Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Nimeupata ujumbe huu toka kwa mtumishi wa Mungu aliye uweka katika gazeti la mwananchi,kiimani tunaambiwa tuamini chochote kilicho katika kitabu Kitakatifu (biblia),...huyu babu yuko kinyume kabisa na biblia,.....tusikimbilie huko,na kama hatujaona huzi ni nyakati za mwisho!!

Tunaishi nyakati za mwisho.
Neno la Mungu linasema waziwazi kuwa nyakati za mwisho zitakuwa ni siku za hatari, hatari kubwa inayomaanishwa hapa ni watu kujitenga na imani na kufuata roho zidanganyazo – 1Tim. 4:1.

Biblia pia inasema, nyakati hizi za mwisho watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama inawezekana, hata walio wateule – Mt.24:23-24.

Ibilisi anahangaika kuwapeleka watumishi wake wengi kwa lengo na kuwavuta na kuwapoteza watu wasikae katika mapenzi ya Mungu, ili hatimaye wakataliwe na Mungu. Kwa sababu hiyo basi, tunapaswa kuwa makini sana na mambo yote yanayotokea nyakati hizi.

Kwa sasa hivi, kwa sababu kanisa bado halijanyakuliwa , mpinga kristo bado hajafunuliwa. Lakini roho yake tayari inatenda kazi.
Neno la Mungu linasema kuwa kutenda kazi kwa roho ya mpinga kristo kunaambatana na ishara na ajabu za uongo ili kuwavuta na kuwapoteza wanadamu – 2Thes. 2:7-12, Uf.13:11-14.

Kwa hiyo ndugu zangu, tunapaswa kuwa makini sana katika kila jambo, tusiwe wepesi wa kuchulikwa na kila upepo unaovuma. Hata kama mtu atasema kuwa anatumiwa na Mungu, bado hatupaswi kuwa wepesi wa kukubaliana naye. Kumbuka Yesu alisema wengi watasema siku ile bwana bwana tulifanya miujiza kwa jina lako naye atasema ondokeni sikuwajua ninyi kamwe.

Ninaposema hivyo simaanishi kuwa miujiza yote inatokana na ibilisi, iko miujiza mingi tu inayotokana na Mungu mwenyewe na haina tatizo kabisa.

Kitu cha msingi hapa ni kuwa tunapaswa kuwa na uwezo wa kutofautisha kipi ni kipi ili tusiingie kwenye mtego wa ibilisi.

Mungu wetu ametupa nafasi wa kuyapima na kuyajaribu mambo yote ili tuweze kutofautisha – 1Thes. 5:20-22, hatupaswi kuudharau unabii wowote bali kwanza tunapaswa kuupima na kuona kama unatoka kwa Mungu au la. Ikiwa ni wa Mungu tutaushika, la sivyo tutautupilia mbali.

Tunaupima unabii kwa namna gani?

Ni kwa kutumia Neno la Mungu pekee.
Biblia inasema katika Isaya 8:20 kuwa ikiwa watu hawaendi sawasawa na Neno la Mungu, kwao hakuna asubuhi. Asubuhi inamaanisha nuru, na kinyume cha nuru ni giza na giza maana yake ni dhambi. Chochote kile ambacho hakipo sawasawa na Neno la Mungu ni giza, ni dhambi.

Tena Neno la Mungu linasema katika 2Kor.13:8 kuwa hatuwezi tukafanya jambo lolote lililo kinyume na kweli ya Neno la Mungu.

Kuna alama zinazoweza kutusaidia kutambua miujiza ya Mungu.

I. Ishara na miujiza ya Mungu inaambatana na hao waaminio – Marko 16:17-18, Luka 10: 17-20. Waaminio ni wale waliompokea Yesu na kumfanya kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao, ni wale waliookoka. Kama mtu hajaokoka kamwe hawezi akatumiwa na Mungu kufanya ishara yeyote. Swali jepesi sasa, huyu babu wa Loliondo ameokoka? (anajua babu mwenyewe yuko upande gani lakini hatu muhukumu kwa hili)

II. Ishara na miujiza huthibitisha Neno la Mungu linalohubiriwa – Marko 16:20. Tujiulize, huyu babu anahubiri Neno lolote la Mungu au anagawa dawa tu? Tukumbuke kuwa Mungu wetu anataka kwanza watu wapone roho zao kabla hata ya kuwaza kupona miili yao. Ndio maana akasema utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na mengine mtazidishiwa. Hata kama mtu atapewa hiyo dawa akapona lakini lazima iko siku atakufa tu, sasa akifa atakwenda wapi? Ndio maana Mungu nahitaji kwanza roho zetu zipone. Huyu babu ni sawa na mganga wa kienyeji tu, hana injili yeyote anyohubiri. Anawaza kuponya miili tu wakati Mungu anahitaji tuanze kwanza kuponya roho zetu.

III. Miujiza ya Mungu wa kweli lazima ifanyike kwa jina la Yesu tu – Marko 16:17, Luka 10:17, Mdo. 3;1-10. Miujiza ya Mungu haifanyike kwa kutumia mizizi ya miti, ni kwa Neno, ambaye ndiye Yesu Kristo.

IV. Neno linalohubiriwa lazima liwaongoze watu kutubu dhambi zao ili wamgeukie Mungu wao – Mdo. 3:19. Sasa pale Loliondo mmesikia kama watu wanatubu dhambi zao na kumrudia Mungu wao au wanapewa dawa tu. Hakuna Mungu hapo, ni uganga tu ndio unaoendelea hapo.

V. Toba ya kweli lazima iwaelekeze watu kwa Yesu – Hes. 21:4-9, Yoh. 3:14-15

VI. Mungu hulituma Neno lake ili kuwaponya watu – Zab. 107:18-20. Mungu anaponya kwa Neno tu, sio kwa mizizi ya miti au chochote kile.

VII. Yesu Kristo alipokuwa anawatuma wanafunzi wake kwenda kuhubiri na kuponya magonjwa aliwaagiza kuwa "mmpewa bure toeni bure" – Mt. 10:8. Sasa mambo ya watu kutoa mia tano yanatoka wapi sasa? Uzima wa Mungu ni bure kabisa, hakuna biashara yeyote inayofanyika, ni karama ya Mungu tu. Kinachoendelea Loliondo hakipo kabisa katika mapenzi ya Mungu, hata kama duniani nzima ingelihamia hapo.

VIII. Karama za Mungu haziwekwi kwa mtu mmoja tu, dunia hii ni kubwa na Mungu hawezi akaweka mtu mmoja tu kwa ajili ya kazi yake – 1Falme 18:20, 19:18. Yule babu kusema kuwa ni yeye peke yake aliyechaguliwa na Mungu kuleta uponyaji, huu ni uongo ulio wazi kabisa, hayo ni masharti ya waganga wa kienyeji kabisa. Karama za Mungu wa Biblia zinaambatana na kuwafundisha wengine jinsi ya kutumiwa na Mungu kama Yesu alivyofanya, sio mtu mmoja tu. Tena, karama za Mungu hazifungiwi na sehemu moja tu. Eti dawa itolewe hapo kijijini tu, hayo ni masharti ya mizimu tu, Mungu hayupo hapo. Yesu alisema enendeni ulimwenguni wote, sio mkae kwenye kijiji kimoja ambacho hata hakifikiki kirahisi – Marko 16:15

Ndugu zangu, nawasihi kwa jina la Bwana na mwokozi wetu Kristo Yesu, tusiwaze tu juu ya uponyaji wa miili yetu na tukasahau uponyaji wa roho ambao ndio wa muhimu zaidi. Hata kama tukipona leo, iko siku tutakufa tu. Kwa hiyo lolote tunalolifanya leo ni muhimu tuhakikishe kuwa linakubalika mbele za Mungu wetu.

Suala hapa sio kupona tu, lakini lazima tujue huo uponyaji unatoka wapi. Wagonjwa wengi tu wa ukimwi na magonjwa mengine sugu wameshapata kuponywa kwa njia ya maombezi tu katika jina la Yesu, lakini ajabu ni kwamba habari zao hazikuvumisha kama hili la Loliondo. Wakati wote imekuwa ni vigumu sana kwa vyombo vya habari kutangaza habari njema kama hizo zinatokea makanisani kwa sababu ibilisi hataki watu waufahamu ukweli huo. Hata zinapotangazwa bado, mwitikio unakuwa ni mdogo sana. Lakini hili kwa kuwa ni la kwake mwenyewe ibilisi ndio maana limepigiwa kelele na vyombo vyote vya habari, hata na viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini wamekuwa mstari wa mbele kulishabikia na kulienzi. Ni kama upepo fulani unawachukua watu wote bila kujijua na kila mtu anawaza kuwahi kunywa hiyo dawa tu. Tusiwe hivyo ndugu zangu, bali tutafakari na kuyapima yote kwa Neno la Mungu.

Mwisho, Mungu akubariki sana na washirikishe wengine ujumbe huu.

Note:Being an anti-christ does not only mean being against christ,but also imitating to be like christ

Kwa hiyo mwingira amekutuma useme hivyo? Mbona yeye mwingira anawadanganya watu watoe mali zao zote kwake na kuwaacha watu hao maskini hali yeye akibaki kuwa tajiri wa kutupwa kwa kutumia mali hizo hizo alizopora kwa watu wema. Ekari 600 za mahindi kule rukwa, hammer, benki, na mimali kibao amevitoa wapi?
 
Aliyeandika hizi habari ndiye nabii wa uongo, kwani babu anahubiri nini? Hebu kamuulize huyu mtumishi yeye anapohubiri watu kutoa zaidi kuliko kuwapatia faraja ktka bwana haendi kinyume na matakwa ya Mungu?
 
Kwa hiyo mwingira amekutuma useme hivyo? Mbona yeye mwingira anawadanganya watu watoe mali zao zote kwake na kuwaacha watu hao maskini hali yeye akibaki kuwa tajiri wa kutupwa kwa kutumia mali hizo hizo alizopora kwa watu wema. Ekari 600 za mahindi kule rukwa, hammer, benki, na mimali kibao amevitoa wapi?

Waliomshambulia babu so far,...

Group 'A'...Majjid Mjengwa ,Jenerali Ulimwengu,Rostam Azizi,....

'B'...Kakobe , Mwingira,.........

My take,...nafikiri hayo makundi yote yana maslahi binafsi katika hili i.e either ya kidini or ya kimaslahi/fedha....lakn siku zote wema hushinda uovu na hivyo sote twajua babu atashinda.......
 
Ndugu kubali tu kuwa watu wanapona. Roho zao wataenda kuziponyesha mbele ya safari. Ni lipi binadamu hawalijui katika ulimwengu wa nyama na roho? Mengi ni marudio hivyo ni jukumu la mwanadamu pekee kujitambua yeye ni nani maana nyenzo zote za kumsogeza karibu na Mungu anazo. Kwa hiyo basi muacheni babu atoe ahueni ( hata kama ni ya muda mfupi) kwa wenye kuhitaji!!!!!!
 
nachelea sana kusema lolote hasa kwenye imani za watu.
waacheni waendao loliondo waende kama imani yao ipo kwa babu.
na waacheni waendao kwa mwingira na wengineo kama imani yao ipo huko.
mwisho wa siku itafahamika tu.
na sio mkataze watu kwenda kwa babu kisa mapato kanisani yanapungua kwan waumini wamebadili ruti
 
Kuna tatizo gani kwenda kuutibu mwili? Hospitali zemewekwa za nini, si kwaajili ya kuutibu mwili!! Kama ungekuwa unaweza kujitibu mwenyewe nyumbani nadhani ungejitibu. Kama kuna mtu anawezakukutibu ugonjwa wako kwanini usimwendee ili akutibu!! Babu anatibu magonjwa ya mwili ambayo watu yanawatesa, na magonjwa hayohayo ndio yaliyowapeleka watu kwa Mwingira wakaombewe, ndiyo yanayomtajirisha mwingira. Mwacheni babu awaponye watu kwani yeye aagui. Babu sio mwizi wa kutumia biblia kama akina Mwingira.
 
Mh. Speaker

Pole sana kwa mahubiri haya yenye nguvu sana na mazuri ila umeyatoa wakati mbaya mno.

Kwa experience yangu ya miaka 11 kwenye wokovu au kuwa ndani ya makanisa ya ki-pentecost kwa bahati mbaya sijaishi kama blind follower, nimeuliza, nimetafuta, nimeona, nimeshuhudia na acha nikueleze au kukudadavulia challenge zifuatazo ambazo wengi wenu mnazo aidha hamjaziona au mmeziona ila hamtaki kuzikubali

1. Wengi wa Watanzania HAWANA dini

Ukirudi kwenye historia ya jinsi dini hizi zilivyoletwa utagundua moja ya challenge kubwa , ni kuzielewa, kuzikubali kutoka moyoni na si kushurutishwa. Ukumbuke ya kuwa kabla ya dini kuja hapa nchini, tulikuwa na dini zetu za asili ambazo ni kuabudu mawe, miti, mizimu, jua, n.k.

Leo hii watu wengi wanafuata dini zao kwa sababu ya WAZAZI WAO, wengi ni wakristo na waislamuk wa kufuata mkumbo wa wazazi wao, mmewaita majina ya kikristo na kiislamu kwa matumaini ya kuwa watazifuata hizo dini. Mmewapeleka makanisani mkawabatiza wakiwa WATOTO, mmewapeleka madrasa na kuwasomesha Quran . Mkiamni hawa watu watakuwa katika njia mnazozitaka nyie. As a result wakiwa wakubwa watu wa dini hizi wengi ndio wazinzi,ushirikina, mafisadi, walafi, waongo, wauaji na wachafu wa kila aina.WHY ? HAWAKUFUATA DINI baada ya kuwa na akili na kujua ukweli wa dini zao.ILA walilazimishwa ( na huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu).

Yakitokea mambo kama ya Loliondo au watu hawa wanashida Fulani basi unaziona rangi zao za ASILI. Kama hao watu wanafanya uchafu nilioutaja hapo juu, kwa nini wasiende Loliondo? NI wangapi leo hii wanaoenda kwa waganga wa kienyeji? N

Kama msingi wa dini ya mtu ni wazazi wake au mkumbo Fulani, basi wengi WAO hawana SUSTAINABLE FAITH, they are faith are weka and can easily swayed by anything as we are seeing now.

NAONA umeshtuka swala la Loliondo, but Loliondio thing are so many kila siku yapo nchi hii, where were are you those days

2. Msimzimishe Roho Mtakatifu
Umesema vyema kuhusu swala la kutomzimisha roho mtakatifu, kumbuka kuwa, ROHO mtakatifu hana formula na hapa inabidi kuwa waangalifu kwenye comments zetu, mawazo yetu na nia zetu.Biblia inasema Mariamu alipomsalimia Elizabeth kitoto cha Elizabeth kikaruka! Roho Mtakatifu connects people in the very same way! Kama Roho wa Mungu( kama unaye) akikueleza jambo Fulani, lazima kuna hekima itatumika, lakini lazima kuna jambo Fulani litadhihirisha hali hiyo.

Babu mpaka sasa hakuna NENO AU ANDIKO lolote la KWENYE biblia analo-li-VIOLATE? Hakuna! Kama miti , ndiko dawa zote zinazkotokea, anasema anatibu kwa jina la YESU! Na maji, JE Ni matendo mangapi ya ki-biblia ambayo leo hiii yakitokea HAYATAAMSHA HISIA nyingi?

Kutokuwa na Roho Mtakatifu pekee ni ishara tosha kuwa wengi wa wakristo ni wafuata mkumbo wazuri na kibaya hawasomi hata biblia yenyewe!

Je unamhukumu mzee kwa andiko lipi? Au je kama kuna mwisho wa dunia dalili zimeanza leo?

3. Imani thabiti kwa watu makini
Nimefurahi sana umetoa angalizo kuwa watu wawe makini! Is this not too late? KILA SIKU WATU si wanaenda makanisani? Wanafundishwa nini huko? WAKRISTO WENGI na watu wa DINI zingine kukimbilia issues kama hizi ni ISHARA TOSHA KUWA WACHUNGAJI WENGI huwa hawafanyi kazi yao kubwa ambayo ni kuimarisha imani za waumini! Wengi hwafanyi haya mmekalia kuozesha ndoa za wajawazito, kuchukua sadaka n.k!!!! This is a proof that many pastors are not doing their Job! Hii itakuja kutokea hata zikianzishwa mahakama za kadhi kwa waislamu, kama zitakuwa so strictly wengi wataondoka kwenye dnini zao,rudia point zangu za mwanzo

4. Kuombea Ukimwi
Personally nimeshiriki kuombea wagonjwa wa Ukimwi, wamepona, I can testify this over and over, kutojulikana kwa haya ni uzembe wa wakristo wenyewe na si failure ya vyombo vya habari. NA mara nyingi wakristo ndio wa kwanza kutoamini!

Lakini challenge ni hii, wanagapi ambao ni wachungaji wanaoombea wagonjwa wa ukimwi? Kama Yesu alisema mtafanya ishara zaidi ya hizi , je wengi wa wachungaji sio matapeli?? KWA NINI HAWAFANYI MIUJIZA? Maana swala la uponyaji NI LA WOTE , MAANA ALISEMA MTAWEKA MIKONO JUU YA WAGONJWA NA WATAPATA AFYA, why this is not happening to our churches from agnlican, Lutheran, moravian , Pentecost, catholic and even in muslims?? Kwa wakristo hayatokei kwa sababu sio WASAFI..KAMA SIO WASAFI na hawa ni wachungaji je waumini wakoje??

KUTOKANA NA MISINGI YAO YA IMANI, NA YA KUWA HAWAPATI UPONYAJI KWENYE IMANI ZAO, BASI WAACHENI WAENDE HUKO, UNLESS NA NYIE MTOE UPONYAJI.
 
<p>
Hamtajua Siku wala Saa Atakayorudi Yesu Kristu
</p>
<p>&nbsp;</p>
asante kwa ujumbe lakini kwanini tusigawane majukumu babu aponye mwili nyie wenye wasiwasi kupoteza mafungu ya kumi na malimbuko mponye roho ////////////////
 
Tafadhali mods mi natoka, nikirudi basi huu ushuzi niukute ktk jukwaa la Dini.....humu ni pahala pa siasa tu
 
Jibuni kwa hoja na evidence please kwamba babu yuko sahihi kama jinsi vigezo vya kibiblia vilivyo tolewa kwamba hayuko sahihi
 
Kwa hiyo mwingira amekutuma useme hivyo? Mbona yeye mwingira anawadanganya watu watoe mali zao zote kwake na kuwaacha watu hao maskini hali yeye akibaki kuwa tajiri wa kutupwa kwa kutumia mali hizo hizo alizopora kwa watu wema. Ekari 600 za mahindi kule rukwa, hammer, benki, na mimali kibao amevitoa wapi?

Huyu ndiyo kabisa mpotoshaji yeye ni business oriented yesu mwenyewe alisema akiwa kama mwanawangu hana hata mahali pa kuweka kichwa chake yaani kulala na kama angetaka angeweza kujilimbikizia mali lakini alisema amejiwekea hazina yake mbinguni. Wizi mtupu.
 
AMEKUELEWESHA KIPI KINACHOWEZA KUMTOFAUTISHA MTUMISHI WA MUNGU NA MTUMISHI WA SHETANI.3.MEKUELEZA UTAZAMIE NINI KTK ZAMA HIZI ZA NYAKATI ZA MWISHO kama YESU alisema zipo siku za mwisho ni nani awezaye kubisha???5.FUATILIA KWA MAKINI NI WATU WENGI TU WAMEAMINI NA WAMEPONA UKIMWI KUTOKA KWA WATUMISHI MBALIMBALI.je Mungu aliposema usije mikono mitupu kwangu ulitaka hizo sadaka watu wakazipeleke kwa Mun gu kwa njia gani?????????? MWISHO NAMPONGEZA SANA SPEAKER KWA KULETA MAFUNDISHO HAYA KWA WAKATI WAKE HASA.NENO LA MUNG U LINASEMA WATU WANGU WANAPOTEA KWA KUKOSA MAARIFA SPEAKER AMEWAPA MAARIFA JINA LA BWANA NA LIBARIKIWE SANA.AMEN N
Mh. Speaker

Pole sana kwa mahubiri haya yenye nguvu sana na mazuri ila umeyatoa wakati mbaya mno.

Kwa experience yangu ya miaka 11 kwenye wokovu au kuwa ndani ya makanisa ya ki-pentecost kwa bahati mbaya sijaishi kama blind follower, nimeuliza, nimetafuta, nimeona, nimeshuhudia na acha nikueleze au kukudadavulia challenge zifuatazo ambazo wengi wenu mnazo aidha hamjaziona au mmeziona ila hamtaki kuzikubali

1. Wengi wa Watanzania HAWANA dini

Ukirudi kwenye historia ya jinsi dini hizi zilivyoletwa utagundua moja ya challenge kubwa , ni kuzielewa, kuzikubali kutoka moyoni na si kushurutishwa. Ukumbuke ya kuwa kabla ya dini kuja hapa nchini, tulikuwa na dini zetu za asili ambazo ni kuabudu mawe, miti, mizimu, jua, n.k.

Leo hii watu wengi wanafuata dini zao kwa sababu ya WAZAZI WAO, wengi ni wakristo na waislamuk wa kufuata mkumbo wa wazazi wao, mmewaita majina ya kikristo na kiislamu kwa matumaini ya kuwa watazifuata hizo dini. Mmewapeleka makanisani mkawabatiza wakiwa WATOTO, mmewapeleka madrasa na kuwasomesha Quran . Mkiamni hawa watu watakuwa katika njia mnazozitaka nyie. As a result wakiwa wakubwa watu wa dini hizi wengi ndio wazinzi,ushirikina, mafisadi, walafi, waongo, wauaji na wachafu wa kila aina.WHY ? HAWAKUFUATA DINI baada ya kuwa na akili na kujua ukweli wa dini zao.ILA walilazimishwa ( na huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu).

Yakitokea mambo kama ya Loliondo au watu hawa wanashida Fulani basi unaziona rangi zao za ASILI. Kama hao watu wanafanya uchafu nilioutaja hapo juu, kwa nini wasiende Loliondo? NI wangapi leo hii wanaoenda kwa waganga wa kienyeji? N

Kama msingi wa dini ya mtu ni wazazi wake au mkumbo Fulani, basi wengi WAO hawana SUSTAINABLE FAITH, they are faith are weka and can easily swayed by anything as we are seeing now.

NAONA umeshtuka swala la Loliondo, but Loliondio thing are so many kila siku yapo nchi hii, where were are you those days

2. Msimzimishe Roho Mtakatifu
Umesema vyema kuhusu swala la kutomzimisha roho mtakatifu, kumbuka kuwa, ROHO mtakatifu hana formula na hapa inabidi kuwa waangalifu kwenye comments zetu, mawazo yetu na nia zetu.Biblia inasema Mariamu alipomsalimia Elizabeth kitoto cha Elizabeth kikaruka! Roho Mtakatifu connects people in the very same way! Kama Roho wa Mungu( kama unaye) akikueleza jambo Fulani, lazima kuna hekima itatumika, lakini lazima kuna jambo Fulani litadhihirisha hali hiyo.

Babu mpaka sasa hakuna NENO AU ANDIKO lolote la KWENYE biblia analo-li-VIOLATE? Hakuna! Kama miti , ndiko dawa zote zinazkotokea, anasema anatibu kwa jina la YESU! Na maji, JE Ni matendo mangapi ya ki-biblia ambayo leo hiii yakitokea HAYATAAMSHA HISIA nyingi?

Kutokuwa na Roho Mtakatifu pekee ni ishara tosha kuwa wengi wa wakristo ni wafuata mkumbo wazuri na kibaya hawasomi hata biblia yenyewe!

Je unamhukumu mzee kwa andiko lipi? Au je kama kuna mwisho wa dunia dalili zimeanza leo?

3. Imani thabiti kwa watu makini
Nimefurahi sana umetoa angalizo kuwa watu wawe makini! Is this not too late? KILA SIKU WATU si wanaenda makanisani? Wanafundishwa nini huko? WAKRISTO WENGI na watu wa DINI zingine kukimbilia issues kama hizi ni ISHARA TOSHA KUWA WACHUNGAJI WENGI huwa hawafanyi kazi yao kubwa ambayo ni kuimarisha imani za waumini! Wengi hwafanyi haya mmekalia kuozesha ndoa za wajawazito, kuchukua sadaka n.k!!!! This is a proof that many pastors are not doing their Job! Hii itakuja kutokea hata zikianzishwa mahakama za kadhi kwa waislamu, kama zitakuwa so strictly wengi wataondoka kwenye dnini zao,rudia point zangu za mwanzo

4. Kuombea Ukimwi
Personally nimeshiriki kuombea wagonjwa wa Ukimwi, wamepona, I can testify this over and over, kutojulikana kwa haya ni uzembe wa wakristo wenyewe na si failure ya vyombo vya habari. NA mara nyingi wakristo ndio wa kwanza kutoamini!

Lakini challenge ni hii, wanagapi ambao ni wachungaji wanaoombea wagonjwa wa ukimwi? Kama Yesu alisema mtafanya ishara zaidi ya hizi , je wengi wa wachungaji sio matapeli?? KWA NINI HAWAFANYI MIUJIZA? Maana swala la uponyaji NI LA WOTE , MAANA ALISEMA MTAWEKA MIKONO JUU YA WAGONJWA NA WATAPATA AFYA, why this is not happening to our churches from agnlican, Lutheran, moravian , Pentecost, catholic and even in muslims?? Kwa wakristo hayatokei kwa sababu sio WASAFI..KAMA SIO WASAFI na hawa ni wachungaji je waumini wakoje??

KUTOKANA NA MISINGI YAO YA IMANI, NA YA KUWA HAWAPATI UPONYAJI KWENYE IMANI ZAO, BASI WAACHENI WAENDE HUKO, UNLESS NA NYIE MTOE UPONYAJI.

POLE SANA NDG YANGU,1.HUJAFUATILIA TIBA YA BABU IPASAVYO ie ni wakati gani babu amewahubiria wateja wake habari za YESU??? jibu ni HAKUNA ni kikombe unaanza tena ndani ya gari . 2.HUKUMSOMA / KUMWELEWA NDG SPEAKER IPASAVYO ie babu ni mganga wa kienyeji kama wengine wowote -
 
Ndugu Speaker!
Kwa jinsi nilivyosoma habari za huyo babu, sidhani kama amesema labda yeye ni nabii au mtume. Wala hajawaambia watu waache dini zao wamfuate yeye. Huoni kuwa maandiko uliyopewa na kutuonyesha hapo juu yanawafaa zaidi wale ambao wamejiita kabisa kwamba ndio manabii na kila mara hudai misadaka mikubwa? Vipi hawa wengine waliowahi kumtabiria Mrema kushinda urais, unakumbuka?

Maandiko haya toka zamani yalilengwa kwa waumini wa kweli, wenye imani na utakatifu ndani ya hiyo dini,wakionywa kutoyumbishwa na ishara za manabii wa uongo. Lakini babu hajasema yeye ni nabii, na pia hatujui imani za waliokwenda huko, au wanaotaka kwenda huko. Mtu mwingine kama mimi ninajijua kabisa si msafi hivyo kiimani, leo ninaumwa halafu ukiwa kiongozi wangu unaniambia eti babu ni nabii wa uongo kwa hiyo nisiende kujaribisha tiba, wakati wewe na madakatri mmeshindwa kunisadia, na tena wewe kiimani ni mchafu tu kama mimi... it simply, doesn't make sense!

Nafikiri watu wanalivalia njuga hili jambo kutokana na hofu tu. Hofu yenyewe ama ni ya kimaslahi [kupungua kwa vichwa (sadaka) kwenye nyumba zingine za ibada] au hofu kwa wasioupenda ukristo, wakiogopa kwamba labda hii itaongeza kukubalika kwa ukristo kwa ujumla.
 
Kuifahamu biblia si kielelezo cha uzima wa roho yako. Unaweza ukaifahamu biblia kama elimu 2. Imani ndiyo imponyayo m2. Hata Yesu alipoponya wa2, hakusema "Nenda nimekuponya" alisema "Nenda Imani yako Imekuponya".
Kumbuka pia haya ni magonjwa. Huwapata walio wema na wabaya. Mungu habagui, ndio maana tunaambiwa "Huwanyeshea mvua walio wema na wabaya"
 
Ndugu Speaker!
Kwa jinsi nilivyosoma habari za huyo babu, sidhani kama amesema labda yeye ni nabii au mtume. Wala hajawaambia watu waache dini zao wamfuate yeye. Huoni kuwa maandiko uliyopewa na kutuonyesha hapo juu yanawafaa zaidi wale ambao wamejiita kabisa kwamba ndio manabii na kila mara hudai misadaka mikubwa? Vipi hawa wengine waliowahi kumtabiria Mrema kushinda urais, unakumbuka?

Maandiko haya toka zamani yalilengwa kwa waumini wa kweli, wenye imani na utakatifu ndani ya hiyo dini,wakionywa kutoyumbishwa na ishara za manabii wa uongo. Lakini babu hajasema yeye ni nabii, na pia hatujui imani za waliokwenda huko, au wanaotaka kwenda huko. Mtu mwingine kama mimi ninajijua kabisa si msafi hivyo kiimani, leo ninaumwa halafu ukiwa kiongozi wangu unaniambia eti babu ni nabii wa uongo kwa hiyo nisiende kujaribisha tiba, wakati wewe na madakatri mmeshindwa kunisadia, na tena wewe kiimani ni mchafu tu kama mimi... it simply, deosn't make sense!

Nafikiri watu wanalivalia njuga hili jambo kutokana na hofu tu. Hofu yenyewe ama ni ya kimaslahi [kupungua kwa vichwa (sadaka) kwenye nyumba zingine za ibada] au hofu wasioupenda ukristo, wakiogopa kwamba labda hii itaongeza kukubalika kwa ukristo kwa ujumla.
Nashukuru sana ndugu, nimekugongea senksi naona haitoshi! Babu wawatu alikuwa kimya, hajajitangaza, hajajiita nabii, mpakwa mafuta, askofu mkuu, mchungaji kiongozi wala mzee wa upako.! Mmmejileta wenyewe halafu mnaanza kumchokonoa. Mnataka awe anasoma ibada kila siku kabla ya matibabu.? Hasomi basi! Na ndivyo alivyopangiwa namna ya kuponya. Mbona Yesu aliponya mpofu kwa tope la mate hamsemi? Kwani kuna formula katika uponyaji? Kumbuka huyu babu hatoi tiba, yeye anatoa uponyaji. Kuna tofauti kati ya tiba na uponyaji. Tiba ina kanini, uponyaji hauna kanuni. Mimi simpingi babu kwani Ukimwi na kansa ni baadhi ya mateso ambayo shetani anayafurahia sana kwa jinsi yanavyotesa wanadamu. Kama dawa imepatikana, its obvious iko against devil.
 
AMEKUELEWESHA KIPI KINACHOWEZA KUMTOFAUTISHA MTUMISHI WA MUNGU NA MTUMISHI WA SHETANI.3.MEKUELEZA UTAZAMIE NINI KTK ZAMA HIZI ZA NYAKATI ZA MWISHO kama YESU alisema zipo siku za mwisho ni nani awezaye kubisha???5.FUATILIA KWA MAKINI NI WATU WENGI TU WAMEAMINI NA WAMEPONA UKIMWI KUTOKA KWA WATUMISHI MBALIMBALI.je Mungu aliposema usije mikono mitupu kwangu ulitaka hizo sadaka watu wakazipeleke kwa Mun gu kwa njia gani?????????? MWISHO NAMPONGEZA SANA SPEAKER KWA KULETA MAFUNDISHO HAYA KWA WAKATI WAKE HASA.NENO LA MUNG U LINASEMA WATU WANGU WANAPOTEA KWA KUKOSA MAARIFA SPEAKER AMEWAPA MAARIFA JINA LA BWANA NA LIBARIKIWE SANA.AMEN N

POLE SANA NDG YANGU,1.HUJAFUATILIA TIBA YA BABU IPASAVYO ie ni wakati gani babu amewahubiria wateja wake habari za YESU??? jibu ni HAKUNA ni kikombe unaanza tena ndani ya gari . 2.HUKUMSOMA / KUMWELEWA NDG SPEAKER IPASAVYO ie babu ni mganga wa kienyeji kama wengine wowote -

Ndugu, sijui uko mlengo gani sidhani kama nimeandika nakala kubisha alichosema Speaker, wewe haujanielewa, nimekupa challenge sinavomface mkristo au ww kuzuia hiyo dawa! swala la kuwa ni ya kweli au uongo, itajulikana hapo baadae, ikiwa ni cha Mungu kitadumu, ikiwa ni cha shetani au binadamu hakitadumu!

Niambie mchungaji nani DSM ambaye anaombea ukimwi leo watu wakienda tu wanapona!! kama hayupo , hauoni ww kama mristo ndio muda wa kuamka kufanya hayo? mmelala na mnaamka pindi wengine wakichukua nafasi zenu, kibaya zaidi nakumabia nimepna watu wakipona Ukimwi , sijajua hujaelewa nini!

Haya zuia watu wasiende sasa Loliondo! mnajipa pressure za bure tu
 
Humu JF kuna baadhi yetu wamekwisha kwenda kwa babu na kupata tiba ya magonjwa sugu.Na wengi wanatumia ID za kubuni.

Jamani jitokezeni mtupatie udhibitisho wa kupona baasda ya kutumia dawa hii ya 'babu' ili na sisi tulioko mbali tuanze kudunduliza ili twende.

Tunawategemea sana waliokwisha kunywa.Tupe matokeo

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom