Mambo nayopenda kwa Waislamu japo ni Mkristo

Mambo nayopenda kwa Waislamu japo ni Mkristo

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Pamoja na ukristo wangu yapo mambo kadhaa nayoyapenda kwa waislamu.

1. Kutoruhusu mtume wao adhalilishwe au kudhihakiwa. Huwezi kumkashfu mtume au kitabu chao cha Quran mbele yao halafu wakutazame tu. Lazima wakuletee noma

2. Mavazi ya staha kwa wanawake
Napenda sana dress code kwa wanawake. Wanavaa mavazi ya staha. Sehemu za ibada huwezi kuvaa kihuni-huni ukaingia

3. Kutengana wanawake na wanaume kwenye ibada zao

4. Kuruhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja kwa mtu mwenye uwezo wa kuwatunza.

5. Utoaji wa sadaka usiotia umasikini

6: Kuharakisha mazishi.

7. Kutomtenga muumini (Hapa uswali ama usiswali ilimradi wewe ni muislamu ukifa hamna longolongo utazikwa mahali popote! Njoo kwetu!

8: Kuharakisha ndoa! Hamna longolongo!
 
Hata mimi kuna vitu nimeona vimenivutia mno kama misiba hata kama siyo ndugu yao utaona wanajitolea mzika na kumsalia.

Siku kama hizi za mfungo wanalisha maskini ili wasishindwe funga, misikitini wanachanganyika maskini na tajiri, kiongozi na kapuka.
 
Vitu vizuri walivyo navyo waislam licha ya kwamba mimi sio mtu wa dini ila vitu vizuri navyoona kwao ni
1. Suala la msiba na mazishi
2. Suala la kuoa

Hawana mambo mengi kabisa katika hivyo vipengele viwili
 
Pamoja na ukristo wangu yapo mambo kadhaa nayoyapenda kwa waislamu.

1. Kutoruhusu mtume wao adhalilishwe au kudhihakiwa. Huwezi kumkashfu mtume au kitabu chao cha quran mbele yao halafu wakutazame tu. Lazima wakuletee nom...
Hata ukitaka kusilimu wala hawana kelele wanakupokea na kanzu na kofia wanakupatia!
 
Back
Top Bottom