#COVID19 Mambo niliyoyaona baada ya kupata chanjo leo

#COVID19 Mambo niliyoyaona baada ya kupata chanjo leo

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,108
Reaction score
5,110
Leo nimechanjwa katika mji mmojawapo wa wilaya. Nilifanya booking online na tarehe yangu niliyochagua ilikuwa jana bahati mbaya jana hawakufungua. Nilichokiona ni:
  1. Pamoja na kueleza kuwa nilikuwa na booking online lakini hiyo haikuwa na uzito ila nilipewa fomu ya kujaza.
  2. Mtumishi alikuwa mmoja huku akifanya kazi ya usajili na kuchanja na kuna wakati alizidiwa.
  3. Makundi maalum ya watu walioainishwa katika awamu hii hayajawa wazi sana kwani nimeshuhuida mtu wa umri chini ya 40 na ambaye hana ugonjwa wowote akiomba achanjwe (Picha za Jokate zimevuruga mambo)
  4. Hapakuwa na faragha na kila mtu alikuwa akiulizwa unatumia dawa yoyote au una ugonjwa wowote
  5. Mwamko ni mkubwa na vituo vya kuchanjia vijipange vizuri.
  6. Pamoja na kuchanja lakini sina kitambulisho chochote kuthibitisha kuwa nimechanja
  7. Kwa kuwa vitambulisho vya uraia na liseni za udereva zinatumika ingefaa pawe na app ambayo ingerahisisha kwani kwa ujazaji ule nina mashaka kuwa makosa yatakuwa mengi na data entry itakuwa na shida.
 
Hata mie nimechanja leo

Nimeanza kuona mwamko unaanza kupanda siku hadi siku watu walikuwa wengi hasa wenye umri wa 50+ japokuwa wa chini ya huo umri walikuwepo

Tatizo hilo la kuandika kidogo linachelewesha watu japokuwa chanjo ni kitu cha dakika moja au mbili na wajaza form walikuwa kama watatu na mchoma chanjo mmoja

Wanao jaza form waongezwe kwa ushauri
 
...
Pamoja na kueleza kuwa nilikuwa na booking online lakini hiyo haikuwa na uzito ila nilipewa fomu ya kujaza....
  1. Mtumishi alikuwa mmoja huku akifanya kazi ya usajili na kuchanja na kuna wakati alizidiwa.
  2. Makundi maalum ya watu walioainishwa katika awamu hii hayajawa wazi sana kwani nimeshuhuida mtu wa umri chini ya 40 na ambaye hana ugonjwa wowote akiomba achanjwe (Picha za Jokate zimevuruga mambo)
  3. ...
... kama kuna mtu anamwangalia Jokate atakuwa na matatizo kichwani. Nani ajuaye afya yake zaidi yake na dr wake? Inawezekana yumo kundi maalumu sijui kwanini watanzania ni wazito sana kuelewa.
 
hongera mkuu, ngoja tuone misukule ya kawe itakaa na msimamo mpaka lini
... mkuu nenda kachanje; afya ni yako! Ukiyasikiliza hayo mataahira yasiyojua hata "test tube" inafananaje utapotea.
 
Back
Top Bottom