Uchaguzi 2020 Mambo ya kujibizana kwenye kampeni ya nini wakati mnaweza kumaliza kila kitu kwenye mdahalo?

Uchaguzi 2020 Mambo ya kujibizana kwenye kampeni ya nini wakati mnaweza kumaliza kila kitu kwenye mdahalo?

Mtuflani Official

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2019
Posts
1,952
Reaction score
4,416
Leo nimemskia Rais Magufuli akijibu hoja ya Lissu kuhusu CHADEMA kutengeneza Majimbo wakipata madaraka.

Dkt. Magufuli ameeleza kwamba mfumo wa majimbo utakua mwanzo wa mfarakano, japo sielewi mfarakano utatokana na nini maana sioni mifarakano USA, Nigeria, India na nchi zingine.

Sisi kama wapiga kura hatupendi kuona mnajibishana kwenye majukwaa. Tunamuomba baba yetu kipenzi Amri Jeshi Mkuu, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akubali mdahalo kati yake yeye na Tundu Lissu ili kumaliza sekeseke lililopo.
 
😆😆😆 unataka kumkimbiza mtu eeeeh?

2519456_1600122094063.png
 
Tumuulize kwanza yeye ni mkatoriki kindakindaki.

Je, kuna mtafaruku wowote unaaotokea hko kwa sababu wakatoriki wamegawanywa na kuongozwa kwa majimbo? Kama jibu ni hapana kwann majimbo ya serikali/ nchi yalete mtafaruku? Ivi ana PhD kweli huyu mgombea
 
Leo nimemskia Rais Magufuli akijibu hoja ya Lissu kuhusu CHADEMA kutengeneza majimbo wakipata madaraka.

Mh Magufuli ameeleza kwamba mfumo wa majimbo utakua mwanzo wa mfarakano, japo sielewi mfarakano utatokana na nini maana sioni mifarakano USA, Nigeria, India na nchi zingine.
Nchi zote walizopigana wa kwa wao yaani civil war ndio wana huo mfumo kuanzia hapo Kenya marekani India Afrika ya kusini Nigeria nk wote hao walitwangana civil war wakaamua kugawana nchi kwa majimbo .Kenya tu hapo utawala wa majimbo ulianza baada ya wakikuyu na wajaluo kutwangana barabara Kikwete akaenda kuwasaidia

Ndio majimbo yakaibuka baada ya kutembezeana marungu na mapanga wao kwa wao
 
Muulize Mwenyekiti wako akiwa kama Mkatoliki ambalo linajiongoza kwa Majimbo,je limeleta mtafaruku?
 
Nchi zote walizopigana wa kwa wao yaani civil war ndio wana huo mfumo kuanzia hapo Kenya marekani India Afrika ya kusini Nigeria nk wote hao walitwangana civil war wakaamua kugawana nchi kwa majimbo .Kenya tu hapo utawala wa majimbo ulianza baada ya wakikuyu na wajaluo kutwangana barabara Kikwete akaenda kuwasaidia

Ndio majimbo yakaibuka baada ya kutembezeana marungu na mapanga wao kwa wao
You are congenital liar
 
Wanasiasa wenyewe wa Tanzania hawako serious na siasa zao Mimi niwe serious nipate faida gani?
Kwa niaba yangu nakuomba ukiona uzi unakuvutia kuchangia positive comment pita tu mwanangu, maana nchi inatakiwa kupata tiba ndani ya miezi hii miwili.
 
Back
Top Bottom