Maajabu ya Ubongo wa Binadamu
1. Hali ya Deja Vu:
Hisia ya kushangaza kuwa tukio unaloliona sasa ulishawahi kuliishi huko nyuma, inayotokana na ubongo kuchelewa kupokea taarifa kwa sekunde chache na kuifanya ionekane kama kumbukumbu ya zamani.
View attachment 3601784
2. Uwezo wa Neuroplasticity: Uwezo wa kipekee wa ubongo kujirekebisha na kutengeneza njia mpya za neva baada ya majeraha au kiharusi, ambapo seli nzima huchukua majukumu ya seli zilizokufa ili kumrudishia mtu uwezo wake.
View attachment 3601785
3. Ndoto za Lucid:
Hali ya kujitambua kikamilifu kuwa uko ndotoni ukiwa umelala, jambo linalokupa uwezo wa kuiongoza na kuicontrol ndoto hiyo kama muongozaji wa filamu, ukifanya mambo yasiyowezekana kama kuruka angani.
View attachment 3601786
4. Athari ya Placebo: Ushahidi kuwa akili ina nguvu ya kuuponya mwili baada ya mgonjwa kupewa dawa isiyo na kemikali yoyote (kama kidonge cha sukari), lakini akapona kwa sababu tu anaamini kwa asilimia mia moja kuwa atapona.
View attachment 3601788
5. Uzalishaji wa Umeme: Wakati ukiwa macho, mawasiliano ya mamilioni ya seli za neva (neurons) yanazalisha nguvu ya umeme inayofikia wati 12 hadi 25, kiasi kinachotosha kabisa kuwasha balbu ndogo ya mwanga wa LED.
View attachment 3601789
6. Kumbukumbu za Uongo:
Tabia ya ubongo kulaghai akili yako kwa kutengeneza au kubadili kumbukumbu za matukio ambayo hayajawahi kutokea kabisa maishani mwako, na kukufanya uamini kwa dhati kuwa ni ukweli.
View attachment 3601790
Matukio Yasiyoelezeka Duniani
1. Pembetatu ya Bermuda: Eneo la siri kwenye Bahari ya Atlantiki ambapo mamia ya meli na ndege zimepotea ghafla katika mazingira ya kutatanisha, bila kuacha ishara ya hatari, mabaki, wala miili ya watu hadi leo.
View attachment 3601802
2. Sauti ya "The Hum": Mlio wa chini unaoendelea kama injini ya mbali unaosikiwa na asilimia 2 tu ya watu katika maeneo fulani duniani, lakini vifaa vya kisasa vinashindwa kuunasia na chanzo chake hakijulikani.
View attachment 3601803
3. Mvua za Wanyama: Tukio la kweli ambapo viumbe kama samaki au vyura hudondoka kutoka mawinguni kama mvua, jambo linalohusishwa na vimbunga vya majini vinavyonyonya wanyama hao, ingawa bado lina maswali mengi.
View attachment 3601804
4. Miamba Inayotembea: Mawe makubwa kwenye Bonde la Kifo (Death Valley) yanayohama yenyewe usiku na kuacha mistari mirefu ardhini, tukio linalodhaniwa kusababishwa na mchanganyiko wa upepo na safu nyembamba ya barafu.
View attachment 3601831
5. Mji wa Kale wa Atlantis: Hadithi ya mji uliokuwa na utajiri na teknolojia ya juu sana uliopotea chini ya bahari ndani ya siku moja, ambao hadi leo wanasayansi hawajui kama ulikuwepo kweli au ni hadithi ya kufikirika.
View attachment 3601808