Hii ni muhimu mno. Nilikuwa nakwenda Morogoro na basi la Abood la mwisho kabisa kutoka Dar.
Nilipata siti ya mwanzo kabisa nyuma ya dereva. Nilikuta kuna binti tayari keshakaa jirani ya siti yangu. Kama ilivyo uungwana nikamsalimia. Binti alinishusha na kunipandisha akachuna.
Nilikuwa nimechoka na mambo yangu, sikumtilia maanani nikauchuna na simu yangu. Tulipofika chalinze nilinunua maji na korosho, kama ilivyo uungwana nimkamkaribisha, demu, kimya. Hapo hapo na yeye alinunua maji akatoa noti ya 10,000. Jamaa akamwambia hana chenji na bus linataka kuondoka. Nikamwambia jamaa (ni wale wanaouza ndani ya bus) ampe nikamlipa. Kwa aibu akatoa asante ya chini chini. Sikumjibu.
Kufika Morogoro sasa, kumbe ilikuwa anaenda kukutana na mwanaume. Jamaa kila akipigiwa simu hapokei na mwisho akazima simu kabisa. Nililijua hili maana alianza kupiga simu toka tupo Mikese.
Nilipakia spare kwenye boot, hivyo tulipofika Moro ilibidi niwe mpole mpaka mizigo ya wengine iishe. Ndio bi dada ikabidi ajilete kipole kuuliza kama mimi ni mwenyeji Morogoro. Nikamwambia si mwenyeji nimekuja mara moja nageuza kesho yake.
Ikabidi sasa usister duu aweke pembeni aanze kufunguka ukweli. Kuwa alikuja kukutana na bwana 'ake na ndie aliemtumia nauli.
Ilikuwa ana Sh. 10,000 tu mfukoni na hajui pa kwenda maana mshkaji kaingia chaka.
Ikabidi nimwambie asubiri nichukue mizigo yangu halafu nitaona cha kumsaidia. Uzuri mwenye spare ilikuwa anazipokelea hapo hapo Msamvu. Nikaenda kuchukua chumba lodge na mgeni wangu nyuma. Baada ya hapo hatukutongozana tena. Alijuwa wajibu wake na maringo alitupa pembeni tena.
Msela wake alikuja kumtafuta asubuhi tukiwa tunajiandaa kuondoka akiomba samahani kuwa simu ili stuck touch akashindwa kupokea. Itoshe kusema kuwa jamaa alitukanwa kila tusi la duniani, mimi na cha maringo wangu tukarudi dar na kuendeleza libeneke kwa miezi kadhaa mbele mpaka nilipoamua kumpotezea kutokana na demu kuwa na shida za kila siku kuliko hata mkimbizi wa Sudan.