Mambo usiyoyafahamu kuhusu Ngamia

Mambo usiyoyafahamu kuhusu Ngamia

Ngamia hunywa maji safi na ya chumvi. Anaweza hata kunywa maji kutoka Bahari ya Chumvi na hakuna kitakachoipata. Hii ni kwa sababu figo za ngamia huchuja maji: hutenganisha na chumvi na kugeuza kuwa maji safi yanayofaa kwa kunywa.

Ngamia pia hula miiba na haidhuru tumbo lake au utumbo wake kwa sababu mate yake huyeyusha miiba kama asidi.

Ngamia ana kope mbili: moja ni nyembamba na ya uwazi, nyingine nene na yenye nyama. Dhoruba ya mchanga inapoanza katika jangwa, hufunga kope lake la uwazi ili kuzuia mchanga usiingie machoni pake.

Ngamia pia anaweza kubadilisha joto la mwili wake: ikiwa ni baridi joto lake huongezeka, ikiwa ni moto katika jangwa la joto joto la mwili wake hupungua. Sifa alizo nazo mnyama huyu mzuri na wa kipekee ni za kuvutia.

Credit: Jr™ Creators!

Kwa kuwa anacheua ila hana kwato mbili, nyama yake msile wala mzoga wake msiguse maana ni haramu kwenu.
 
Mshana si watu wangeweza kucheza za gizwa na kuwa na aliyonayo ngamia.. Si wangeyafanya? Eeeeh

Wana sayansi hawajaja wa jaribu kweli kuona kama yao anapewa binadamu?
 
Niliwahi kumpanda kwenye zoo flan hivi, sikujua kama ni mrefu vile, nina phobia ya height teh teh, kasheshe kwenye kushuka Ngamia akagoma kunishusha hatariiii🙌 ilikua ni bad and good experience ever
 
Niliwahi kumpanda kwenye zoo flan hivi, sikujua kama ni mrefu vile, nina phobia ya height teh teh, kasheshe kwenye kushuka Ngamia akagoma kunishusha hatariiii🙌 ilikua ni bad and good experience ever
Sasa wewe si ungeruka TU 🤣 🤣 🤣
 
Mkojo na maziwa ya ngamia hutumia kutibu kisukari. Pia ngamia ni mnyama asiyekubali kumuingilia ngamia walozaliwa tumbo moja, hadi umletee ngamia wa mbali .mkimfunga kitambaa na kumlazimisha ndugu yake waingiliane anaweza ua nyumba nzima

Wametajwa kwenye quran:
{ أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلۡإِبِلِ كَيۡفَ خُلِقَتۡ }
[Surah Al-Ghāshiyah: 17]

Ali Muhsin Al-Barwani:
Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
 
Ngamia hunywa maji safi na ya chumvi. Anaweza hata kunywa maji kutoka Bahari ya Chumvi na hakuna kitakachoipata. Hii ni kwa sababu figo za ngamia huchuja maji: hutenganisha na chumvi na kugeuza kuwa maji safi yanayofaa kwa kunywa.

Ngamia pia hula miiba na haidhuru tumbo lake au utumbo wake kwa sababu mate yake huyeyusha miiba kama asidi.

Ngamia ana kope mbili: moja ni nyembamba na ya uwazi, nyingine nene na yenye nyama. Dhoruba ya mchanga inapoanza katika jangwa, hufunga kope lake la uwazi ili kuzuia mchanga usiingie machoni pake.

Ngamia pia anaweza kubadilisha joto la mwili wake: ikiwa ni baridi joto lake huongezeka, ikiwa ni moto katika jangwa la joto joto la mwili wake hupungua. Sifa alizo nazo mnyama huyu mzuri na wa kipekee ni za kuvutia.

Credit: Jr™ Creators!

Peponi kuna ngamia? Je nao wameoa mabikira wangapi?
 
Nasikia kumchinja ni mpaka dua ifanyike
Mambo mengine ni kuongeza chumvi tu na hayana uhalisia.Hata kusema ukipiga dua anakubali achinjwe jaribu uone kama itatokea.Ni wapole ndio ila sio kwamba hawawezi kujitetea inapomuhitaji kufanya hivyo,teke lake moja tu linakuulia mbali,pia anaweza kung'ata akakuvunja vunja au kukuua kabisa kwa domo lake alilojaaliwa.Ni kama Twiga tu kama unazijua sifa za Twiga.
 
Mambo mengine ni kuongeza chumvi tu na hayana uhalisia.Hata kusema ukipiga dua anakubali achinjwe jaribu uone kama itatokea.Ni wapole ndio ila sio kwamba hawawezi kujitetea inapomuhitaji kufanya hivyo,teke lake linakuulia mbali,pia anaweza kung'ata akakuulia mbali kea domo lake alilojaaliwa.Ni kama Twiga tu kama unazijua sifa za Twiga.
Hatari sana
 
Back
Top Bottom