Mambo wasiyoyapenda wanaume ndani ya ndoa

Mambo wasiyoyapenda wanaume ndani ya ndoa

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
1. MWANAMUME HAPENDI KUFOKEWA
Hata Kama amekosea; jaribu kumuonyesha kosa lake pasipo kumfokea au kumvunjia heshima.

2. MWANAMUME HAPENDI KUULIZWA MASWALI MENGI KWA WAKATI MMOJA
Ukimuuliza swali halafu yeye anakua kimya au anaduwaa; ujue hana jibu au anajisikia vibaya kuhusu jibu ambalo anatakiwa kutoa. Mpe muda ajipange kutoa jibu usimlazimishe siyo mtumwa wako.

3. MWANAMUME ANAHITAJI MUDA WA KUKAA KIMYA; USIMLAZIMISHE KUONGEA
Zaidi sana anapopita kwenye hali ngumu au changamoto fulani; wanaume wengi hupenda kukaa kimya huku akiwaza nini cha kufanya. Tofauti na wanawake, ambao wakati wa changamoto ndipo wanataka kuongea zaidi.

Wanaume wengi hawapendi kuongea kama hawana suluhisho la shida iliyopo mbele yao hivyo Kama wewe ni mtu sahihi kwake jifunze kumsoma mumeo ili ujue nyakati zake ngumu ili usimame kwenye zamu yako.

4. MWANAMUME HAPENDI MKE MWENYE KIHEREHERE
Yani hata kama bado hajakwambia, kaa ukijua kwamba wanaume hawapendi kuwa na mke ambaye hapitwi na jambo.

Mwanamke anayetaka kuchangia kila kitu au kuongea-ongea sanaaaa! Mmmhhh! Unamchosha mwanamumeo.

5. MWANAMUME HAPENDI MKE WAKE AWE NA MARAFIKI WEEENGIII; KIBAYA ZAIDI SANA ETI NI MARAFIKI WA KIUME

Wanaume wengi wana WIVU; (NA HIYO NI ASILI YAO). Hivyo mwanamume hapendi kuona mke wake yuko bize “ku-entertain” wanaume wengine (HATA KAMA HAKUNA MAHUSIANO MABAYA).

Mara huyu ni rafiki yangu tulisoma nae, niliwahi fanya nae training, ni mwalimu wa kwaya, oohh huyu tulifanya nae kazi, bla, bla , bla zako zitakuvunjia mji tumia akili ipasavyo.

6. MWANAMUME HAPENDI KUNYANYASIKA

Wanaume wengi ni rahisi kusumbuliwa na hali au hisia ya kujiona duni (Inferiority Complex).

Zaidi sana kama MKE ndiye mwenye kipato kikubwa, au elimu kubwa, umri mkubwa, au anatoka familia yenye nguvu zaidi kuliko ya mume. ( Lakini ni kwa hasiyejiheshimu)

Hapo inabidi mwanamke awe makini sana maana kitu kidogo tu kinaweza sababisha mwanaume adhanie kwamba tayari anadharaulika. Mwanamke anahitaji HEKIMA ya juu kuishi na mume mwenye shida ya kujidharau.(Faida ya MKE MWENYE HEKIMA inatenda kazi Sana mahali hapa).

7. MWANAMUME, HAPENDI KUPOTEZA MAMLAKA AU SAUTI YAKE KWA MKE WAKE
Mwanamume akiona dalili za kupoteza mamlaka yake na kukosa sauti kwa mkewe, basi hujaribiwa kutafuta mahali pengine pa kuonyesha hiyo mamlaka.( MCHEPUKO)

Ni rahisi KUMPENDA Mke mwenye UTII ;Vilevile, ni rahisi KUMTII Mume mwenye upendo.
 
Ongeze na hii.

Hakuna kitu mwanaume hapendi na anachukua hatua mapema sana kuchepuka kama unaombwa game afu hutoi unatoa sababu zisizo na ukweli wiki nzima, Na haulali na chupi au uchi, unalala na nguo nzito.
 
Mwanaume mwanaume!!, bado mnahangaika na wanaume? Hata umtii vipi, atakutafutia sababu tu.

Utaskia huyu mwanamke ni boring , hana content.Mwanamke mwenye content ataambiwa ni mjuaji.

Just do you, acheni kufake personalities kisa mwanaume.

Anayekupenda,atakupenda jinsi ulivyo.
 
Back
Top Bottom