Mambo ya kuepuka kama wewe ni dereva wa Automatic Transmission Car

Mambo ya kuepuka kama wewe ni dereva wa Automatic Transmission Car

G.25

Hii elimu kubwa saana, naomba nikushukuru maana pia umenifungua ufahamu wangu kuhusu magari pia. Labda iweke vizuri hii elimu, gia umetaja mbili za kuteremkia mlima mkali D2 mpaka L.

"unachotakiwa kufanya ni kushift leaver kwenda kwenye gia kubwa kutoka D unaenda D2 mpaka kwenye L"

Hebu weka vyema D2 na L ndiyo za kushukia mlima au ulikuwa unaelekeza avuke D2 kuelekea kwenye L ambayo ndiyo gia ya kushukia mlima mkali??

Natanguliza shukrani mkuu
Hauwezi kutoka D kwenda L moja kwa moja bila ya kupitia D2! Ukilazimisha D kwenda L moja kwa moja itaenda kwenye Neutral maana ujumbe utakaotumwa kwenye Control Box utakuwa ni Syntax "Error" kama ifanyavyo ukihama from D to R!
So the best option ni kutopanick, shift from D to D2 then baada ya sekunde kadhaa/chache peleka kwenye L.
 
Namaanisha gari likiwa linatumika kwenye spidi kali..yaani kubadili gia chapchap..kama hivo D UENDE R HAPO KWA PAPO
Unajua kuwa kutoka D kwenda R kuna N? Kwanini imewekwa hapo? Ukiisukuma kwa bahati mbaya gear lever itahama kutoka D kwenda N. Kutoka N kwenda R haiingii hadi gari isimame ukanyage brake pedal.

Mtu akitoka D then N then R ameamua kwa makusudi kuharibu gari na huyo mtu hamna mafunzo yatakayomsaidia.
 
Sasa mkuu kwenye automatic ukiwa uko kwenye D halafu unaraka urudi nyuma si utasimama kwanza ndio upeleke Gear Lever kwenye R?? au ni automatic ipi wewe unayodhani
Tena kuna N katikati ya D na R.
 
Unajua kuwa kutoka D kwenda R kuna N? Kwanini imewekwa hapo? Ukiisukuma kwa bahati mbaya gear lever itahama kutoka D kwenda N. Kutoka N kwenda R haiingii hadi gari isimame ukanyage brake pedal.

Mtu akitoka D then N then R ameamua kwa makusudi kuharibu gari na huyo mtu hamna mafunzo yatakayomsaidia.

Sasa mkuu mbona mnanichanganya wewe na G.25 yeye amesema ukishift kutoka R kwenda D gari likiwa kwenye motion haina shida linakubali bila hata ya kusimama!!... Which is which?? Ni mimi sijamuelewa au nimeQuote vibaya...mkuu G.25 karibu
 
Yeah lakini mpaka usimame kwanza au hata ukiwa kwenye mwendo wa taratibu??
Kinachoshauriwa ni usimame kabisa ndio uhamishe from D to R lakini wengi huwa wanahamisha kabla gari haijasimama kabisa.
 
Sasa mkuu mbona mnanichanganya wewe na G.25 yeye amesema ukishift kutoka R kwenda D gari likiwa kwenye motion haina shida linakubali bila hata ya kusimama!!... Which is which?? Ni mimi sijamuelewa au nimeQuote vibaya...mkuu G.25 karibu
Kuna zile unageuza faster faster unajikuta gari kabla haijasimama kabisa ushaweka N then unatupia R hata gari utaisikia inasimamishwa na gear. Lakini sio uko 30kph eti unaweka R from D its impossible unless umeamua kuharibu gari.
 
Sawa mkuu nimekuelewa hapo sasa
 
Teknolojia ya vyombo vya usafirishaji inabadilika kwa kasi sana kadri miaka inavyokwenda. Leo hii makampuni mengi yanayotengeneza magari yanazalisha magari mengi yenye uwezo wa kujibadilisha gia yenyewe (Automatic Transimission Cars) tofauti na hapo zamani.

Kuna tofauti kubwa sana ya kiutendaji kati ya magari haya ya automatic na yale ya manual. Magari haya ya automatic ni rahisi sana kuyaendesha kwa kuwa sehemu kubwa ya mfumo wa utendaji wake ni wa kisasa kabisa. Ila kuna vitu vya msingi usivyotakiwa kufanya wakati unaendesha magari haya ili kuongeza maisha ya gear box (Transmission Box).

1. Usipaki gari lako bila kubana Parking Brake

Mara nyingi madereva wamekuwa wakipaki magari yao kwa kuweka transmission handle kwenye herufi P, bila ya kuengege Parking Brake. Kama wewe ni mmoja wao tafadhali acha kufanya hivyo kwa sababu Parking Pawl, kichuma kinachoizuia gari kuondoka wakati imewekwa kwenye Park ni kidogo sana na hakijatengenezwa kwa kazi hiyo. Hivyo ikitokea mtu akaligonga gari lako kidogo kuna uwezekano mkubwa wa gari lako likaanza kutembea kama ulikuwa hujalizima. Pia kipande cha Parking Pawl kilichovunjika kinaweza kikaleta matatizo makubwa katika gear box yako.

2. Epuka kutumia Gear kubwa kama brake

Mara nyingi wakati unashuka milima mkali na gari ya manual huwa tunashusha gari katika gear kubwa kama namba 2 au 1 ili kupunguza kasi ya mwendo. Usijaribu kufanya hivyo kwa gari ya automatic transmission, kwa sababu itasababisha kuchubuka na kulika kwa vyuma vya ndani ya transmission box na kuleta usumbufu hapo baadae.

3. Usibadili Gear wakati mzunguko wa engine wa gari ni mkubwa

Kubadili gear wakati mzunguko wa engine wa gari lako ni mkali ni kitu kibaya kwa sababu itasababisha kulika kwa clutch plates za ndani ya gear box yako na kukuletea matatizo hapo baadae.

4. Usibadili Gear ya mbele kwenda ya nyuma moja kwa moja au ya nyuma kwenda ya mbele moja kwa moja bila ya kusimamisha gari kwanza

Simamisha gari lako kabisa kabla ya kuamua kubadili gear ya kutoka mbele na kurudi nyuma au vinginevyo. Kufanya hivyo bila kusimamisha gari lako kutapelekea uharibifu mkubwa katika gear box yako.

5. Hakikisha engine inapata joto la kutosha kabla ya kuanza kuendesha gari lako

Kama ulilipaki gari lako muda mrefu sana no bora ukaliacha kwa muda baada ya kuliwasha ili engine ipate joto la kutosha na kufanya vimiminika vyote vya katika gari kutawanyika na kufika katika maeneo husika katika kiwango stahiki.

6. Usipitishe muda wa kufanya service mara kwa mara

Wengi tumekuwa na tabia ya kupitisha muda wa kuyafanyia service magari yetu mara kwa mara. Maisha na ubora wa gari lako hutegemea sana muda wa service hasa kubadili oil za engine na transmission box, brake pads, air filter na vingine vingi.

Karibuni kwa nyongeza na hoja nyingine kama zipo tujifunze

Credits: www.swahilitech.com
kuna hydrolic zinauzwa lts 4 za toyota genuene zinauzwa laki na 20 nimeambiwa ukiweka hiyo bas hufanyi seevise hadi km elf 50 hadi elf 60 je ni sahihi hilo na oil qurtz elf 5000 ni km 5000 je nanyenyewe sawa maana mimi nafanya kila mwezi nafilisha km 3500 au zaid kidogo haifiki elf 4
 
Ngoja wataalam waje aisee..
 
Lakini niliwahi kusikia kuwa hizo hydraulic OG ndio nzuri kwa gari...hizi fake sio nzuri....Anyways siwezi sema mengi coz sijathibitisha kiundani zaidi...
 
Kipengele namba 4. Ulichoongelea kutoka D kwenda R wakati gari linatembea, ulivoeleza sio sahihi,
Tukianzia kwenye gari la manual, wakati linayembea huwezi ingizi revers gear, ukijaribu kuingiza inakwangua sana na kamwe haitakubali kungia, hiyogear ndani ya gearbox inazunguka anticlockwise, hivo ni mpka gari lisimame ndo inaingia"
Tukirudi kwenye mada, hizi gari za outo zimeadvance zaidi kitecnologia na hata kiutendaji, kumbuka hizi gari kwa asilimia kubwa zinaendeshwa na systeam ya umeme, na zinakuwa na controlbox ambayo ndo brain ya gari,
Unavoshift gear ukiwa unaendesha unakuwa ni umeswitch tu umeme ambao utatuma taarifa kwenye controlbox ya gearbox halafu controlbox ndo itaruhusu gearbox kuingage hicho ulicho aply, yote haya hufanyika kwa nukta hiyo hiyo! ( kuna gearbox ambazo zina waya za umeme tu zilizoingia ndani yake, na kuna zenye gear linked pamoja na waya hizi ndo za kizamani kdg)
Kwenye manual ukiingiza revers wakati unaenda mbele, kwa mfano gia ikiingia ama itakata crankshaft au gearbox yote ivurugike ivunje meingear,
Kwa outo yenyewe ni tofauti ( ina akili) haihitaji nguvu wala ushindani, uki apply revers wakati inaenda mbele, itashift vzr tena kirahisi tu, lakini controlbox itaondoa taarifa ya mwanzo (kwenda mbele) na haitatuma taarifa ya pili (revers) kwa sababu tu haijafuata procedure. Hivo gari itabaki NEUTRAL hata ukipoga resi na shifter ipo kwe revera itaendelea kuserereka kwenda mbele. Ni mpaka usimame ushift tena ndo itarespond. Na huu ndo mfumo wake wa kujilinda dhidi ya vilaza!
Nadhani mleta uzi haja-practice kile alicholeta, nakumbuka nilikuwa najifunza gari kwa kugongea sehemu sasa nilivyojuajua kwenye kuingiza gia namba 4 nilikuwa naingiza huku naogopa kwamba isije ikaenda reverse (si unajua tena ukiwa lena gia namba mbili unaweza ukaingiza 5). Sasa ndo nikaambiwa haiwezekani gari kuingia reverse wakati inakwenda na kweli nikatest na confidence ikaongezeka na hata automatic haiwezekani kuingia reverse
 
Hiyo no 2 embu nieleweshe vizuri. Nnavyoelewa mm hizi L,2,1 ziliwekwa pia kama sehemu ya engine braking. Mathalani ukiwa kwenye mteremko mkali na gari ikawa na mzigo basi hizi gia zinasaidiana na breki za kawaida kuhakikisha dereva anaimudu gari.. Otherwise kwann ziliwekwa? Nieleweshe mkuu
 
Ni kweli mkuu...gari sijaendesha sana..nipo katika hatua za mwanzo mwanzo..kwa hiyo siyo kila kitu najua.....Ushanifahamu
 
by the way gari za kisasa likiwa linatembea kwenda mbele mara kwa bahat mbaya ukataka weka R huwa haikubali had lisimame hivo linakusaidia kutoharibu vitu
Apa alichomaanisha kwamba magari ya automatic transmission yanakuwa na
P, R, N, D, D2, L
Sasa kwa uendeshaji wetu unakuta mtu kapiga moto [emoji469] mwingi na Gari imetembea au ipo katika mteremko anachofanya anaweka Neutral (N) ili kufanya Gari iserereke bila kufyonza mafuta.
Na udereva huuu wanafanya sana watu wa daladala wanaoendesha automatic transmission
 
Hiyo no 2 embu nieleweshe vizuri. Nnavyoelewa mm hizi L,2,1 ziliwekwa pia kama sehemu ya engine braking. Mathalani ukiwa kwenye mteremko mkali na gari ikawa na mzigo basi hizi gia zinasaidiana na breki za kawaida kuhakikisha dereva anaimudu gari.. Otherwise kwann ziliwekwa? Nieleweshe mkuu
Yeah ni kweli usemavyo L 2 & 1 huwa zinakuwa kama Engine braking..Hizo ni low gears ambazo hutumika kupandia milima na miteremko mifupi (isio mikali sana)
 
Nadhani mleta uzi haja-practice kile alicholeta, nakumbuka nilikuwa najifunza gari kwa kugongea sehemu sasa nilivyojuajua kwenye kuingiza gia namba 4 nilikuwa naingiza huku naogopa kwamba isije ikaenda reverse (si unajua tena ukiwa lena gia namba mbili unaweza ukaingiza 5). Sasa ndo nikaambiwa haiwezekani gari kuingia reverse wakati inakwenda na kweli nikatest na confidence ikaongezeka na hata automatic haiwezekani kuingia reverse
manual rivas inaingia vizuri tu
 
Back
Top Bottom