, na kuna aina ngapi za kampuni?
 
Kwa sasa makampuni unaweza kufungua kwenye mtandao. Hili limerahisishwa kwa kiasi fulani. BRELA
Tembelea hiyo link. Kuna aina kuu mbili Private na Public companies. Pamoja na kurahisishwa huko nakushauri upate huduma za wataalamu ili akusaidie kufanya kazi hii kwa ukamilifu wake.

Darasa ni tamu sana, naomba kujua taratibu za kufungua kampuni, na kuna aina ngapi za kampuni?
 
Karibu

QUOTE="Cowman, post: 26225725, member: 123321"]Asante mkuu hakika nimekuelewa.[/QUOTE]
 
Asante sana Nyumbalao! nimefatilia uzi hadi mwisho! nimefurahi sana! ninampango wa kufungua kampuni mwezi wa tano. hivyo nimesoma michango yote kwa umakini mukubwa! ubarikiwe wewe! na wachangiaji wote!
 
Kwa kampuni mpya ni rahisi tuu, nenda TRA sasa watakupa form za kujaza na vilevile kama ni kampuni limited ujifanyie makadirio na ujiandae kulipa au uwe na withhold ya rental kama wao wameshaipokea then unalipa watakupa tax clearance bila shida . Ila ngoja niweke cavier hapa hizo ni generality aiondoe wewe kupata ushauri kutoka kwa washauri wa mada husika maana uzi huu ni wakutoa information
Je naweza pata Tax clearance kabla ya Memorandam
 
Ni vyema ukianza vizuri toka mwanzo inakupa nafasi njema yakufanya mambo kwa ufanisi.
Karibu

Asante sana Nyumbalao! nimefatilia uzi hadi mwisho! nimefurahi sana! ninampango wa kufungua kampuni mwezi wa tano. hivyo nimesoma michango yote kwa umakini mukubwa! ubarikiwe wewe! na wachangiaji wote!
 
Huwezi kupata Tax clearance ambayo unatolewa na TRA bila kwanza kuwa umekamilisha usajili wa Kampuni Brela. Ila kama unataka ya binafsi hiyo unaweza kwenda tu TRA ukawaeleza kuwa unataka TIN yako iwe ya biashara watakukadiria na watakupa Tax clearance. Lakini kwa Company LTD ni lazima uwe umemaliza hatua zote na kupata full registration kabla ujaja TRA kwa TIN na Tax clearance kwa ajili ya kuomba leseni Halmashauri unayokaa.
Nafikiri nimejitahidi kueleza kama bado unaweza kuuliza tena.

Brela Tayari mkuu
 
Sasa kama Brela tayari unakwenda TRA mkuu. Ila umesajili nini Company ltd, Partnership au Business name maana zote hizo zina tofauti wake na ninaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kukushauri zaidi. Ila safari sasa ya kusajiliwa kuwa mlipa kodi wa biashara ndio inaanza

Brela Tayari mkuu
 
Ukiwa ndio tunamalizia siku ya mwisho ya kupeleka estimates kwa mwaka 2018 naamini utakuwa umepeleka na vile vile umelipa kuonyesha uzalendo wako. Kuna jambo moja ambalo limekutana nalo hapa mwishoni naomba nalo nilitolee ushauri ni kwamba kodi za mabango zimetoka kutoka halmashauri ya miji zimeamia TRA sasa kampuni nyingi ndogo hazijaonyesha au hazijasema kama zina mabango sasa ni vyema ukaangalia kama unayo ukalipe nayo usije pata matatizo huko siku za mbele. Nawasilisha
 
Ukiwa robo ya mwaka imeisha na hivyo makadirio yako ya mwaka huu umepeleka. Sasa ni muda muafaka wa kuangalia jinsi gani unatimiza malengo yako ya mwaka huu na vilevile kufanya masoko katika kukamilisha uwepo wako wa biashara. Nawatakieni kila la heri.
 
Katika kufuatilia kwa makini iliyoambatanishwa ni ratiba ya malipo mbalimbali ya kodi kwa kipindi ya robo wa pili wa mwaka 2018. Naomba kuwasilisha
 
Attachments

  • Ratiba ya kod.jpg
    Ratiba ya kod.jpg
    151 KB · Views: 128
Mashine za Risiti za Kielektroniki ni Nini?

Mashine za Risiti za Kielektroniki ni mashine zilizotengenezwa kwa ajili ya kutumika katika biashara kwa ajili ya kudhibiti usimamizi kwa ufanisi katika maeneo ya uchambuzi wa mauzo na mfumo wa udhibiti wa mali na ambao unafuata masharti yaliyoelezwa na sheria.

Aina za Mashine za Risiti za Kielektroniki (EFD)

Mashine ya Rejista ya Kodi ya Kielektroniki (ETR)

Mashine hii hutumiwa na wafanyabiashara wa rejareja na wale wanaouza bidhaa kwa kutembeza kwa wateja.

Printa ya Risiti ya Kielektroniki (EFP)

Mashine hii inatumiwa na vituo vya mauzo ya rejareja vilivyounganishwa kikompyuta. Imeunganishwa kwenye mtandao wa kompyuta na kuhifadhi miamala yote ya mauzo au taarifa zilizowekwa kwenye kumbukumbu zake.

Chombo cha Kutia Saini za Kielektroniki (ESD)

Kifaa kilichotengenezwa kuthibitisha kwa kusaini waraka wowote wa fedha ulioandaliwa na kompyuta kama vile ankara ya kodi. Kifaa hiki hutumia program maalum ya kompyuta kuzalisha namba maalum (Saini) ambazo huambatishwa na kuchapwa kwenye kila ankara inayotolewa na mfumo wa mtumiaji.

ANGALIZO:

Unawajibika kutoa risiti au ankara kwa kila mauzo na kutoa taarifa za mabadiliko/hitilafu zozote za mashine kwa Kamishna ndani ya saa 24. Msambazaji wa mashine atasakinisha, kupanga na kushughulikia hitilafu za mashine ndani ya saa 48.

Umenukuliwa kutoka tovuti ya TRA
 
Mkuu Nyumbalao je nikiuza kwa mkopo itanihitaji nitoe risiti?

Ikiwa jib ni ndio je ikitokea mteja akashindwa kulipa na akawa hana uwezo wakulipa (bad debts) je nitafanyaje?

Hii kodi inayokatwa katika mashine ya EFD inauhusiano gani na inayotozwa katika faida ya makampuni?
 
Yapu ukiuza unatoa risiti iwe cash au kwa mkopo ikiwa mkopo umetani bad debts baada ya kudhibitisha kweli umefuatilia unaweza kutoa kama garama za zinazoruhusiwa kutolewa (as allowable tax expenses)
Efd kwa ujumla haikati kodi unaweza kukusanya kodi ukiwa wewe ni VAT registered hapo unaweka ile sehemu ya kodi ya VAT na kuipeleka serikalini kama unavyotakiwa na sheria.
Kuna watumiaji wengi tu wa EFD ambao sio VAT registered wewe unatoa tu risiti yaani kila mfanyabiashara ambaye ana mauzo ya zaid ya Tshs 14m anatakiwa kuwa na EFD.
Hii inasaidia nini sasa ni jitihada za serikali katika kukusanya kodi wakataka kujua kuwa mauzo halali ya mtu ni kiasi gani ili wasiwe wanamuumiza katika makadirio sasa yakishajulikana haya ni rahisi mtu alete matumizi inakuwa rahisi kujua faida na hivo serikali inaweza kujipatia kodi yake ya mapato bila kuwaumiza wananchi. Ni kwa bahati mbaya tu EFD imepata jina baya ila ni kifaa muhimu sio tu kutunza kumbukumbu zako za biashara bali inakupa uhalisia wa biashara yako.

Mkuu Nyumbalao je nikiuza kwa mkopo itanihitaji nitoe risiti?

Ikiwa jib ni ndio je ikitokea mteja akashindwa kulipa na akawa hana uwezo wakulipa (bad debts) je nitafanyaje?

Hii kodi inayokatwa katika mashine ya EFD inauhusiano gani na inayotozwa katika faida ya makampuni?
 
asante kwa majib mazuri, Je mtu anayetoa risiti kwa machine ya EFD yupo subject na ile asilimia 18% incase kwamba yye siyo vat registered?

Kama jibu ni ndio nauza product ya faida 3000 yenye faida ya 300/= na nikitumia EFD 3000*18% ntatozwa 540/= je imekaaje kwa upande wa mlipa kodi?
 
Jua aina mbalimbali ya kodi hodhi (Withholding Taxes) na viwango vyake.

upload_2018-4-13_21-44-16.png
 
Hapana kama hauko VAT Registered asilimia 18 haitokei kwenye machine yako ila kama uko lazima itokee. Kwahiyo kama wewe sio utatoa tu risiti kama kawaida na itakuwa inaandika nonregistered na hayo mauzo yako yatarekodiwa.
Ahsante

Back
Top Bottom