Mambo ya mazoea ambayo yakageuka kuwa kama sheria

Mambo ya mazoea ambayo yakageuka kuwa kama sheria

Mtoto mwenzako akija unaona kama atamaliza na wewe hautashiba vzuri, ila hii bana haikua nzuri😂 Full kujifunza uchoyo

Huo ulikuwa si uchoyo ila ndo hali halisi..mwanzoni si mnawekewa hadi kwenye sinia sasa watoto wakiongezeka ina maana sinia halitotosha na uwezekano wa kuongezewa inategemeana na huruma ya mwenye jiko
 
Jamaa hana mambo ya kishamba, ila sista kujifanya mtu wa maadili sana. Jamaa salamu yake ni aisee EXT vipi? Nikijibu freshi imetosha. Mi kwangu sioni kama ni ishu sana.

Habari yako dada/kaka imetosha hio! Mambo ya shkamoo huwa na kwepa.
Mimi kutamka shikamo hadi leo mzito, huwa nasema shiamo.
Kuna watu wanapenda shikamo kama inaongeza CD4 vile...
 
Sisi kipindi hicho kijijini hakuna umeme, mshua kanunua tv na jenereta, kuangalia tv ni jumamosi na jumapili tu, kipindi hicho TvT kuna sijui ITV kulikuwa na ile tamthilia ya Taswira ya kina kanumba na ray.

😂😂😂 daah huu uzi umenirudisha home.. michezo ya kaole ya ITV au ua jekundu TVT na tiketi ya kuangalia uwe umeoga la sivyo.. bafuni
 
Hahahaa wakati inaingizwa chumbani unaweza toa machozi. Kipindi cha mitihani TV ilikua hailali sebleni, after taarifa ya habari meza inasukumwa tu kuelekea chumbani.

Wazazi walikuwa ni wakatili 😂😂😂..
Hapo unaanza kufikiria vingi, mawazo kibao yaani wenzio wakianza kusimulia kesho weww utachangia nini
 
😂😂😂 daah huu uzi umenirudisha home.. michezo ya kaole ya ITV au ua jekundu TVT na tiketi ya kuangalia uwe umeoga la sivyo.. bafuni
Sasa hivi unaona madogo under 5 wanaingia youtube wenyewe kuangalia katuni, haijui hustle katika hizi mambo kabisa.
 
Hapo penye wali na maharage pamenigusa sana

Yani mambo ya mijini sometimes naona kama yamekua primitive sana, unakuta mtu kapika pilau vizuri halafu maharage yamekosekana unakuta kaweka kachumbali peke yake
Ni jana tu wife kanifanyia huu ukatili mkuu
 
Mimi kutamka shikamo hadi leo mzito, huwa nasema shiamo.
Kuna watu wanapenda shikamo kama inaongeza CD4 vile...
Mimi shkamoo kawaida sana kutoa ila sio kwa watu ambao unaanza kujiuliza niamkie au nisiamkie
 
Mimi pia sipendi kusalimia shikamoo pia kuna watu wanahisi shikamoo ni kitu kikubwa mno .

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna siku mama mmoja jirani alileta kesi nyumbani kuwa simsalimii shikamoo, akawakuta washua nao wasela. Nadhani alijutia maamuzi yake.
😀😀😀😀
 
Sasa hivi unaona madogo under 5 wanaingia youtube wenyewe kuangalia katuni, haijui hustle katika hizi mambo kabisa.

Bora iwe watoto wa jirani. Unawajua wale watoto wa uzeeni, unaweza kuta amemkalia kwenye kitambi na smartphone yake anaperuzi huku anachekewa tu
 
Wazazi walikuwa ni wakatili 😂😂😂..
Hapo unaanza kufikiria vingi, mawazo kibao yaani wenzio wakianza kusimulia kesho weww utachangia nini
Wakatili mno, hapo anaisukuma huku anajua kabisa anakukomoa😂😂.
 
Back
Top Bottom