Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

@Nyumbalao

Mkuuhivi kama unafungua Duka la kuuza vifaa vya ujenzi au duka la kuuza nguo vitu gani ni muhimu kuzingatia Kwa mujibu wa sheria?

Inachukua muda gani kusajiri kampuni na kupata documents zote kupitia kampuni yenuna gharama zenu zikoje Kwa hii huduma?

Pia ningependa kuuliza kama una utaalamu kwenye import tax, duty, other costs of importation and how to minimise them.
 
Aisee nimesoma tax pale chuo cha kodi.. Mkuu uko dip sana.. Nmependa unavyochaichambua Ita, VAT act na taa.. ongera sna
 
Mkuu nna mpango wa kufungua kampuni ya mikopo midogo microcrédit. Na nnapanga kufikia mwez wa sita ianze oparation msaada pls pakuanzia, na hii inakuwa aina ipi ya kampuni nk nk. Informations zozote za muhimu naomba tafadhali
 
Hongera wewe ni mjasiriamali kweli kweli naonba unatoka duka dogo la nguo mpaka, Ujenzi halafu na kuimports.
Kwa swala la duka dogo hapa huwa nalo ni tata lakini ngoja ni dadafue kama hivi. Kwanza ni vizuri hata kwa udogo huo hukakikishe umesajili jina la biashara yako Brela au ukiona hiyo sio issue unaenda kubadilisha TIN yako kuwa ya biashara ambapo sasa utakuwa unakadiriwa na TRA kila mwanzo wa mwaka na kulipa kodi ya mapato kila robo mwaka. Sasa mapato yako yakizidi million 14 kwa mwaka unatakiwa kununua EFD machine nakuanza kutoa risiti zinazopeleka taarifa zako TRA na kukusaidia kutunza kumbumbuu zako za biashara. Kama nilivyokwisha kusema sijui kwanini hiki kifaa mwanzoni kilipata jina baya kiasi bado inaonekana kama ni mzigo kwa wafanyabiashara nyingi ila ikiweza kuitumia hii mashine vizuri kuibiwa kwako inaweza kuwa ngumu sana na unakuwa na taarifa sahihi juu ya biashara yako. Ukifika level ya millionn 19 kwa mwaka unatakiwa kutengenezewa hesabu na mtaalamu wa mahesabu kwa hesabu zako kukaguliwa huduma hii wafanyabiashara wetu nao wengi wamekuwa wanaikimbia lakini kila mmiliki wa biashara mkubwa anajua umuhimu wa Auditor katika shughuli yake. Hili ni jicho la tatu kwenye mfumo wako linatakiwa kuangalia mambo mengi na hivyo hivyo kukushauri jinsi ya kufanya biashara yako vyema.
Tatu sasa ukiwa na mauzo zaidi ya millioni mia kwa mwaka unatakiwa kusajiliwa kwenye VAT na hivyo kutoa risiti zinazokuwa na VAT na manunuzi yako yenye VAT yatapungua na hivyo kufanya marudisho kila mwezi (Monthly returns) kwenye mfumo wa VAT na hivyo kuanza kuwa mfanyabiashara mkubwa ukianza vyema toka mwanzo kufika huku ni rahisia na kwa haraka.

Kwenye import tax nchi yetu iko vizuri sana kuliko watu wengi ambavyo wangetaka kukiri vitu vyote unavyotaka kuagiza viko wazi kwenye documents ya page 497 angalia hiyo link hapo https://www.tra.go.tz/images/EAC-CET-2017.pdf na kama haviko unaweza kwenda na invoice yako pale strong room wakakutafutia au hata watu waclearing and forward walio na uelewa nzuri wanaweza kukusaidia sana. Na ndio maana hakuna mtu anaweza kuimport vitu kwa sheria zetu bila kutumia hawa clearing agent ni watu muhimu. Kwenye garama hasa ni katika manunuzi na usafirishaji ndiko maeneo unayoweza kupunguza . Ninao wataalamu kwenye idara hizo za imports ambao naamini wameiva ukitaka nitakupa mawasiliano yao.

Kufungua kampuni nayo siku hizi imerahishwa kiasi fulani ila kitu cha muhimu sana unachotakiwa kuwa nacho ni kitambulisho cha taifa (NIDA ID) ukiwa na hicho na TIN number unakuwa mwazo mzuri haitakiwi kuzidi siku kumi. Brela wameboresha miundo mbinu yao.
Naamini nimeweza kukujibu kwa kina kama kuna mahali ujaelewa niko tayari kuendelea kudadavua zaidi.
Alamsiki

@Nyumbalao

Mkuuhivi kama unafungua Duka /dogo la flem la kuuza vifaa vya ujenzi au duka la kuuza nguo vitu gani ni muhimu kuzingatia Kwa mujibu wa sheria?

Inachukua muda gani kusajiri kampuni na kupata documents zote kupitia kampuni yenuna gharama zenu zikoje Kwa hii huduma?

Pia ningependa kuuliza kama una utaalamu kwenye import tax, duty, other costs of importation and how to minimise them.
 
Nakushukuru ni kwa neema tu, nimeamua kushare kile ninachokijua najua wako wengi wazuri zaidi ila kila nichokijua nitakitumia kuelimisha jamii yangu kwa manufaa ya taifa hili.

Aisee nimesoma tax pale chuo cha kodi.. Mkuu uko dip sana.. Nmependa unavyochaichambua Ita, VAT act na taa.. ongera sna
 
Salama mkuu kwa habari ya ufunguzi wa kampuni masharti ya post [HASHTAG]#227[/HASHTAG] hapo juu ni ya lazima ndio basic. Na hii ya kwako leseni yako inatolewa na wizara ya viwanda na biashara ni Category A License. Brela wameboresha kila kitu kinafanyika online.

Mkuu nna mpango wa kufungua kampuni ya mikopo midogo microcrédit. Na nnapanga kufikia mwez wa sita ianze oparation msaada pls pakuanzia, na hii inakuwa aina ipi ya kampuni nk nk. Informations zozote za muhimu naomba tafadhali
 
Shukrani Mkuu, hakika unaitendea haki taaluma yako. Nitakutafuta nikiwa tayari.

Hongera wewe ni mjasiriamali kweli kweli naonba unatoka duka dogo la nguo mpaka, Ujenzi halafu na kuimports.
Kwa swala la duka dogo hapa huwa nalo ni tata lakini ngoja ni dadafue kama hivi. Kwanza ni vizuri hata kwa udogo huo hukakikishe umesajili jina la biashara yako Brela au ukiona hiyo sio issue unaenda kubadilisha TIN yako kuwa ya biashara ambapo sasa utakuwa unakadiriwa na TRA kila mwanzo wa mwaka na kulipa kodi ya mapato kila robo mwaka. Sasa mapato yako yakizidi million 14 kwa mwaka unatakiwa kununua EFD machine nakuanza kutoa risiti zinazopeleka taarifa zako TRA na kukusaidia kutunza kumbumbuu zako za biashara. Kama nilivyokwisha kusema sijui kwanini hiki kifaa mwanzoni kilipata jina baya kiasi bado inaonekana kama ni mzigo kwa wafanyabiashara nyingi ila ikiweza kuitumia hii mashine vizuri kuibiwa kwako inaweza kuwa ngumu sana na unakuwa na taarifa sahihi juu ya biashara yako. Ukifika level ya millionn 19 kwa mwaka unatakiwa kutengenezewa hesabu na mtaalamu wa mahesabu kwa hesabu zako kukaguliwa huduma hii wafanyabiashara wetu nao wengi wamekuwa wanaikimbia lakini kila mmiliki wa biashara mkubwa anajua umuhimu wa Auditor katika shughuli yake. Hili ni jicho la tatu kwenye mfumo wako linatakiwa kuangalia mambo mengi na hivyo hivyo kukushauri jinsi ya kufanya biashara yako vyema.
Tatu sasa ukiwa na mauzo zaidi ya millioni mia kwa mwaka unatakiwa kusajiliwa kwenye VAT na hivyo kutoa risiti zinazokuwa na VAT na manunuzi yako yenye VAT yatapungua na hivyo kufanya marudisho kila mwezi (Monthly returns) kwenye mfumo wa VAT na hivyo kuanza kuwa mfanyabiashara mkubwa ukianza vyema toka mwanzo kufika huku ni rahisia na kwa haraka.

Kwenye import tax nchi yetu iko vizuri sana kuliko watu wengi ambavyo wangetaka kukiri vitu vyote unavyotaka kuagiza viko wazi kwenye documents ya page 497 angalia hiyo link hapo https://www.tra.go.tz/images/EAC-CET-2017.pdf na kama haviko unaweza kwenda na invoice yako pale strong room wakakutafutia au hata watu waclearing and forward walio na uelewa nzuri wanaweza kukusaidia sana. Na ndio maana hakuna mtu anaweza kuimport vitu kwa sheria zetu bila kutumia hawa clearing agent ni watu muhimu. Kwenye garama hasa ni katika manunuzi na usafirishaji ndiko maeneo unayoweza kupunguza . Ninao wataalamu kwenye idara hizo za imports ambao naamini wameiva ukitaka nitakupa mawasiliano yao.

Kufungua kampuni nayo siku hizi imerahishwa kiasi fulani ila kitu cha muhimu sana unachotakiwa kuwa nacho ni kitambulisho cha taifa (NIDA ID) ukiwa na hicho na TIN number unakuwa mwazo mzuri haitakiwi kuzidi siku kumi. Brela wameboresha miundo mbinu yao.
Naamini nimeweza kukujibu kwa kina kama kuna mahali ujaelewa niko tayari kuendelea kudadavua zaidi.
Alamsiki
 
Habari za asubuhi, kwa mwenye kampuni binafsi sheria za kodi zimelenga kuwasaidia sana, ila watu wengi hawajui kwa kuwa wao ni watengeneza mali sheria za kodi zimetungwa ili ziwawekee mazingira mazuri wao kutengeneza mali maana utengenezaji wa mali ndio unasaidia taifa kusonga mbele. Nawasihi mtumie huduma za ushauri hasa za kufanya mipango ya kodi kwa ajili ya kampuni yako (Tax Planning) ni kitu kizuri sana itakusaidia kulipa kodi zote zinazokuangukia lakini vilevile itakuza biashara yako. Mfano unakuta mtu anakampuni yeye na mkewe lakini wanamiliki magari ambayo wanatumia kwenye shughuli za uzalishali mali kwa kampuni waliyonayo sasa kwanini msihamishe magari hayo kwenye kampuni ukapata kwa asilimia kubwa uchakavu wa kila mwaka (depreciations), matengenezo ya gari na mafuta ikawa ni garama halali kabisa za kampuni. Kuna mambo kadhaa ya kuangalia pata ushauri mahususi kutokana na biashara yako.
 
Kwa wale walio ajiri watu kwenye biashara zao na unalipa PAYE na SDL nakuomba uzingatie vilevile kujiorodhesha WCF ni asilimia moja tu 1% inaongezeka kwenye payroll yako. Ni sheria sahihi ya kujali wafanyakazi wako shime tufuate sheria stahiki.
 
Bado miezi miwili mawasilisho ya mahesabu ya mwisho wa mwaka 2017(Annual Financial Accounts) ambazo zimekaguliwa zinatakiwa kuwasilishwa TRA. Wenye makampuni anzeni kufanyia kazi hilo mara nyingi unakuta watu wanasubiri mpaka siku za mwisho natoa wito kufanyia kazi mapema iwezekanavyo.
 
SDL utalipa tu mpaka pale utakapokuwa na wafanyakazi wanne na zaidi hayo ndio matakwa ya sheria. Kwahiyo kama mko wawili tu hamna haya ya SDL. Na rate ya mwaka huu ni 4.5% Ahsante
Mimi nalipishwa SDL za vibarua je hii ni halali?
 
Brela ndugu hao ndio wasajili. TCCIA wanaweza kukupa ushauri jinsi ya kufanikisha lakini ni vyema utafute lawyer aliyebobea kwenye hii kitu inakuwa rahisi.
Ahsante
Hii thread kwanini nilichelewa kuiona huenda mambo mengine yasinge kwama
 
Pole ila wakati mwingine madini yanaweza kuwa mbali ukachukua muda kufikia lakini ukiendelea utafika na kufanikiwa
Hii thread kwanini nilichelewa kuiona huenda mambo mengine yasinge kwama
 
Kodi ya mapato kikawaida huwa unakadiriwa kutoka kwenye faida au mapato ukitoa matumizi. Na kitaratibu kampuni huwa hakadiriwi kodi ila yenyewe ndio inajikadiria kutokana na mahesabu inayotegemea kupata mwaka husika. Katika kanuni za kawaida ukianza biashara na mtaji mkubwa inategemewa utapata faida kubwa na hivyo kulipa kodi kubwa. Naamini hapo nitakuwa nimejieleza sawia
Mkuu, ivi kama nataka kufungua kampuni ya kilimo (kulima mboga mboga na kufuga) taratibu zikoje? Kodi je?

Naomba mawazo tafadhali!!
 
Taratibu za kufungua kampuni ni sawa na nyinginezo unaweza kusoma uzi mzuri wa lembu huu hapa Hatua 10 Rahisi za Kusajili Jina la Biashara Kupitia Website ya BRELA
Kwa maswala ya kilimo moja ya kitu kikubwa kwenye kodi chenye nafuu ni kwamba dhamani ya jengo linatolewa lote kwenye mwaka wa kwanza wa kuanza kazi hivo mara nyingi uwekezaji mkubwa unaweza usilipe kodi ya mapato kwa miaka hiyo ya mwanzo mwanzo. Ila baada ni kama biashara nyingine. Ila kodi kama SDL zitahusika. Nakupeleka PAYE ambayo siyo yako wewe unakuwa wakala baada ya wafanyakazi kukatwa. Naomba niweke angalizo ni vyema kutafuta mtaalamu akaangalia swala lako kwa undani ili kutoa suluhisho sahihi maelezo haya ni kwa elimu tu.
ahsante

Mkuu, ivi kama nataka kufungua kampuni ya kilimo (kulima mboga mboga na kufuga) taratibu zikoje? Kodi je?

Naomba mawazo tafadhali!!
 
Kwa waliona makampuni na majina ya biashara ni muda wa kuhakikisha ume update taarifa zako brela. Maana usichelewe kufanya hivyo ukawa siku unatakiwa kutafuta mkopo Benki wakawa wanashidwa kupata taarifa zako na hivyo kukunyima mkopo.
 
Back
Top Bottom