Habari Za wandugu wa JF,
Nimeamini kuwa kilichosemwa na BIBLIA hakitabadilika hata kama ni kwanini.
1.WATU HAWA WANAMACHO LAKINI HAWAONI, WANAMASIKIO LAKINI HAWASIKII.
2. WENGI WATAKUJA KWA JINA LA MUNGU.
Tusibabaishwe na mganga wa Loliondo ukweli hakuna Mungu wa namna hiyo yeye angetumia tu jina la Mganga wa kienyeji sio Mungu unajua ni kwanini?
a. Dawa ya Mungu hainaga masharti, hata ukipewa sio masharti kama ya Loliondo eti hakuna mtu mwingine kukupa dawa hiyo ukanywa zaidi ya yeye peke yake swali: Watumishi wa Mungu Loliondo ni yeye peke yake? kama wengine wapo kwanini wasisaidiane? si kumpa tu mtu maji anakunywa??
b. Kwanini mti huo kama umefunuliwa na Mungu ukitumiwa na wengine usiponye?? Maana yake Mungu ameanza lini kutufundisha ubinafsi na uchoyo?
Nikomee hapa nitarudi!
View attachment 24640
nani aliekuambia miujiza ya mungu haina masharti.
kama ni msomaji mzuri wa biblia nakukumbushia mifano hii
1.kipindi cha musa,wana wa izraeli walion'gatwa na nyoka musa aliwatengenezea nyoka wa shaba na kila aliekuwa mgonjwa akimuangalia yule nyoka anapona.
2.kipindi cha joshua katika kuuteka mji wa yeriko,waliambiwa wauzunguke mji ule mara saba na utakua himaya yao,kwa mawazo ya kawaida wasingeamini ila walifanya hivyo na kweli ngome zikaanguka.
3.kipindi cha naamani mkuu wa jeshi la shamu alikua na ukoma,aliamuriwa akaoge mto yordan mara saba ndipo apate kupona na kwa kufanya hivyo alipona.
4.kipindi cha ibrahimu,mkewe sara alikua hana mtoto na alipata wageni waliokua malaika nyumbani kwake akawaandalia chakula.kwa ule ukarimu tu walimtabilia kipindi kama mwaka unaofata atakumbatia mtoto.
5.kipindi cha petro,walipokua na petro na yohana wakienda kusali walikutana na kiwete mlangoni tena ni ombaomba akawapigia kelele akisema mnisaidie,petro akamuuliza nikusaidie nini akasema nipate kutembea,petro akamjibu simama na uondoke sasa,na kweli kwa maneno wakatembea.
6.kipindi cha yesu,kulikua na mama alikua akitokwa damu miaka mingi lakini alivyogusa pindo la yesu tu zikakoma palepale.
7.kipindi cha paulo,walifungwa gerezani paulo na silla walifanya kuimba na kuabudu mpaka milango ya gereza ikafunguka.
8.kipindi cha nuhu,maasi yalizidi mji huo mungu akaamua kuteketeza kwa gharika na kuamuru kila kiumbe kitakachotaka kupona kiingie ndani ya safina,lakini wapo ambao hawakuamini na walikufa.walipona walioingia tu.
mifano ni mingi tu,sasa huyu babu wa loliondo ndio kipindi chake hichi kwa wote wenye magonjwa sugu.IMANI YAKO TU.