Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Nimeona list iliyotolewa na Brela makampuni yaliyo update taarifa zao ni machache sana nawashauri wadau update taarifa zako Brela sio kitu kigumu na kama inakuletea shida unaweza kuwasiliana nami tunaweza kukusaidia
 
Siku zinakaribia muda wakulipa kodi ya robo ya pili kama ulifanya makadirio ni mwezi huu.
Kubwa lao ni kwamba kwa wale wanaopeleka audited financial zinatakiwa kwenda TRA by tarehe 30 June tafadhali wahi. Ahsante
 
Habari mkuu nyumba lao

Hivi naweza kufungua kampuni ambayo itakuwa inamiliki maduka ya jumla mikoa na wilaya tofauti tofauti?

Kama jibu ni ndiyo, kwenye kodi nalipa kama kampuni au kwa mauzo ya duka moja moja?
 
Mkuu naomba kuuliza...

Mfano, marekani kuna kampuni inajiita ABC softwares... Ila na mimi nataka nifungue kampun inayo itwa ABC marketing hapa tanzania.

Je kuna shida yeyote kama nikitumia ilo jina??
 
Ndiyo unaweza, kwenye swala la kodi utalipa kwenye kampuni maana inatengenezwa consolidated accounts hii ni kwa kodi ya mapato. Na kodi nyingine zote za mwezi kwa mwezi kama SDL, PAYE, VAT returns na Withholdings inaweza kulipwa kutoka head office

Habari mkuu nyumba lao

Hivi naweza kufungua kampuni ambayo itakuwa inamiliki maduka ya jumla mikoa na wilaya tofauti tofauti?

Kama jibu ni ndiyo, kwenye kodi nalipa kama kampuni au kwa mauzo ya duka moja moja?
 
Kaka hiyo aina shida, Maana kila nchi ina utaratibu wake. Ila Brela nao kuna majina kutokana na umaarufu wake wanaweza wasikuruhusu kusajili kwa kutumia jina hilo hilo ila unaweza kubadilisha vitu vichache nayo ikawa sawa.

Mkuu naomba kuuliza...

Mfano, marekani kuna kampuni inajiita ABC softwares... Ila na mimi nataka nifungue kampun inayo itwa ABC marketing hapa tanzania.

Je kuna shida yeyote kama nikitumia ilo jina??
 
Kaka hiyo aina shida, Maana kila nchi ina utaratibu wake. Ila Brela nao kuna majina kutokana na umaarufu wake wanaweza wasikuruhusu kusajili kwa kutumia jina hilo hilo ila unaweza kubadilisha vitu vichache nayo ikawa sawa.
Mkuu! Naweza kukucheki PM?
 
Hii ya returns za Brela unaenda unajaza fomu au ni online kama wafanyavyo TRA?
 
Hapo napangojea

Kampuni ya kilimo ni kama kampuni nyingine tu. Tofauti kubwa ni kwamba investment mfano wa jengo inapewa uchakavu (Depreciation) ya 100% kwa mwaka wakwanza wakati nyingine ni asilimia 4% ambayo inaweza kukufanya usiwe na kodi ya mapato kwa miaka ya mwanzo ila baadaye utalipa. Kwenye kodi nyingine kama SDL utalipa tu kama unawafanyakazi 4+.
 
Aisee naomba kujua ukiwa na TIN binafsi na unataka kufungua kampuni na umeshamaliza kusajili Brela hio kampuni, Je ile TIN yko binafs ndio itatumika au inabd Ukaazie/kupatiwa nyingine TRA?
 
Aisee naomba kujua ukiwa na TIN binafsi na unataka kufungua kampuni na umeshamaliza kusajili Brela hio kampuni, Je ile TIN yko binafs ndio itatumika au inabd Ukaazie/kupatiwa nyingine TRA?
Utapewa TIN mpya ya kampuni ambapo kwa mfumo wa sasa No ya usajili ya cheti cha kampuni inakuwa ndiyo no ya TIN. Lkn ili upate TIN ni lazima upeleke TIN zenu wanahisa ambapo mtajaza fomu za kuonyesha TIN zenu binafsi
 
Ukisajili business name, je TIN unatumia ya individual, yaani ya mtu mwenyewe biashara au watatoa nyingine?
 
Ukisajili business name, je TIN unatumia ya individual, yaani ya mtu mwenyewe biashara au watatoa nyingine?
Utatumia TIN ile ile ya kwako "individual" lkn kama na kama tu majina ya biashara na TIN ni yenye kuwa sawa. Kama kuna kasoro ya majina wataangalia kwa mfano "standard ID ya usajili kwa sasa ni National ID" hivyo utalazimika kufanya marekebisho ya jina TRA ili yaendane na lililosajiliwa BRELA kwa kutumia "national id". Hivyo ukishawasilisha ushahidi wa vyeti vya usajili wa jina kutoka BRELA, TIN itafanyiwa "ammendment" na kusoma jina lako pamoja na jina la biashara. Mfano JOHN ISAACK MENSAH T/A IPILIMO CONSULTANT
 
Kwa waliona makampuni na majina ya biashara ni muda wa kuhakikisha ume update taarifa zako brela. Maana usichelewe kufanya hivyo ukawa siku unatakiwa kutafuta mkopo Benki wakawa wanashidwa kupata taarifa zako na hivyo kukunyima mkopo.
Shida ya wengi ni returns za nyuma hazijafanywa, pia hawana hesabu zilizo kaguliwa, sababu system inataka hizo nyaraka ndipo uupdate. au iko kivingine?
 
Utatumia TIN ile ile ya kwako "individual" lkn kama na kama tu majina ya biashara na TIN ni yenye kuwa sawa. Kama kuna kasoro ya majina wataangalia kwa mfano "standard ID ya usajili kwa sasa ni National ID" hivyo utalazimika kufanya marekebisho ya jina TRA ili yaendane na lililosajiliwa BRELA kwa kutumia "national id". Hivyo ukishawasilisha ushahidi wa vyeti vya usajili wa jina kutoka BRELA, TIN itafanyiwa "ammendment" na kusoma jina lako pamoja na jina la biashara. Mfano JOHN ISAACK MENSAH T/A IPILIMO CONSULTANT
SAFI SANA, KUNA MTU NILIMWELEKEZA THE SAME ILA MBISHI SANA....Very clear
 
Shida ya wengi ni returns za nyuma hazijafanywa, pia hawana hesabu zilizo kaguliwa, sababu system inataka hizo nyaraka ndipo uupdate. au iko kivingine?
Ni kweli kabisa
Kwa kuongezea vlvl unakuta wanashea/wakurugenzi hawana TIN na vitambulisho vya Taifa. Utashangaa mkurugenzi hana TIN na kampuni ilipata vipi TIN ni kutokana na kutumia vishoka ktk usajili upande wa TRA, matokeo yk kampuni nyingi zilizopata TIN kwa dizaini hii hata nini kwa upande wa TRA kama kampuni wanawajibika vp hawajui. Hakika JF kupitia uzi huu umesaidia sana kwa mfuatiliaji
 
Mkuu Nyumbalao nakushukuru sana kwa ushauri na muda wako kutuelimisha masuala haya ya kodi na jinsi ya kuendesha kampuni kwa ujumla. Nimefarijika na pia nimepata ABC za namna gani naweza kuanza na kuisimamia kampuni, binafsi nimejitahidi kusoma comment zote ili angalau nipate na experience kidogo kutoka kwa wadau ambao kwa namna moja au nyingine walikumbana na changamoto za kodi.
Mambo ambayo binafsi nimeyapata kutoka kwako ni suala zima la kuwashirikisha wataalum wa fani husika pasi na kufanya mambo yote mwenyewe hata kama ni gharama, japo nimeona wadau wameelekeza kuhusu kuwakodi wa taalamu hata kwa part time. Kingine ni kuhusu kuzifuata sheria na kanuna za kuendesha biashara nashukuru sana na nimesubscribe ili niendelee kupata nondo zaidi.
 
Back
Top Bottom