Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Mkuu hata hiyo wastanj unayosema jamaa wanazingua kiasi kwamba inanibidi nisilaze kabisa
Unaonekana ni mshamba, Siti ziko moderate na unaweza kukaa vyema tu, ukiona hivyo hujaishusha kwa wastani. Hakuna mtu atakwazika kwa kuilaza kwa wastani, kwanza muomba wa nyuma yako kuwa unajisikia kulala kidogo hivyo unaomba kuilaza kidogo siti yako.

Most of guys wanaelewa sana.
 
1. Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae. Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kuuliza "Eti hapa tumefika wapi?" 🙄🙄🙄
Hii ilinikuta uswahilini, niliwapita wakaazi , nilipotelea chochoro, nikatokezea bafuni
Nilivyorudi kuuliza njia nkikaambiwa tulidhani unaenda kuoga tulikuwa tunajadili wa kukuletea maji
 
Hii ni muhimu mno. Nilikuwa nakwenda Morogoro na basi la Abood la mwisho kabisa kutoka Dar.

Nilipata siti ya mwanzo kabisa nyuma ya dereva. Nilikuta kuna binti tayari keshakaa jirani ya siti yangu. Kama ilivyo uungwana nikamsalimia. Binti alinishusha na kunipandisha akachuna.

Nilikuwa nimechoka na mambo yangu, sikumtilia maanani nikauchuna na simu yangu. Tulipofika chalinze nilinunua maji na korosho, kama ilivyo uungwana nimkamkaribisha, demu, kimya. Hapo hapo na yeye alinunua maji akatoa noti ya 10,000. Jamaa akamwambia hana chenji na bus linataka kuondoka. Nikamwambia jamaa (ni wale wanaouza ndani ya bus) ampe nikamlipa. Kwa aibu akatoa asante ya chini chini. Sikumjibu.

Kufika Morogoro sasa, kumbe ilikuwa anaenda kukutana na mwanaume. Jamaa kila akipigiwa simu hapokei na mwisho akazima simu kabisa. Nililijua hili maana alianza kupiga simu toka tupo Mikese.

Nilipakia spare kwenye boot, hivyo tulipofika Moro ilibidi niwe mpole mpaka mizigo ya wengine iishe. Ndio bi dada ikabidi ajilete kipole kuuliza kama mimi ni mwenyeji Morogoro. Nikamwambia si mwenyeji nimekuja mara moja nageuza kesho yake.

Ikabidi sasa usister duu aweke pembeni aanze kufunguka ukweli. Kuwa alikuja kukutana na bwana 'ake na ndie aliemtumia nauli.
Ilikuwa ana Sh. 10,000 tu mfukoni na hajui pa kwenda maana mshkaji kaingia chaka.

Ikabidi nimwambie asubiri nichukue mizigo yangu halafu nitaona cha kumsaidia. Uzuri mwenye spare ilikuwa anazipokelea hapo hapo Msamvu. Nikaenda kuchukua chumba lodge na mgeni wangu nyuma. Baada ya hapo hatukutongozana tena. Alijuwa wajibu wake na maringo alitupa pembeni tena.

Msela wake alikuja kumtafuta asubuhi tukiwa tunajiandaa kuondoka akiomba samahani kuwa simu ili stuck touch akashindwa kupokea. Itoshe kusema kuwa jamaa alitukanwa kila tusi la duniani, mimi na cha maringo wangu tukarudi dar na kuendeleza libeneke kwa miezi kadhaa mbele mpaka nilipoamua kumpotezea kutokana na demu kuwa na shida za kila siku kuliko hata mkimbizi wa Sudan.
Shida za kila siku ndio zilimfanya Jamaa wa Moro aingie mitini.
 
Wakati watu wakiwa wanakata tiketi wanaangalia majina. Siku moja nasafiri, kuangalia list ya abiria kwenye chat, nikaona jina Irene Emmanuel si nikajiweka pembeni yake. Kilichonipata ndio hiki sasa!!!!
Kumbe zigo lenyewe ndio hili, nilisafiri kwa kukalia nusu tako toka Dar hadi Kigoma.

View attachment 2594669
Mkuu, hukufidia mateso ya kukaa nusu tako toka Dar hadi Kigoma, ungemuomba hata akunyonye japo kwa kuibia wakati umemfunika shuka ili abiria wengine wasimuone.
 
Umenikumbusha one time kuna huyu binti kwenye basi la mkoa alileta huu uswahili. Amepanda kwenye basi amevaa jeans, sweater, na kablouse. Basi hana hata pochi yaani yupo kisela sana.

Kilichotokea ni period ilimuanza ghafla bila kujua. Kilichofanya nijue ni alivua sweater lake na kulitumia kama kujifunika sasa mimi nilikuwa na sweater na zile shuka za kimasai. Nikamuuliza mbona umevua sweeter na gari wamewasha AC haikutesi?!

Akajibu kama vile mtu mwenye mawazo na aibu fulani. Ilinichukua dakika chache kunotice kuwa hakuwa sawa na nikashajua huyu ametumia sweater kujificha. Nikamwambia kwa sauti ya chini sana unahitaji msaada. Hakunijibu zaidi ya kuinama kama anaona aibu halafu anaweka lile tabasamu la aibu fulani.

Nikamwambia niandikie kwenye sms unataka msaada gani. Nikampa simu yangu aandike namba yake nikamtext akaanza kuchat akanambia ameingia Period hapo hana uhakika na kinachoendelea ila anahisi amechafua siti sasa hajui pa kuanzia.


Aiseee ni MUNGU tu alisimamia ile situation maana gari lilikuwa na utingo mwanaume tu. So ikabidi nimfuate nimpange kuwa atusaidie wakiona hata kituo cha mafuta wasimame konda akanielewa. Tukasimama akasema abiria tuchimbe dawa kidogo. Watu wakaanza shuka. Akachukua sweta akaliweka pale kwenye siti halafu nikampa shuka langu la kimasai akajifunika mwili mzima so muda tunatoka nashuka nae hakuna mtu alishtukia chochote hadi tunafika chini. Nikamwambia atangulie chini me nakwenda tafuta pedi. Nikaenda mnunulia duka liko huko barabarani kipande kidogo toka pale kwenye sheri nikamletea.

Akajiweka sawa suruali yake ilikuwa imechafuka akaisuuza na maji akavaa hivyo hivyo nikamwambia valia na hilo shuka la kimasai. Tukarejea kwenye gari. Aisee ikawa kama ni mke wangu sasa namna tulivyorudi na kukaa kwenye gari alijiegemesha kwenye kioo me namwambia niegemee kama unataka kulala.

Tulishuka sote stand ya Moshi alikuwa anataka kwenda nikamwambia sidhani kama utakuwa katika hali nzuri kuendelea na safari katika hali hiyo na muda umekwenda twende nyumbani sio mbali na hapa ukaweke mambo sawa uwe safi kesho utaendelea na safari ndugu zako waelezee situation wakitaka watumie picha kabisa halafu tukimbie na huu msala wa kuchafua siti.

Akakubali. Tulishuka sote akafika nyumbani akatoa nguo zote akazifua na kuzianika. Ilibidi nimnunulie kufuri mpya na pedi zingine za brand nzuri.

Nilimpa risala sana ule usiku. Kwamba kwann mtoto wa kike unasafiri kirahisi vile huoni namna umejihatarisha. Yaani unasafiri haubebi kitenge hata viwili na hata pedi tatu za dharula maana hata usipopata wewe anaweza pata mwanamke mwenzako ukamsitiri. Nikamwambia sasa usingekutana na mimi leo si ungefedheheka sana.

Kesho yake nikamsindikiza jioni aende kwa kwao huko Arusha. Na baada ya hapo tuliendelea kuwasiliana she is someone very close to me now.
Jamaa unajua Ku-care. Bonge la movie yaani. Hongera sana.
 
Kama una watoto wadogo zaidi ya mmoja lazima uchukue siti yote ya watu wawili.
Kuna safari nimesafiri na abiria ana watoto wawili na kachukua siti moja.
Ni wasumbufu mmoja anaumwa na kuharisha.
Ikawa sina budi kumpakata mtoto mmoja hadi mwisho wa safari.

Usinywe maji mengi kuepuka usumbufu wa mkojo.
 
8. Usipake pafyumu kali za kukereketa wenzio. Sambamba na hilo piga mswaki vizuri ni kero kukaa na abiria anayenuka mdomo hasa anapokusemesha.
Nyongeza:
Kama hutumii maji kutakasa O unategemea zaidi toilet paper, basi hakikisha usafi wa huo mtaa unakidhi viwango vya TBS

Kama tumbo lako hujaa gas ukila beans, basi siku ya safari kula kitu kisicho na gas ili uepuke kusingizia watoto au majirani hewa inapochafuka.
 
Ukikaa seat moja na wala ugoro wanaotema mate hovyo hasa wamasai au wasukuma kulakula kila kitu hapana, na ukipokea simu ongea kwa sauti ya chini tu
 
Kuna siku nilikua nimelewa sana halafu kwenye bus nilipanda kama staff(dereva tunajuana,classmate wangu)....
Sasa ile naingia tu harufu ya konyagi ikasambaa bus lote..

Kuna mwanamke akaropoka"naona mmepakia pipa la komoni humu mnatukera"...kumbe naenda kukaa nae kwenye seat moja,,,nilisafiri kwa manyanyaso...

Mwisho dereva akaniita nikaenda kukaa nae pale mbele akaninunulia na konyagi nyengine...
Utqf*rwa
 
Unaonekana ni mshamba, Siti ziko moderate na unaweza kukaa vyema tu, ukiona hivyo hujaishusha kwa wastani. Hakuna mtu atakwazika kwa kuilaza kwa wastani, kwanza muomba wa nyuma yako kuwa unajisikia kulala kidogo hivyo unaomba kuilaza kidogo siti yako.

Most of guys wanaelewa sana.
I wish ungekuwepo uweze kusadiki ninayoyasema, anyway inawezekana me ni mshamba kweli
 
Back
Top Bottom