Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

kanywe dawa. Usihofu. Kwani siku mchungaji akisema wasiokunywa dawa watakufa wewe utafanyajaje?
 
kanywe dawa. Usihofu. Kwani siku mchungaji akisema wasiokunywa dawa watakufa wewe utafanyajaje?

kifo kipo na kila mtu atakufa.
Lakini watu hawataki kufa ndio maana tunaenda hosp na sehemu nyingine kuongeza siku za kuishi.
Je unakumbuka hofu ya kuingia karne ya 21?
 
Wana JF wenzangu, maisha hayawezi kuwa rahisi kiasi hicho, NEVER!, wagonjwa tuna hulka ya kutaka shortcuts/quick fixes au majibu rahisi kwa mambo magumu, nawasikitikia wale ambao walikuwa wanapata ARV na sasa wamezitupa baada ya kupata kikombe cha babu, huyu babu hakuanza leo wale wenye VVU waliopata hicho kikombe wakati anaanza, majority wameshakufa! (samahanini kwa kuwa hampendi ukweli huu)
Proof ya kupona VVU si rahisi kama watu wanavyojitangaza, vipimo vya kawaida vya VVU (rapid HIV tests) kuwa negative si ushahidi tosha, kuna vipimo zaidi ya hapo, kwa wale walio kwenye ARV nawashauri mkishapata kikombe usiache ARV, kwa kuwa mbele yako kuna kazi kubwa ya ku_prove kuwa mwili wako hauna VVU
 
Halafu mbaya zaidi kuna mabasi mengi sana (nimehesabu zaidi ya 15, kuna watu vichaa wanapeleka hadi hizi Hino za injini nyuma)

Pia kama unaenda usichukue gari ndogo ndogo (mf. Starlet) kumenyesha kidogo na sijui kama ni mwisho au itaendelea ila hata Hiace hazifai sababu ya utelezi na pia ile mvua imepanua mahandaki yaliyokuwepo, be cautious!

Huna haja ya kubeba maji, soda, bia za kopo, toilet pepa, juice (hasa hizi ready made unless umetengeneza ya kwako home) tayari kuna wajasiriamali wameshaona tatizo na ku-cover (bei ni almost za kawaida ila zinatofautiana kati ya watoa huduma)

Maliwato bado ni tabu sana, kama unawza bebe portaloo!
 
Huo umati kuisha labda babu asitishe, otherwise kila siku afadhali ya jana watu ni wengi mno. Babu tunakuombea Mwenyezi Mungu aendelee kukutia nguvu.
 
Kwa kipindi kifupi,Mchungaji mstaafu wa KKKKT ameweza kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na 'kutibu' magojwa sugu yaliyoshindikana hospitalini kwa kutumia 'dawa' itokanayo na kuchemsha mizizi na majani pamoja na imani.
Serikali 'imebariki' tiba hiyo kwa ama kukataa kuifungia isitumike kwa sababu haijathibitishwa kitaalam au kwa kutoa vyombo vya ulinzi kumlinda 'babu' ,dawa zake na wanaoenda pale kupata 'tiba'.
Sipingani na wale wanaoenda pale kupata huduma hii ya kiimani lakini wasiwasi wangu upo pale itakapo gundulika si tiba wala lolote,je serikali itachukua hatua gani.
Je kama ni tiba kweli ba watu wakapona,serikali itafanyaje kuhakikisha watu wengi zaidi wanaipata.
Kubwa zaidi ni je kwakuwa dawa hii ina nguvu kubwa ya kiimani kwa Mungu,siku mchungaji huyu akisema 'ameoteshwa' na Mungu kuwa wale wote walioenda kwake na kupata dawa kisha kupona wanatakiwa kurudi kwake wakiwa sh laki moja na asiyefanya hivyo atakufa ndani ya siku kadhaa,wewe na serikali mtafanyaje.
Najaribu kuona kitu kama hicho kinaweza kutokea,hii ni imani na fumbo.

Kwanza umeandika amejipatia umaarufu kwa kutibu....baadaye unauliza ikigundulika hiyo tiba si lolote serikali itafanyaje? Hiyo tiba haiwezi kuwa si lolote kwa kuwa imeshatenda miujiza tayari na tuna ushuhuda mwingi tu......!!!

Mungu aliyeweza kufikisha watu wote huo kule Loliondo kulivyo mbali atawasaidia lolote lile litakapotokea....manake kule hatuendi kutibiwa na Babu.....Mungu ndiye anatibu kupitia kwake....utukufu na heshima tunamrudishia Mungu na kumshukuru kwa kumtumia Mchungaji.....!

Kufa kuko palepale na anayejua utakufa lini na kwa namna gani ni Mungu aliyetuumba na kumuumba Mch pia.....siku ikifika imefika....sioni shida kufa kwa kuwa na imani na Mungu na kuamini yeye amemtumia Mch kutibu magonjwa sugu....naona shida kufa nikiwa sina imani na uwezo wa Mungu.....Mungu anaona sirini na ndani ya mioyo yetu kwamba tunamtumaini yeye,na anaheshimu hilo,kama imani yetu imejaribiwa na tukashindwa kutambua hilo,atatusamehe na tutaendelea kuwa watoto wake.....!!!!
 
hivi jamani ni kweli?maana nataka kujiaandaa kufunga safari kwa shida yangu nilionayo..mwenye ushuhuda atuambie fatadhali..
 
hahahahahaha ahahahaha ahahah. yaani ni noma, wabongo wengi ni wagonjwa, najua wengi hawasemi, ila asilimia kubwa walioenda huko kwa babu ni ngoma, hahahahahahaaaaaaaaaaaa, nandiomaana husikii waliopona wakijitokeza hadharani
kama mimi nilivyo mgonjwa na avatar yako!!!
 
hivi jamani ni kweli?maana nataka kujiaandaa kufunga safari kwa shida yangu nilionayo..mwenye ushuhuda atuambie fatadhali..[/QUOTE

ACHA KUPOTEZA MUDA KUTAFUTA USHUHUDA, NENDA FASTA
 
WAKATI miundiombinu ikizidi kuharibika Loliondo, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali ameagiza magari kutozwa ushuru na kupiga marufuku waandishi wa habari kumhoji Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwaisapile bila kibali.

Marufuku hiyo aliyoitangaza jana, inahusu pia upigaji picha za Mchungaji huyo maarufu kama Babu ambaye anatoa dawa ya magonjwa mbalimbali yakiwamo ya kisukari, Saratani, Kifafa na Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi).

Kwa uamuzi wa Lali, magari binafsi hivi sasa yanatozwa Sh. 2,000 wakati makubwa na ya biashara kama mabasi, malori na pick-up, yanayobeba abiria yanatozwa kati ya Sh. 5,000 na Sh. 10,000 na fedha hizo ni kwa ajili ya kuboresha mazingira ya eneo la tiba.

Kwa sasa wateja wa Mchungaji huyo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), wamekuwa wakilalamikia kuzagaa kwa takataka na uchafu kikiwamo kinyesi cha binadamu huku mvua zikianza kunyesha na kuzua hofu ya magonjwa ya mlipuko.

Kuhusu waandishi wa habari kumwona Mchungaji Mwasapila na hata kumpiga picha, alisema itabidi kwanza kupata kibali kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

“Hivi sasa mwandishi yeyote anayetaka kumhoji au kupiga picha yake, lazima aende Arusha katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupata kibali maalumu,” Lali alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidori Shirima alipoulizwa alihoji, “hakuna kitu kipya, Mchungaji Mwasapila amekwishaeleza kila kitu kuhusu dawa yake sasa ahojiwe nini tena?”

Aidha, Mamlaka ya Udhibiti wa Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imesema haijaandaa utaratibu wa kudhibiti viwango vya nauli kwa ajili ya magari yanayokwenda Loliondo kupeleka wateja wa Mchungaji huyo, kwa kuwa suala hilo ni la dharura.

Mkurugenzi wa Sumatra wa Mkoa wa Arusha, Ahmadi Kilima, alisema , walikuwa wamesajili mabasi sita yanayofanya safari kati ya Loliondo na Arusha, lakini kutokana na kugundulika kwa dawa hiyo, magari ya aina mbalimbali yamejitokeza kusafirisha abiria.

Alisema, Mamlaka hiyo sasa haiwezi kupanga kiwango cha nauli ya Loliondo kwa magari mengine isipokuwa yaliyosajiliwa, ambayo nauli halali ni kati ya Sh. 13,500 na Sh. 35,000.

Hata hivyo, alisema uongozi wa Arusha na wadau wa usafirishaji, wanalifanyia kazi suala la kupanda nauli ya Loliondo ili kuja na kiwango kimoja.

Alisema, ni vyema suala hilo likafanyiwa kazi haraka ili abiria wajue wanatozwa kiasi gani, kwani suala hilo liko kiholela zaidi kwa kila mmoja kutangaza bei yake.
 
Sumaye atinga Loliondo Send to a friend Thursday, 17 March 2011 22:52 0diggsdigg

Waandishi Wetu

sumaye1.jpg
Frederick Sumaye

WAKATI mamia ya watu wakiendelea kumiminika kupata tiba ya dawa ya magonjwa sugu kwa mchungaji wa KKKT katika Kijiji cha Samunge, Wilayani Loliondo, jana ilikuwa zamu ya Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kupata kikombe cha babu huyo.
Hatua ya Sumaye ni mwendelezo wa uwazi kwa viongozi wanaokwenda Samunge siku za karibuni tofauti na awali ambao baadhi ya vigogo walidaiwa kwenda kupata tiba hiyo kwa kificho.Lakini, kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ambaye alifika Samunge, Loliondo siku tatu zilizopita na kunywa kikombe cha Babu, jana Sumaye naye alifika kijijini hapo kunywa kikombe hicho.

Akiongozana na watu kumi wa familia yake, Sumaye alifika kijijini Samunge saa 7 mchana ambapo alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Loliondo, Elias Wawalali ambaye kwa kutumia njia maalumu ya viongozi alipelekwa moja kwa moja kwa Mchungaji Mwasapile na kunywa dawa hiyo.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaofika kijijini Samunge kunywa dawa hiyo ya maajabu kwa mchungaji Mwasapile ambaye alisema kuwa anatoa tiba hiyo baada ya kuoteshwa na Mungu.

Mchungaji Loliondo awajibu Kakobe, MwingiraKatika hatua nyingine, Mchungaji huyo jana alivunja ukimya na kuwajibu baadhi ya viongozi wa dini waliomtuhumu kuwa tiba anayotoa ni ya nguvu za giza akisema kuwa waliotoa tuhuma hizo wana mtazamo wa kifedha zaidi na siyo imani.

Miongoni mwa viongozi ambao walitoa matamshi makali dhidi ya Mchungaji Mwasapile, ni Askofu Zakary Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efata ambao walikaririwa na vyombo vya habari wakituhumu tiba hiyo kwamba ni ya nguvu za giza.

Lakini, jana Mchungaji Mwasapile alisema,“..Hao (Kakobe na Mwingira) hawapo kiimani, wana mtazamo wa kifedha zaidi.

Ninachowaomba, wasiwazuie wengine kuja kupata tiba na wao wakitaka waje kupata tiba hii.”Alisema viongozi hao na watu wengine wasifikirie kuwa yeye anatoa tiba hiyo ili kutafuta sifa binafsi, kwa madhehebu, dini au kikundi fulani cha watu bali kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Mchungaji huyo pia alitoa tahadhari akiwataka watu kutowatorosha wagonjwa hospitalini kwa ajili ya kuwapeleka kwake wakiwa mahututi.Aliwataka wananchi wajihadhari na utapeli ulioibuka kwa baadhi ya watu kuwa wana dawa hiyo akisisitiza kuwa tiba yake ameoteshwa na Mungu na hakuna yeyote anayetoa bali yeye.

Wakati huo huo, Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia Tanzania (Chawatiata), kimedai kushangazwa na viongozi wa Serikali kupanga foleni mchana kweupe kupata huduma ya dawa kwa Mchungaji Ambikilile Mwasapile wakati wanapoenda kwa waganga wengine wa kienyeji, huenda kwa kujificha.

Kauli hiyo imekuja, siku chache baada ya vigogo wengi serikalini kwenda kwa mchungaji huyo maarufu kwa jina la 'Babu' wakiwamo Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustino Mrema na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa. Dawa ya mchungaji huyo imejizolea umaarufu wa kutibu magonjwa sugu kiasi cha kuwafanya hata wagonjwa kutoka nje ya nchi kuja nchini kutibiwa.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Katibu Mkuu wa Chawatiata, Mittam Magombeka alisema waganga wa tiba asilia wamekuwa wakidharauliwa na hata kuonekana kuwa ni aibu kupata tiba kwao.Jambo hilo alisema limekuwa likiwafanya baadhi ya wale wanaoamini tiba hizo kwenda kwao kwa siri ili wasionekane na watu.Habari hii imeandaliwa na Musa Juma, Elizabethy Suleyman, Exuper Kachenje
 
Hello,
My greeting to you My name is Shania, single and never married, how are you i hope you are fine and well sounded in good health, i am a good hearten girl loving and caring humble and respectful. i would like to know more about you, please if you do not mind write me with this address (misshania99@yahoo.com)i hope to hear from you soon, because i have something very important to share with you.
Shania

misshania99@yahoo.com
 
Hello,
My greeting to you My name is Shania, single and never married, how are you i hope you are fine and well sounded in good health, i am a good hearten girl loving and caring humble and respectful. i would like to know more about you, please if you do not mind write me with this address (misshania99@yahoo.com)i hope to hear from you soon, because i have something very important to share with you.
Shania

misshania99@yahoo.com

r u nigerian or tanzanian??sorry for that



















































am kiddin
 
Mbona ukiritimba? Sasa sisi tulioko huku mtambaswala tutapaje habari za mchungaji kama kuandika habari zake hadi kwa kibali? Jamani tupeni haki yetu ya kupata habari. Wewe Wawa Lali weeee!
 
dah yani hakuna kupitwa,hata kama huumwi una-renew licence in case kuna chochote kiondoke chenyewe
 
Back
Top Bottom