Mambo ya kuzingatia ukifikia nyumbani kwa mtu

Mambo ya kuzingatia ukifikia nyumbani kwa mtu

Kwa jinsi nilikuwa naona wageni wanavosemwa vby nyumbani kwetu.niliamua siendi KWA ndugu zaidi ya kusalimia au kuwa naenda na kuondoka.naweza kula msosi ila kulala na kuamkia hapo NEHIII.of coz hata mi sipendi wageni wasumbufu ambae akija ht donesheni hatoi.hata kusaidia usafi hakuna.utakuwa unapeleka makosa
Unaandika mavi.

Una uharo kichwani?

Fikiria umetoka Mtwara, umemleta mama yako Muhimbili hospital kufanyiwa Chemotherapy.

Matibabu yanachukua week tatu na siku kadhaa...

Unajua gharama za kukaa lodge siku 40+?

Wakati huo kaka yako amejenga Chamazi
 
Unaandika mavi.

Una uharo kichwani?

Fikiria umetoka Mtwara, umemleta mama yako Muhimbili hospital kufanyiwa Chemotherapy.

Matibabu yanachukua week tatu na siku kadhaa...

Unajua gharama za kukaa lodge siku 40+?

Wakati huo kaka yako amejenga Chamazi.
Mama Debora za asubuhi?
Hongera kwa mvua ya leo najua kama ulifanya tendo umefurahia kwakuwa kuna ubaridi.
Hongera kwa mawazo yako, hili ni jukwaa huru na unaruhusiwa ila tu lugha walau iendane na JF na pia kama mama na mwanamke mwenzangu:
Lakini haijalishi unauguza ama la , salimia , sepa waachie watu wale maisha yao.
Nakupenda .
 
1. NJOO NA MAHITAJI YAKO MADOGO-DOGO
Njoo na mswaki wako, sabuni yako ya kuogea na dawa yako ya meno, taulo na mahitaji yako mengine madogo-madogo. Kuna wageni wanaomba hadi nguo za...... kwa wenyeji ,sio vizuri.

2. USIFUNGUE FRIJI WALA MAKABATI
Usifungue friji ya wenyeji au makabati bila kuambiwa ufanye hivyo. Mgeni unasikia kiu omba maji kwa wenyeji sio unaanza kufungua friji bila ruhusa eti unatafuta maji ya kunywa. Ukihitaji kitu omba kwa wenyeji sio kuanza kupekuapekua.

3. USIBAKI SEBULENI
Wenyeji wakiingia kulala usibaki sebuleni unatazama TV ingia chumbani kwako. Sambamba na hilo mkiwa mnatazama TV sebuleni usianze kushika rimoti na kubadili channel bila ruhusa ya wenyeji.

4. USIZIDISHE MUDA WA KUKAA
Ukifika ni vizuri uwajulishe wenyeji wako utakaa hadi lini na usizidishe muda labda wenyeji wakuombe wenyewe. Kama uliwaambia utakaa wiki ikifika ondoka sio unasubiri hadi wakuulize unaondoka lini.

5. USIINGILIE MAZUNGUMZO
Ikatokea wenyeji hasa mke na mume wana mjadala wao wa mambo yao binafsi usipende kuingilia na kujifanya mshauri bila kuombwa kufanya hivyo. Labda wanapanga wapike nini siku hiyo mgeni usharukia kuchagua chakula kaa kwa kutulia. Katika jambo lolote wanalojaldili subiri uombwe ushauri.

6. USI-TEMBELEE MAJIRANI
Usitembelee majirani "ooh jamani mie ndo mpwa wa huyu jirani yenu nimeona niwasalimie".... Pata ruhusa ya wenyeji wako kwanza kabla hujaanza kuzunguka kwa majirani. Sambamba na hilo usilete wageni hapo ulipofikia bila kumtaarifu Mwenyeji wako.

7. KULA VYAKULA VILIVYOPO
Jitahidi kula chakula kinachowekwa mbele yako na kama vinakupa shida basi nunua hivyo vyakula sio "ooh maharage yananiumiza tumbo" kanunue nyama ulete wakupikie.

8. USITUMIE VIFAA VYA WENYEJI
Usianze kutumia vifaa vya wenyeji bila ruhusa mfano unaanza kuwasha computer au vifaa vya mazoezi . Usianze kuzunguka nyumba na kuingia kila mahali labda mwenyeji wako akuoneshe sio kukagua nyumba nzima na kuingia vyumba ambavyo hujaambiwa.

9. SAIDIA KAZI
Tandika kitanda chako na safisha chumba ulichopewa kulala. Saidia kazi za hapo nyumbani ulipofikia labda wakukataze wenyeji. Sambamba na hilo utakapoondoka acha chumba katika hali ya usafi kama ulivyokikuta.

10. USIJE MIKONO MITUPU
Usije mikono mitupu beba zawadi kidogo kwa wenyeji wako.
Umenena yote. Mwenye kusikia na asikie
 
Unazijua gharama za kukaa hotel siku 40+ ukiuguza mgonjwa Muhimbili wewe?
Inategemea mtu na mtu, wapo watu wanaishi hoteli miaka hata mitatu, wanakwenda likizo dubai na mareknai, kila birtday wanazawadiwa magari ya kifajhari, sasa KAMA UMEYAKOSEA maisha -usiwajumuishe watu wote.
 
Namkumbuka Baba yangu Mdogo mmoja akitoka Kijijini anakuja na Vyakula vyake kama Mchele n.k vinapikwa wanakula vikiisha tu anasepa🤠🤠🤠🤠
 
Back
Top Bottom