Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
halafu kitu kibaya ni kupenda mali za jirani yako ila za kwako usipozipenda nani atazipenda?Wamefanyaje wachaga? Au marathon ya kutafuta mali imekukimbiza kwao?
Acha kupalilia umaskini wewe. Yaani unatakiwa kula vizuri, kulala pazuri, kusomesha watoto vizuri, kumtumikia Mungu vizuri kwa mali zako halafu ulete uzembe wa kusema ati hampendi mali😅😅
Mungu alituumba tutawale buana! Wewe unafikiria kumtawala mke tuu.... sasa bila mali unatawaaje na unatawala nini
Kuongezeka ni sifa ya Mungu na baraka zake kwetu wanadamu. Yeye muumba mwenyewe ametaka tuongezeke kwa mali na na baraka na kuvitawala sasa tunaanzaje kuanza kuacha kupenda mali?
Kupenda mali sio kosa kosa ni kupenda mali zaidi ya tunavyompenda Mungu na zaidi tunavyopendana
Mhubiri 5:19
"Kama Mungu anampa mtu utajiri na mali na kumjalia fursa ya kufurahia hayo, basi binadamu ashukuru na avifaidi hivyo alivyojipatia kwa jasho lake. Hiyo ni zawadi kutoka kwa Mungu."
Mwenyewe aliyetuumba anataka tuwe na mali ili tuweze kumtumikia yeye na kutatua changamoto zetu kwa sifa na utukufu wake. Sasa wewe chukia mali wakati aliyekuumba anakudai mali zake😅😅
Methali 3:9-10
"Mheshimu Mwenyezi-Mungu kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Hapo ghala zako zitajaa nafaka, na mapipa yako yatafurika divai mpya."
Mwanzo 1:28
"Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.”
Kumbukumbu la torati 8:8
"Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo."
Hakuna aliyeitwa na Mungu akawa maskini ila utajiri wao huakuja bila bidii na haukuwakosanisha na Mungu
Ibrahimu alikua na mali nyingi, Daudi alikua na mali, Yakobo alikua alikua na mali,......
Hebu rejea Ndoa ya Jeff Boaz na ya nani huyu mmiliki wa microsoft halafu utapata jibu kupenda mali kwa wanawake kumeathiri vipo upendo kati yaoNdivyo ili Matola bila UTII wa mke kwa mume; na bila UPENDO wa mume kwa mke hakuna mahusiano
Sasa sijui mwanaume kama anaogopa kutafuta mali atamlishaje na kumvika mke wake
Waefeso 5:22-33
Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake. Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote.
Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake. Alifanya hivyo ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji, kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safi kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo. Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. ( Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunza kanisa, maana sisi ni viungo vya mwili wake).
“Kwa sababu hiyo, mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja.” Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na kanisa lake. Lakini yanawahusu nyinyi pia: Kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.
utii unakuja panapo upendo,,,hiyo ni automatic,,,usijetegemea no upendo utii upatikaneWaefeso 5:22-33
Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake. Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote.
Yesu alimwambije Zakayo
utii unakuja panapo upendo,,,hiyo ni automatic,,,usijetegemea no upendo utii upatikane
utakaa sana hapo
Haya twende pole pole kuna sehemu kwenye huo uzi pameandikwa watu sisifanye kazi/wasitafute maliZakayo alikua mkuu wa watoza ushuri lakini hakuwa anatoza ushuru kwa haki. Alikua mla rushwa na aliwatendea watu matendo ya kinyang'anyi halafu hapohapo akawa anautamani ufalme wa Mungu. Ndipo Yesu akauona moyo wake na matendo yake nguvu ya Mungu ikamuingia zakayo na kuamua kushinda nyumbani. Hapo ndipo zakayo alipojitafakari na kuamua kurudisha mali alizoiba
Na wewe Yesu aingie moyoni kwako akashinde nyumbani kwako ukajitafakari ni mambo mangapi umeyafanya kwa udhaifu na uzembe hata ukashindwa kufanya kazi za Mungu sababu ya kukosa mali ya kufanyia hizo kazi. Ukasimame na kutafuta mali uweze kujikimu wewe na mkeo na familia, uweze kutoa sadaka safi, zaka, na malimbuko
Luka 19:1-9
Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa akipita katika njia za mji huo. Palikuwa na mtu mmoja huko mjini aitwaye Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watozaushuru, na pia mtu tajiri. Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu. Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo. Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.” Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha. Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunungunika wakisema, “Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi.” Lakini Zakayo akasimama, akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyanganya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.” Yesu akamwambia, “Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu.
Wakati sisi tunazungumzia jinsi mali inavyozorotesha mahusiano ww unatuambia habari za mali na kumwabudu Mungu Dah ndio maana division zero haziishii
Hebu rejea Ndoa ya Jeff Boaz na ya nani huyu mmiliki wa microsoft halafu utapata jibu kupenda mali kwa wanawake kumeathiri vipo upendo kati yao
Ngoja nikufafanulie kuhusu huko kupenda mali kunakozungumziwaNa upendo huo ndio mume ametakiwa amlishe na kumvisha mke wake. Sasa utamvika na kumtunzaje kama hutafuti mali
Waefeso 5: 28-29
Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali HUULISHA na KUUTUNZA, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
Mama D unatema madini..thank you sana. Wakati mwingine kuchukia Hela ni dalili za uvivu..hahahahaaaZakayo alikua mkuu wa watoza ushuri lakini hakuwa anatoza ushuru kwa haki. Alikua mla rushwa na aliwatendea watu matendo ya kinyang'anyi halafu hapohapo akawa anautamani ufalme wa Mungu. Ndipo Yesu akauona moyo wake na matendo yake nguvu ya Mungu ikamuingia zakayo na kuamua kushinda nyumbani. Hapo ndipo zakayo alipojitafakari na kuamua kurudisha mali alizoiba
Na wewe Yesu aingie moyoni kwako akashinde nyumbani kwako ukajitafakari ni mambo mangapi umeyafanya kwa udhaifu na uzembe hata ukashindwa kufanya kazi za Mungu sababu ya kukosa mali ya kufanyia hizo kazi. Ukasimame na kutafuta mali uweze kujikimu wewe na mkeo na familia, uweze kutoa sadaka safi, zaka, na malimbuko
Luka 19:1-9
Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa akipita katika njia za mji huo. Palikuwa na mtu mmoja huko mjini aitwaye Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watozaushuru, na pia mtu tajiri. Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu. Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo. Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.” Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha. Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunungunika wakisema, “Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi.” Lakini Zakayo akasimama, akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyanganya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.” Yesu akamwambia, “Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu.
Hahahah mmeshindwa kuelewana tu, the appropriate statement ilikuwa “epukeni tamaa”