Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Sinabudi kumshukuru mungu kwa kumpatia dawa babu yetu wa Loliondo kwahajili
ya kutibu magonjwa KATILI bin SUGU yaliyokosa dawa zake hapa duniani kwahajili
ya kutibu ukimwi,kansa,kisukari nk. Nasema ahsante mungu,ahsante babu wa loliondo. Lakini kunakitu nimegundua kuhusiana na watu wanaotuletea habari hizi
kupitia mablog,magazeti,radioni na hata kwenye luninga toka habari hizi ziwe hot
cake takribani wiki tatu hivi. -Swali langu ni -Hivi kwanini hakuna mtu yeyote aliyeji
tokeza hapa jamvini live au kwenye media zingine na kukili kuwa mimi ni mmoja kati ya watu waliotoka au waliopo loliondo kwa babu kwa kusumbuliwa na ukimwi au kansa au kisukari na sasa nimepona baada ya kutumia dawa za babu huyo wa
loliondo? Badala yake utakuta watu au mtu anakuja hapa jamvini au kwenye media
zingine na kusema ooooh....huyo babu si mchezo anatibu kila kitu! au utamsikia
mtu anasema mimi nilimpeleka rafiki yangu kwa babu na sasa amepona. Au utasi
mimi nilidrive na familia yangu kwa safari ya shida sana hadi loliondo,lakini baada ya mateso ya kadha wa kadha hatimae familia yangu ilipata dawa na sasa wote wamepona (yeye kajitoa hapo) na sasa tumerudi. Mwingine oooooh.... nilimpeleka
shangazi au mjomba kwenye machela,lakini baada ya kunywa dawa ya babu'ghafla
alisimama na sasa amepona kabisa. Swali langu la pili ni -hivi kwanini mtu usiseme
kuwa wewe ndiye muhusika? ulikuwa unaumwa ukimwi au kansa au kisukari na sa
sa umepona kupitia babu? kwanini kila mtu anatuletea habari ya loliondo kupitia
ushuhuda wa mtu mwingine? kwani ukiwa muwazi na kukiri wewe ndiye muhusika
mwenyewe itaaribika nini?
Mie nafikiri tufike sehemu tuwe wawazi hasa kwenye mambo tata kama haya ili iwe
faida kwa jamii mzima. - Nawasilisha waungwana

Mungu ibariki Tanzania,Mungu mbariki babu wa Loliondo


unaangalia chombo gani cha habari wewe? Jana kwenye TBC kuna mama amekiri ametoka kwa babu siku kadhaa amekunywa dawa ya kisukari amepona hanywi tena dawa na anakula vyakula tofauti ameenda kupima sijui wamemwambia iko sita mi sielewi mambo ya kisayansi, na kwa sasa anakula chakula chochote kile na amepona ana nguvu kabisa, anadai alipelekwa pale akiwa na hali mbaya sana.
 
Hee Babu kawa maarufu jamani tunaomba dawa iwe inaponya dah ila huo umati hata hewa itakuwa matatizo.

Kila la heri waendaji mje mtupatie taarifa
 
Jamani eeee Watanzania wenzetu sidhani kama kuna kosa mtu kwenda kujaribu kutibiwa tatizo alilo nalo kwa bei rahisi, Kila mtu anapenda afya yake, Asiyekubali kushindwa si mshindani, Kakobe endelea kuomba wafuasi wakufuate sio kumharibia mwenzako, sidhani kama wewe anakuharibia kwa njia moja au nyingine, kwanza ufanyavyo hivyo kila mtu anakukimbia, wanamfuata babu wa LOLIONDO.
 
ukijaribu kutazama katika hali iliyosasa loliondo kwa babu utapata taswira ya mambo yafuatayo
1.watanzania wamekosa tumaini, kwani adui maradhi bado anawaandama
2. Hospitali zetu ni magumashi ndo maana hata vigogo wa serikali wamekimbilia Loliondo kupata kitu cha jero
3. ukiwa na shida mwenye nacho huzidi kukunyonya, babu alioteshwa kutoa tiba kwa jero, ila wengine wamechukulia advantage kupandisha bei ya nauli maradufu
4. watanzania side effect haina maana tunachohitaji dawa
5. hatuna serikali makini, kwani nionavyo mimi ingetakiwa ifanye uchunguzi wa dawa hiyo ndiyo iruhusu kuendelea kutolewa kwa wanaohitaji, angalizo hivi kama ikithibitika ni sumu ni wangapi walikwisha kuitumia na ni wangapi watakuwa wameathirika
 
Habari Za wandugu wa JF,
Nimeamini kuwa kilichosemwa na BIBLIA hakitabadilika hata kama ni kwanini.

1.WATU HAWA WANAMACHO LAKINI HAWAONI, WANAMASIKIO LAKINI HAWASIKII.
2. WENGI WATAKUJA KWA JINA LA MUNGU.

Tusibabaishwe na mganga wa Loliondo ukweli hakuna Mungu wa namna hiyo yeye angetumia tu jina la Mganga wa kienyeji sio Mungu unajua ni kwanini?
a. Dawa ya Mungu hainaga masharti, hata ukipewa sio masharti kama ya Loliondo eti hakuna mtu mwingine kukupa dawa hiyo ukanywa zaidi ya yeye peke yake swali: Watumishi wa Mungu Loliondo ni yeye peke yake? kama wengine wapo kwanini wasisaidiane? si kumpa tu mtu maji anakunywa??
b. Kwanini mti huo kama umefunuliwa na Mungu ukitumiwa na wengine usiponye?? Maana yake Mungu ameanza lini kutufundisha ubinafsi na uchoyo?

Nikomee hapa nitarudi! View attachment 24640
 
IS this a breaking news?

KWAMBA NI KUTOKA KWA MUNGU AU KWA SHETANI SIJUI, NINACHOJUA MIMI NI KWAMBA NILIKUWA MGONJWA NA SASA NIMEPONA
 
Hebu ngoja tuone, hivi kumbe Mfalme Naamani yeye hakupewa masharti? Sijui bana haya mambo mie, kikubwa matendo yangu tu, the rest are details
 
tukumbuke huyu sio mtu wa kwanza tanzania kutamka kitu kama hicho.. kuna yule dada wa Kanyigo miaka ya 1990s katikati, James Brwn, Mzee wa Tegeta na NDUKAI.. where are they.....
 
Nenda ukanywe dawa kwa babu acha ubishi watu wanashuhudia kupona.

Sio kila mtu anakalama....wachache wamebarikiwa
 
hawa ndio mababu wanaotibu ukimwi mwisho wa siku wanakufa nao
 
watanzania tunapenda sana kuishi.. hatutaki kusacrifice maisha yetu.... kama ni kufa tutakufa tu........ hadi jana mzee kashajikusanyia bilion 1.3...... great business
 
Hebu ngoja tuone, hivi kumbe Mfalme Naamani yeye hakupewa masharti? Sijui bana haya mambo mie, kikubwa matendo yangu tu, the rest are details

Hapo kwenye bold tu nimechoka!!

IS this a breaking news?

KWAMBA NI KUTOKA KWA MUNGU AU KWA SHETANI SIJUI, NINACHOJUA MIMI NI KWAMBA NILIKUWA MGONJWA NA SASA NIMEPONA

Muhimu kupona iwe imetoka kwa Mungu ama la Unachojua ni uizima kwanza. Imani bora kabisa hii!!
 
Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kutuletea mkombozi huyu. Kama kaishawaponya wengi, huo ni ushahidi tosha kuwa hachezi hapo, anatibu watu na hayo anayoyafanya ni masharti aliyooteshwa. Tuheshimu mipango yake, tumsaidie kwa kuiomba Serikali iwahudumie wanaokwenda huko japo sehemu ya malazi na huduma nyingine muhimu.
 
Habari Za wandugu wa JF,
Nimeamini kuwa kilichosemwa na BIBLIA hakitabadilika hata kama ni kwanini.

1.WATU HAWA WANAMACHO LAKINI HAWAONI, WANAMASIKIO LAKINI HAWASIKII.
2. WENGI WATAKUJA KWA JINA LA MUNGU.

Tusibabaishwe na mganga wa Loliondo ukweli hakuna Mungu wa namna hiyo yeye angetumia tu jina la Mganga wa kienyeji sio Mungu unajua ni kwanini?
a. Dawa ya Mungu hainaga masharti, hata ukipewa sio masharti kama ya Loliondo eti hakuna mtu mwingine kukupa dawa hiyo ukanywa zaidi ya yeye peke yake swali: Watumishi wa Mungu Loliondo ni yeye peke yake? kama wengine wapo kwanini wasisaidiane? si kumpa tu mtu maji anakunywa??
b. Kwanini mti huo kama umefunuliwa na Mungu ukitumiwa na wengine usiponye?? Maana yake Mungu ameanza lini kutufundisha ubinafsi na uchoyo?

Nikomee hapa nitarudi! View attachment 24640


Wewe kinachokuuma ni nini? Watu wanapona kwa nguvu ya Mungu aliyeamua kumtumia kiumbe wake huyu. Au wewe Mwanga nini? Hebu acha hizo. Halafu huu upuuzi wako unakuwaje Breaking News?!! Hakina Tanzania hii ina mijitu ya ajabu sana.
 
Ndugu, ujue kuna kitu kinaitwa karama. Na karama ni tunu ya bure kutoka kwa Mungu anayopewa mtu kama Mungu atakavyo kwa faida ya wengi. Kwa hiyo basi huwezi kumlazimisha Mungu ampe kila mmoja karama hiyo. Huwezi sema kwa nini mchungaji huyo tu kapewa na si wengine? Mungu kaamua hivyo! Kasome vizuri maandiko.
 
Back
Top Bottom