Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Watu, ambao wanaaminika kuwa na akili vichwani wanahoji kwanini auze dawa hiyo kama ni maono ya Mungu!!!...
Mi kwa hasira nitawaita hawa wote wa jamii hii kuwa ni WAPUMBAVU!...unategemea mtu huyu ataoperate namna gani kutoa dawa kwa watu wa dunia yote, then asipate hata mkate wa shs.500, na kisha afe kwa njaa?
Mbona wahubiri wanaojiita manabii, wapakwa mafuta, mitume na majina meengi ya kujitukuza, mbona wanapokea fedha nyingi sana za sadaka toka kwa waumini wao, kwanini wanamwonea wivu babu kuchangisha siing 500 tu?

Sasa mtu atatoa huduma hiyo BURE, kwa muda gani, maana huduma hii inaonekana itakuwa ya kudumu!
Walalamishi hawa wamepoteza heshima mbele ya jamii, maana wanaonekana wamejaa wivu sana kwa babu!

Wataendelea kusema sana, lakini dawa inatolewa, inaponya, na mwishowe wenyewe watashuka kwenye madhabahu zao na kwenda kutibiwa!


hii ndio mipumbavu inayokimbilia kanisani na kushindwa kutoa hata sh 500

BAIBO IMESEMA WAZI NA ALAANIWE APOKEA BURE ....Wee waache wabaki kusubiri bure na NANII ZAO...
 
mmhh
hizi stori za lolliondo zimekuwa nyingi sana humu JF
na hata sielewei ..

kuna mtu ambaye anaweza kunielewesha ni nini kinaendelea huko???

tafadhali usinijibu kama huna nia ya kunijulisha
AD.....

kuna babu anascan virusi vya ukimwi na anatibu magonjwa sugu. Ametoshwa na mungu.
 
Unajuaje kama waendao hawaumwi? Wengi wanatembea wakionekana wana afya lakini wanaumwa, magonjwa mengine ni siri yao wagonjwa na madaktari. Sidhani mtu mzima atahangaika kwenda kote huko kwenye huo msururu kupoteza muda tu. Usitake kuona wana upele au wamepauka ngozi ndo useme ni wagonjwa. Wengine wako hatua za awali, wengine wanaumwa vitu ambavyo havisemeki au kuonekana kwa macho. Waache waende tu kama wanaweza kufika na kuondoka, utaratibu si umewekwa wakifika wanakunywa na kuondoka siku hiyo hiyo?
 
Bango waliopona mkuu,
Babu kajificha loliondo ndani ndani.
Barabara ya kwenda kwake mbofu ile mbaya, wamemvumbua wagonjwa wa magonjwa sugu walio pona!
Na hao ndio bango la babu,
Babu hana cha kwenda ch 10 au star TV kama akna Ndodi yeye ni huko kijiji cha mbali
 
Nilichosikia toka kwa wenyeji hutumia dawa ya MUGARIGA kama sumu kwa kuwindia wanyama kwa kuipaka kwenye mikuki na mishale ili kuulia wanyama!sijui mwenye data zaidi aweza kutupasha!
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Nimepata kisa kimoja cha kweli kilichotokea huko Loliondo kwa Babu Mchg daktari bingwa wa magonjwa sugu.Baba mmoja jina nalihifadhi kwasasa tuliwahi kufanyakazi pamoja General Tyre Division ya Finance kipindi cha nyuma kabla haijafisadiwa na mafisadi Papa.

Baba pamoja na ndugu jamaa na marafiki walifunga safari ya kwenda Loliondo[private car] kwa Babu kwaajili ya kupata kikombe [dawa].walifika Loliondo salama salimini,Baba akaongoza msafara wa jamaa na ndugu waliosafiri pamoja toka Arusha akapewa kikombe cha Babu akaondoka mara ghafla akaanza kujisikia vibaya moto ukawa unamuunguza ndani ya tumbo akakimbilia maporini katika hali ya kutaka kujiokoa.

Ndugu na jamaa waliofutana na Baba baada ya kupata kikombe cha Babu wakamtafuta lakini hawakufanikiwa kumwona wakaamua kurejea mahali walipoliacha gari lakini pia hawakumkuta wakadhani pengine atakuwa amekutana na marafiki zake akaamua kutangulia Arusha wakaamua kuondoka kufika nyumba hawakumkuta.Wakamtafuata kwa ndugu wa karibu bila mafanikio siku ya pili wakaamua kutuma ujumbe wa watu kadhaa[Ndugu] kwenda Loliondo kwaajili ya kumtafuta,iliwachukua siku mbili wakafanikiwa kupata habari kwamba alikwenda kijiji cha mbali kidogo na mahali Babu anapogawa dawa walipofika huko wakapewa maelezo kwamba ni kweli kuna mtu kutoka mjini alifika majira ya saa mbili usiku akiwa amechoka na kuchanaganyikiwa shati kalishikilia mkononi alipohojiwa kulikoni akawaeleza kwamba yeye ni mchawi haswa amewahi kushiriki matendo mengi ya kutoa kafara watoto wachanga ili awe tajiri na kulinda kibarua chake.Wenyeji wakaamua kumtafutia sehemu ya kulala lakini Baba akakataa kata kata akawa anazidi kutua siri za uchawi wake na kuwalaani waliomshawishi kuja kwa Babu wa Loliondo akajiapiza akifanikiwa kurejea nyumba atawafanyizia mbaya.Baada ya muda akaanguka na kuaga dunia majira ya saa nne usiku huo huo ndugu zake wakaonyeshwa kaburi na shati lake wakalitambua.

Kazi ya kufukua mwili wa Baba ikaanza mara moja na siku hiyo hiyo wakarejea Arusha kwaajili ya mazishi ya heshima.Habari za mkasa zikaaza kuzagaa unajua tena mswahili atakunyima chakula lakini jambo atakwambia.
 
katuni%2Bmajira%2B15.3.11.jpg
 
na hapo nani mchawi wa mwenzie

Heshima kwako Pdidy,

Mkuu hii kitu si utani au habari za udaku sitarajii mzahaa hata kidogo ndiyo maana nimelihifadhi jina la mhusika kwakuwa najua wapo wanajamvi watakao guswa kwa njia moja au nyingine na msiba wa Baba yetu mpendwa aliyetangulia mbele ya haki.

Wafanyakazi waliowahi kufanyakazi Genaral Tyre kuanzia mwaka 1975 mpaka mwaka 2006 mnaweza kufika nyumbani kwa marehemu Sekei karibu na halmashauri wilaya ya Arumeru,pia unaweza kupitia njia ya Ricks Club ni rahisi zaidi kufika na kuona sehemu ya msiba.Unaweza kuniPM kwa maelezo zaidi.

Mwenzetu katangulia mbele ya haki,ni njia yetu sote muhimu zaidi tujiandae.
 
polen mkuu najua sio utan ila namie nikaona nikupe kisanga kilichotokea..polen sana sanas huyo babu namfahamu nimeona na jina lake wakati wakimtafuta ndugu zake kwenye magazeti polen sana sana
Mungu aw\atie nguvu mmmhhhuuzuni
 
polen mkuu najua sio utan ila namie nikaona nikupe kisanga kilichotokea..polen sana sanas huyo babu namfahamu nimeona na jina lake wakati wakimtafuta ndugu zake kwenye magazeti polen sana sana
Mungu aw\atie nguvu mmmhhhuuzuni


Heshima kwako Pdidy,

Aksante mkuu nimekuelewa.
 
Aisee hapa kwetu kuna maza mmoja tumemkuta nae nasikia kigwagula sasa Mumewe alikwenda kupata kikombe baada ya siku kadhaa kuna mambo ya kama ya kumfichua hayo mambo yake ya uwanga moja ya hayo ni kukamatwa kwa mganga aliyemtuma kwenda kuwanga sehemu!!!

Mh babu wa Loliondo kweli Nourmer!!
 
Wacha waumbuke tu kama wameuwa mpaka vichanga kwa sababu ya kafara aaaghh inatia uchungu sana
 
Tahadhari! Hebu tujiulize. Hivi dawa ya babu kama ni sumu ya kuondoa pole pole itakuwaje? Nani anajua athari zake? Huyu Babu mwenyewe umri umeenda inawezekana akili zake zimeanza kupoteza majira lakini kila mtu anakimbia huko.

Hiii sii hoja hoja ni kwamba Hivi kweli watanzania uwezo wa kufikiri umefika mwisho?
Hivi tutaendelea kubahatisha mambo mpaka lini? Wasomi wako wapi?Madaktari nao wamefta mkia kama Kakobe? Je? Serikali nayo inaongozwa kwa bahati nasibu.Madhara yakitokea watatuambia JANGA?

Kwa staili hii tusitegemee kupata maendeleo kwa lolote katika nchi hii. Na ninani alaumiwe kwa hili?

CHUKUA HATUA LEO USISUBIRI KESHO.

Poleni watanzania mtakaodhurika na mogariga.

Kaka pole sana
Unaelekea unawasiwasi wa kukosa kazi.either unafanya kazi kwenye NGO's za ngoma na unaona clients wanapungua.Don't stick in idea.
 
naamini watz wengi tunaendeshwa na matukio, yani pamoja na changamoto nyingi sana tulizo nazo tayar watu wamesahau wame-concentrate kwenye tukio la Loliondo huku bado mgawo wa umeme ukiendelea kutukamua, ya Dowans bado ni kizungumkuti, katiba mpya serikali wamehodhi hoja na watu wamekaa kimya, maisha yanazid kuwa magumu bidhaa ni bei juu mno................................watz tusiendeshwe na matukio yasiyo ya msingi tukasahau hoja zinalolitafuna taifa
 
Back
Top Bottom