Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Darasa ni tamu sana, naomba kujua taratibu za kufungua kampuni, na kuna aina ngapi za kampuni?
Je naweza pata Tax clearance kabla ya MemorandamKwa kampuni mpya ni rahisi tuu, nenda TRA sasa watakupa form za kujaza na vilevile kama ni kampuni limited ujifanyie makadirio na ujiandae kulipa au uwe na withhold ya rental kama wao wameshaipokea then unalipa watakupa tax clearance bila shida . Ila ngoja niweke cavier hapa hizo ni generality aiondoe wewe kupata ushauri kutoka kwa washauri wa mada husika maana uzi huu ni wakutoa information
Asante sana Nyumbalao! nimefatilia uzi hadi mwisho! nimefurahi sana! ninampango wa kufungua kampuni mwezi wa tano. hivyo nimesoma michango yote kwa umakini mukubwa! ubarikiwe wewe! na wachangiaji wote!
Je naweza pata Tax clearance kabla ya Memorandam
Asante mkuu!Ni vyema ukianza vizuri toka mwanzo inakupa nafasi njema yakufanya mambo kwa ufanisi.
Karibu
Brela Tayari mkuuHuwezi kupata Tax clearance ambayo unatolewa na TRA bila kwanza kuwa umekamilisha usajili wa Kampuni Brela. Ila kama unataka ya binafsi hiyo unaweza kwenda tu TRA ukawaeleza kuwa unataka TIN yako iwe ya biashara watakukadiria na watakupa Tax clearance. Lakini kwa Company LTD ni lazima uwe umemaliza hatua zote na kupata full registration kabla ujaja TRA kwa TIN na Tax clearance kwa ajili ya kuomba leseni Halmashauri unayokaa.
Nafikiri nimejitahidi kueleza kama bado unaweza kuuliza tena.
Karibu
Brela Tayari mkuu
Mkuu Nyumbalao je nikiuza kwa mkopo itanihitaji nitoe risiti?Mashine za Risiti za Kielektroniki ni Nini?
Mashine za Risiti za Kielektroniki ni mashine zilizotengenezwa kwa ajili ya kutumika katika biashara kwa ajili ya kudhibiti usimamizi kwa ufanisi katika maeneo ya uchambuzi wa mauzo na mfumo wa udhibiti wa mali na ambao unafuata masharti yaliyoelezwa na sheria.
Aina za Mashine za Risiti za Kielektroniki (EFD)
Mashine ya Rejista ya Kodi ya Kielektroniki (ETR)
Mashine hii hutumiwa na wafanyabiashara wa rejareja na wale wanaouza bidhaa kwa kutembeza kwa wateja.
Printa ya Risiti ya Kielektroniki (EFP)
Mashine hii inatumiwa na vituo vya mauzo ya rejareja vilivyounganishwa kikompyuta. Imeunganishwa kwenye mtandao wa kompyuta na kuhifadhi miamala yote ya mauzo au taarifa zilizowekwa kwenye kumbukumbu zake.
Chombo cha Kutia Saini za Kielektroniki (ESD)
Kifaa kilichotengenezwa kuthibitisha kwa kusaini waraka wowote wa fedha ulioandaliwa na kompyuta kama vile ankara ya kodi. Kifaa hiki hutumia program maalum ya kompyuta kuzalisha namba maalum (Saini) ambazo huambatishwa na kuchapwa kwenye kila ankara inayotolewa na mfumo wa mtumiaji.
ANGALIZO:
Unawajibika kutoa risiti au ankara kwa kila mauzo na kutoa taarifa za mabadiliko/hitilafu zozote za mashine kwa Kamishna ndani ya saa 24. Msambazaji wa mashine atasakinisha, kupanga na kushughulikia hitilafu za mashine ndani ya saa 48.
Umenukuliwa kutoka tovuti ya TRA
Mkuu Nyumbalao je nikiuza kwa mkopo itanihitaji nitoe risiti?
Ikiwa jib ni ndio je ikitokea mteja akashindwa kulipa na akawa hana uwezo wakulipa (bad debts) je nitafanyaje?
Hii kodi inayokatwa katika mashine ya EFD inauhusiano gani na inayotozwa katika faida ya makampuni?
asante kwa majib mazuri, Je mtu anayetoa risiti kwa machine ya EFD yupo subject na ile asilimia 18% incase kwamba yye siyo vat registered?
Kama jibu ni ndio nauza product ya faida 3000 yenye faida ya 300/= na nikitumia EFD 3000*18% ntatozwa 540/= je imekaaje kwa upande wa mlipa kodi?