Mambo nayopenda kwa Waislamu japo ni Mkristo

Mambo nayopenda kwa Waislamu japo ni Mkristo

Hapo unapimwa ujasiri kama kweli mmeshindwa kuendelea na ndoa au mmepata hasira tu..

Watu wanamaliza Eda na wanaschana kabisa..

Mtu anakuona kama Kaka yale hata ukivaa nini, Au anakuona kama mwanaume mwenzie tu..unavaa bikini yako anapita anakusalimia anakuachia hela ya matumizi ya siku, Anasepa na maisha yanaendelea...

Hata ukikaa uchi anapita anakusalimia Na anasepa 😅😅😅
Kuna muda mapenz yanakuwa kama karaha 🤣🤣
Sasa mfano eda ni miezi 3 nikiondoka wiki ya pili inakuaje? (Sijatimiza hiyo miezi)
 
Ukisoma Quran Kigezo cha kuoa wake wengi ni Uadilifu..

Quran 4:3 (Sura An-nisai aya ya 3)

.....basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi oeni mmoja tu.....

Lakini ukienda Kusoma Mbele zaidi ya Sura hiyo hiyo aya ya 129 Quran inasema..

....Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia (Mkiamua kufanya hivyo). Kwa hivyo msimili (Msilalie upande mmoja)..moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamchamngu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu.....

Kama utaangalia Aya hiyo inatoa maelezo ya Aya hiyo ya 3 kuwa binadamu wa kufanya Uadilifu ni wachache sana na hata ukijifanya wewe utafanya uadilifu ila huwezi
Haya mavitabu ya dini yamejaa contradiction kibao halafu hayaeleki.

Ninayo Quran, ngoja nikasome hizo aya nitarudi.
 
Kuharakisha mazishi kuna tija gani?

Hoja ya kuokoa gharama haina mashiko, kuna watu wanapenda mazishi yao yawe ya kifahari na yatumie gharama.
Kurahishisha mazishi kwa ajili ya kumpumzisha Muumini wao sehemu salama..

Kuna vitu Vitatu katika uislamu huwa vinahitaji vifanyika haraka sana na mara moja vinapotokea..

-Mtu akitaka kuoa/Kuozeshwa
-Kuzika
-Mtu akitaka Kusilimu/Kuwa mwislam..

Hizi kufanyika haraka sana Kwa sababu ya Uharaka wa Ibada hizo..

Unaweza ukaacha kumuozesha mtu halafu likatokea Jambo wakakosana na ndoa ikawa haipo (Wewe ukabeba dhambi sawa na kuvunja ndoa )
Mtu kataka kusilimu ukaacha kumsilimisha Ikatokea kafariki au kaghairi wanaamini kuwa wewe ndo unabeba Lawama huko Akhera kwa kutokutimiza kilichopaswa kufanyika
 
Haya mavitabu ya dini yamejaa contradiction kibao halafu hayaeleki.

Ninayo Quran, ngoja nikasome hizo aya nitarudi.
No contradiction mkuu hapo just maelezo zaidi ya hiyo aya ya kuoa ndo maana huwa nawashangaa wanaosema wanapenda kuoa wake wengi..

Mimi Kwenye dini sasa hivi nilishajitoa huko..
Unakuwa umejifungia kwenye Kibox
 
Unaondoka unaenda wapi??
Na kwanini?
Yaani sababu ya kuondoka?
Eda Ni miezi minne kama sikosei
Ukitizama eda ipo makusudi kumfanya mwanamke na mwanaume wasiachane.

Kwenye uislamu mume na mke kutengana according to their beliefs huwa mbingu na ardhi zinatetemeka... Sijui ni kweli kwa maana hizi hadithi mi nazisikia kwenye vijiwe vya alkasusu mujarab.
 
Pamoja na ukristo wangu yapo mambo kadhaa nayoyapenda kwa waislamu.

1. Kutoruhusu mtume wao adhalilishwe au kudhihakiwa. Huwezi kumkashfu mtume au kitabu chao cha Quran mbele yao halafu wakutazame tu. Lazima wakuletee noma

2. Mavazi ya staha kwa wanawake
Napenda sana dress code kwa wanawake. Wanavaa mavazi ya staha. Sehemu za ibada huwezi kuvaa kihuni-huni ukaingia

3. Kutengana wanawake na wanaume kwenye ibada zao

4. Kuruhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja kwa mtu mwenye uwezo wa kuwatunza.

5. Utoaji wa sadaka usiotia umasikini
Kuna huyu mtangazaji maarufu southfrica nayeye leo kapost kuvutiwa na uislamu naona ameona watu wanavyotia bidii kwenye ibada kipindi hichi cha ramadhani
Pamoja na ukristo wangu yapo mambo kadhaa nayoyapenda kwa waislamu.

1. Kutoruhusu mtume wao adhalilishwe au kudhihakiwa. Huwezi kumkashfu mtume au kitabu chao cha Quran mbele yao halafu wakutazame tu. Lazima wakuletee noma

2. Mavazi ya staha kwa wanawake
Napenda sana dress code kwa wanawake. Wanavaa mavazi ya staha. Sehemu za ibada huwezi kuvaa kihuni-huni ukaingia

3. Kutengana wanawake na wanaume kwenye ibada zao

4. Kuruhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja kwa mtu mwenye uwezo wa kuwatunza.

5. Utoaji wa sadaka usiotia umasikini
Hata huyu mtangazaji maarufu southafrica amevutiwa na uislamu , naona ameona watu wanavyotia bidii kwenye ibada kipindi hichi cha ramadhani aise watu wapo serious sana na ibada
 

Attachments

  • Screenshot_20240320-072925_Facebook.jpg
    Screenshot_20240320-072925_Facebook.jpg
    125 KB · Views: 3
Back
Top Bottom