Mambo ya Msingi Sana katika maisha

Hii namba 12...Ndio ugonjwa mkubwa wa wakazi wa Daslam.....wataalam wanaita .....''Burnout".........
 
Yaani hotelini kabisa nimelipia hela halafu nibakishe chakula?
Mi hua nasafisha kila kitu, respect itakuja kwa ustaarabu mwingine
Ukiagiza chakula hotelini, kumaliza chakula kwenye sahani ni ishara ya heshima na shukrani kwa mlo waliokuandalia. Inaonyesha kuwa unathamini jitihada zao.

Hata hivyo, kama ni kwa ndugu yako pakua kile kinachokutosha, ikitokea umepakuliwa acha chakula kidogo kuonyesha umeshiba, Muhimu zaidi ni kuwa na adabu na kushukuru.
 
Jitahidi sana kutokuelezea shida zako kwa kila mtu labda zimekufika shingoni na kwa watu maalum
Usijionyeshe unapesa pesa inajionyesha yenyewe
Usiwakate watoto unaoona kabisa hii damu yako wala usiwatolee maneno machafu
Sasa mwanangu kwanini nisijionyeshe kama Nina pesa Ata kama Sina maana kwa mfano ata mahusiano huwezi Pata bila ya ku-brag docio(kujisifu) labda wa watu wengine ndugu, mke, na marafiki s vyema kujionesha kwamba na hapa ipo sana
 
Namba 8 ni ngumu sana. Anaweza kukugeuzia kibao akakusemea kwa mumewe kuwa unamtaka. Kwa lugha rahisi anakuwahi kabla ww hujamsemea kwa mumewe
 
👉Point ya nyongeza. Ukikopeshwa na ukabahatika kuzipata fedha ndani ya muda usisubiri paka upigiwe ujiongeze rudisha hela ya watu

👉MTU akija kukukopa hela usimuulize ni ya kazi gani wewe mpe tu kama unayo.

👉Ukipanda kwenye basi jitahidi kumsalimia jirani utakaemkuta kwenye siti

👉Ukienda kusalimia, usikae sana watu wana bajeti zao
 
Safi sana mkuu
 
Sasa mwanangu kwanini nisijionyeshe kama Nina pesa Ata kama Sina maana kwa mfano ata mahusiano huwezi Pata bila ya ku-brag docio(kujisifu) labda wa watu wengine ndugu, mke, na marafiki s vyema kujionesha kwamba na hapa ipo sana
Pesa ya kujionesha itakupa mpenzi/mke na rafiki wa uongo. Pesa ikiisha hao wote watakukimbia. Trust me. I once went through all that.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…