Mambo ya ajabu yaliyonifanya nikashindwa kuishi vijiji vya kanda ya Ziwa

Hapo ni usukumani! Niulize kwanini? Maneno haya au lafudhi hii ni kisukuma "wananzengo, watu wazima kuchapwa viboko, wizi wa mazao shambani, nk"
 
Point no 6 ni tabia za Wasukuma...Iyo ni ukwel mtupu.
Walifanya nikajua kuongea kisukuma bila kupenda japo nilifundishwa na binti mmoja ivi
 
Haya mambo hata Bukoba mjini yapo tena katika mitaa yake mingi tu.
 
Mengi ni mazuri tena kama sio yote
Nimeishi Geita vijijini kwa miaka kama mi 3 naweza kusema wanajitahidi sana kwa ustraabu na uchapakazi
Hawaombi Cha mtu na Wana ushirikiano mkubwa
Kuhusu kufumaniwa ni kweli kabisa hivyo unatakiwa kumjua msichana kabla ya kumtongoza na kulala nae sio unatongoza yeyote
Kushirikiana kwenye misiba na majanga ya wizi ni kuzuri wanafanya hivyo ili siku ukipata janga iwe rahisi kukusaidia mbona hata mjini watu wasioshirikiana na wengine wanaachiwa msiba wao!
Kununua kwenye maduka ya wenzao sio kweli waha wapo na wanauza vizuri sana tena kwenye minada wamejaa ila baadhi hupenda ujue lugha Yao maana wao hawajui kiswahili vizuri na biashara inahusisha lugha (huoni hata mijini wachina na wahindi huweka mswahili dukani ili kupata wateja vizuri!) lugha ni muhimu
 
Hawajawahi sungu sungu kukuburuza kwenda kutemya? Hapo ndio maajabu na watu wanakula mboko vibaya
Niliwahishudia mahali fulani huku usukumani mwaka 2013 aise kwamara ya kwanza nikajua nisherehe nikamuuliza mzee mmoja akaniambia sio sherehe kuna watu watalia kesho.

Basi siku hiyo vijana walikesha wanaimba uwanja wa shule.Kesho yake ikafika picha linaanza wananzengo wote tukaitwa uwanjani tukazingirwa na sungusungu hakuna kutoka.
Likaanza zoezi la kupiga kura mimi hapo sielewi chochote nasikia kila mtu aliyejirani nami pale anamtaja mtu fulani namimi nikasema namuandika huyuhuyu .kumbe zile kura zilikuwa zinawahusu watu wote wenye makosa kwenye ile jamii.

Yule jamaa aliyekuwa anatajwatajwa na niliyempigia kura alikuwa anamakosa kama matata wizi,kutembea na wake za watu na ugomvi .jamaa alikuwa na kura nyingi sana.
Sasa wote waliokuwa na kura nyingi waliitwa mbele aise walikula mboko nyingi sana iase na faini juu.

Yule mwamba aliyekuwa anatajwa alikula fimbo mia moja na faini ya ng'ombe wawili.

Usukumani kuna mambo. Tembea uone na ujifunze
 
ni kweli wasukuma ovyo kabisa
Nimeishi maeneo hayo miaka ya themanini wakati huo Sungusungu wamepamba moto. Ukituhumiwa uchawi, na wengi wa wachawi walikuwa kinamana wakongwe, wanakusindikiza. Huko kusindikizwa ni kupelekwa porini na kuuwawa na maiti kutupwa katika shimo wao huyaita maduara. Kipindi hicho kilikuwa cha kusikitisha sana. Viongozi wa hao Sungusungu walikuwa ni Watemi ambao walitawazwa na wananchi wa eneo husika. Walikuwa ndio waamuzi wa mwisho katika kila jambo. Kwa sasa kidogo hali imetulia na mambo hayo hayafanyiki kama ilivyokuwa kipindi hicho.
 
iko kijiji cha ujamaa bila shaka kili approve mawazo ya mwalim🤣
 
Dah nimecheka sana
 
Ukiacha la fumanizi la mchongo mengine naona yapo sawa tu,kila jamii na utaratibu wao wa kuishi
 
Baadhi nina ushahidi nayo mfano apo masumbwe mtu akifa usipoenda mazikoni faini inakuhusu
 
Ni kweli ushamba nao unachangia, hao wanawezana wao kwa wao tu.
 
Kwa upande fulani ni ujinga. Unalipa kodi kwaajili ya maendeleo ikiwemo miundombinu, sasa inakiawaje tena uje unichangishe au uniambie nikatengeneze barabara.

Tuwawajibishe hawa watawala.
Pamoja na kulipa kodi, je wasipotengeneza milele au for 80 years tutaisubiri tu serikali na kuendelea kuchangia?

Ndio maana barabara za Moshi tunajiongeza, kwa mfano hapa Kiboriloni mita 150 na Maili 6 pale pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…