Mambo ya Dating Apps: Kupata Mapenzi Huko ni Rahisi au Unapoteza Muda?

Mambo ya Dating Apps: Kupata Mapenzi Huko ni Rahisi au Unapoteza Muda?

Last_Joker

Senior Member
Joined
Nov 23, 2018
Posts
174
Reaction score
261
Hivi ukiingia kwenye dating apps, unatafuta mapenzi au unatafuta maumivu? Watu wengi wanajaribu bahati yao huko, na wengine wanajikuta wakipoteza muda huku wakichanganywa na maswipe right na swipe left. Inajulikana kuwa hizi apps zimejaa watu wa kila aina – wengine wanatafuta penzi la kweli, wengine burudani tu, na wengine hawajui wanatafuta nini hasa. Swali ni, ni rahisi kweli kupata mtu anayekufaa huko au ni njia ya kupoteza muda na mwisho wa siku kuachwa na moyo uliovunjika?

Wapo ambao wanasema wamepata wenzi wao wa maisha kupitia apps hizi, lakini hiyo ni ndoto kwa wengi. Hebu fikiria, unakutana na mtu mtandaoni, mnaanza kuchat na hata kupanga mipango ya kukutana. Lakini mara nyingi unaishia kugundua kwamba huyo mtu hana nia ya dhati au yuko na watu wengine kadhaa. Sasa inakuwa ngumu kujiamini – mara unajua tu kuna mtu ana “backup,” mara unaambiwa yuko busy, au anasahau hata ku-reply meseji zako.

Pia, suala la kuamini ni changamoto kubwa. Kwani, kwa jinsi apps hizi zinavyofanya kazi, kila mtu ana profile ya kupendeza, picha zenye pozi kali, na “bio” tamu tamu. Lakini ukweli unajulikana tu baada ya kukutana na kugundua kwamba watu wengine wameweka profile bandia au hawaendani na yale waliyokuonyesha awali. Unajua kuna wengine wanaingia huko kisaikolojia hawako sawa, wana shida zao ambazo wanatafuta kuzificha au kujisahaulisha kwa muda.

Kwa upande mwingine, kuna wale wanaopata urahisi wa kuzungumza na watu wapya. Kama una aibu ya kuanzisha mazungumzo kwa mtu mtaani, basi dating apps zinakupa nafasi ya kujifunza na kujenga ujasiri. Wengine wanasema ni nafasi nzuri kwa wale wenye majukumu mengi, ambao hawana muda wa kutoka mara kwa mara na kukutana na watu wapya. Lakini je, ni kweli inaweza kuwa njia bora ya kupata penzi la kweli au ni kutafuta watu wa kupotezeana muda tu?

Unadhani app hizi zinasaidia kweli au ni michezo tu ya kutafuta mapenzi ya muda mfupi? Kama umewahi kujaribu, ulijifunza nini? Na kwa wale ambao hawajawahi kuingia huko, kwa nini unahisi ni ngumu kujaribu? Twende tuchangie uzoefu na mitazamo yetu juu ya hizi dating apps – ni matumaini au ni ndoto tu?
 
Mtaani hamna watu? wameisha?

Bongo hizo apps ni kwa ajili ya wauzaji na wanunuaji kukutana. Unapata pisi inakufuata ulipo fasta kuliko ambulance au fire. Pia wala nauli wamejaa huko pamoja na matapeli.

Ingia field, mwanaume face your fears tongoza, mwanamke jiweke feminine utongozwe.
 
Hivi kweli unaenda kutafuta mtu serious kwenye hizo dating site? au unakutana na wauza nyap, unategemea mwanamke serious atajiunga kwenye hizo dating apps, nenda kwenye mikusanyiko utakutana na wanawake wa kutosha, kwenye mikutano ya injili, nenda makanisani, misikitini, usiache kuhudhuria msibani kunawaga na pisi za ukweli, uzuri wake huwezi ukanyimwa namba, ukikaa kwenye dalala na mdada msemeshe usiweke phone masikioni
 
Ndio sehemu yenye matapeli wa mapenzi huko kuwa makini Kuna tinder hiyo ndio haifai hata kidogo
 
Ngoja leo niweke ushuhuda wangu:

Mwaka 2019, kuna dating app moja inaitwa Tan tan, ilikua ndo ina trend sana, kipindi hiko nna mwaka mmoja mtaani tangu nimalize chuo, sikua nimeajiriwa so muda mwingi nlikua idle tuu, nkajiunga na ile app lengo ilikua ni sehemu ya kupotezea muda tuu, katika pita pita zangu, nkabahatisha mtoto mmoja anaishi sinza kipindi hiko alikua anasoma IFM mwaka wa pili, tuliendelea na chatting mpaka tukaja kuwa wapenzi, kitu kilichonishangaza ni kuwa yule demu alikua bikra, na mimi ndo nliyeitoa, tuliendelea kuwa kwenye mahusiano, akaja akapata mimba ila aliitoa coz alikua anaogopa nyumbani kwao wangemzingua, basi kutokana na hiyo issue hata mahusiano yetu hayakuchukua muda mrefu, tukaachana, ila mpaka leo tunawasiliana:

Note: Alikua bikra na nimempata kwenye dating app nyie hamuogopi 😂🤔,
 
In addition

Kuna dating app moja inaitwa Boo, juzi juzi tuu hapa nimepata demu mmoja, mtoto wa kichaga, binti anaonekana katulia tuu, ni vile sijamuelewa sana, nshakula kama mara tatu hivi 😃😃😃😃😃

Wakuu kumbukeni kwenye hizi dating app kuna watu wa kila aina, wapo wanawake wana tabia nzuri kabisa za kuwa mke wa mtu na unaweza ukamuotea huko

Kitu cha msingi cha kuzingatia usiingie huko kwenye dating app focus yako ikiwa ni kupata mtu sahihi, kule ingia kama sehemu ya ku refresh mind tuu, ikitokea ukabahatisha basi hiyo ni bahati yako, ikiwa kinyume chake pia kubaliana na hali
 
Mtaani hamna watu? wameisha?

Bongo hizo apps ni kwa ajili ya wauzaji na wanunuaji kukutana. Unapata pisi inakufuata ulipo fasta kuliko ambulance au fire. Pia wala nauli wamejaa huko pamoja na matapeli.

Ingia field, mwanaume face your fears tongoza, mwanamke jiweke feminine utongozwe.
🤣 halaf watu cjui wanaogopa nin kutongoza wakat hao dada walioko uko mitaani ndo hao hao waliojiunga na izo dating site
 
Back
Top Bottom