Sinabudi kumshukuru mungu kwa kumpatia dawa babu yetu wa Loliondo kwahajili
ya kutibu magonjwa KATILI bin SUGU yaliyokosa dawa zake hapa duniani kwahajili
ya kutibu ukimwi,kansa,kisukari nk. Nasema ahsante mungu,ahsante babu wa loliondo. Lakini kunakitu nimegundua kuhusiana na watu wanaotuletea habari hizi
kupitia mablog,magazeti,radioni na hata kwenye luninga toka habari hizi ziwe hot
cake takribani wiki tatu hivi. -Swali langu ni -Hivi kwanini hakuna mtu yeyote aliyeji
tokeza hapa jamvini live au kwenye media zingine na kukili kuwa mimi ni mmoja kati ya watu waliotoka au waliopo loliondo kwa babu kwa kusumbuliwa na ukimwi au kansa au kisukari na sasa nimepona baada ya kutumia dawa za babu huyo wa
loliondo? Badala yake utakuta watu au mtu anakuja hapa jamvini au kwenye media
zingine na kusema ooooh....huyo babu si mchezo anatibu kila kitu! au utamsikia
mtu anasema mimi nilimpeleka rafiki yangu kwa babu na sasa amepona. Au utasi
mimi nilidrive na familia yangu kwa safari ya shida sana hadi loliondo,lakini baada ya mateso ya kadha wa kadha hatimae familia yangu ilipata dawa na sasa wote wamepona (yeye kajitoa hapo) na sasa tumerudi. Mwingine oooooh.... nilimpeleka
shangazi au mjomba kwenye machela,lakini baada ya kunywa dawa ya babu'ghafla
alisimama na sasa amepona kabisa. Swali langu la pili ni -hivi kwanini mtu usiseme
kuwa wewe ndiye muhusika? ulikuwa unaumwa ukimwi au kansa au kisukari na sa
sa umepona kupitia babu? kwanini kila mtu anatuletea habari ya loliondo kupitia
ushuhuda wa mtu mwingine? kwani ukiwa muwazi na kukiri wewe ndiye muhusika
mwenyewe itaaribika nini?
Mie nafikiri tufike sehemu tuwe wawazi hasa kwenye mambo tata kama haya ili iwe
faida kwa jamii mzima. - Nawasilisha waungwana
Mungu ibariki Tanzania,Mungu mbariki babu wa Loliondo
unaangalia chombo gani cha habari wewe? Jana kwenye TBC kuna mama amekiri ametoka kwa babu siku kadhaa amekunywa dawa ya kisukari amepona hanywi tena dawa na anakula vyakula tofauti ameenda kupima sijui wamemwambia iko sita mi sielewi mambo ya kisayansi, na kwa sasa anakula chakula chochote kile na amepona ana nguvu kabisa, anadai alipelekwa pale akiwa na hali mbaya sana.