Mambo muhimu ya mahusiano ya kufahamu kabla ya ndoa

halafu kitu kibaya ni kupenda mali za jirani yako ila za kwako usipozipenda nani atazipenda?

kupenda kitu kinakupa thamani ya kukitunza zaidi.

Binafsi napenda jaman
big up Mama D
 
Hebu rejea Ndoa ya Jeff Boaz na ya nani huyu mmiliki wa microsoft halafu utapata jibu kupenda mali kwa wanawake kumeathiri vipo upendo kati yao
 
utii unakuja panapo upendo,,,hiyo ni automatic,,,usijetegemea no upendo utii upatikane

utakaa sana hapo
 
Namba 15 iwe namba moja tafadhali.

Ukweli ni kwamba, kwenye ndoa lazima kila mmoja wenu akubali kubadilika. Kwa yale yanayofaa na yale yasiofaa pia.

Unatakiwa kujua kuwa, ndoa ni kama Ujauzito uliokusudiwa. Mwanzoni kila mmoja huwa na furaha.

Inafata kipindi kigumu cha kuteseka. Lazima ukubali mabadiliko ya mwenzako, kama ambavyo mjamzito analazimika kukubali mabadiliko ya mwili wake.

Kisha, huja kipindi cha Uchungu zaidi. Mwanamke akaribiapo kujifungua, uchungu humpata. Ule usio na kifani. Ndivyo katika ndoa, unafikia kipindi una tamani kabisa kujitoa. Lakini uvumilivu huleta matunda.

Alafu inafikia kipindi cha kuponya vidonda. Yale yote yaliyokuletea vidonda huanza kupotea.

Kisha, furaha hutamalaki ndani ya familia.

Usipokubaliana na mabadiliko ya lazima, ndoa itakushinda.

Usiingie katika ndoa kutafuta unafuu wa jambo lolote. Bali ingia kwa kuwa umeshajitoa kuingia katika ndoa na kuahidi kubadilika.

Wengine huingia kupata unafuu wa maisha. Wengine huingia kupata unafuu wa majukumu. Wengine huingia kupata unafuu wa upweke. Usiingie katika ndoa ili kupata unafuu wa maneno ya waja. Na kadhalika, na kadhalika.

Hao wote, huishia kuiona ndoa chungu.

Mungu awasimamie nyote.
 
Yesu alimwambije Zakayo

Zakayo alikua mkuu wa watoza ushuri lakini hakuwa anatoza ushuru kwa haki. Alikua mla rushwa na aliwatendea watu matendo ya kinyang'anyi halafu hapohapo akawa anautamani ufalme wa Mungu. Ndipo Yesu akauona moyo wake na matendo yake nguvu ya Mungu ikamuingia zakayo na kuamua kushinda nyumbani. Hapo ndipo zakayo alipojitafakari na kuamua kurudisha mali alizoiba

Na wewe Yesu aingie moyoni kwako akashinde nyumbani kwako ukajitafakari ni mambo mangapi umeyafanya kwa udhaifu na uzembe hata ukashindwa kufanya kazi za Mungu sababu ya kukosa mali ya kufanyia hizo kazi. Ukasimame na kutafuta mali uweze kujikimu wewe na mkeo na familia, uweze kutoa sadaka safi, zaka, na malimbuko


Luka 19:1-9
Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa akipita katika njia za mji huo. Palikuwa na mtu mmoja huko mjini aitwaye Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watozaushuru, na pia mtu tajiri. Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu. Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo. Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.” Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha. Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunungunika wakisema, “Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi.” Lakini Zakayo akasimama, akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyanganya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.” Yesu akamwambia, “Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu.
 
utii unakuja panapo upendo,,,hiyo ni automatic,,,usijetegemea no upendo utii upatikane

utakaa sana hapo


Na upendo huo ndio mume ametakiwa amlishe na kumvisha mke wake. Sasa utamvika na kumtunzaje kama hutafuti mali

Waefeso 5: 28-29
Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali HUULISHA na KUUTUNZA, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
 
Haya twende pole pole kuna sehemu kwenye huo uzi pameandikwa watu sisifanye kazi/wasitafute mali
 
Wakati sisi tunazungumzia jinsi mali inavyozorotesha mahusiano ww unatuambia habari za mali na kumwabudu Mungu Dah ndio maana division zero haziishii


Kwahiyo unataka watu wasitafute mali sababu mali zinazorotesha mahusiano!?
Ndio kusema pia sababu ajali zinaua watu wasinunue magari wala viwanda visitengeneze magari🤣🤣

Hizo sio akili za binadamu wallah labda za kuku😅😂😂😂
 
Ngoja nikufafanulie kuhusu huko kupenda mali kunakozungumziwa

Kwanza fikiria yafuatayo
~Ni wanawake wangapi wameacha ndoa zao na kuwafuata wenye pesa ni wanaume wangapi ambao wamekimbia wake zao na kukubali kuolewa sababu ya pesa.
~Ni wanawake wangapi wameua waume zao sababu ya mali ni wanaume wangapi wameacha wake zao ili waponde mali peke yao au na wanawake wengine.
~Ni kesi ngapi zipo mahakamani wanawake wanadai talaka ili wagawane mali.

Ukishapata majibu huko ndio kupenda mali kumaliza ngumziwa ambako kuna kosesha furaha na ndoa nyingi kufarakana

Nije kwenye point yako sasa wewe unavyofikiria ni kwamba watu wakioana basi wakae ndani kuangaliana tu wasifanye hata kazi kitu ambacho sio sahihi.

Naona unaleta na mifano ya biblia ambayo haiendani kabisaaaaa na mada tajwa.

Hapo kama unatetea swala la tamaa ya kupenda pesa/mali inabidi ueleze ni kwa jinsi gani tamaa ya pesa haipunguzi furaha kwa wapendanao na sio kuzungumzia eti watu wasifanye kazi hebu soma hoja ya (8) halafu ya (12) halafu rudi ya (7) halafu nenda ya (9) ukishasoma hayo ndio utajua kupenda kupi /tamaa ipi inazungumziwa hapo maana naona unaleta maneno mengiiiiii halafu hayaeleweki
 
Kha! Hivi una umri gani!?
Nimekuhurumia ghafla
Umri wako toa 2 halafu ujibu kwa hoja na mifano ya dunia ya sasa sio mambo sijui ya Nuhu mara Adam na Eva mara Abrahamu Kalala na kijakazi hapana iyo kitu
 
Mama D unatema madini..thank you sana. Wakati mwingine kuchukia Hela ni dalili za uvivu..hahahahaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…