Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Basi, tuliosoma Cuba kwa balozi Polepole tumeshafahamu hata hicho kipengele ambacho haujakisimulia!

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

[emoji23][emoji23] Hakuna kipengele nilichoacha acha kujijengea picha la kutisha
 
11. Usile hovyo hovyo njiani hasa vyakula vyenye harufu kali kama mayai na chips.

12. Ukipishana kauli na abiria mwenzako usitumie lugha za matusi, heshimu watu usiowajua.

13. Ukikaa na binti mzuri jitahidi basi kumliwaza kwa stori nzuri na mwisho wa safari omba namba.
13.usisubiri mwisho wa safari kama anashuka katikati?utakosa no...!
no haina formular ya kuombwa either mwanzoni,katikati au mwishoni wa safari.
 
Mwezi ulio pita nlkua naelekea moshi nme panda kweny bus nme kaa na mdada ni mrembo ki ukweli, tatizo lili anzia singida pale alipo anza kurudisha chenchi kupitia dirishani .imagine mtu kila saa ana rudisha chenchi while bus lina enda nli jiskia ovyoo sana na yeye aliona aibu ikabidi ni act normal asiji sikie vibaya lakini moyoni alini kwaza ..
 
1. Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae. Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kuuliza "Eti hapa tumefika wapi?" 🙄🙄🙄

2. Kuwa mstaarabu unapoingia kwenye basi hasa kama tayari unajua siti yako haina haja ya kugombania mlangoni.

3. Sikiliza nyimbo na video za kwenye simu yako kwa kutumia earphones kwani kinachokufurahisha wewe kwa mwingine yawezekana ni kero.

4. Usiongee na simu kwa sauti kubwa hasa mambo yako binafsi kwani hakuna anayehitaji kujua mambo yako.

5. Kuwa mwangalifu unaposinzia epuka kumlalia jirani yako unaposinzia. Sambamba na hilo soma gazeti lako kwa uangalifu sio unalitandaza hadi linagusa pua ya mwenzako.

6. Usilazimishe kuchungulia dirishani kila mara wakati umekaa siti ya katikati, hiyo ni kero kwa aliyekaa dirishani.

7. Kama unasafiri na watoto wakatie siti yao isiwe kero kwa jirani yako. Unasafiri na watoto watatu kwenye siti moja ni kero kwa jirani yako na kwa watoto.

8. Usipake pafyumu kali za kukereketa wenzio. Sambamba na hilo piga mswaki vizuri ni kero kukaa na abiria anayenuka mdomo hasa anapokusemesha.

9. Msome abiria uliyekaa naye kama hapendi kusemeshwa usimsemeshe semeshe, mwache, wengine wana mambo yao kichwani, wengine wanaenda kwenye misiba, wengine wamefukuzwa na waume zao huko walikotoka, sio kila mtu anapenda kuongea safarini.

10. Kama unajijua una tatizo la kutapika safarini jiandae mapema kwa kuwa na vifaa vya kukusaidia kwenye hali hiyo.

Ongezea la kwako hapo kama unalo.
Usivae jezi ya Arsenal unaposafiri
 
Aisee juzi kati nimetoka zangu dodoma narudi dar si nikasema ngoja niende kukata tiketi ya Bm maana ndio gari mara nyingi natumia nikienda zangu dom kwenye mambo yangu sasa nikachelewa ilikuwa kama saa kumi hivi jioni ikabidi nivizie gari za kutoka mwanza aisee nikapanda Isamilo Mungu wangu sirudiii tena panda ilo gari au hayo magari ya kutoka mwanza wasukuma jaman jamani nimepanda gari wamejaaa wasukuma tupu alaf sasa hawana ustaarabu gari halina kiyoyozi wamefunga vioo alaf sisi abiria wa njian tumesimama ukiwaambia wafungue viooo hawataki alaf ndani wamepanda na samaki yani gari lina harufu Mungu mkubwa nikapata siti aisee kuna sijui mmama hat am ustaarabu hana akanyooshaa mkuu kuweka kwenye zile kingo za kuwekea mkono yani aliniboa nikaanza kuniuliza hivi huyu haoni kama mimi nimekaa hapa yani wasukuma jamani hapo kwenye kufunga vioo tu ndio balaa yani siwezi panda tena hayo mabasi yani nilijuta njia nzima niliuwa na mlaani yule mkata tiket kwanza ainidanganya tiketi imeandikwa ally’s shubaamiti wasukuma
[emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukipanda basi za ABC hakuna huo ujinga wa kuingia na chakula,mnashuka hotelini mnakula vizuri tu mnamaliza ndio basi linaindoka,dk 10 kwa chai,dk 30 kwa chakula cha mchana
Napenda sana utaratibu wa ABC kwakweli
 
Umenikumbusha one time kuna huyu binti kwenye basi la mkoa alileta huu uswahili. Amepanda kwenye basi amevaa jeans, sweater, na kablouse. Basi hana hata pochi yaani yupo kisela sana.

Kilichotokea ni period ilimuanza ghafla bila kujua. Kilichofanya nijue ni alivua sweater lake na kulitumia kama kujifunika sasa mimi nilikuwa na sweater na zile shuka za kimasai. Nikamuuliza mbona umevua sweeter na gari wamewasha AC haikutesi?!

Akajibu kama vile mtu mwenye mawazo na aibu fulani. Ilinichukua dakika chache kunotice kuwa hakuwa sawa na nikashajua huyu ametumia sweater kujificha. Nikamwambia kwa sauti ya chini sana unahitaji msaada. Hakunijibu zaidi ya kuinama kama anaona aibu halafu anaweka lile tabasamu la aibu fulani.

Nikamwambia niandikie kwenye sms unataka msaada gani. Nikampa simu yangu aandike namba yake nikamtext akaanza kuchat akanambia ameingia Period hapo hana uhakika na kinachoendelea ila anahisi amechafua siti sasa hajui pa kuanzia.


Aiseee ni MUNGU tu alisimamia ile situation maana gari lilikuwa na utingo mwanaume tu. So ikabidi nimfuate nimpange kuwa atusaidie wakiona hata kituo cha mafuta wasimame konda akanielewa. Tukasimama akasema abiria tuchimbe dawa kidogo. Watu wakaanza shuka. Akachukua sweta akaliweka pale kwenye siti halafu nikampa shuka langu la kimasai akajifunika mwili mzima so muda tunatoka nashuka nae hakuna mtu alishtukia chochote hadi tunafika chini. Nikamwambia atangulie chini me nakwenda tafuta pedi. Nikaenda mnunulia duka liko huko barabarani kipande kidogo toka pale kwenye sheri nikamletea.

Akajiweka sawa suruali yake ilikuwa imechafuka akaisuuza na maji akavaa hivyo hivyo nikamwambia valia na hilo shuka la kimasai. Tukarejea kwenye gari. Aisee ikawa kama ni mke wangu sasa namna tulivyorudi na kukaa kwenye gari alijiegemesha kwenye kioo me namwambia niegemee kama unataka kulala.

Tulishuka sote stand ya Moshi alikuwa anataka kwenda nikamwambia sidhani kama utakuwa katika hali nzuri kuendelea na safari katika hali hiyo na muda umekwenda twende nyumbani sio mbali na hapa ukaweke mambo sawa uwe safi kesho utaendelea na safari ndugu zako waelezee situation wakitaka watumie picha kabisa halafu tukimbie na huu msala wa kuchafua siti.

Akakubali. Tulishuka sote akafika nyumbani akatoa nguo zote akazifua na kuzianika. Ilibidi nimnunulie kufuri mpya na pedi zingine za brand nzuri.

Nilimpa risala sana ule usiku. Kwamba kwann mtoto wa kike unasafiri kirahisi vile huoni namna umejihatarisha. Yaani unasafiri haubebi kitenge hata viwili na hata pedi tatu za dharula maana hata usipopata wewe anaweza pata mwanamke mwenzako ukamsitiri. Nikamwambia sasa usingekutana na mimi leo si ungefedheheka sana.

Kesho yake nikamsindikiza jioni aende kwa kwao huko Arusha. Na baada ya hapo tuliendelea kuwasiliana she is someone very close to me now.
Mkuu uka_take advantage kabisa ya hiyo misfortune ya Binti
 
Back
Top Bottom