Kipengele namba 4. Ulichoongelea kutoka D kwenda R wakati gari linatembea, ulivoeleza sio sahihi,
Tukianzia kwenye gari la manual, wakati linayembea huwezi ingizi revers gear, ukijaribu kuingiza inakwangua sana na kamwe haitakubali kungia, hiyogear ndani ya gearbox inazunguka anticlockwise, hivo ni mpka gari lisimame ndo inaingia"
Tukirudi kwenye mada, hizi gari za outo zimeadvance zaidi kitecnologia na hata kiutendaji, kumbuka hizi gari kwa asilimia kubwa zinaendeshwa na systeam ya umeme, na zinakuwa na controlbox ambayo ndo brain ya gari,
Unavoshift gear ukiwa unaendesha unakuwa ni umeswitch tu umeme ambao utatuma taarifa kwenye controlbox ya gearbox halafu controlbox ndo itaruhusu gearbox kuingage hicho ulicho aply, yote haya hufanyika kwa nukta hiyo hiyo! ( kuna gearbox ambazo zina waya za umeme tu zilizoingia ndani yake, na kuna zenye gear linked pamoja na waya hizi ndo za kizamani kdg)
Kwenye manual ukiingiza revers wakati unaenda mbele, kwa mfano gia ikiingia ama itakata crankshaft au gearbox yote ivurugike ivunje meingear,
Kwa outo yenyewe ni tofauti ( ina akili) haihitaji nguvu wala ushindani, uki apply revers wakati inaenda mbele, itashift vzr tena kirahisi tu, lakini controlbox itaondoa taarifa ya mwanzo (kwenda mbele) na haitatuma taarifa ya pili (revers) kwa sababu tu haijafuata procedure. Hivo gari itabaki NEUTRAL hata ukipoga resi na shifter ipo kwe revera itaendelea kuserereka kwenda mbele. Ni mpaka usimame ushift tena ndo itarespond. Na huu ndo mfumo wake wa kujilinda dhidi ya vilaza!