Mambo ya kuzingatia wakati wa Kula chakula mkiwa jumuiya!

Mambo ya kuzingatia wakati wa Kula chakula mkiwa jumuiya!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KULA CHAKULA MKIWA KWENYE JUMUIYA!

Anaandika Robert Heriel.

Kula chakula napo kunauungwana wake, ambao hauna budi kufuatwa, hasa ukiwa unakula watu zaidi ya mmoja, iwe ni kwenye familia, Ugenini,kwenye matukio Kama HARUSINI, misibani n.k. Kula kitasha inaweza kujifanya ukapendwa, Kula Kama ngedere hovyo hovyo linaweza kukufanya uchukiwe.

Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati WA Kula hasa kwenye mikusanyiko au jumuiya za watu;

1. Jaza chakula kwenye kijiko uwiano unaolingana na mdomo wako, usijaze kupitiliza mpaka ukapanua mdomo wako kupitiliza,

2. Usifungue mdomo wako kiasi cha Meno kuonekana wakati unaingiza kijiko mdomoni.

3. Usigongeze kijiko kwenye Meno utasababisha sauti zitakazowakera wengine,

4. Ukishaweka chakula mdomoni ufunge mdomo kisha tafuta kiungwana, na Kwa vile uliweka saizi inayowiana na mdomo wako hautatoa milima kwenye mashavu.
Tafuna walau mara Saba mpaka kumi chakula ili kimeng'enywe vizuri.

5. Ukichota chakula na kijiko hakikisha usiigonge sahani, ikatoa miliomilio ya kipuuzi. Utawakera wengine.

6. Unapokunywa Juisii kwenye Bilauri au kikombe iweke kwenye uvungu WA mdomo WA chini, na sio uiweke katikati ya mdomo WA juu au wachini, pia usiing'ate Bilauri au kikombe kwa Meno.

7. Usiongee wakati wa kula isipokuwa ukiwa umemaliza kumeza
Kuongea wakati unakula utafanya watu waona chakula cha mdomoni mwako na hiyo wengine hujisikia vibaya na kuona kinyaa. Pia kuongea wakati WA kula Kwa wengine kunaambatana na kurusha mate au vijipande vya chakula nje. Hii inaweza wakera wenzako.

8. Ikiwa mtakaa watu wengi katika meza moja au mkeka wakati WA Kula, mkae Kwa kuzingatia Jinsia, umri na mahusiano baina yenu. Ikiwa familia inawatu wa nje Kama mashemeji alafu mkawa mnakula meza moja, mtu na Shemeji yake wasikae mkabala(yaani Kwa kuangaliana) wakae Mshazari. Halikadhalika na Wakwe usikae nao Kwa kuangaliana(mkabala) wakae aidha upande wa kushoto au kulia wa meza.

9. Ikiwa mnautaratibu wa kuomba kabla ya Kula, muombaji awe mwanafamilia unayemjua, na mtu wa Imani uliyoithibitisha

10. Usile polepole wala usile harakaharaka
Ni vyema wakati wa kuanza Kula muwe familia yote na wakati WA kumaliza mmalize Kwa pamoja, sio mtu akae mezani Kwa zaidi ya Dakika 45 mpaka Lisaa.

11. Mgawanyo WA chakula usiwe wa kibinafsi
Kwamba Baba apewe kingi na vyakula vizuri mfano paja na vinono vingine, isipokuwa mtu yeyote ndani ya familia hasa Baba, mama na watoto anaweza Kula chakula chochote. Ni jukumu la Baba kuhakikisha chakula kinakuwa chakutosha, na sio ubinafsi kuendekezwa. Mfano, tabia ya kusema maziwa ni yababa au supu ni yababa iondolewe, isipokuwa Baba aongeze bajeti ya maziwa au chakula hiko ili familia yote ipate kukitumia.

12. Muandaaji wa chakula jikoni na muwekaji mezani awe msafi akiwa amefunika nywele zake.

13. Chakula cha usiku kiliwe kabla ya saa mbili na nusu usiku, ili kuufanya mmeng'enyo WA chakula kufanya kazi mapema kabla ya Mwili kulala katika hatua za juu. Hii itapunguza magonjwa yasiyojulikana na yasiyoambukiza,

14. Chakula cha usiku kisiliwe kingi Sana, itaepusha magonjwa yasiyojulikana na yasiyoambukiza, pia itaondoa ndoto mbaya, na kuamka ukiwa na njaa Kali, kutokana na uzalishwaji wa enzyme za mmeng'enyo kuzalishwa nyingi usiku.

15. Ni vizuri wakati WA Kula muda mwingi uutumie ku-focus na chakula kuliko kuangalia watu au huku na huko.

16. Chakula cha usiku itapendeza kikipikwa na Mama mwenye nyumba, Mke wa familia, au kama hayupo au kuna udhuru wa namna yoyote basi Dada mkubwa wa Familia. Msaidizi wa kazi asaidie kuandaa tuu viungo na vyombo kwaajili ya kupikwa na Mama.

17. Baada ya Kula, mtoa vyombo atenganishe mabaki ya vyakula kwenye Sahani ayaweke sehemu ya kutupia takataka, kisha vyombo aviweke vikiwa vikavu vikavu, asichanganye mabaki ya sahani Kwa pamoja kwenye beseni la vyombo.

18. Kuosha vyombo, vyombo vioshwe Kwa Wavu au Sponji au kitu chochote, Ila wavu usiguse mabaki ya chakula, kwani yatanasa kwenye wavu na haitakuwa salama tofauti na ukisuuza Kwanza sahani ndipo uoshe na wavu uliowekwa sabuni. Mwiko uoshwe mara baada ya kutumika kupikia,masufuria yalowekwe baada ya kupikia.

19. Kunywa maji Dakika arobaini na tano kabla au baada ya Kula.

20. Chakula kitolewe kulingana na Umri na jinsia ya wanafamilia
Hii itasaidia kutokuwa na malumbano yasiyo na maana, na Wanafamilia kuwa na Afya njema. Mume apendelee vyakula vyenye Potassium na zinc kiasi Kama vile Matunda ya ndizi zakuiva, matikiti, Maboga, kachumbari ya Nyanya, kitunguu, hoho na pilipili. Hii itaongeza Libido na uume kusimama ukiwa Imara.
Kwa stamina, Mihogo na vyakula vya wanga angalau kila baada ya siku mbili ingawaje asipendelee Sana kwani huzalisha Calories nyingi zitakazomfanya anenepe.

Vyakula vya Karanga, korosho, na jamii ya Aina hizo ni muhimu kwa mwanamke na Mwanaume kuongeza Libido na ongezeko la shahawa.

Kwa mwanamke, vyakula vya protein Kama vile mayai, maharage Kwa aina zake, Maziwa ni muhimu Kwa mwili kuwa na rutuba na kuvutia zaidi.

Maji Kwa kila mwanafamilia ni muhimu Kwa kuzingatia Umri na Kilo zake za mwili. Angalau Lita mbili Kwa kila mmoja wapo Kwa wakazi wa Maeneo ya baridi, Lita tatu kwa wakazi wa Maeneo ya joto. Hii itasaidia Blood Circulation kuwa katika Hali nzuri, magonjwa yote yanayohusiana na Mzunguko wa damu yatadhibitiwa mfano Kisukari, Shinikizo la damu, Kukosa nguvu za kiume au za kike. Maji ya kutosha kwenye Damu husaidia Cell za mwili kufanya kazi vizuri ipasavyo.

Ngozi kuwa nzuri ya mvuto ni matokeo mazuri ya kuzingatia unywaji wa Maji. Mtu anayekunywa maji ya kutosha hata asipopaka Mafuta ngozi yake huvutia na kuwa nzuri.

21. Epuka Kula vitu vya mtaani bila kuvipasha tena Kwa Moto hasa vitu vya uswahilini. Mfano, Kachumbari za kwenye chipsi unazowekewa, Mishikaki na Vigondi, juisi za barabarani, Na wakati mwingine Ice creams.

Nyingi kama sio zote haziandaliwi katika Mazingira mazuri, hivyo kupata Minyoo ni uhakika.
Utashangaa unapata kichefu chefu kisichoisha.

Hii itawafaa zaidi wenye watoto wadogo chini ya miaka 14. Ni Bora mama uwapikie watoto mwenyewe chipsi kuliko ukanunue.

22. Kula Kwa wakati, Kama ni kila baada ya masaa sita fanya hivyo ili kuuweka mwili katika mfumo mzuri, zingatia mwili ni mfumo uliojumuisha mifumo mingi inayofanya kazi pamoja. Mfumo WA chakula Usiathiri mfumo wa Damu, ambapo utaathiri mfumo wa ufahamu. Unawezà kuweka Asubuhi saa 3:00-3;30 mchana saa 8:00-8:30 usiku 1:30-2:00

23. Usiweke chumvi nyingi, sukari nyingi, wala Mafuta mengi kwenye chakula. Zingatia kuwa kila chakula kina sukari, chumvi na Mafuta. Kuongeza ziada tena kwa wingi itaathiri mwili sehemu Fulani au Kwa ujumla.

24. Oga ndio Ule chakula cha usiku. Ikiwa umeoa au kuolewa
Oga kisha Kula chakula, alafu pumzika walau Lisaa limoja au mawili ndipo ule chakula kingine(fanya mapenzi na Mumeo au Mkeo). Mwili utakuwa kwenye fomu. Kisha pumzikeni mnaweza kulala hivyohivyo au mkae walau nusu saa ndio mkaoge.

25. ikiwa unatumia Kilevi, basi nyama ni muhimu zaidi na zaidi kwako. Au vyakula vya protein Kama Samaki wakubwa. Usinywe kilevi kikali tumbo likiwa wazi, tanguliza nyama na sio wanga. Maana Kwenye pombe kuna Ngano ambayo ni wanga, hivyo kuendekeza wanga utajikuta na kitambi au unene usiohitajika.

26. Msile chakula kimoja mfululizo zaidi ya siku mbili. Pia msile chakula sehemu moja mfululizo ndani ya siku ishirini na nane, angalau mara moja mbadilishe mazingira aidha Kwa kutoka Out mkiwa na vyakula vyenu au mkienda kununua hukohuko Out. Chakula hata kikiwa kizuri na kitamu namna gani kuliwa eneo lilelile lililozoeleka hupoteza ladha yake.

Hiyo pia katika tendo la ndoa. Lisiliwe katika mkao uleule mfululizo na lisilowe mazingira yaleyale Kwa zaidi ya siku ishirini na nane. Hii inamaanisha angalau Kwa mwezi mara moja umtoke Out mkafanye tendo la ndoa nje ya mazingira yenu. Kama hamna pesa basi mnaweza kufanyia hata Nje ya jumba Lenu ikiwa linauzio wa uhakika.

26. Mwanamke asiandae chakula akiwa katika Desturi yake. Mpe likizo Mkeo Kwa kumpikia ndani ya hizo siku tano au Saba ndani ya mwezi. Ukiweza mtoe out.

27. Chakula kisipikwe na Mtu mmoja yuleyule mfululizo kwani hata awe MPISHI vipi kitapoteza mvuto na ladha, na ndio maana wanaume wajanja mara moja moja Kwa wiki huingia jikoni hasa Kama hawana kazi na wanarudi nyumbani mapema.

28. Mpishi asile chakula kabla hajapumzika walau Kwa Lisaa limoja ili kutengeneza Hamu ya kula. Akaoge, akae anywe maji atulie. Hii itamfanya akifurahie chakula naye.

Zingatia chakula hujenga akili na Afya ya Mwili. Kupuuza chakula ni kupuuza akili yako mwenyewe, ni kupuuza Afya yako mwenyewe.

Kufikia hapo Taikon sina laziada.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Arusha
 
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KULA CHAKULA MKIWA KWENYE JUMUIYA!

Anaandika Robert Heriel.

Kula chakula napo kunauungwana wake, ambao hauna budi kufuatwa, hasa ukiwa unakula watu zaidi ya mmoja, iwe ni kwenye familia, Ugenini,kwenye matukio Kama HARUSINI, misibani n.k.
Kula kitasha inaweza kujifanya ukapendwa, Kula Kama ngedere hovyo hovyo linaweza kukufanya uchukiwe.

Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati WA Kula hasa kwenye mikusanyiko au jumuiya za watu;

1. Jaza chakula kwenye kijiko uwiano unaolingana na mdomo wako, usijaze kupitiliza mpaka ukapanua mdomo wako kupitiliza,

2. Usifungue mdomo wako kiasi cha Meno kuonekana wakati unaingiza kijiko mdomoni.

3. Usigongeze kijiko kwenye Meno utasababisha sauti zitakazowakera wengine,

4. Ukishaweka chakula mdomoni ufunge mdomo kisha tafuta kiungwana, na Kwa vile uliweka saizi inayowiana na mdomo wako hautatoa milima kwenye mashavu.
Tafuna walau mara Saba mpaka kumi chakula ili kimeng'enywe vizuri.

5. Ukichota chakula na kijiko hakikisha usiigonge sahani, ikatoa miliomilio ya kipuuzi. Utawakera wengine.

6. Unapokunywa Juisii kwenye Bilauri au kikombe iweke kwenye uvungu WA mdomo WA chini, na sio uiweke katikati ya mdomo WA juu au wachini, pia usiing'ate Bilauri au kikombe kwa Meno.

7. Usiongee wakati WA Kula isipokuwa ukiwa umemaliza kumeza,
Kuongea wakati unakula utafanya watu waona chakula cha mdomoni mwako na hiyo wengine hujisikia vibaya na kuona kinyaa.
Pia kuongea wakati WA kula Kwa wengine kunaambatana na kurusha mate au vijipande vya chakula nje. Hii inaweza wakera wenzako.

8. Ikiwa mtakaa watu wengi katika meza moja au mkeka wakati WA Kula, mkae Kwa kuzingatia Jinsia, umri na mahusiano baina yenu.
Ikiwa familia inawatu wa nje Kama mashemeji alafu mkawa mnakula meza moja, mtu na Shemeji yake wasikae mkabala(yaani Kwa kuangaliana) wakae Mshazari. Halikadhalika na Wakwe usikae nao Kwa kuangaliana(mkabala) wakae aidha upande wa kushoto au kulia wa meza.

9. Ikiwa mnautaratibu wa kuomba kabla ya Kula, muombaji awe mwanafamilia unayemjua, na mtu wa Imani uliyoithibitisha

10. Usile polepole wala usile harakaharaka.
Ni vyema wakati wa kuanza Kula muwe familia yote na wakati WA kumaliza mmalize Kwa pamoja, sio mtu akae mezani Kwa zaidi ya Dakika 45 mpaka Lisaa.

11. Mgawanyo WA chakula usiwe wa kibinafsi,
Kwamba Baba apewe kingi na vyakula vizuri mfano paja na vinono vingine, isipokuwa mtu yeyote ndani ya familia hasa Baba, mama na watoto anaweza Kula chakula chochote.
Ni jukumu la Baba kuhakikisha chakula kinakuwa chakutosha, na sio ubinafsi kuendekezwa,
Mfano, tabia ya kusema maziwa ni yababa au supu ni yababa iondolewe, isipokuwa Baba aongeze bajeti ya maziwa au chakula hiko ili familia yote ipate kukitumia.

12. Muandaaji WA chakula jikoni na muwekaji mezani awe msafi akiwa amefunika nywele zake.

13. Chakula cha usiku kiliwe kabla ya saa mbili na nusu usiku, ili kuufanya mmeng'enyo WA chakula kufanya kazi mapema kabla ya Mwili kulala katika hatua za juu. Hii itapunguza magonjwa yasiyojulikana na yasiyoambukiza,

14. Chakula cha usiku kisiliwe kingi Sana, itaepusha magonjwa yasiyojulikana na yasiyoambukiza, pia itaondoa ndoto mbaya, na kuamka ukiwa na njaa Kali, kutokana na uzalishwaji wa enzyme za mmeng'enyo kuzalishwa nyingi usiku.

15. Ni vizuri wakati WA Kula muda mwingi uutumie ku-focus na chakula kuliko kuangalia watu au huku na huko.

16. Chakula cha usiku itapendeza kikipikwa na Mama mwenye nyumba, Mke wa familia, au kama hayupo au kuna udhuru wa namna yoyote basi Dada mkubwa wa Familia.
Msaidizi wa kazi asaidie kuandaa tuu viungo na vyombo kwaajili ya kupikwa na Mama.

17. Baada ya Kula, mtoa vyombo atenganishe mabaki ya vyakula kwenye Sahani ayaweke sehemu ya kutupia takataka, kisha vyombo aviweke vikiwa vikavu vikavu, asichanganye mabaki ya sahani Kwa pamoja kwenye beseni la vyombo.

18. Kuosha vyombo, vyombo vioshwe Kwa Wavu au Sponji au kitu chochote, Ila wavu usiguse mabaki ya chakula, kwani yatanasa kwenye wavu na haitakuwa salama tofauti na ukisuuza Kwanza sahani ndipo uoshe na wavu uliowekwa sabuni.
Mwiko uoshwe mara baada ya kutumika kupikia,masufuria yalowekwe baada ya kupikia.

19. Kunywa maji Dakika arobaini na tano kabla au baada ya Kula.

20. Chakula kitolewe kulingana na Umri na jinsia ya wanafamilia.
Hii itasaidia kutokuwa na malumbano yasiyo na maana, na Wanafamilia kuwa na Afya njema.
Mume apendelee vyakula vyenye Potassium na zinc kiasi Kama vile Matunda ya ndizi zakuiva, matikiti, Maboga, kachumbari ya Nyanya, kitunguu, hoho na pilipili. Hii itaongeza Libido na uume kusimama ukiwa Imara.
Kwa stamina, Mihogo na vyakula vya wanga angalau kila baada ya siku mbili ingawaje asipendelee Sana kwani huzalisha Calories nyingi zitakazomfanya anenepe,

Vyakula vya Karanga, korosho, na jamii ya Aina hizo ni muhimu Kwa mwanamke na Mwanaume kuongeza Libido na ongezeko la shahawa.

Kwa mwanamke, vyakula vya protein Kama vile mayai, maharage Kwa aina zake, Maziwa ni muhimu Kwa mwili kuwa na rutuba na kuvutia zaidi.

Maji Kwa kila mwanafamilia ni muhimu Kwa kuzingatia Umri na Kilo zake za mwili. Angalau Lita mbili Kwa kila mmoja wapo Kwa wakazi wa Maeneo ya baridi, Lita tatu Kwa wakazi wa Maeneo ya joto.
Hii itasaidia Blood Circulation kuwa katika Hali nzuri,magonjwa yote yanayohusiana na Mzunguko wa damu yatadhibitiwa mfano Kisukari, Shinikizo la damu, Kukosa nguvu za kiume au za kike,
Maji ya kutosha kwenye Damu husaidia Cell za mwili kufanya kazi vizuri ipasavyo.

Ngozi kuwa nzuri ya mvuto ni matokeo mazuri ya kuzingatia unywaji wa Maji.
Mtu anayekunywa maji ya kutosha hata asipopaka Mafuta ngozi yake huvutia na kuwa nzuri.

21. Epuka Kula vitu vya mtaani bila kuvipasha tena Kwa Moto hasa vitu vya uswahilini. Mfano, Kachumbari za kwenye chipsi unazowekewa, Mishikaki na Vigondi, juisi za barabarani, Na wakati mwingine Ice creams.

Nyingi kama sio zote haziandaliwi katika Mazingira mazuri, hivyo kupata Minyoo ni uhakika.
Utashangaa unapata kichefu chefu kisichoisha,

Hii itawafaa zaidi wenye watoto wadogo chini ya miaka 14. Ni Bora mama uwapikie watoto mwenyewe chipsi kuliko ukanunue.

22. Kula Kwa wakati, Kama ni kila baada ya masaa sita fanya hivyo ili kuuweka mwili katika mfumo mzuri, zingatia mwili ni mfumo uliojumuisha mifumo mingi inayofanya kazi pamoja. Mfumo WA chakula Usiathiri mfumo wa Damu, ambapo utaathiri mfumo wa ufahamu. Unawezà kuweka Asubuhi saa 3:00-3;30 mchana saa 8:00-8:30 usiku 1:30-2:00

23. Usiweke chumvi nyingi, sukari nyingi, wala Mafuta mengi kwenye chakula. Zingatia kuwa kila chakula kina sukari, chumvi na Mafuta. Kuongeza ziada tena kwa wingi itaathiri mwili sehemu Fulani au Kwa ujumla.

24. Oga ndio Ule chakula cha usiku. Ikiwa umeoa au kuolewa,
Oga kisha Kula chakula, alafu pumzika walau Lisaa limoja au mawili ndipo ule chakula kingine(fanya mapenzi na Mumeo au Mkeo).
Mwili utakuwa kwenye fomu.
Kisha pumzikeni mnaweza kulala hivyohivyo au mkae walau nusu saa ndio mkaoge.

25. ikiwa unatumia Kilevi, basi nyama ni muhimu zaidi na zaidi kwako. Au vyakula vya protein Kama Samaki wakubwa.
Usinywe kilevi kikali tumbo likiwa wazi, tanguliza nyama na sio wanga.
Maana Kwenye pombe kuna Ngano ambayo ni wanga, hivyo kuendekeza wanga utajikuta na kitambi au unene usiohitajika.

26. Msile chakula kimoja mfululizo zaidi ya siku mbili. Pia msile chakula sehemu moja mfululizo ndani ya siku ishirini na nane, angalau mara moja mbadilishe mazingira aidha Kwa kutoka Out mkiwa na vyakula vyenu au mkienda kununua hukohuko Out.
Chakula hata kikiwa kizuri na kitamu namna gani kuliwa eneo lilelile lililozoeleka hupoteza ladha yake.

Hiyo pia katika tendo la ndoa. Lisiliwe katika mkao uleule mfululizo na lisilowe mazingira yaleyale Kwa zaidi ya siku ishirini na nane. Hii inamaanisha angalau Kwa mwezi mara moja umtoke Out mkafanye tendo la ndoa nje ya mazingira yenu.
Kama hamna pesa basi mnaweza kufanyia hata Nje ya jumba Lenu ikiwa linauzio wa uhakika.

26. Mwanamke asiandae chakula akiwa katika Desturi yake. Mpe likizo Mkeo Kwa kumpikia ndani ya hizo siku tano au Saba ndani ya mwezi. Ukiweza mtoe out.

27. Chakula kisipikwe na Mtu mmoja yuleyule mfululizo kwani hata awe MPISHI vipi kitapoteza mvuto na ladha, na ndio maana wanaume wajanja mara moja moja Kwa wiki huingia jikoni hasa Kama hawana kazi na wanarudi nyumbani mapema.

28. Mpishi asile chakula kabla hajapumzika walau Kwa Lisaa limoja ili kutengeneza Hamu ya kula. Akaoge, akae anywe maji atulie. Hii itamfanya akifurahie chakula naye.

Zingatia chakula hujenga akili na Afya ya Mwili. Kupuuza chakula ni kupuuza akili yako mwenyewe, ni kupuuza Afya yako mwenyewe.

Kufikia hapo Taikon sina laziada.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Arusha
Hawa ndiyo Wabunge wanaoruka sarakasi bungeni
 
mkuu ongezea na matumizi ya tooth piki na vile vitambaa vya mezani vya kujifutia
 
Hawa kina junior wanasikitisha sana wakati wa kula .
 
kesho njoo na mambo ya kuzingatia unavyotembea public.

next, mambo ya kuzingatia unavyotumia
Public transport

then, unapokua mlimani city

Then..

Aisee muda mdogo sana
 
na tukila mbuzi tutumie masharti yote hayo????[emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]
 
Back
Top Bottom