Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

jibu liko kwenye maneno ya Mungu mpendwa. acha uvivu, kasome utaelewa. achana na watu wanaoongea kw ahisia bila ufahamu. ni neno la Mungu pekee litakalokuondolea wasiwasi. imani bila neno la Mungu si imani ya kumpendeza Mungu kwani waabudu halisi watamwabudu katika roho na kweli. zingatia kuwa kweli ni neno la Mungu, basi hakuna zaidi. si miujiza wala ndoto, ni NENO LA MUNGU.

ubarikiwe sana

Glory to God

.
Hapo itakuwa nami nitamimina Roho wangu, watoto wenu wake kwa waume watatabiri, wazee wenu wataota ndoto na vijana wenu wataona maono.
Miss Jude, hili ni Neno la Mungu? Au labda kutakuwa na uchakachuaji?
.
 
.
Hapo itakuwa nami nitamimina Roho wangu, watoto wenu wake kwa waume watatabiri, wazee wenu wataota ndoto na vijana wenu wataona maono.
Miss Jude, hili ni Neno la Mungu? Au labda kutakuwa na uchakachuaji?
.

ni neno la Mungu kwa viwango vyote!

ila nakutahadharisha kuwa kwa kuwa imeandikwa hiyo, basi si kibali cha moja kwa moja cha kuamini kila ndoto. ndoto hizi zapaswa kuwa consistent na tabia ya Mungu. kumbuka hata shetani huleta ndoto na maono. hata kule jangwani kwenye majaribu ya Bwana, shetani alitaka Yesu amjaribu Mungu kwa kuwa iliandikwa kuwa akijirusha chini mungu atamletea malaika zake mguu wake usijikwae. so asomaye na afahamu. ni Neno tu litalakolotuweka huru, si ndoto!

Glory to God
 
Hello,
My greeting to you My name is Shania, single and never married, how are you i hope you are fine and well sounded in good health, i am a good hearten girl loving and caring humble and respectful. i would like to know more about you, please if you do not mind write me with this address (misshania99@yahoo.com)i hope to hear from you soon, because i have something very important to share with you.
Shania

misshania99@yahoo.com
Mh hiv hii post c nimeiona kule mapenz mahusiano na urafik na watu wametahadharishwa inakuaje sasa emb ngoja nkachungulie tena
 
Wenger said, "Plz feel mercy mzee, one cup can't do athing, may b gallon may do something "
 

Attachments

  • 188941_1309139824716_1717213941_548869_3085198_n.jpg
    188941_1309139824716_1717213941_548869_3085198_n.jpg
    19.8 KB · Views: 105
Serikali inapokwenda kwa ‘Babu Loliondo’


picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 16 March 2011

Uchambuzi


babu_233.jpg




SERIKALI imepata mbia katika ‘kupambana na maradhi.’ Imeruhusu mchungaji Ambilikile Mwasapile – Babu wa Loliondo – kuendelea kufanya tiba kwa kutumia dawa ambazo hazijathibitishwa na mamlaka yoyote ya serikali.
Kuanzia wizarani, mkoani, wilayani, tarafani, hadi kijijini, serikali imebariki mchungaji Mwasapile kufanya kazi za kitabibu, huku yenyewe ikitumia muda mwingi kumtangaza.

Mkolezo wa hatua ya serikali unaongezwa na baadhi ya maaskofu na wachungaji ili kutoa ushuhuda. Baadhi ya walioajiriwa tayari wametoa ushuhuda, kwamba dawa inayotolewa inafanya kazi bila matatizo.

Kitendo cha serikali kutoa kibali kwa “Babu wa Loliondo,” na kutumia rasilimali za taifa na muda kutetea kinachotendeka, ni mkwamo wa aina yake.
Katika mazigira ya kawaida, serikali au chombo chochote kinachoshughulika na huduma za umma, kilipaswa kujiweka mbali na imani hizi.

Kwa mfano, serikali ingeweza kusema, “wanaotaka kwenda kwa mchungaji Loliondo ruhusa, bali “tiba ya ukimwi haijapatikana.” Haikufanya hivyo. Badala yake, imeruhusu taifa kurejea katika ujima.

Kushindwa kwa serikali kuingilia “tiba ya babu” kumetokana na mchoko wa kupigwa mbele, nyuma, kushoto na kulia. Hivyo imehofu kuonekana inapuuza wananchi.
Hata hivyo, hatua ya serikali kushabikia kile kinachoitwa “tiba ya imani,” ni sawa na kushindilia mwiba mwilini badala ya kuung’oa.

Mchungaji Mwasapile anasema dawa yake inayotokana na mizizi na magamba ya mti unaoitwa Muugamuryaga, kwa lugha ya kabila la Kisonjo, ambalo ndiyo wenyeji wa tarafa ya Sale, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha, inatibu maradhi sugu ya kisukari, ukimwi, saratani na kifua kikuu.

Sasa serikali imejipa kazi ya ziada na iliyopo nje ya mipango yake ya bajeti. Kwanza, imetumia muda mwingi kutangaza kazi za “babu wa Loliondo” kuliko kutenda kazi zake.
Kwa muda wa wiki mzima mawaziri wa Kikwete, waziri wa afya na ustawi wa jamii, Dk. Haji Mponda na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera, uratibu na bunge) William Lukuvi, wamefanya kazi kubwa ya kumtangaza mchungaji.

Wakati Dk. Haji akitaka kusitishwa kwa muda kwa huduma zinazotolewa kwa kuwa dawa hiyo haijathibitishwa, Lukuvi alinukuliwa akisema serikali haiwezi kuingilia imani za dini za watu kwa kuwa si sera yake.
Hapa napo kuna tatizo la uelewa. Babu hajaongelea suala la dini. Anashughulika na imani. Ndiyo maana kila mwamini na muumini anayetishiwa na maradhi aliyotaja anakwenda kwake. Angehubiri dini asingekuwa na mtu.

Hata hivyo, Lukuvi alikiri kuwa serikali haifahamu lolote kama dawa inayotolewa ni salama kwa afya ya watu wake. Alisema kazi ya kuichunguza dawa hiyo inayofanywa na wataalamu wa serikali, bado haijakamilika.

Pili, serikali imelazimika kupeleka kwa “babu” manesi ili kusaidia kazi za kitabibu. Hawa si manesi kutoka hospitali binafsi – hao hawaamini katika yale yanayotendeka – ni manesi kutoka hospitali za umma.

Tatu, nje ya mipango yake ya bajeti, serikali imepeleka askari polisi kuimarisha kazi ya ulinzi. Imegharimia usafiri wa watendaji na zana za kazi.
Lakini hatujaona serikali inayoamini dawa ya “Babu wa Loliondo” ikiondoa wagonjwa wa kansa waliojazana katika hospitali ya Ocean Road na kuwapeleka huko kupata matibabu. Wala hatujaona serikali ikichukua helikopta kumbeba “mtu wa Mungu” na kumpeleka Ocean Road akiwa na gudulia lake, kunywesha dawa wagonjwa.

Mkakati huu ungesaidia kupunguza msongamano Loliondo; ungesaidia serikali kupunguza gharana za kuhudumia wagonjwa waliopo hospitali na ungeifanya serikali ifanye kazi nyingine muhimu za utawala. Kwa nini sasa hospitali zijae wagonjwa, wakati maji ya dawa yapo?

Serikali imeshindwa kumsajili babu ili iweze kupata mapato. Taarifa zinasema kila siku ya Mungu, “Babu wa Loliondo” anakusanya kati ya Sh. 5 milioni na Sh. 20 milioni. Kwa hesabu hii, serikali inapoteza karibu zaidi ya Sh. 2 milioni kwa siku.
Lakini kuna hili pia: Umuhimu wa habari za tiba ya Loliondo unachangiwa na habari za uvumi zinazoeleza mambo kadhaa bila uthibitisho. Kwa mfano, kuna taarifa kuwa baadhi ya vigogo serikalini wameishakwenda huko kupokea tiba; majina yao yanatajwa lakini hayaripotiwi kwenye vyombo vya habari.

Uvumi huu unanogesha soga na kuongeza hamasa ya kwenda Loliondo. Mpaka sasa hakuna mtu aliyepona na kujitokeza hadharani kutoa ushahidi juu ya tiba hiyo. Nyingi ya habari zinazotoka zinanukuu watu wengine wanaodaiwa kupona.

Ni kweli kwamba masuala ya imani yana mipaka isiyoweza kuvukwa na mtu yeyote asiyekubaliana na mambo ya imani, lakini kwa kuwa serikali nayo inaumwa, na kwa hiyo imeamua kwenda Loliondo kutibiwa, hatunabudi kuhoji hicho kinachotendeka.
Kimsingi mwitikio wa watu kuhusu tiba ya Loliondo unaashiria mambo mengi katika taifa. Kinachojitokeza wazi ni ukweli kuwa huduma za afya katika taifa ni mbaya mno.

Pamoja na mezoea kuwa huduma hizi ni mbaya kwa watu maskini na wa vijijini, lakini sasa imedhihirika kuwa ni mbaya kwa wengi zaidi. Taarifa zimetaja hata baadhi ya wanasiasa, viongozi wa dini na wafanyabiashara wakubwa kuwa wanakwenda Loliondo.

Wenye fedha na nafasi ndani ya taifa, ambao walizoea kwenda Ulaya na India kupata tiba ya saratani, ukimwi, shinikizo la damu na kisukari, wengi wao wanaripotiwa kunywa dawa ya babu.
Fedha nyingi ambazo zingetumika kuboresha huduma za afya katika taifa, zimekuwa zinatumika kwenda nje ya nchi, lakini bado walewale waliozoea kukomba fedha za umma kwenda nje, wanamiminika Loliondo.

Wakati naandika makala hii, rafiki yangu mmoja alinitumia ujumbe wa simu ya mkononi, uliosheheni utani unaoweza kufanana na ukweli. Ulisema, “Usione kimya, niko kwenye foleni Loliondo toka Jumanne. Namba yangu ni 1561. Huku hakuna kuzamia. Ukizamia au kutoa rushwa hauponi.”

Anasema, “Nyuma yangu namwona mheshimiwa Ole Sendeka, Halima Mdee, Anne Kilango, Tundu Lissu na Rostam Aziz ambaye taarifa zinasema amekuja kuganga Dowans yake ili inunuliwe…Huwezi kuamini hata Mzee wa Upako yuko hapa. Naye ni mtu wa 1569.

“Mama Rwakatare ni wa 1621. Nitakuwa nakujuza kila kitu, ila network (mtandao) ni shida sana. Kwa mbali namwona Shibuda (John Shibuda), Mbowe (Freeman Mbowe), Samwel Sitta na Athony Diallo wamekamata kikombe. Tafadhali njoo na wewe.”

Ni utani. Utani mtupu unaoenea kwa kasi mitaani, lakini ni jambo linaloweza kutokea endapo serikali itaendelea kukumbatia mchungaji kutaka kuponyesha raia wake huku yenyewe ikishindwa kuchukua hatua za haraka kuboresha hospitali zake na vituo vyake vya afya.

Sasa serikali imeamua kukimbilia Loliondo kana kwamba Mchungaji Mwasapile anatibu ufisadi. Iliishatamkwa kuwa ufisadi hauna dini wala rangi na kwa hiyo, ufisadi hauna imani kwa Mungu.
Mchungaji Mwasapile anatibu kwa imani. Je, mafisadi wamepata imani lini ya kuweza kuponyeshwa na tiba ya Loliondo? Tusubiri tuone.
 
Hi wanajamii F.
Siku zote watu ambao ni wazima huwa hawajui maumivu ya wale walio wagonjwa.. na pia mtu ambae anaishi kwenye nyumba ya umeme hawezi kujua matatizo ya yule anayeishi kwenye kibatari au taa ya chemli. huyu anayesema anatilia shaka dawa ya babu yeye aendelee na msimamo wake na kama anawagonjwa kwake asiwapeleke kwa babu ili wasipate matibabu, ila ajue kuwa kuwa kuna siku ataulizwa kuwa mbona nilileta mtabibu lakini hukuwapeleka wagonjwa?
 
Serikali kwa sasa iko desperate so babu kwao ni ahueni
 
Kama uu mgonjwa nenda kwa babu na kwa wale wazima endeleeni kupost vituz umu JF.
 
babu ni mganga wa jadi.
-------the end-----
Dah!! Aisee!! Tafakari tena mkuu....Unaruhusiwa kufuta usemi .....Wakuu hili jambo la kwa Babu binafsi nafikiri nimapema mno kulizungumzia kwa kiwango hiki ,labda kama lingelikua limeshaleta madhara kwa watumiaji otherwise sioni kama we use our time profitable coz kama usanii basi wa Babu atapambana na Mungu mwenyewe na kama jambo kuu kitaifa yapo makuu tena yanayo igusa jamii mojakwamoja .Watu wanakwenda kwa Babu lakini hawajui mustakbali wa nchi yao ukianzia Mfumuko wa bei,Tatizo la umeme,Mijadala ya katiba na mengine mengi ya msingi so kama ma great thinker we have to think big about sio kila siku babu babu na siku ukija gundua ni kweli katumwa na Mungu?acha wenye imani waende na wewe ulie na kinyume naimani yao unapotezea tunabaki jamvini kuendelea kulipigania TAIFA letu.
 
Nafikiri Bw. Kubenea unaweza kushauri serikali watoe taarifa kupitia madaktari wenye klinik za wagonjwa wa magonjwa anayotibu babu watoe ushuhuda. Lakini hebu fikiria wakifanya hivyo ni watu wangapi wataongezeka kwa babu gafula.
Sababu hawajafanya hivyo ni kwa sababu wameprove wagonjwa wao kupona na hawataki kuadvertise .

Kama mwandishi mkubwa hebu jipeleke kwa babu utujuze kimakini zaidi . This is not politics . Ww umejuaje babu anapata hizo hela wakati hujafanya huo utafiti!too low for your type broda.
 
jibu liko kwenye maneno ya Mungu mpendwa. acha uvivu, kasome utaelewa. achana na watu wanaoongea kw ahisia bila ufahamu. ni neno la Mungu pekee litakalokuondolea wasiwasi. imani bila neno la Mungu si imani ya kumpendeza Mungu kwani waabudu halisi watamwabudu katika roho na kweli. zingatia kuwa kweli ni neno la Mungu, basi hakuna zaidi. si miujiza wala ndoto, ni NENO LA MUNGU.

ubarikiwe sana

Glory to God

Miss judith, I think u are right! I'm satisfied with ur quote. Stay blessed.
 
Dah leo Babu Loliondo kutokana na foleni kuwa kubwa ikabidi awaambie watu wapange foleni tofauti ya UKIMWI kushoto na kisukari kulia. Unaambiwa mstari ule wa kushoto (Wa ukimwi) haukuwa na mtu hata mmoja, babu akafurahi kuwa waathirika wamepungua sasa akawa anataka kumwaga ile dawa ya ukimwi! Duh watu wakaanza kupiga kelele "hhaaaa babu usimwage bwana, huwezi jua babu acha bwana tuko hapa leo siku ya tano babu" ikabidi babu ashangae vipi tena!
mashikolomageni wewe ulikuwa mstari upi? kulia au wa kushoto?
 
MwanaHALISI toleo la J'tano, 16-22, 2011. Uk3 katika article yenye title " SERIKALI INAPOKWENDA KWA BABU" KUBENEA ANASEMA NANUKUU " ... Serikali imeshindwa kumsajili babu ili iweze kupata mapato. Taarifa zinasema kila siku ya Mungu, "Babu wa loliondo " anakusanya kati ya sh.5 milioni na sh.20 million. Kwa hesabu hii, serikali inapoteza karibu zaidi ya sh. 2milion kwa siku." mwsho wa kunuku.
Wakuu hii imekaaje? Nawasilisha
 
Uislamu upo wazi hauna löngolongo umekamilika na walishasema BABU "NO". Tatizo ukiristo haujakamilika ndo maana babu kajitokeza kila mtu anaongea lwake leo kakobe, kesho pengo mara upako hakuna dira kabisa.
 
Aliyepika hiyo picha kaenda nje kidogo ya ukweli by 2inches mixing imemshinda:lol:!!!
 
Back
Top Bottom