Mambo ya kizingatia kama unataka kwenda China kwa safari ya kibiashara

Mambo ya kizingatia kama unataka kwenda China kwa safari ya kibiashara

Siku nyingine toa credit kwa muandishi wa andiko maana hivi ni from experience na sio copy and paste tu ndio maana unashindwa jibu maswali vizuri. All in all unaweza kupata mawazo ya Biashara na kujifunza juu ya Biashara China bure kwenye page zangu za Instagram, X na tiktok kama @kelvinkibenje
 
Ndio maana hata kujibu maswali ya watu huwezi acha uchizi
Chizi ni wewe. Swali Gani halijajibiwa? Briefly, Sina muda wa kusoma comments zote, wanao ni quote ndiyo ninaowajibu kwani ndiyo nonaopata notification zao
 
BIASHARA CHINA INATENGEZA MATAJIRI WENGI, Tena vijana na wewe unaweza kuwa mmoja wao.
.
lakini pia unaweza kupoteza mtaji wako wote ikiwa kuna mambo hutoyafaham mapema.
.
Sasa kabla hujaenda china, hakikisha unayajua haya mapema ili safari yako iwe ya mafanikio makubwa.

1. Pata passport yako Mapema, Ni vizuri pia kama Mfanyabiasha mwenye malengo makubwa kuwa na passport.

2. Fatilia Visa yako. Ubalozi wa china uko Masaki. Pata visa yako mapema ili ukate tiketi mapema upate kwa bei nzuri.

3. Pata tiketi yako mapema ya ndege. Mashirika ya ndege ni mengi na kila shirika lina uzuri wale uharaka, mizigo, chakula na huduma. Nauli ya kwenda China na kurudi ni kati Tsh 3,000,000/- ( bei hubadilika kulingana na season na muda uliokata na shirika).

3. Pata tiketi yako mapema ya ndege. Mashirika ya ndege ni mengi na kila shirika lina uzuri wale uharaka, mizigo, chakula na huduma. Nauli ya kwenda China na kurudi ni kati Tsh 3 ( bei hubadilika kulingana na season na muda uliokata na shirika).

4. Usiende china hujui utanunua nini, Usiende china kwa lengo la kuagizisha bidhaa kwa oda hasa kama ni mara ya kwanza. Kama una mtaji mkubwa Fahamu ni mji gani bidhaa zako utapata na utafikaje kwenye huo mji kutoka Ghuanzou.

5. Download app ya Wechat, Hii ni kama whatsapp kwa china, Itakusaidia kukusanya mawasiliano ya supplies na kuwasiliana

6. Pata laini ya China ukifika. Itakusaidia kwenye mambo mengi

7. Kabla hujaanza safari ni muhimu kutambua ni nani ambaye atakupokea, na utafika hoteli gani.
8. Download VPN kabla ya kwenda China kwani huko hutoweza kutumia Google, Whatsapp, instagram, tiktok nk bila VPN hata ukiwa kwenye Wi-Fi ( naweza kukupatia pia laini za china au Dubai kabla hujaenda ili ukifika uwasiliane na wenyeji wako na utumie mitandao yote bila VPN

9. Download app ya DiDi ( ndio Uber /bolt za china) itaokoa gharama zako kuliko kutumia Tax za kawaida

10. Tafuta mtu akufundishe kutumia metro🚇( ni Tren za haraka za ardhini kama daladala) ni Rahisi na nafuu mno.

11.kama una mtaji wa chini ya 15M na hutaki kuupoteza usiende china kwanza, kwa competition ya sasa ni ngumu bidhaa za 10M kukupa 20M ambayo itarudisha gharama zako, mtaji na faida. Ila China ni sehemu nzuri kwenda kujifunza Biashara hivyo kama lengo ni kujifunza nenda

12. Mara ya kwanza, usiweke kukaa chini ya week moja labda kama una mwenyeji. China masoko yako mbali, utahitaji kutumia muda mwingi kupata machimbo

13. Ukifika kusanya business card za kutosha za suppliers. Zitakusaidia

14. Beba kiasi cha pesa ya Kichina (RMB) kabla ya kwenda.

15. Njia za malipo ukiwa china ni cash na mobile payment kama Alipay & Wechat pay zaidi ( hakikisha unakua na Alipay)

16. Beba dawa zako kama unajijua una ka_ugonjwa Kako au unashikwa mafua kirahisi, kichwa nk.

17. Ukiwa china jichanganye na wenzako hasa wenyeji wa china, Hii itakusaidia kujua fursa zaidi na machimbo.

18. Kunywa maji ya chupa ya dukani na usipendelee kunywa maji ya Bomba
Pia washauri wawe makini na hao wenyeji wa kibongo, maana huwa wanatabia ya kukuongezea bei kwenye bidhaa unazonunua then later wanaenda fata cha juu chao kwa mchina
 
Back
Top Bottom