Mambo nayopenda kwa Waislamu japo ni Mkristo

Mambo nayopenda kwa Waislamu japo ni Mkristo

Niliuliza hivi; Kwanini mtu akitaka kusilimu lazima apewe jina la kiarabu..
Mfano, Bahati anataka kusilimu, kwanini sasa aitwe Abdul badala ya kubaki na Bahati lake.. Je kuna shida na Majina yasiyo ya kiarabu?

Naomba jibu kama unajua.
Jina upo huru kuchagua mwenyewe ila sio la kimisheni kama unalo ulilolipenda au unatajiwa majina kadhaa utakalopenda unapewa rasmi majina mazuri na maana zake,Jina Abdul halipaswi kuitwa kifupi hivyo ni lazima liwe Abdul manaf,!Abdul latif au Abdul razzak watu hulikatisha tuu!
 
Ningekuwa Mwislamu ningekuwa nimeishaoa mimi. Yaani ningeoa binti anayevaa ushungi siku zote, lile joto na ngozi nyororo hatari tupu.

Halafu binti asingekuwa ananiropokea wala kunijibu hovyo sababu dini inawakataza mara kwa mara. Tena ningeoa yule ameshika dini haswa yani nafanya mambo yangu kwa amani.

Ila nisingeoa mke mwingine. Kwa vile sio Mwislamu nasubiri mpaka nifike angalau 30 uko ndio nioe.
 
Jina upo huru kuchagua mwenyewe ila sio la kimisheni kama unalo ulilolipenda au unatajiwa majina kadhaa utakalopenda unapewa rasmi majina mazuri na maana zake,Jina Abdul halipaswi kuitwa kifupi hivyo ni lazima liwe Abdul manaf,!Abdul latif au Abdul razzak watu hulikatisha tuu!
Je inawezekana mtu akasilimu na akabaki na jina lake la kiafrika kama vile Matinde, au lazima apewe list ya majina ya kiarabu achague analolipenda?
 
Pamoja na ukristo wangu yapo mambo kadhaa nayoyapenda kwa waislamu.

1. Kutoruhusu mtume wao adhalilishwe au kudhihakiwa. Huwezi kumkashfu mtume au kitabu chao cha quran mbele yao halafu wakutazame tu. Lazima wakuletee nom...
Usipende usichokijua mkuu!

Ukristo ndio halisi na njia sahihi,lakini shetani aliuteka sana Kwa dini hizi na madhehebu Ili ifanyike biashara na ukristo uchukiwe kama hivi uonavyo wewe!

Niishie hapo
 
Niliuliza hivi; Kwanini mtu akitaka kusilimu lazima apewe jina la kiarabu..
Mfano, Bahati anataka kusilimu, kwanini sasa aitwe Abdul badala ya kubaki na Bahati lake.. Je kuna shida na Majina yasiyo ya kiarabu?

Naomba jibu kama unajua.
Uislam unataka watu wapewe majina mazuri i.e majibu yenye maana nzuri. So, unaweza itwa Nuru au Lightness, Haikande au Masanja au John na bado ukawa ni Muislam. Hii ya kuwalazimisha watu kuchukua majina ya Kiarabu ni upotofu tu na mazoea. Hakuna ulazima.
 
Ooh.. okay.. Kuna sheikh aliniambia haiwezekani uwe muislamu asiye na jina la kiislamu.. sikuridhishwa na hilo jibu.
Alisema uongo kabisa. Majina yanahusiana na utamaduni na mazingira mtu atokayo. Alichosema Mtume ni kuwapa majina mazuri watoto wenu. Ila sio lazima aitwe jina la kiarabu. Unaweza kuwa muislamu na ukaitwa Jonathan au Tonge, au Samaki.
 
Pamoja na ukristo wangu yapo mambo kadhaa nayoyapenda kwa waislamu.

1. Kutoruhusu mtume wao adhalilishwe au kudhihakiwa. Huwezi kumkashfu mtume au kitabu chao cha quran mbele yao halafu wakutazame tu. Lazima wakuletee nom...
6: Kuharakisha mazishi.

7. Kutomtenga muumini (Hapa uswali ama usiswali ilimradi wewe ni muislamu ukifa hamna longolongo utazikwa mahali popote! Njoo kwetu!

8: Kuharakisha ndoa! Hamna longolongo!

Nb: Hii dini imekaa kijamaa zaidi! Angalia namna ya kusali, mavazi, ulaji, ukaaji na watu n.k!

Nb: Upande ule umekaa kibepari! Angalia namna ya kusali, mavazi,sadaka, n.k!

Nb: Dini zote mbili ongezea na uyahudi zimejaa chuki dhidi ya mwenzake! Bifu la mwarabu dhidi ya myahudi na mzungu likaingizwa mpaka kwenye dini!

Nb: Dini zote zimetengenezwa na kuundwa na watu!

Nb: Huwezi kutenganisha asili za tamaduni za watu na dini zao( Huwezi kuutenganisha utamaduni wa kiarabu na uislamu ,pia kwa umagharibi na ukristo au uyahudi na dini yao!)

Nb: Mungu hana dini!

Ni mtazamo tu!
 
Back
Top Bottom