Hongera wewe ni mjasiriamali kweli kweli naonba unatoka duka dogo la nguo mpaka, Ujenzi halafu na kuimports.
Kwa swala la duka dogo hapa huwa nalo ni tata lakini ngoja ni dadafue kama hivi. Kwanza ni vizuri hata kwa udogo huo hukakikishe umesajili jina la biashara yako Brela au ukiona hiyo sio issue unaenda kubadilisha TIN yako kuwa ya biashara ambapo sasa utakuwa unakadiriwa na TRA kila mwanzo wa mwaka na kulipa kodi ya mapato kila robo mwaka. Sasa mapato yako yakizidi million 14 kwa mwaka unatakiwa kununua EFD machine nakuanza kutoa risiti zinazopeleka taarifa zako TRA na kukusaidia kutunza kumbumbuu zako za biashara. Kama nilivyokwisha kusema sijui kwanini hiki kifaa mwanzoni kilipata jina baya kiasi bado inaonekana kama ni mzigo kwa wafanyabiashara nyingi ila ikiweza kuitumia hii mashine vizuri kuibiwa kwako inaweza kuwa ngumu sana na unakuwa na taarifa sahihi juu ya biashara yako. Ukifika level ya millionn 19 kwa mwaka unatakiwa kutengenezewa hesabu na mtaalamu wa mahesabu kwa hesabu zako kukaguliwa huduma hii wafanyabiashara wetu nao wengi wamekuwa wanaikimbia lakini kila mmiliki wa biashara mkubwa anajua umuhimu wa Auditor katika shughuli yake. Hili ni jicho la tatu kwenye mfumo wako linatakiwa kuangalia mambo mengi na hivyo hivyo kukushauri jinsi ya kufanya biashara yako vyema.
Tatu sasa ukiwa na mauzo zaidi ya millioni mia kwa mwaka unatakiwa kusajiliwa kwenye VAT na hivyo kutoa risiti zinazokuwa na VAT na manunuzi yako yenye VAT yatapungua na hivyo kufanya marudisho kila mwezi (Monthly returns) kwenye mfumo wa VAT na hivyo kuanza kuwa mfanyabiashara mkubwa ukianza vyema toka mwanzo kufika huku ni rahisia na kwa haraka.
Kwenye import tax nchi yetu iko vizuri sana kuliko watu wengi ambavyo wangetaka kukiri vitu vyote unavyotaka kuagiza viko wazi kwenye documents ya page 497 angalia hiyo link hapo
https://www.tra.go.tz/images/EAC-CET-2017.pdf na kama haviko unaweza kwenda na invoice yako pale strong room wakakutafutia au hata watu waclearing and forward walio na uelewa nzuri wanaweza kukusaidia sana. Na ndio maana hakuna mtu anaweza kuimport vitu kwa sheria zetu bila kutumia hawa clearing agent ni watu muhimu. Kwenye garama hasa ni katika manunuzi na usafirishaji ndiko maeneo unayoweza kupunguza . Ninao wataalamu kwenye idara hizo za imports ambao naamini wameiva ukitaka nitakupa mawasiliano yao.
Kufungua kampuni nayo siku hizi imerahishwa kiasi fulani ila kitu cha muhimu sana unachotakiwa kuwa nacho ni kitambulisho cha taifa (NIDA ID) ukiwa na hicho na TIN number unakuwa mwazo mzuri haitakiwi kuzidi siku kumi. Brela wameboresha miundo mbinu yao.
Naamini nimeweza kukujibu kwa kina kama kuna mahali ujaelewa niko tayari kuendelea kudadavua zaidi.
Alamsiki