BurtonSat_Shop
Member
- Dec 20, 2019
- 60
- 91
Biblia ukiisoma usisome kwa kutumia sana ufahamu wa aliekufundisha hayo maandiko kama ni Mchungaji wako,Askofu wako au Muinjilisti wako au hata Sheikh wako.Katika Biblia tumepewa roho wa kweli atakae tufundisha ile kweli,ambayo haineni kwashauri lake ila shauri la MUNGU (YOHANA 16:13) kwasababu wanadamu woote asili yetu niya upotevu toka Kwa Adamu na Hawa,uzao wetu ulianzia njee ya Eden kwa upotevu.Yesu alikuja ili kuturudisha Eden(kwenye uwepo wa Mungu) lakini alipoondoka alituachia msaidizi wa kutupa ile kweli ambayo ni Roho wa Mungu
Biblia sio kitabu cha Wakristo ni kitabu cha kifalme toka Mwanzo mpaka Ufunuo,Yesu akuja kwa ajili ya wakristo Yesu alikuja kwaajili ya wanaomini injili yake ya ufalme wa mbinguni(Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila amuaminie asipotee YOHANA 3:16) Hivi ni wanao amini tu kile alichohubiri Yesu.
Yesu kwa maisha yake ya injili alihubiri juu ya ufalme wa Mbinguni tu
Mathayo 4:17
" Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia"
Na mifano yake katika injili yake ilikuwa ni ufalme wa Mungu/mbinguni umefanana....ufalme wa Mungu/Mbinguni umefanana.....ufalme wa Mungu/Mbinguni umefanana.... hivyo hivyo kwa sehemu kubwa ya mafundisho yake
Hivyo Yesu hakuja kuubiri ukristo duniani maana kwa maisha yake yoote hakuwai kuingia Kanisani aliingia katika Misikiti ya kiyahudi(Masinagogi) lakini hawakuyapokea mafundisho yake kabisa ndio maana alisema jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni akiwa na maana watu alio wahubiria wa misikitini wamemkataa na wamempokea watu wapembeni ambao kwasasa ndio Wakristo na makanisa yameanza baada ya kifo cha Yesu kupitia mitume wake,lakini baya zaidi nalo liona makanisani hawaubiri tena alichoubiri Yesu Kristo wanahubiri ya kwao na sio tena Ufalme wa Mungu japo wanatumia kitabu cha Kifalme.Yesu hakutaka mumuhubiri yeye alitaka tuhubiri u habari za ufalme kwanza kisha ndio habari zake au habari nyingine (utafteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa Mathayo 6:33)
Lakini hata Mtume Paulo mwenyewe alikuwa anawahubiria watu kwanza juu ya ufalme wa mbinguni ndio habari za Yesu zinafata
Matendo Ya Mitume 28:30-31
"Akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea,akihubiri habari za ufalme wa Mungu, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu.