Hii ni kwa kufuta mpangilio wa gia jinsi zilivopangwa mkuu! Na mwendo, kwenye outo ukikosea gari linabaki neutral, unavotumia gia kupunguza mwendo kinachotokea ni badala ya ingine kuendesha gari, sasa ni ingine ndo inayozuia gari lisiende, sasa kama mwisho wa injin ni RPM 6000 na upo kwenye D unaendeshea rpm 3000 ukirudisha kwenye D2 ( changedown) utaona rpm inapanda, sasa kama ukitoka D uko speed ukashusha gia leaver mpaka L. ambapo ikikubali kufanya kazi RPM ya injin italazimishwa kufikia zaidi ya 6000 (ambayo ni nje ya kipimo) haita kubali itajiacha neutral"
Kama ilivo kwa manual, ikiwa gear namba 5 iko speed, ukataka kuingiza namba moja haitakubali, na sababu ni kama ikiingia inaenda kupandisha rpm ya ingin nje kabsa ya kipimo, lazima kimoja kiharibike, injin au gearbox! Kiufupi usiruke gia wakati wa changedown ukiwa kwenye mwendo mkubwa haitakubali iwe manual au outo"